Monday, August 3, 2015

KUTEKWA NYARA!! USHUHUDA WA KUSISIMUA

“Nilikamatwa na kuteswa na polisi wa Misri kwa kuhoji imani yangu katika Uislamu” 
Na Mark Gabriel

Ilikuwa saa 9 kamili alfajiri wakati baba yangu aliposikia mlango wa nyumba yetu ukigongwa. Wakati alipofungua mlango, watu 15 hadi 20 waliingia kwa haraka ndani wakiwa wamebeba silaha za Urusi Kalashnikov za uvamizi. Walikimbilia ghorofani wakipitapita kila mahali katika nyumba wakiwaamsha watu na kunitafuta mimi. Walikuwa wametapakaa kila mahali mle ndani kabla mmoja wao hajanikuta nimelala kitandani mwangu. Wazazi wangu, kaka zangu na wenzi wao na watoto walikuwa wameamka, wakilia na kuhofia sana wakati hao watu waliponiburuza na kuondoka na mimi. Kila mtu wa eneo lile alisikia habari za vurumai hizo. Nilipelekwa mahali palipoonekana kama jela na nikawekwa rumande. Asubuhi yake wazazi wangu kwa hasira na majonzi walijaribu kutafuta kwamba nini kilichonitokea. Moja kwa moja walienda kituo cha polisi na kudai “mtoto wetu yuko wapi? Lakini hakuna yeyote aliyejua lolote juu yangu. Nilikuwa katika mikono ya polisi wa siri wa Misri.

Matukio Yaliyosababisha Kukamatwa Kwangu Miaka kumi na tano iliyopita nilikuwa Imamu wa msikiti katika jiji la Giza, Misri, mahali ambapo yale mapiramidi maarufu ya Misri yamepangwa. (Imam wa msikiti ni wadhifa unaofanana na mchungaji wa kanisa la Kikristo) Nilihubiri ujumbe wa wiki siku za ijumaa kuanzia saa 6 hadi 7 mchana, ikiwa ni pamoja na kufanya wajibu zinginezo zilizonihusu.
Ijumaa moja ujumbe wangu wa wiki ulikuwa Jihad. Niliwaambia watu 250 waliokuwa wamekaa uwanjani mbele yangu Jihad katika uislamu inatetea taifa la Kiislam na Uislam dhidi ya mashambulizi ya maadui. Uislam ni dini ya amani na itapigana na yule anayepigana nayo tu. Hawa makafiri, wamataifa, wapotoshaji, Wakristo na wanaomhuzunisha Allah, Wayahudi, mbali ya wivu wa Uislam wa amani na Mtume wake; walieneza uongo kwamba Uislam ulienezwa kwa upanga na kwa nguvu kali sana zenye vurugu. Makafiri na washitaki wa Uislam hawayakubali maneno ya Allah.

Katika hatua hii nilinukuu kutoka katika Koran “wala usimuue yeyote ambaye uuaji kwa Allah umekatazwa ila kwa sababu ya haki” (Surah 17:33 Koran Tukufu). Nilipozungumza maneno haya ndio kwanza nilikuwa nimetoka kuhitimu Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Kairo Misri. Chuo Kikuu cha zamani na chenye fahari zaidi cha Kiislam duniani. Kinafanya kazi kama mamlaka ya kiroho ulimwenguni mwote. Nilikuwa nafundisha katika Chuo Kikuu na nilikuwa Imam siku za mwisho wa juma katika msikiti huu. Nilikuwa nakihubiri kile walichonifundisha, lakini kwa ndani nilihitaji kuyaweka mawazo yangu kwenye nafsi yangu. Hata hivyo, nilijua kile kinachowapata watu waliohitilafiana na agenda za Al-Azhar. Watafukuzwa na wasingeruhusiwa kufundisha Chuo Kikuu kingine chochote katika Taifa hilo.

Nilifahamu kwamba nilichokuwa nakifundisha pale msikitini na katika Al-Azhar hakikuwa kile nilichokiona katika Koran, ambayo nilikuwa nimeikariri yote nikiwa na umri wa miaka 12. Kilichonichanganya zaidi ni kwamba niliambiwa nihubiri kuhusu Uislam wa upendo, wema na msamaha. Wakati huo huo wale waumini wakereketwa; wale ambao ndio waliotarajiwa kuishi kwa kutenda Uislam kamili; walikuwa wakiyapiga mabomu Makanisa na kuua Wakristo. Kwa wakati huohuo vuguvugu la jihad lilikuwa limepamba moto ndani ya Misri. Matukio ya mashambulizi na kupigwa mabomu, dhidi ya Wakristo yalikuwa ya kawaida sana. Ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.

Kuutafuta UkweliWakati mwingi nilijaribu kutazama kimantiki aina ya Uislam niliokuwa naufanya kwa kujiambia nafsi yangu “Sawa, hauko mbali sana na ukweli. Kwanza kuna mstari katika Koran kuhusu upendo, amani, msamaha na huruma. Unachotakiwa tu ni kutojali kipengele kinachohusu jihad na cha kuua wasiokuwa Waislam.” Nilipitia kila tafsiri ya koran nikijaribu kukwepa Jihad na kuua wasio Waislamu, bado niliendelea kugundua utekelezaji wa hayo ukiungwa mkono. Wanazuoni walikubali kwamba Waislam lazima wakazie Jihad kwa makafiri (wale wanaoukataa Uislam na waasi wale wanaoucha Uislam). Bado Jihad haikuwa na maelewano na mistari iliyozungumzia kuishi kwa amani na wengine. Mikanganyo yote katika Koran ilikuwa kweli inasababisha matatizo kwa imani yangu. Nilitumia miaka 4 kusomea Digrii yangu ya kwanza, nilihitimu nikiwa wa pili kati ya wanafunzi elfu sita. Halafu kulikuwa na miaka mingine 4 kwa ajili ya Digrii yangu ya pili na mitatu zaidi kwa ajili ya Ph.D (udaktari wa falsafa) yote nikisomea Uislam.

Ninafahamu mafundisho vizuri katika sehemu moja pombe imekatazwa; katika sehemu nyingine imeruhusiwa (linganisha Surah 5:90-91 na Surah 47:15). Katika sehemu moja Koran inasema Wakristo ni watu wema ambao wanampenda na kumwabudu Mungu mmoja, kwahiyo mnaweza kuwa marafiki nao (Surah 2:62,3:113-114). Halafu unakuta mstari mwingine unaosema Wakristo lazima waslim, walipe kodi la sivyo wauwawe kwa upanga (Surah 9:29) Wanazuoni wanasuluhisho la kitheolojia kwa matatizo haya, lakini nashangaa ni jinsi gani Allah, mwenye enzi na mwenye nguvu sana, awe aidha amejichanganya mwenyewe namna hii kubwa au anabadili nia yake kwa kiasi kikubwa namna hii, hata nabii wa Kiislam Mohammed, aliitekeleza imani yake katika njia ambazo zinapingana na Koran. Koran inasema Mohammed alitumwa ili kuonyesha rehema za Mungu kwa ulimwengu. Lakini alikuja kuwa dikteta wa kivita, akishambulia, kuua na kuchukua mali na kupora ili kufadhili himaya yake. Iweje hivyo iwe ni kuonyesha rehema?

Allah, Mungu aliyefunuliwa katika Koran, sio Baba wa Upendo. Inasema kwamba anatamani kuwaongoza watu upotevuni (Surah 6:39,126). Hawasaidii wale walioongozwa nae upotevuni (Surah 30:29) na anatamani kuwatumia kujaza watu kuzimu (Surah 32:13). Uislamu umejaa ubaguzi dhidi ya wanawake, dhidi ya wasio Waislam, dhidi ya Wakristo na zaidi hasahasa dhidi ya Wayahudi.

Chuki imejengwa katika dini. Historia ya Uislam ambayo ilikuwa ndio eneo langu nililobobea hasa, ingeweza ikaainishwa kama mto wa damu. Mwishoni nilifikia mahali ambapo nilikuwa nahoji imani na Koran pamoja na wanafunzi wangu katika Chuo Kikuu. Baadhi yao walikuwa wanachama wa vuguvugu la ugaidi na walighadhibika. “Huwezi kuushutumu Uislam. Ninini kimetokea? Unatakiwa utufundishe. Unatakiwa kukubaliana na Uislam”. Chuo Kikuu kikasikia kuhusu hilo, na niliitwa kwa ajili ya mkutano Desemba 1991. Kufupisha mkutano, nikawaambia kilichokuwepo moyoni mwangu. Siwezi tena kusema kwamba Koran imekuja moja kwa moja toka mbinguni au toka kwa Allah. Huu hauwezi kuwa ufunuo wa Mungu wa kweli. Haya yalikuwa maneno ya kufuru kubwa katika mtazamo wao. Wakanitemea mate usoni, mtu mmoja akanitukana “wewe mkufuru! mbegu haramu!” Chuo Kikuu kikanifukuza na kuita kikosi cha polisi wa siri wa Misri.

Gereza la Misri

Kutumia muda pamoja na polisi wa siri wa Kimisri ni tofauti sana na kutembelea gereza la Marekani. Kwa siku tatu sikupewa chakula wala maji. Katika siku ya nne, mahojiano yakaanza. Aliyekuwa akiniuliza maswali alikaa nyuma ya meza nami nimekaa upande wa pili. Nyuma yangu walikuwepo maofisa wa polisi wawili au watatu. Walikuwa na uhakika kuwa nilikuwa nimehubiriwa injili na kubadlilika kuwa Mkristo, kwa hiyo mhojaji akakazania kunisumbua.. “Ni mchungaji gani uliyezungumza naye? Umekuwa ukitembelea kanisa gani? Kwanini umeukana Uislam?”

Aliniuliza maswali mengi. Safari moja nilisita kwa muda mrefu hadi nilipojibu. Aliwaashiria wanaume waliokuwa nyuma yangu. Waliukunja mkono wangu na kuushikilia chini ya dawati. Aliyekuwa akiniuliza maswali alishikilia sigara iliyowashwa. Alinikaribia na kuizimia juu ya mkono wangu. Bado kovu lile ninalo hadi leo. Pia ninalo kovu kwenye mdomo wangu mahali alipopafanyia jambo hilohilo.
Mara nyingine alitumia sigara pale alipokasirika na mara nyingine maofisa walinipiga usoni. Jinsi aliyekuwa akinihoji alivyoendelea, hasira na shinikizo ndivyo zilivyoongezeka kuwa kubwa kwake. Mara moja walileta mbanio wa mkaa mle chumbani. Nilishangaa hili ni la nini? Kisha aliyekuwa ananihoji alitaka kuzungumzia suala lake, niligundua kilichokuwa kikiendelea. Ule mbanio ulichomwa ukawa mwekundu sana na ofisa mmoja aliukandamiza kwenye nyama za mkono wangu wa kushoto.
Walinitaka nikiri kwamba nimebadili dini lakini nikawaambia, “sijaukana Uislam, nilikisema tu kile ninachoamini. Mimi ni mtu wa taaluma, mimi ni mtu ninayefikiri. Nina haki ya kujadili somo lolote la Uislam. Hii ni sehemu ya kazi yangu na sehemu ya maisha yangu ya kitaaluma. Nisingeweza hata kuota ndoto za kubadilika kutoka katika Uislam. Ni damu yangu, desturi yangu, lugha yangu, familia yangu na maisha yangu. Lakini kama mkinishutumu kwa kubadilika kutoka katika Uislam kwa yale ninayowaambieni,basi niondoeni kwenye Uislam. Sitajali kuwa nje ya Uislam.”

MbwaBaadae maofisa walinichukua hadi kwenye mlango wa chumba kidogo na kusema “kuna mtu akupendae sana ambaye anataka kukutana na wewe”. Nikauliza, “ni nani?” Nilitumaini alikuwa mmoja wapo wa watu wa familia yangu au rafiki aliyenitembelea au kunitoa nje ya gereza. Wakasema, “Humfahamu lakini yeye anakujua” Walifungua mlango wa chumba na ndani nikaona mbwa mkubwa.

Hapakuwapo na kitu kingine chochote mle chumbani. Watu wawili waliniingiza mle chumbani na wakaniacha humo na kufunga mlango. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza moyo wangu kulia kwa nguvu. Moyoni mwangu nilimlilia Muumba wangu; “Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, wewe ndie utakae nitunza. Unawezaje kuniacha katika mikono hii miovu? Sifahamu kile wanachojaribu kunitendea, lakini nafahamu utakuwa pamoja nami na siku moja nitakuona Wewe na kukutana na Wewe”. Nilitembea hadi katikati ya chumba kile kitupu na nikaketi chini kwenye sakafu nikiwa nimepishanisha miguu yangu mtindo wa x. Mbwa alikuja na kuketi chini mbele yangu. Dakika zilipita huyu mbwa akiwa amenitazama kwa makini.

Nilimwangalia macho yake yakiwa yananitazama kuanzia juu hadi chini tena na tena. Niliomba ndani ya moyo wangu kwa Mungu ambaye nilikuwa simfahamu bado. Yule mbwa akasimama na akaanza kutembea kwenye duara kunizunguka mimi, kama vile mnyama aliye tayari kula kitu fulani. Kisha akaja upande wangu wa kulia na kulamba sikio langu kwa ulimi wake. Nilikuwa nimechanganyikiwa sana. Alikaa pale, na nililala usingizi. Nilipokuja kuamka yule mbwa alikuwa kwenye kona ya kile chumba. Alinikimbilia, kama vile kusema habari ya asubuhi. Kisha akalamba sikio langu la kulia tena na akakaa upande wangu wa kulia.

Wakati maofisa walipofungua mlango waliniona nikiomba na mbwa akiwa kaketi pembeni yangu. Nilimsikia mmoja wao akisema “Siwezi kuamini kuwa huyu mtu ni mwanadamu. Huyu mtu ni ibilisi ni Shetani”. Katika hatua hii hata mimi sikufikiri kwamba aliyekuwa akinihoji ni mwanadamu. Nilikuwa nimewekwa ndani kwa kule tu kuuhoji Uislam, sasa imani yangu ilikuwa kweli imetikiswa. Muda huu wote familia yangu ilikuwa ikijaribu kutafuta pale nilipokuwa. Hawakufanikiwa hadi pale mjomba wangu, ambaye alikuwa na cheo kikubwa katika bunge la Misri aliporudi nyumbani. Mama yangu alimwita akilia kwa huzuni, “Kwa wiki mbili hatujui alipo mwenetu, amekwenda”. Mjomba wangu alikuwa na mawasiliano yaliyokuwa yakihitajika. Siku kumi na tano baada ya kutekwa kwangu nyara alikuja gerezani na kunipeleka nyumbani.

Mwaka Mmoja Bila ImaniKwa mwaka mmoja niliishi bila imani. Sikuwa na Mungu wa kumuomba, wa kumuita au kumwishia. Niliamini katika uwepo wa Mungu ambaye alikuwa mwenye rehema na haki, lakini sikuweza kufahamu Mungu wa jinsi hiyo ni nani. Je, alikuwa ni mungu wa Waislam, wa Wakristo au Wayahudi au alikuwa mnyama; kama vile ng’ombe wa Kihindu? Sikuwa na maarifa ya jinsi ya kumtafuta.

Unatakiwa kufahamu kwamba kama Mwislam akifikia hitimisho kwamba Uislam sio wa kweli na akiwa hana dini ya kugeukia, atakuwa na wakati mgumu sana katika maisha yake. Imani iko katika kiini cha maisha ya mtu wa Mashariki ya Kati.

Hawezi kufikiria namna ya kuishi bila kumjua Mungu wake. Kwa kipindi chote hiki cha mwaka mmoja, mwili wangu ulidhihirisha maumivu ambayo yalikuwa kwenye roho yangu. Ijapokuwa nilikuwa na mali za aina zote nilizohitaji, nilipata pigo la uchovu wa ndani sana kwa kule kujaribu mfululizo kutumia ufahamu wangu kupata picha ya Mungu wa kweli anavyofanana.
Nilikuwa naumwa na kichwa mfululizo . Nilikwenda kwa daktari ambaye alikuwa ni ndugu wa familia yetu. Akafanyia uchunguzi kichwa changu kwa (kipimo cha scan) lakini hakuona tatizo lolote. Aliniandikia dawa zitakazonisaidia.

Hotuba Ya MlimaniNiliishia kulitembelea duka la dawa lililokuwa karibu kila wiki mara mbili ili kupata paketi ya vidonge. Nilikuwa nachukua kidogo kidogo nikitarajia maumivu ya kichwa yangeondoka moja kwa moja. Baada ya kwenda pale dukani kwa kitambo yule mfamasia akaniuliza, “Ni nini kinachoendelea kwenye maisha yako?” Nikamjibu, “Sina tatizo lingine ila jambo moja tu. Ninaishi bila Mungu sifahamu Mungu ni nani” Akaniambia, “Lakini wewe ulikuwa Profesa katika Chuo Kikuu kinachoheshimika zaidi nchini Misri. Familia yako inaheshimika sana katika jumuiya hii” “Hiyo ni kweli” Nilijibu, ‘lakini nimegundua upotofu mwingi katika mafundisho yao. Siamini tena kama nyumba yangu na familia yangu wamejengwa katika misingi ya ukweli. Nimekuwa nikijifunika siku zote katika uongo wa Kiislamu, sasa najiona niko uchi. Nawezaje kuujaza utupu ulioko moyoni mwangu? Tafadhali nisaidie’ “Sawa” Alisema, “Leo nitakupa vidonge hivi na nitakupatia kitabu hiki-Biblia”

Nilikichukua kile kitabu nyumbani na kukifungua bila mpangilio maalum. Macho yangu yakaangukia Matayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, jicho kwa jicho na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie na la pili.” Mwili wangu wote ukaanza kutetemeka. Nilikuwa nimesoma Koran na maneno maisha yangu yote hata mara moja sikukutana na maneno yenye uvuvio kama haya. Nilikutana uso kwa uso na Bwana Yesu Kristo, nikapoteza muda mwingi bila kufanya chochote.

Ilionekana kana kwamba nilikuwa nimeketi juu ya mawingu juu ya kilima; na mbele yangu alikuwepo mwalimu mkuu kuliko wote ulimwenguni akiniambia habari za siri za mbinguni na moyo wa Mungu. Ningeweza kulinganisha kwa urahisi Biblia na na kile nilichokua nimekisoma kutoka katika miaka yangu mingi ya kusoma Koran; na hapakuwepo na shaka katika ufahamu wangu tena kwamba hatimaye nimekutana na Mungu wa kweli. Bado nilikuwa nasoma hadi alfajiri ya siku iliyofuata, na kwa dhati niliyatoa maisha yangu kwa Yesu.

Imani MpyaNiliendelea Kufanya Kazi Kwenye Biashara za Baba yangu na sikumweleza lolote juu ya imani yangu mpya. Ukweli ni kwamba alinipeleka Afrika ya Kusini mwaka 1994 ili kunitafutia nafasi zaidi za biashara. Nilipokuwepo kule nilikaa siku tatu pamoja na familia moja ya Kikristo ya kutoka India. Tulipoachana walinipa msalaba mdogo ukiwa kwenye mkufu ili nivae shingoni. Msalaba huu mdogo ulisababisha badiliko kubwa maishani mwangu. Baada ya siku chache zisizofikia juma moja, baba yangu aliugundua mkufu shingoni mwangu akachukia sana kwa sababu, kulingana na mila za Kiislamu, ni wanawake tu wanaoruhusiwa kuvaa mikufu kwenye shingo zao. “Kwanini unavaa mkufu huu?” aling’aka.
Ilikuwa kana kwamba ulimi wangu uliongea wenyewe na si mimi wakati nilipojibu, “Baba huu sio mkufu huu ni msalaba unamwakilisha Yesu, aliyekufa juu ya msalaba kama huu kwa ajili yangu, yako na watu wote wa ulimwengu mzima. Nilimpokea Yesu kama Mungu na Mwokozi wangu, na nakuombea na familia nzima mumpokee Yesu Kristo.” Kwanza baba yangu alizimia pale pale mtaani tulipokuwa. Alipozinduka alikuwa amekasirika sana kiasi kwamba hata kuongea ilikuwa shida, alininyooshea kidole. Kwa sauti kali mithili ya farasi akasema; “kaka yako amebadili dini ni lazima nimuue leo” Popote alipokuwa akienda baba yangu alizoea kubeba bunduki kwapani iliyokuwa kwenye mfuko wa ngozi. (Matajiri wengi wa Misri hutembea wamebeba bunduki). Aliichomoa bunduki yake na kunielekezea. Nilianza kukimbia nikishuka mitaani na nilipochepuka kwa kukata kona nikasikia risasi ikipita nyuma yangu. Niliendelea kukimbia ili kusalimisha maisha yangu.

Dada yangu alinifanyia rehema na kukusanya vitu vyangu kutoka katika nyumba ya wazazi wangu. Yeye pamoja na mama yangu walinipa kiasi cha fedha na nikaingia ndani ya gari langu na kuanza kuendesha jioni ya tarehe 28 Agosti 1994. Kwa miezi mitatu nilijitahidi kusafiri kupitia kaskazini mwa Misri, Libya, Chad na Kameruni. Hatimaye nikatua Kongo. Wakati ule nikaugua malaria. Walinitafutia daktari Mmisri wa kunipima, akasema hadi asubuhi nitakuwa nimeshakufa, wakafanya mipango ya kupata jeneza kutoka ubalozi wa Misri ulioko Kongo ili kunisafirisha kunipeleka nyumbani. Kwa mstuko mkubwa wakaniona nimeamka kesho yake asubuhi. Nilitoka hospitali baada ya siku tano na nikaanza kuwaambia watu kila mahali kuhusu kile Yesu alichonitendea.

Maisha nikiwa kama Mfuasi wa Yesu KristoMiaka kumi imepita tangu nilipompokea Bwana Yesu kama mwokozi wangu. Aliniita na kunipa uhusiano wangu binafsi na yeye, kitu ambacho Uislamu hautoi kamwe. Kamwe sijaacha kulia kwa ajili ya watu wangu Waislamu ambao niliwaacha nyuma, nikimwomba Mungu awakomboe toka katika giza la Uislamu. Kiasi kikubwa cha taarifa zisizo sahihi zimekuwa zikishirikisha watu kwa njia ya vyombo vya habari na tovuti.

Lengo langu ni kuwasaidia watu waone waziwazi ni kwanini watu hawa hufanya kile wanachokifanya. Sitaki kuwachochea watu wakasirike, ila nataka kuwahamasisha kuamini– kuamini ili Uislamu uanguke na kuwaachilia mateka wake, katika jina la Yesu.

Kama Yesu Kristo angekuwa anaishi na sisi leo, angesafiri kwenda nchi za Kiislamu. Angeingia misikitini na kuhubiri neno la Mungu na ujumbe wa wokovu sawa na alivyofanya katika Hekalu miaka 2000 iliyopita. Angewatembelea Waislamu majumbani mwao au angekutana nao kwenye maeneo yao ya kufanyia kazi. Angewaponya Waislamu ambao ni wagonjwa. Angetangaza msamaha wa Mungu kwa Waislamu watenda dhambi. Angekabiliana na Waislamu kwa kweli yake, na angewaeleza kuhusu siri ya mbinguni kwa upendo huruma na uangalifu.

Asingewaogopa, asingefikiri kwamba baadhi yao ni magaidi na wangeweza kumuua au kumdhuru. Yesu Kristo angewaonyesha Waislamu njia ya kwenda mbinguni kupitia Yeye mwenyewe.

Bwana Yesu Kristo asingewageuzia Waislamu kisogo. Hii ni changamoto yangu kwa Kanisa. Kunjueni mikono yenu kwa Waislamu. Waonyesheni ushuhuda wa Kristo. Waambieni Yesu alikufa kwa ajili yao. Wapeni tumaini kwamba dhambi zao zitasamehewa. Moyo wangu unamlilia Bwana kwa ajili ya Kanisa la Mashariki ya Kati liguswe na Roho wa Mungu na kuwafungulia milango Waislamu ili waje kwenye maarifa ya Kristo.

Mark Gabriel ni mwandishi wa kitabu cha Uislamu na Ugaidi (Islam and Terrorism-Charisma House) Makala haya yamechukuliwa kutoka katika kitabu hicho.

Mungu mpendwa ninafahamu kwamba dhambi zangu zimenitenga na wewe, na nataka kukiri dhambi zangu. NASIKITIKA NIMEKUKOSEA. Ninajua kwamba unanipenda ulimtoa Yesu afe msalabani badala yangu, akichukua adhabu ya dhambi zangu. AKSANTE. Sasa hivi nakuomba uingie na kuyatawala maisha yangu. Ninajitoa nafsi yangu kwako. Tafadhali anza kuyaongoza maisha yangu. NAKUHITAJI. Aksante kwa kunipa uzima wa milele. Katika jina la Yesu ninaomba. Amina.

Tunatoa vijarida, vipeperushi, kanda za kaseti na za video za aina mbalimbali zinazofunua na kuchambua mafundisho yote makubwa ya Uislamu. Taarifa hizi ni za uhakika kwa kujibu swali lolote unaloweza kuwa nalo kuhusu Uislamu. Saidia kueneza ukweli. Vitu vyote hivyo utavipata bure kama ukiagiza.

Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW