Monday, August 3, 2015

JE, MBINGU YA YEHOVA NI SAWA NA PEPO YA ALLAH?

MBINGU YA YEHOVA:
Luka 20:34-36
Yesu akawaambia wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa, lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule. Na kule kufufuka katika wafu hawaoi wala hawaolewi. wala hawawezi kufa tena. Kwa sababu huwa sawa sawa na malaika, nao ni wana wa Mungu kwa vile walivyo wana wa ufufuo.

Maandiko haya yanatuthimbitishia Wakristo kuwa tutakapofufuliwa na kuingia mbinguni, hakuna mambo ya kuolewa wala kuoa, maana tutakuwa na miili ya kiroho (1 Korintho 15:43-54) Aidha maandiko yanatufundisha kuwa ufalme wa Mungu siyo kula wala kunywa bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Tazama Warumi 14:17). Mungu wetu anafundisha wazi wazi kuwa kule mbinguni katika ufalme hakuna njaa, wala kiu wala jua kutupiga (Ufunuo 7:16-17.)

PEPO AU MBINGU YA ALLAH ITAKUWA HIVI:
i). Maghorofa
Qurani 39:20 Suratul Zumar (makundi/vikosi)
Lakini waliomcha mola wao watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa chini (mbele) yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyenzi Mungu, Mwenyenzi Mungu havunji ahadi yake.
ii) mito ya maji, maziwa, ulevi, asali na matunda
Qurani 47:15 Suratul Muhammad
Mfano wa pepo waliyoahidiwa watawa (wacha Mungu itakuwa hivi). Imo mito ya maji yasiyovunda, na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao na mito ya asali iliyosafishwa. Tena humo watapata matunda ya kila namna, na samahani kutoka kwa mola wao. Basi hao watakuwa sawa na wale wataokaa motoni na kunyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao?.
Je Matunda hayo ni sawa na ya wapi?
Qurani 2:25 Suratul Al- Baqarah (ngombe jike)
Na wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake. Kila mara watakapopewa matunda humo kuwa ni chakula watasema “haya ndiyo yale tuliyopewa zamani (ulimwenguni) kwani wataletewa (matunda hayo) hali yatakuwa yamefanana (na yale waliyokuwa wakiyajuwa ulimwenguni wataletewa kwa sura hiyo lakini utamu mwingine kabisa) na humo watapata wake waliotakasika (na kila mabaya na machafu) na watakaa milele humo.
iii). Watapata wanawake aina hizi na nyama za ndege
Qurani 56:15-23 Suratul Al Waaqiah (Tukio) nanukuu aya ya 21-23 tu
Na nyama za ndege kama watakavyotamani (wenyewe). Na wanawake wenye macho mazuri na makubwa (ya vikombe). (wanapendeza na safi) kana kwamba ni lulu zilizofichwa (katika machaza yake, ndio kwanza zinapasuliwa)
Qurani 37:48-49 Suratul As-Saaffat (Wapangao mistari)
Na pamoja nao watakuwa wanawake wenye macho mazuri makubwa. (Safi) wanawake hao kama mayai (ya mbuni) yaliyohifadhiwa.
Qurani 37:44-46 Suratul As-Saaffat (Wapangao mistari)
Wako juu ya vitanda (viti vya enzi vya fahari), wamekabiliana (wanazungumza). Wanazungushiwa gilasi zenye (vinywaji) safi.Vyeupe yenye ladha kwa hao wavinywao.
Kupitia aya hizi tumeona kuwa Allah Sub-haana Wataala Mungu anayeabudiwa na Waislamu ametoa ahadi ya kuwaingiza Waislamu peponi (mbingu) na kuwa watapata mito ya maji, mito ya maziwa na ulevi na pia mito ya asali vilevile watapata matunda, nyama ya ndege na pia wataozeshwa na Allah mungu wao wanawake wenye macho makubwa kama mayai ya mbuni. na wengine makubwa kama vikombe.
Jambo la kushangaza zaidi ni pale tunaposoma kitabu cha Hadithi, maana imani ya Dini ya Uislamu imejengwa pia katika vitabu vya hadithi. Soma
Qurani 42:10 Suratul Ash-Shuura (mashauriano)
Mkihitalifiana katika jambo lolote (rejeeni kitabu cha Mwenyenzi Mungu na Hadithi za mtume kwani)…
Tunaposoma kitabu cha Hadithi ya mtume kiitwacho Sunnan Ibn-1- Majah vol 5 ukurasa wa 546 Hadithi No: 4337 kuna maelezo haya

Im simuliwa na Abu' Umama ya kuwa mjumbe wa Allah (baraka na amani ya Allah iwe juu yake) alisema Allah hatamruhusu yeyote kuingia peponi ila kwa idhini ya Allah, Mwenye nguvu na utukufu naye atamwozesha mwanamume wake sabini na mbili. Wawili watakuwa mabikira (mahurul-ain) yaani wanawake wa peponi wenye macho makubwa, na sabini watakao warithi ambao watu (mabwana zao) wametupwa katika moto wa jahanamu kila mmoja wao (hao wanawake) wana uke wa kupendeza. Na mwanamume, Nguvu ya uume wake katika kujamiana hautapinda (kusinyaa) bali utadumu sana
Kwa kiingereza Hadithi hii inasomeka hivi:-

Abu-Umama (Allah be pleased with him) reported that Allah's messenger (peace and blessings of Allah be upon him)said Allah will not admit anyone in the paradise but Allah the mighty and Glorous, will marry him with seventy two wives two will from virgins (haurine) with big eyes and seventy will be his inheritance from the people of the Hell- Fire (1).Everyone of them will have apleasant vagina and he (the man) have sexual organ that does not bend down (during sexual intercouse)

Hivi ndivyo Allah Mungu wa Waislamu alivyoahidi. Hili ni jambo ambalo kwa Mkristo linamshangaza sana kwani jambo hili linalofundishwa na Allah halipo kabisa kwa Mungu wetu Yehova hapa ulimwenguni ndiko kwenye ulevi,matunda,nyama za ndege, kuoana, maghorofa, magari, mito, bahari na vinginevyo.
Tafakari, je huyo Allah ni nani?

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW