Monday, August 3, 2015

MUNGU HANA DINI

Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: DINI, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.

Dini ni jaribio la mwanadamu kuwa na uhusiano na Mungu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .

YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI
Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.

ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1 Petro 3:18

YESU YU HAI
Kristo alikufa kwa ojili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu, kama yanenavyojil maandiko.1 Wakorintho 15:3,4

YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.Yohana 14:6
Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.
Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .
INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.

UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.Yohana 1:12
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.Waefeso 2:8,9
INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO
Tazama, nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .
Kumpokea Yesu Kristo ni:
Kujua wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
Kumtegemea Mungu kwa kukusamehe kabisa.
Kumkaribisha Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani, ili uwe kama anavyopenda.
swa3

Je, ni picha gani aliye mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambaye ungependa awe mfano wa maisha yako?
Yafuatayo ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea Kristo ndani ya maisha yako?

UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA
Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.
Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin.
Je, sala hii ni sawa na haja ya moyo wako?
Kama sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.

YESU YUMO MAISHANI MWAKO
Sasa, je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje?
Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20.
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwanba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.

ALIYE NA YESU, ANAO UZIMA WA MILELE
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwana. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu. 1 Yohana 5:11-13
Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa. (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.

USIYATEGEMEE MAWAZO YA MOYO WAKO.
Unaweza kujisikia leo unalfuraha kisha kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako. Waebrania 13:8.
swa4
Ukweli wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.
Tunaunganishwa na uwezo wa ukweli kwa imani.
Tunapotii ukweli, hali ya kujisikia ya moyo (maoni) huongozwa vyema.
Tunamtegea Mungu na ukweli wake wala sio hali ya kujisikia ya moyo.
Tukifanya dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.
Basi, usitegemee mawazo yako, bali utegemee ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.

KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU
Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.
Yesu ameingia katika maisha yako. (Ufunuo 3:20)
Umesamehewa dhambi zako. (Wakolosai 1:14)
Umefanyika kuwa mwana wa Mungu. (Yohana 1:12)
Utazidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)
Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako?
Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.
Tuombe tukiwa huru.
Na sasa je?

JINSI YA KUKUA KIROHO
Kama mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:
Zungumza na Mungu kwa maombi (Yohana 15:7)
Soma Neno la Mungu (Matendo 17:11)
Uwe mwaminifu kwa Mungu (Yohana 14:21)
Mshuhudie Kristo kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)
Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)
Umruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)

NI MUHIMU KWA WAKRISTO KUSHIRIKIANA
Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25)
Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikirundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako.
Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.
Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.
Max Shimba Ministries Org

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW