Monday, August 10, 2015

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA NANE)


Kuna tofauti kubwa sana kati ya Isa wa Quran na Yesu wa Biblia. Quran inakiri kuwa Isa wake si chochote bali ni mtume tu .

ISA WA QURAN SI CHOCHOTE ILA NI MTUME TU
1.Qurani inasimulia kuhusu Isa bin Maryamu hivi.
Qurani 5;75 Suratul Al Maidah (Meza)
Masihi bin Maryamu “si chochote ila mtume (tu).” (Na) bila shaka mitume wengi wamepita kabla yake (Hawajaona?) na mamake ni mwanamke mkweli (na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na kwenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo?) Tazama jinsi tunavyo wabainishia aya, kisha tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).
Hapa tunaona Quran inasimulia kuwa masihi Isa si chochote ila mtume tu. Huu ndio mtego ambao Allah anautumia kwa Waislam, eti Isa ni Yesu na Yesu si chochote bali ni mtume tu. Ili kujua kama Allah anasema ukweli, lazima tulinganishe na maneno ya Biblia ambayo ndio yana mamlaka zaidi ya Quran na yalisemwa miaka 632 kabla ya Quran kuandikwa.

YESU ANAMAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI
Biblia inatuambia katika Injili kutokana na Matayo kuwa:
Mathayo 28:18
Yesu akaja kwao akasema nao akawambia, “nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Yesu kwa mdomo wake anakiri kuwa Mamlaka yote ya Mbinguni na duniani amepewa yeye na haya madai ni kinyume kabisa na madai ya Allah ambayo yanasema kuwa eti Yesu si chochote kile bali ni Nabii tu. Kumbuka Yesu alisema haya maneno takribani ya miaka 632 kabla ya Allah kuja na kudai kuwa Yesu si chochote kile. Sasa, Allah alikuwa wapi miaka yote hii 632 ? Kwanini Allah asinge sema haya madai kwenye Injir na akasubiri miaka 632 baadae? Hakika Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia.

Malaika Gabrieli naye anashuhudia kuwa, Yesu ni Mkuu na Mwana aliye juu.
Luka 1:30-33
Malaika akamwambia, “Usiogope Mariamu kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukuwa mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyu atakuwa mkuu ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

Yesu na yeye anaendelea kusema kuwa, Baba alimpa Mamlaka ya wote wenye Mwili na zaidi ya hapo Yesu anakiri kuwa anao utukufu kama wa Baba yake:
Yohana 17:1-2
Maneno hayo aliyasema Yesu;akainua mikono yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba saa imekwisha kufika Mtukuze mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa Mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

Warumi 14:9
Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii awamiliki waliokufa na walio hai pia.
Ushahdi wa aya hizo hapo juu unatuambia kuwa Yesu ana mamlaka kwa watu wote wenye mwili na pia ni mfalme wa milele. Haya madai ni kinyume kabisa na madai ya Allah katika Quran kuwa eti Yesu Kristo si chochote kile.

Leo tumejifuinza kwa mara nyingine tena kuwa Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia kwa kuwa Isa wa Quran yeye si chochote ila ni mtume tu.

Katika huduma yake,

Max Shimba

Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2015

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW