Friday, August 7, 2015

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA NNE)



Je, Mama wa Isa ndiye wa Yesu Kristo?
Hapo awali tumeona kuwa mama wa Isa anaitwa Maryamu, Surah 3:45 na pia mama wa Yesu anaitwa Mariamu Mathayo 1: 18-21, Marko 6: 3-4 lakini kufanana kwa majina hakuwezi kamwe kumaanisha kuwa ni mtu mmoja, kwani walio na jina hilo ni wengi. Biblia inatufundisha hivi.

Yohana 19:25 – Na penye Msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama, Mamaye, na ubu la mamaye Mariamu wa Klopa na Mariamu Magdalena.

Hapa tunaona Mariamu watatu. Ili kutambua tofauti baina ya Mariamu mama wa Isa na mama wa Yesu, lazima tulinganishe ujumbe wa Qurani na Biblia. Qurani inasimulia kuhusu baba na kaka wa Mariamu mama wa Isa hivi.

Suratul 66:12 – Na Maryamu mtoto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampuliza humo roho yetu, (inayotokana na sisi) na akayasadikisha maneno ya mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa).
Surah 19:28 – Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati.

Hapa tunaona kuwa Maryamu mama wa Isa, baba yake ni Imrani na kaka yake aliitwa Haruni. Tusomapo Biblia inatueleza kuwa Amrani aliwazaa hawa:-
Hesabu 26:59 – Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao.
Pia soma 1 Nyakati 6: 1-3 na Kutoka 6:20.

Huyo Amrani aliishi miaka mingi kabla ya Yesu na tena ametokana na kizazi cha Lawi mtoto wa watu wa mzee Yakobo. Mwanzo 29:34; Kutoka2:1-10
Ikiwa Mariamu wa Qurani baba yake ni Imrani basi atakuwa ameishi miaka 1500 kabla mama yake Yesu wa Biblia hajazaliwa!

Je, Mariamu mama wa Yesu ametokana na kizazi gani?Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Yesu anaitwa mwana wa Daudi Mathayo 1:1; Marko 10:47 na Luka 1:27, 32, ndiyo maana pia Yesu anaitwa Simba wa Yuda Ufunuo 5:5. Hivyo basi ukoo aliyetoka Yusufu na Mariamu wa Yesu ni mmoja.

Hivyo basi Maryam wa Quran ambaye aliishi miaka 1500 kabla ya Mariam wa Biblia hakuwa mama yake Yesu. Zaidi ya hapo, Maryam wa Quran ni daya ya Musa na Haruni ambao waliishi Misri.
Leo tumeendelea kujifunza kuwa Maryam wa Quran sio na ni tofauti na Mariam wa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana na tuendelee kujifunza tofauti katika ya Isa wa Quran na Yesu wa Biblia.

Max Shimba

Max Shimba Ministries

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW