Thursday, August 6, 2015

QURAN SIO MANENO YA ALLAH WALA MUNGU


Ndugu msomaji,

Huu ni MSIBA mkubwa sana kwa Waislam wote duniani. Waislam wamekuwa na tabia ya kusema kuwa, eti Quran yote ni maneno ya Allah. Unapo wauliza, huyo Allah aliwezaje ongea na Muhammad, wanabakia kimya na kuanza kukutukana. Zaidi ya hapo, leo nitawawekea ushahid tosha kuwa Quran sio maneno ya Allah.

Haya ungana nani kwa ushahidi:

SHETANI ANASEMA KWENYE QURAN
Surah Al Hijr 39. Shetani akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,

Kwenye Surat Al Hijr, tumesoma kuwa Shetani ndie anazungumza katika hiyo aya ya 39. Kumbe basi, Shetani ni msemaji ndani ya Qurani.


HAPA TUNASOMA KUWA ZAKARIA NA YEYE NI MZUNGUMZAJI KATIKA QURAN
Surat Maryam: Zakaria Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.

Waislam, hivi Quran ni maneno ya nani? 

Endelea kupata darasa hapa:

MARYAM NA YEYE NI MSEMAJI KATIKA QURAN
Surat Maryam aya 18: Maryamu akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.

Waislam, mbona na Maryam anasema kwenye Quran? Au siku hizi Maryam amekuwa Allah? Huu ni Msiba mkubwa sana kwa Waislam.

MALAIKA NAO WANASEMA KWENYE QURAN
Surat Maryam aya 21: Malaika akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.

Ndugu msomaji, kwanini Waislam wanapenda kusema uongo namna hii, eti Quran yote ni Maneno ya Allah? Mbona tunasoma viumbe wengine wakisema ndani ya Quran? 


ISSA BIN MARYAM NA YEYE ANASEMA KWENYE QURAN
Surat Maryam  aya 36: Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.

Issa na yeye alisema kwenye Quran. Lakini Muhammad yeye hakuwai sema chochote kile kwenye Quruani wala kuzaliwa kwake hakukutajwa kwenye Quran. Huu ni Msiba mkubwa sana kwa WAISLAM.

SWALI LANGU KWA WAISLAM NI DOGO SANA:

1. NI NANI MSEMAJI KATIKA QURAN?
2. QURANI NI MANENO YA NANI?

Mkiweza nijibu kwa aya na bila shari, leo hii nitasilimu na kuwa Muislam.

Waislam huwa wanasema kama huamni kuwa Quran ni maneno ya Mungu, basi teremsha aya kama za Quran, huku tukifahamu kuwa kuna aya nyingi ambazo wasemaji wake ni wengine na sio Allah.

Sasa, huu utata tunawaachia waislam waje hapa kutujibu bila ya kuweweseka.

QURAN NI MANENO YA NANI?



Karibu sana kwa Yesu aliye hai ambaye ndie NENO LA UZIMA.

Max Shimba

Max Shimba Ministries

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW