5Yesu akawaambia: “Jihadharini mtu ye yote asiwadanganye. 6Wengi watakuja kwa Jina Langu wakidai, ‘Mimi ndiye’, nao watawadanganya wengi.
YESU ANATUAMBIA TUWE WAANGALIFU, kwasababu wengi watakuja kwa Jina lake na kudai kuwa ni Yesu amerudi tena. Huu ushahid ndio ule uliopo kwenye Quran ambayo imetungwa na au umba Yesu mwengine na kumpa jina la Isa.
Utumiaji wa Jina la Yesu, Yeshua, Isa, au Esah haiimaanishi moja kwa moja kuwa huyo anaye tajwa ni Yesu wa kwenye Biblia. Ushahid halisi unapatika kwenye Biblia peke yake na sio vitabu vingine vilivyo tungwa na kuja baada yake. Yesu alimjibu Pilato katika Yohana 18:37 Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.’’ na katika Yohana 17: 17 7Uwatakase kwa ile kweli, Neno Lako ndilo
kweli.
Ili kujua kama Isa wa Quran ni yule yule na au ndie Yesu wa Biblia basi hatuna budi Kumlinganisha Isa wa Quran kwa kutumia aya za Biblia na tuone kama anapita. Katika Biblia, tumeambiwa kuwa Yesu alikufa katika Msalaba, huu ushahidi upo kwenye Matayo 27:50, Marko 15:37, Luka 23:46, Yohana 19:30, 33, Matendo 7:52. Lakini katika Quran tunaambiwa kiuwazi kabisa kuwa Isa hakufa Msalabani bali Simoni wa Cyrene ndie alisulubiwa badala ya Isa.
Ushahid huu upo wazi kabisa kuwa Isa wa Quran na Yesu wa Biblia ni wawili tofauti na YESU WA BIBLIA HAWEZI KUITWA NA AU FANANISHWA NA ISA WA QURAN. Wakristo wa Uarabuni ambao tumesha kutana nao mara nyingi, wao wameniambia kuwa Yesu wa Biblia anaitwa Yasu na hilo jina ndilo lipo kwenye Biblia za Kiarabu na sio ISA . Zaidi ya hapo, Wakristo wa Uarabuni hawatumii jina la Isa kwasababu Isa ni Mtume/Nabii wa Allah ambae sio Mwana wa Mungu.
Leo tumejifuinza kwa mara nyingine tena kuwa Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia kwa kuwa Isa wa Quran yeye sio Mwana wa Mungu.
Katika huduma yake,
Max Shimba
Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2015
No comments:
Post a Comment