Sunday, August 2, 2015

ALLAH SIO MUNGU (SEHEMU YA TATU)

ALLAH NA WOTE WANAOMWABUDU WATAISHIA JEHANAM
Mwisho wa wanaomwabudu Allah ni wapi? Tunajua kuwa Wakristo tutaishi na Mungu wetu Yehova milele (tazama 1Thesalonike 4:13-17 na Ufunuo 21:3-7) Hivyo Mungu wetu hana mwisho ni wa milele. Lakini tunaposoma Qurani na Hadithi za Muhammad, mtume wa Waislamu tunaona mafundisho haya…
Qr. 51 au Surat Adh-Dhaariyat 56 (sur aya upepo) yasema, Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu

Qr. 6 Surat Al An-Am 128 (Sura ya wanyama)
Na (wakumbushe) siku atakapowakusanya wote (awaambie) "Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu" na marafiki wao katika wanadamu (watawagombania) waseme "mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao, na tumefikia muda wetu uliotuwekea" Basi (Mungu) atasema:"moto ndio makazi yenu, mtakaa humo milele.. katika aya hizi tunaona kuwa majini pamoja na watu wote watatupwa motoni. Je Allah naye ni vipi? Tunaposoma kitabu cha hadith za mtume (s.a.w) cha Sahih al-Bukhari Vol: VI Hadithi No: 371.ukurasa wa 353 Kuna maneno haya:

Qr. 50 au Surat Qaf 30 (kuapa)
Siku tutakayoiambia Jahanamu, ‘Je! Umejaa?’ Nayo itasema ‘Je kuna ziada (zaidi? Naije tu!
Imesimuliwa na Anas kuwa: mtume alisema watu watatupwa jahanamu, Naye Allah ataiuliza jahanamu akisema je umejaa nayo jahanamu itasema kwani kuna nyingine zaidi na ije tu? Mpaka Allah atakapo ingiza mguu wake nayo jahanamu itasema inatosha! Inatosha

Hadithi hii ya Anas inasomeka hivi:
Na Allah atasema Je, kuna wa ziada (kuja)? Nayo Jehanam itamuuliza Mwenyezi mola, wakisema je, kuna waziada (kuja)? hadi Mwenyezi Mungu atakapouweka mguu wake ndani ya moto wa jehanam na kisha moto utasema, YATOSHA!

Katika aya hii tunaona Allah mungu wa Waislamu anaiuliza Jehanamu kama imejaa, nayo Jehanamu itamuuliza Allah je, kuna zaidi. Yaani swali hili linaonyesha kuwa Jahanamu ilikuwa bado haijajaa, Maelezo ya Hadithi hii inadhibitisha kuwa Allah ataingiza mguu katika Jahanamu na ndipo Jahanamu itakaposema kuwa inatosha! Inatosha!, yaani imejaa kwa tendo la Allah kuingiza mguu wake humo. Jambo hili ni tofauti kabisa na ilivyo kwa Mungu wetu Yehova., Mungu wetu ameiweka jahanamu maalum kwa ajili ya watu wabaya, na ibilisi, pamoja na malaika zake. Tafadhali soma aya hizi; Mathayo 25:41,46, Ufunuo 20:10, 21:8.

Aya hizi zote zinaonyesha kuwa mwisho wa wabaya, Ibilisi na malaika zake ni katika ziwa la moto. Swali kwako Ndugu mpendwa,

Je, Allah ni nani?Ni matumaini yangu kuwa umeweza kujua kwa undani kupitia Qurani na Biblia na vitabu vya Hadith za mtume wa Waislamu aitwae Muhammad kuwa Allah Sub-Haana Wataala Mungu anayeabudiwa na Waislamu. Siyo Yehova Mungu tunaye muabudu Wakristo.
Unapoijuwa hii kweli ukiwa Muislamu nakuomba kwa neema yake Kristo Bwana wetu umpokee KRISTO YESU maishani mwako ili uweze kuitoroka ibada ya shetani na kujiokoa nafsi yako na mauti ya milele………
Karibu kwa Yesu Kristo wetu.
Ufunuo 3:30 Yeye anasimama mlangoni kwako anabisha!!! Usichelewe kumfungulia.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW