Monday, August 3, 2015

JE, MJI ALIO UCHAGUA ALLAH NI SAWA NA WA YEHOVA?

MJI WA ALLAH:
Qurani 27:91 An-Naml (sisimizi/mchwa/wadudu chungu)
Bila shaka nimeamrishwa nimuabudu mola wa mji huu (wa Makka) ambaye ameutukuza na ni vyake tu (Mwenyezi Mungu) vitu vyote…
Qurani 3:96 Suratul Aal-Imran (watu wa Imram)
Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyo Makka yenye baraka na uwongozi kwa ajili ya walimwengu wote.
Qurani 106:3-4 Suratul Quraysh (Makureshi-kabila)
Basi nawamuabudu Bwana wa nyumba hii (Al-ka'ba) Ambaye anawalisha (wakati Waarabu wenzi wao wamo) katika njaa na anawapa amani wakati wenzi wao wamo katika khofu.
Hivyo tunaona kuwa Allah ndiye bwana wa Al-ka'ba kadiri ya aya hii na Al-ka'ba iko katika Makka. Kupitia aya hizi tunaona Allah mungu anayeabudiwa na Waislamu amechagua mji wa Makka kuwa ndio mji wake mtakatifu na tena Muhammad (s.a.w) aliamrishwa amuabudu mola wa mji huo wa Makka ambaye ndiye Allah.

MJI WA YEHOVA:Je, Mungu wetu aitwae Yehova alichagua mji gani? Endelea ……..
Mji aliouchagua Mungu wetu Yehova ni huu…
2 Nyakati 6:4-6
Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza kwa mikono yake, akasema, Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wowote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu yeyote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo, na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli.
Maandiko hayaelezi mji mwingine wowote aliouchagua Mungu wetu hapa duniani bali ni mji wa Yerusalemu tu. (tazama 2 Nyakati 12:13,Ezra 6:12; 7:15,27; Zaburi 26:8; Zakaria 2:12)

Kupitia aya hizi tunaona Mungu wetu Yehova, mji wake aliouchagua niYerusalemu. Neno Yerusalemu ni la lugha ya Kiebrania na maana yake ni "chimbuko la amani". Hata Waisraeli walipokuwa mbali na mji wa Yerusalemu bado walipiga magoti na kuelekeza nyuso zao Yerusalemu. (Tazama Danieli 6:10). Mji aliouchagua Yehova ni Yerusalemu, na mji aliouchagua Allah ni Makka. Na hii ndio tofauti ya mji wa Allah na Yehova.

Leo tumejifunza tena kuwa Allah wa Quran sio Mungu wa Biblia. Allah sio Mungu bali ni kiumbe bandia.
Max Shimba Ministries Org.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW