Wednesday, July 1, 2015

Uislam na Sayansi: Mitazamo Iliyosahauliwa Imekumbukwa

Uislam na Sayansi:
Mitazamo Iliyosahauliwa Imekumbukwa 

Toleo la Juni 2006
Je, maneno kama aljebra, alkali, pombe, astrolabe, naphtha, na zircon kitu gani kinachoyapatanisha hasa? Maneno haya yote ni ya Kiingereza yaliyotoholewa kutoka katika Kiarabu na maneno ya Kiajemi yanayoturudisha nyuma kwenye miaka ya 700-1150 BK, wakati kituo cha kujifunza Sayansi bila shaka kilikuwa Mashariki ya Kati.

Watu wengi yawezekana wasijue mchango muhimu uliotolewa kwa sayansi na hesabu kutoka Mashariki ya Kati. Ifuatayo ni orodha fupi ya mafanikio ya mambo haya, na kisha hutafiti kauli za kisayansi zilizomo katika Korani. Lakini kuna maendeleo mengi makubwa ya kitabibu ambayo hayajatajwa hapa; huleta sifa kwa mjadala wake wenyewe.
 
Sayansi ya Mashariki ya Kati ya Zamani
Hata Wasumeria wa kwanza (3500-2000 KK) walikuwa na mchanganuo wa wanyama wote waliowajua. (Wadudu wakubwa kama vile nzige walijumuishwa pamoja na ndege, kama viumbe warukao.) Wamisri wa zamani na Wababeli walitumia nyota ili kuwasaidia kujua ni wakati gani wangeanza kupanda. Watu hao wa zamani walikuwa na maendeleo kadhaa katika kutengeneza meli, ufugaji wa wanyama, na upasuaji, hata upasuaji wa kichwa. Wamisri walitumia dawa ya meno tangu mwaka 2500 KK. Mitatu kati ya michango muhimu sana ya kisayansi ni kuandika, kulima pamoja na sayansi na teknolojia ya vitu yabisi kama vyuma.
 
Pengine mafanikio ya juu zaidi kielimu ya ulimwengu wa zamani yalikuwa maktaba ya mji wa Alexandria. Hapa kulitunzwa mamia ya maelfu ya juzuu za nakala asilia au nakala za fasihi nyingi za ulimwengu wa watu wa wakati ule.
Uhandisi na Uhandisi Majengo wa Zama za Kale
Wamisri walikuwa na gubeti tangu 2500 KK. Katika uhandisi majengo, kila mtu anajua mapiramidi ya kuvutia nchini Misri na mahekalu (Ziggurats) ya Sumeria na Babeli.
 
Kitu kisichojulikana sana ni kuwa Kaskazini-mashariki mwa Iran kulikuwa na bwawa kubwa, lililoibuka hasa katika mwaka 1800 KK, kushinikiza wahamiaji wengi katika nchi za India na Iran. Bwawa nchini Yemen liliufanya ufalme wa Sheba kuwa kituo maalum cha kilimo na biashara hadi hapo lilipovunjwa pia zaidi ya karne moja kabla ya Muhammad. Ujenzi wa mifereji, bustani zinazoning’inia, na miji yenye kuta nene ni mambo ya kuvutia hata leo. Na kwa hakika, kama ungeliweka Mji wa Ashuru, Ninawi kati ya Ufaransa na Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, pasingekuwa na upande wowote ambao ungeweza kuuteka. Hatimaye ulitekwa, lakini ni kwa sababu tu mto wa Khosr ulipofurika na mafuriko yake yalivunja sehemu ya ukuta wa mji huo..
Mashariki ya Kati ya Kale na Hesabu
Haya majengo ya kiuhandisi yasingeweza kujengwa kama pasingekuwa na msaada wa hesabu. Wababeli wa zamani walikuwa na mfumo wa kuhesabu hadi 60. Walipendelea namba zinazoshabihiana; kwa mfano, wangegawa a/b kama *l/b. Wababeli wa zamani walikuwa wa kwanza kutumia aljebra kwa hesabu za mistari na hesabu za mchanganyiko wa namba na herufi (quadradic problems). Chati iitwayo Plimpton 322 ni chati ya namba za Pythagorean (a^2 + b^ + c^2). Wababeli walibuni vipimo vya namba za mraba kama uchoravyo mstatili na kisha kuhesabu ukubwa wa eneo. Kimahesabu, watu hawa hawakutumia kitu chochote zaidi ya vipimo vya mraba (squares). Wakati huo huo Wababeli walikuwa na thamani tofauti ya pai (pi), na iliyokuwa sahihi zaidi ilikuwa 3.125. Mwanamahesabu wa Kiarabu wa karne ya 10 Abu’l-Wafa’ alisema watu waliotoa elimu ya kimahesabu walikuwa mafundi sanaa (wanasanaa) na wasanii.
 
Hesabu za maumbo ya pembetatu za Wamisri zilikuwa bora kuliko za Wababeli, kwa sababu Wamisri walikuwa na ufahamu juu ya kona, na walikuwa na ile thamani ya pai ya 31/7 au 3.16. Hii si mbali na 3.14159. Na hii imo katika nyaraka za Rhind Paparas—paparas (mwaka wa 1650 KK) na Paparas ya Moscow iliyokuwapo wakati ule ule. Majengo mengi ya Kimisri yalikuwa na pande za 3 kwa 4, lakini hawakujua juu ya nadharia ya Pythagoras (Pythagorean theorem). Sayansi na hesabu nyakati za zamani zilikuwa za "kivitendo". Pengine hii ndiyo sababu, kwa shauku tu, hapakuwa na yeyote aliyekuwa na wazo la "sifuri" hadi ilipogunduliwa nchini India.
Aljebra Zilitoka Wapi?
Hesabu ya aljebra ya kwanza tunayoifahamu ilikuwa imehifadhiwa katika Paparas ya Rhind iliyotolewa nakala na mwandishi wa Kimisri aliyeitwa Ahmes (mwaka wa 1650 KK.). Huu ni muda mrefu sana kabla Musa hajazaliwa. Wakati huo huo Wayunani walikuwa wakipendelea zaidi hesabu za maumbo, Wachina walikuwa wakikokotoa hesabu za mchanganyiko wa namba na herufi kabla Kristo hajazaliwa, na Wahindu (kwenye miaka ya 628-1150 BK) walikokotoa na kupata majibu ya maswali tata zaidi ya hesabu. Huko Baghdadi Muhammad ibn Musa al-Khowarizmi/Khawarizmi (mwaka wa 825 BK), Abu Kamil (mwaka wa 900 BK) na al-Karkhi (mwaka wa1100 BK) waliziendeleza hesabu za aljebra zaidi. Kwa kiasi kikubwa sana ziliziambukiza hesabu za Ulaya wakati Robert wa Chester alipotafsiri kitabu cha al-Khowarizmi kwenye mwaka wa 1140 BK kiliitwa kwa Kilatini Liber Algorism, maana yake kwa ujumla ni "Kitabu cha al-Kowarizmi." Na neno algorism baadaye lilikuwa algorithm and aljebra [kwa lugha ya kimahesabu].
 
Hapa chini jedwali laorodhesha baadhi ya wanasayansi wa Mashariki ya kati na wale wa Kiarabu pamoja na wanamahesabu.
 
Avicenna (Ibn-Sina) 979/980-1037 BKLicha ya kuwa tabibu muhimu sana kati ya enzi za Warumi na enzi ya leo, alikuwa mwanasayansi pia, mwanafalsafa, na mjenga hoja aliyeandika takriban kazi sanifu zipatazo 200. Albert Magnus wa England alijifunza mengi kutoka kwake
Averroes (Abu al-Walid Muhammad bin Ahmad ibn Muhammad ibn Roshd) 1126-1198 BKAlimsujudu [mwanafalsafa] Aristotle. Alisema mengi juu ya umaskini na masumbuko kutokana na jinsi Waislam walivyowachukulia
Avempace (Ibn Gabirol) 1021-1058 BKMwanafalsafa wa Kiyahudi na Kihispania aliyemwuunga mkono Aristotle
al-Karkhi miaka ya 1100 BKMichango mbalimbali katika kwa hesabu za Aljebra
Kemia/Alkemia na Fizikia
Makhalia wa Abbasid wa Baghdadi walikuwa na shulu ya Alkemia kwenye ya karne ya 9 au ya 10. Kazi za kwanza kabisa za Alkemia ya Kiarabu nusu ni za Kiarabu na nusu ni Kisiria. Khalid mwana wa Yezid (alikufa mwaka 708 BK) mwanafunzi wa mtawa wa Kisiria Marianus, alikuwa mwandishi wa kwanza wa Kiislam juu ya Alkemia, kufuatana na kitabu Kitab-al-Fihrist. Vipaji vya Wanaalkemia viliharibiwa kwa kujaribu kubadili madini ya "risasi" na vitu vingine kuwa dhahabu, lakini katika mchakato huo waligundua mambo mengi hii ni pamoja na Kemia pia. Wafuatao ni baadhi ya wanakemia maarufu wa Kiajemi na Kiarabu.
 
Geber (Jabir ibn-Hayyan) Kwenye miaka ya 760-815Mwanaalkemia wa Kiarabu aliyechuja chachu kitaalam na kutengeneza tindikali itokanayo na maji na naitrojeni. Alianza utafiti juu ya kubadili maumbo ya vitu yabisi (metals) na alivutiwa sana na kimiminika kiitwacho Zebadi (Mercury). Alikuwa mwenye sifa na maarufu kiasi kwamba kemia ikapewa jina la utani "Usanifu wa Jabir"
Ibn al Haytham Alikufa mwaka 1039 BH [Baada ya Hija]Alisomea mambo ya shinikizo, sumaku na sayansi ya mambo ya mwanga. Alisema kuwa huwa tunaona kwa kutumia mwanga unapoyaingia macho yetu, si miale ambayo jicho hutupa nje.
Quth al-Din 1236 BKAlielezea umbo la upinde wa mvua
Rhazes (Al-Razi) kwenye miaka ya 850-925Mkemia wa kiajemi (na mwana anga) aliyetengeneza chokaa ya kuta za nyumba ya Paris na alijifunza madini ya shaba na kristole (crystalline) yaani antimony
Abdul Salam of Pakistan. 1926-1996 BKAlishiriki tuzo ya Nobel ya mwaka 1979 katika Fizikia. Alikuwa Qadiani ambaye Waislamu wengi humchukulia kama wenye mafundisho potofu wasio waislamu
Geber (Jabir ibn-Hayyan) (alikufa mwaka 808 BK 193 BH [Baada ya Hija]) alikuwa Msufi mwenye imani ya kujikana mwenyewe kwa ajili ya mambo ya kiroho. Alikuwa na maabara huko Dameski. Vitabu vyake 200, vinane kati ya hivyo vilikuwa vya kemia, kujumlisha vitabu juu ya usindikaji, kutengeneza rangi, na uzito pamoja vipimo mbalimbali. Ama kwa hakika, wengine waiita kemia jina la utani "usanifu wa Jabir." Alitengeneza mezani iliyoweza kupima hadi uzito wa 1/6 ya gramu. Wakati watu wa Ulaya wa baadaye walidhani kuwa Phlogiston iliongezwa kwenye vitu vilipounguzwa, lakini Jabir alielewa kwa usahihi kwamba nguvu ya vitu vilivyoungua ilikuwa ikitoka, na kuacha mabaki ya majivu yasiyounguzika. Aligundua karatasi isiyounguzwa na moto, kizuia kutu, na kilichozuia maji kwenye nguo. Kwa uhalisia, alikuwa na wito wa karibu toka kwa watu japo alishauri kuwa maabara ya kikemia yalipaswa kuwa mbali na miji. 

‘Izz al Din al Jaldaki (alikufa mwaka 1360 BK 762 BH) yeye alipendekeza utumiaji wa vifuniko vya mdogo na pua (masks) ili kujilinda dhidi ya hewa hatari zinazotokana na utendaji kazi wa kikemikali, na kwamba maji yaweza kufanywa salama kwa kuyafanya mvuke kisha kuupoza kuwa maji tena. Kemikali zingeweza kuongezwa kwenye sabuni ili kuzuia nguvu za kikemikali zinazoharibu nguo. Yeye aliweza kutenga dhahabu na shaba kwa kujua kuwa dhahabu ni madini pekee ambayo hayawezi kuyeyuka ndani ya tindikali ya kinaitrojeni. Aliandika vitabu vingi, na viwili kati ya hivyo vilikuwa zaidi ya kurasa 1,000 kila kimoja.
Ibn al Haytham (alikufa mwaka 1039 BK / 431 BH) alikaribishwa na mtu katili na maarufu Khalifa al-Hakim kwenda Misri baada ya kuongelea juu ya faida za mto Nile. Alipendekeza kujengwa kwa Bwawa la Aswan ili kuboresha umwagiliaji. Hata hivyo Al-Hakim alilikataa pendekezo hilo. Al-Haytham alichunguza msukumo wa hali ya hewa na uzito wa sumaku ya dunia. Alisoma juu ya mwanga na kuakisiwa kwake pamoja na mambo ya mwanga kwa ujumla. Al-Haytham aliandika takriban vitabu 200, 47 vya hesabu na 58 vya uhandisi.
Elimu ya Ibn al-Haytham ya fizikia ni ya kukumbukwa ukizingatia kuwa Muhammad aliyosema katika hadithi zake juu ya moto na majira mbalimbali. Na hivi ndivyo isemavyo Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na. 1290 uk. 309. "Abu Huraira alitaarifu kuwa: Mtume wa Allah (na amani iwe juu yake) alisema: Moto ulilalamika mbele za Bwana ukisema: ‘O Bwana, baadhi ya sehemu zake zimeteketeza watu wengine.’ Kwa hiyo uliruhusiwa kupumua kwa namna mbili, namna mojawapo ya kupumua ni wakati wa hari na nyingine ni wakati wa majira ya joto (summer). Hii ndiyo sababu utakuta kuna joto jingi sana (wakati wa joto-summer) na baridi nyingi sana (wakati wa hari-winter)."

Unajimu
Kama majina ya kiingereza ya Aldebaron, Rigel, Atik, Algerib, Caph, Deneb, Sadr, na nyota zingine zaidi ya 40 yanaonekan kuwa ni ya kiarabu, ni kwa sababu ndiyo zilivyo. Kwa kuangalia katika jangwa wakati wa giza la usiku, wanajimu wa Kiarabu waligundua nyota nyingi ambazo hazikujulikana hapo awali. Waarabu na Waajemi walisoma sayansi mbalimbali, lakini walionekana kuwa na upendeleo maalum katika unajimu. Wafuatao ni baadhi ya wanajimu waliokuwa maafuru zaidi. 

Abu-Maaschor (Albumazar)
805-885 BK

Kazi zilizotafsiriwa katika Kilatini, ikiwemo Flores Astrologici, na kutokana kazi hiyo tunapata neno astrolojia (astrology). Alifikiri kuwa ulimwengu uliumbwa wakati sayari 7 zilipoumbwa zikiambatana na nyota.

Al-Khowarazmi (kwenye mwaka 825 BK

Alikuwa msomi katika nyanja za masomo mengi, alichapisha kitabu cha kwanza cha Kiarabu chenye maelezo juu ya unajimu.

Muhammad ben Begir al-Batani (Albategnius)
Kwenye miaka ya 850-929 BK

Alisahihisha baadhi ya orodha za hesabu za Watolemi. Ndiye aliyeleta hesabu za maumbo ya pembetatu katika Mashariki ya Mbali. Kazi zake zilichapishwa katika Kilatini na Melanchthon.

Avempace (Ibn Gabirol)
1021-1058 BK

Mwanafalsafa wa Kiyahudi na Kihispania aliyempenda Aristotle
Hatua ya kwanza ya unajimu wa Kiislamu ulianza kuvuka vizuizi vilivyokuwa katika Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na. 3726 uk. 149: kujifunza juu ya unajimu ni kujifunza juu ya nguvu za kimiujiza (mazingaombwe). Sunan Abu Dawud juzuu ya 5 sehemu ya 1480 na. 3896 uk. 1095 katika Kiingereza yasema kitu kile kile, isipokuwa inatumia neno "astolojia."

Baada ya hayo, Waislamu walikusanya kazi mbalimbali za Kiyunani, Kiajemi na hata wanajimu wa Kihindi. Kitabu cha kwanza cha Kiyunani juu ya unajimu (yasemekana kiliandikwa na Hermes Trismegistus) na kutafsiriwa katika Kiarabu mwaka 742 BK (125 BH) Khalifa wa Kiabbasid al Mansur alikuwa mnajimu wa Kiajemi Nawbakht, na baadaye mwanawe wa kiume, aliambatana naye.
 
Wanajimu wengine ni pamoja na ‘Ali Ibn ‘Isa al Astrolabi, kutokana na huyu tunapata neno astrolabe, japokuwa chombo hiki kwa ajili ya kupima latido na miinuko yenye vipimo sawa kiligunduliwa kwa mara ya kwanza 300-100 KK.
 
Mnamo mwaka 772 BK, al Mansur alimtumia Abu Yahya al Batriq kutafsiri kazi za Ptolemi Claudi na vitabu vingine vya Kiyunani al Mansur alikuwa ameviomba kutoka kwa Mfalme wa Benzatini. Mohammad al-Farazi alitafsiri hata kitabu cha Kihindi juu ya unajimu. Kwa kujenga juu ya yote haya, Khowarizmi (kwenye mwaka wa 825 BK) aliandika kazi yake Orodha ya Ukokotoaji na Kupanga Mpangilio wa Nafasi za Viumbe wa Mbinguni.
 
Hata hivyo baadaye Waarabu na Waajemi walifanya mambo mengi zaidi ya kurudia tu elimu ya mambo yaliyopita. Fakhr al Din al Razi (aliyekufa 1209 BK 606 BH) alihoji tamko la Aristotle kwamba nyota hazibadili nafasi zake na ziko mbali na dunia, pia tamko lisemalo kuwa miondoko ya viumbe vingine vya mbinguni yote hufanana na ni sawa sawa. Hii ilikuwa miaka 300 kabla ya Kopernika, aliyekufa mwaka 1543 BK Sayari uk. 12 inasema kuwa huko nyuma katika mwaka 275 KK. Aristarko wa Samos alisema mbingu hulizunguka jua, na si dunia, lakini kila mmoja enzi zile "alijua" kuwa jambo hilo lilikuwa uchizi. Baadhi ya Wayunani na Warumi walifundisha kwamba dunia ilikuwa mviringo, na kuwa watu waliishi katika mkabala wa pande za mzunguko wa dunia pia.
 
Wayunani na Warumi wengine walifundisha kuwa dunia ilikuwa mviringo, na kwamba watu waliishi katika mkabala wa pande za mzunguko wa dunia pia, kufuatana na Lactantius (260-325 BK) Kitabu cha Kanuni za Kimungu Sehemu ya 24 uk. 94.
 
Sura 2:258 inasema Ibrahimu alisema Allah ndiye husababisha jua litokeze kutoka Magharibi. Mchango wa maoni ya al-Razi sura 2:258, yasema kuwa hakuna uthibitisho kuwa jua hutokeza Mashariki wala Magharibi, kwa sababu mwendo wake halisi yawezekana ukawa tofauti kabisa na tunachokiona. 
Al-Battani/Batani
 kutoka Dameski aligundua ni jinsi mwaka, uliohesabiwa kutegemea jua, ulivyokuwa mrefu, lakini alikosea thamani ya urefu wake halisi kwa dakika 2 na sekunde 22. Waislamu walijenga sehemu nyingi kubwa za tathimini na matazamio, lakini kubwa kuliko zote duniani kwa wakati ule ilijengwa Maraghah mnamo mwaka 1258 BK (657 BH).

Kwa upande mwingine, mwanzo wa kushikwa kwa jua au mwezi ulitolewa [si sahihi kabisa] katika al-Tabari juzuu ya 1 uk. 236.
Maandiko Mbalimbali na Unajimu
Ukristo, Uyahudi na Uislamu vyote hufundisha kuwa kuna Mungu aliuumba ulimwengu katika mpangilio sanifu, Zaburi 91:1-2 yasema, "Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga zahubiri kazi ya mikono yake."
 
Korani 41:53 katika tafsiri ya Yusuf ‘Ali’ yasema, "Muda si mrefu Tutawaonesha ishara Zetu katika Mikoa (ya mbali zaidi) ya dunia, na katika nafsi zao wenyewe, hadi itakapodhihirika kwao..." Hata hivyo, katika tafsiri nyingine yasema, "Tutawaonesha wanadamu ishara/mipangilio Yetu katika upeo wa mitizamo/ulimwengu vile vile ndani yao wenyewe hadi watakaposhawishika kuwa huu ufunuo ni kweli" Tafsiri ya N.J. Dawood inafanana katika kuiongelea dunia, kama ilivyo tafsiri ya Ahmadiyya wa Maulawi Sher Ali inayosema, ". . . Ishara katika sehemu zote za dunia,..." (herufi ulalo zatokana na nakala asilia.)
 
Badala ya "Pande za (mbali zaidi) (za dunia), inasema ""ulimwengu" katika tafsiri ya Mohamad Farooq-i-Azam Malik. Tafsiri ya Arberry ilichukua mtizamo wa papo hapo, ikisema "Ishara Zetu katika peo za macho…" Licha ya hayo hata hivyo, Korani yasema kuwa Allah huonesha ishara katika mambo ya asili mahali fulani mbali sana nasi.
Vimondo
"Mbingu ya chini sana ina taa [nyota], na ‘Tumetengeneza [Taa] hizo (kama) makombora ya kutokomeza mbali Waovu, na kuandaa kwa ajili yao Adhabu ya Moto Uwakao.’" Sura ya 67:5
 
"Uumbaji wa nyota hizi ni kwa makusudi matatu, nayo ni upambaji wa anga, kama makombora kuwapiga mashetani, na kama ishara za kuwaongoza wasafiri. Hivyo, kama mtu yeyote atajaribu kutafuta tafsiri tofauti, atakuwa amekosea na huko itakuwa akipoteza juhudi zake…" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sehemu ya 3 kabla ya na. 421 uk. 282.
 
Vimondo (nyota zilipukazo na cheche angani) wakati mwingine hurushiwa mashetani wanaojaribu kusikiliza siri za mbinguni. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na. 902 na rejea ya 674 uk. 243.
 
Vimondo ni kwa ajili ya kuwapiga malaika [wabaya] kabla hawajasambaza walichokisikia. Wakati mwingine malaika wabaya huwaambia siri manabii wa uongo [wachawi], isipokuwa, kabla hawajapigwa. Ibn-i-Majah juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.194 uk.110.
 
Radi hushambulia jinni (majinni) Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 24 na.5538 uk.1210.
 
Nyota hulinda dhidi ya Shetani al-Tabari juzuu ya1 uk. 223.
Jiografia
Baadhi ya wachora ramani maarufu wa Kiarabu walikuwa Ya’quibi, Ibn Haukal, Mas’udi, Makdisi / Mokaddasi, Ibm Khurdadhbih wa Samarra, Abakri, Yakut, na Abulfeda. al-Idrisi alikuwa mwanajiografia mwenye uelewa mpana sana, aliyemwonesha Hastings Uingereza na Paris, Ufaransa [barani] Ulaya, na Cantona [nchini] China. Katika karne ya kumi mwanabaharia wa Kihispania na Kiarabu alijaribu kukatisha bahari ya Atlantic kutoka Lisbon.
Kwa upande mwingine, dunia hukaa juu ya samaki mkubwa kufuatana na historia ya Kiislamu al-Tabari juzuu ya 1 uk.220 (839-923 BK). Hivyo, kama walivyo Watu wa Ulaya, Waajemi na Waarabu walikuwa na hadithi za kitamaduni nyingi za kupambana nazo.
Sura ya 18:85-86 inasema kuwa mtawala Zul-Qarnain, alifuata kuchwa kwa jua na kugundua kuwa lilizama chini ndani ya chemichemi za tope. Sasa hivi tunajua kuwa jua halizami katika chemichemi za tope, lakini Waislamu wa enzi za kale waliamini hili kama lilivyo, kama inavyosema al-Tabari juzuu ya 1 uk.234. Na kama mfano wa pili, "[Dhu al-Qarnaiyn] alivyoshuhudia kuchwa kwa jua katika sehemu ya kupumzika kwake ndani ya dimbwi la jeusi na ukungu wa kunata kama tope." Kufuatana na al-Tabari juzuu ya 5 uk.173-174.
Chakula cha Kisayansi
Wakati baadhi ya viungo hulimwa Mashariki ya kati, Mashariki ya Kati ilikuwa na mlango wazi kwa namba kubwa ya viungo vya Asia. Hata leo chakula cha Mashariki ya kati huwa ni aina nyingi na vya ladha tofauti tofauti za kuvutia kwa sababu ya uzoefu wa viungo mbalimbali kwa karne nyingi zilizopita. Kahawa ilitumika kwa mara ya kwanza Mashariki ya kati. Kwa kuwa kahawa kinywaji kinachosisimua, viongozi wa dini ya Kiislamu walijaribu kupiga marufuku matumizi yake hapo mwanzoni. Waislamu wa kawaida walidai kuwa kahawa ilikuwa nzuri, kwa sababu iliwasaidia kuwa macho kwa ajili ya maombi usiku, na kisha pole pole viongozi wa dini ya Kiislamu walibadilisha nia zao.
Kutengeneza Jambia
Nje ya Japan, majambia au panga nzuri zaidi ulimwenguni ziliitwa majambia ya Kidameski kutoka Siria. Majambia hayo yalikuwa yametokana na siri ya "kufua vyuma", kwamba chuma kilichopozwa pole pole chaweza kuwa kigumu na kikali zaidi kuliko chuma kilichopozwa haraka sana. Kwa bahati mbaya, njia waliyoitumia kukamilisha jambo hilo ilikuwa kuchoma jambia lililokuwa moto na jekundu "ndani ya mwili wa mtumwa mwenye misuli na afya".
Mizinga ya Kijeshi
Waislamu waliivamia Constantinople angalau mara kumi kuanzia mwaka 670 BK, lakini hawakuweza kuiteka kamwe, -hadi waipokutana na mfanyabiashara wa Kichina. Mfanyabiashara huyo alikubali kuwauza Wabenzantini 10,000 waliokuwa wametekwa ndani ya mji wenye baruti; [Waislamu] hawakukubali kwani walisema walikuwa wameshapata moto kutoka kwa Wayunani, hii ilikuwa mafuta ya petroli iliyochujwa na iliweza kuelea juu ya maji na ingeweza kuwashwa. Kwa hiyo yule mfanyabiashara aligeuka na kuwauzia baruti hiyo Waturuki wapatao 80,000 hadi 100,000, waliotengeneza mabomu/mizinga ya kienyeji na hivyo kuangushwa kuta mwezi Mei 29-30 1453 BK. Waturuki waliwashinda Wayunani katika miaka saba iliyofuata, na walipigana hata kuelekea Kaskazini kama vile Austria tangu 1526-1528.
Falsafa na Hoja za Kweli
Wakati Wakristo wa Kinestoria walipofukuzwa toka Siria na Mtawala Zeno, wengi wao walikwenda kutulia Uajemi na kisha Baghdadi. Wengi wao walitunza elimu ya dawa na falsafa ya Kiaristotle.
Avempace, aliyejulikana pia kama Ibn Gabirol (1021-1058 BK) alikuwa mwanafalsafa wa Kiyahudi aliyeishi katika eneo la Kiislamu nchini Hispania. Alikuwa mtetezi wa falsafa ya Aristotle pia. Mwislamu Averroes (1126-1198 BK) alikuwa mtu aliyemsujudu Aristotle kwa hali ya juu sana.
Thomas Aquinas (kwenye miaka ya 1125-1274), ambaye alikuwa kipenzi wa Aristotle pia, aliandika kazi iitwayo Juu ya Upekee wa Ufahamu Kielimu dhidi ya Waverrosti. Mulla Sadra alibadilisha wazo la kifalsafa la Irani kutoka kuwa Mplatoniki na kuwa Muaristotle kama alivyofanya Thomas Aquinas barani Ulaya.
Kosmolojia-Hoja ya Kalem kuhusu Uwepo wa Mungu
Kalem maana yake ni "a milele" katika Kiarabu na hoja ya Kalem kikosmolojia ni hoja ambayo Wakristo na Waislamu pia wanaweza kuitumia kuonesha kuwa kuna Mungu. Norm Geisler katika Baker Encyclopedia of Christian Apologeticsuk.399 yaiita hoja hii kuwa ni "hoja ya kikosmolojia yenye muundo tambarare."
  1. Kila kilichoumbwa kilikuwa na chanzo cha uumbwaji wake.
  2. Ulimwengu kulikuwa na muda ambapo ulipoumbwa.
  3. Kwa hiyo ulimwengu ulikuwa na chanzo cha uumbwaji wake.

Wazo hili lapingana na wale wote wasioamini katika uwepo wa Mungu, wanaojaribu kusema kuwa kitu fulani chaweza kuwepo bila kusababishwa na chochote kabisa.
Watu waliounga mkono hoja ya Kalem ni pamoja na Waislamu Alfarabi, Al-Ghazali, Avicenna, na mwanatheolojia Mkristo Bonaventura. Mwanafalsafa Mkristo aliyeona udhaifu katika hoja hii alikuwa Thomas Aquinas. Yeye alitambua kuwa iliwezekana kuwa Mungu angaliweza kuifanya dunia katika kipindi cha milele iliyopita, na hapakuwa na uthibitisho kutokana na uumbaji wa asili kuwa Mungu aliumba ulimwengu katika muda fulani maalum au katika kipindi cha milele. Aquinas alitetea zaidi toleo la juu la hoja ya kikosmolojia. Kila kitu kilicho na chanzo (ikiwa kiliumbwa katika muda fulani maalum au katika kipindi cha milele iliyopita) kilikuwa kimeumbwa na kitu fulani.

Zoolojia: Sayansi ya Wanyama
Watu wa mabara yote dunia waliishi kwa kuamini bila uthibitisho kamili juu ya mambo mbalimbali. Wachina walikuwa na madragoni wao (wazuri) yaani miungu. Watu wa Ulaya nao walikuwa na madragoni wao wabaya, majitu ya kufikirika baharini (sea monisters), na vinginevyo vilivyoitwa cockatrix. Waarabu waliamini katika muungu mithili ya mnyama mwenye pembe moja usoni na mkia wa simba na katika ndege wazuri ajabu wakubwa kama tembo wenye mayai ambayo hata majini walikataa kuyabeba. Majini yalitengenezwa kutokana na moto wakati wanadamu walitengenezwa kutokana na uchafu (udongo). Hata hivyo Mugharrihum walikuwa na majini ndani yao. Abu Dawud juzuu ya 3 na.5088 rejea ya 4436 uk.1415-1416.
Nzige ni matokeo ya chafya za samaki kufuatana na hadithi Ibn-i-Majah juzuu ya 4 na.3227 uk.409
Sura ya 16:69 yasema kuwa katika matumbo/miili ya nyuki kuna kinywaji kitamu (asali) ambacho ni kizuri kwa uponyaji wa wanadamu. Hiyo ni ishara kutoka kwa Allah. Kwa hakika asali ilitengenezwa hasa nje ya mwili wa nyuki; na hii ndiyo sababu wana masega ya asali.
Ng’ombe, hutoa maziwa kati ya mfumo wa uchafu na maziwa. Sura 16:66.
Hakuna wanyama waishio juu ya uso wa dunia wala viumbe wote warukao angani, walio na makazi maalum kama wanadamu wafanyavyo, kufuatana na sura ya 6:38.
Punda wa jike, aliuawa kwa kupondwa mawe na nyani wengine kwa kujamiana kusiko halali. Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sehemu ya 26 na. 188 uk. 199. Haijulikani kuwa jambo hili halikuwa halali kufuatana na sheria ya nani.
Ikiwa mtoto kafanana zaidi na baba au mama kwa upande mwingine kulitegemea "mihebuko" yao wakati wa kujamiiana. Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sehemu ya 49 na.275 uk.190; Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sehemu ya 8 na.7 uk.9.
Pua
"Alisimulia Abu Huraira: Mtume alisema, ‘Ikiwa mtu yeyote kati yenu ataamka toka usingizini na kujitawadha, anapaswa kuosha pua yake kwa kuweka maji ndani yake na kuyapenga nje mara tatu, kwa sababu Shetani amekaa kwenye sehemu ya juu ya pua usiku mzima." (1)
 
Imani hii ya zamani inaendelea hadi leo, kama rejea (1) ioneshavyo. Inasema, "Tunapaswa kuamini kuwa Shetani hukaa juu ya sehemu ya pua ya mtu, japo hatuwezi kuelewa ni kwa vipi, kwa kuwa hii ni sawa na ulimwengu usioonekana ambao hatujui chochote juu yake isipokuwa kile Allah anachotuambia kupitia Mtume wake." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sehemu ya 10 na.516 uk.328.
Shetani hukaa katika pua za watu usiku inapatikana pia katika Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 2 na.462 uk.153 (pia rejea 450), Sunan Nasa’i juzuu ya 1 na.91 uk.167
 
Kusukutua kwa kuyasukuma maji kwenye kaa la mdomo na puani hufukuza dhambi nje ya mdomo na pua. Ibn-i-Majah juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.282 uk.163. Lakini uhakikishe umesafisha pua yako mara nyingi iwezekanavyo. Ibn-i-Majahjuzuu ya 1 kitabu cha 1 na. 406 uk.228.
Kupenga na hedhi ni matendo ya Shetani. Ibn-i-Majah juzuu ya 2 na.969 uk.87. Wakati hedhi yaweza kuwa na mambo ya kiusafi, kusema kuwa wanawake kwa maumbile yao hutenda matendo ya Shetani kila mwezi kuzidi kiasi.
Kwa maana hiyo, kupiga mwayo hutoka kwa Shetani kufuatana na Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sehemu ya 125 na.242 uk.157 na juzuu ya 8 kitabu cha 73 sehemu ya128 na.245 uk.158
Jicho Ovu na Korani
Jicho ovu ni hali halisi. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sehemu ya 36 na.636 uk.427, juzuu ya 7 kitabu cha 71 sehemu ya 86 na.827 uk.538. Soma pia Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 55 sehemu ya 9 na.590 uk.386.
 
Jicho ovu ni kweli. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3506, 3507 uk.39.
 
"…Ushawishi wa jicho ovu ni hali halisi." Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5426 uk.1192. Soma pia Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5424-5427 uk.1192.
 
Amir bin Rabia alisemekana kuwa alitoa jicho ovu kwa mtu fulani. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3508 uk.40.
 
Hata hivyo nywele za Muhammadi zilikuwa tiba ya jicho ovu. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 72 sehemu ya 65 na.784 uk.518.
 
Wakati Muhammadi aliponyolewa nywele zake, wafuasi wake walitaka kudaka kila kipande cha unywele wake kwa ajili ya kukitunza. Muhammadi kwa ukarimu alisambaza nywele zake kwa watu. Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2991-2994 uk.656-657.
 
Ndumba hutibu jicho ovu. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3510, 3511 uk.41; juzuu ya 5 na.3512 uk.42.
 
Albadiri inaruhusiwa dhidi ya jicho ovu na inge Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3513-3518 uk. 42-44.
 
Muhammad alitumia ndumba [nguvu za kimazingaombwe] dhidi ya jicho ovu na wanyama jamii ya mjusi wenye sumu Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3525 uk.48.
 
Muhammad alimpa ‘Aisha ndumba ili kutibu jicho ovu. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na. 5445,5447-5450 uk.1196.
 
Muhammad aliamini katika jicho ovu, na kulikuwa na hirizi dhidi yake al-Tabari juzuu ya 39 uk.134.
 
Sura mbili za mwisho (113 and 114) ziliandika juu ya ubaya wa jicho ovu kufuatana na Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3517 uk.41.
 
Hata hivyo, sura za 113 na 114 hazimo katika toleo la Ibin Mas’ud katika Korani (The Fihrist uk.57). Kuondolewa huko hakukuwa kwa bahati mbaya. Ilitaarifiwa kuwa Ibn Mas’ud alisema, "Hirizi mbili-Sura za [113, 114] si Kitabu cha Mungu." (www.AnsweringIslam.org/distortionInTheQuran.htm)
Ibn Mas’ud alikuwa katibu muhtasi wa Muhammad. Muhammad aliwaambia watu wengine wajifunze kutoka kwa Ibn Mas’ud na wengine watatu. (Bukhari juzuu ys 6 kitabu cha 60 sehemu ya 8 na.521 uk.486-487).
Mambo Yasiyo ya Kawaida
Mtu anapaswa kutumia mafuta maalum ya kufishia macho mara nyingi isivyokawaida Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3498 uk.35-36.
 
Tumia mafuta maalum ya kusafishia macho au mawe mororo (pebbles) mara nyingi isivyo kawaida. Abu Dawud juzuu ya 1 na.35 uk.8.
 
Mawe mengi isivyo kawaida kwa ajili ya kujisafisha mwenyewe ni vema zaidi Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2982 uk.655.
 
Jisafishe mwenyewe kwa udongo mara nyingi isivyo kawaida [dongo gumu]. Sunan Nasa’i juzuu ya 1 na.43 uk.149.
 
Wakati wa kwenda haja, mtu anapaswa ajipanguse kila wakati na mawe mororo mara nyingi isivyo kawaida. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 2 na.458-463 uk.153-154…. Mawe matutu kufuatana na Abu Dawud juzuu ya 1 sehemu ya 21 na.40 uk.10.
 
Muhammad kwa kawaida alikula tende mara nyingi isivyo kawaida. Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 15 sehemu ya 4 na.73 uk.38.
 
Kwenye maombi, hakikisha kuwa unamaliza na rakah mara nyingi isivyo kawaida. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1632-1644 uk.362-364.
 
Usiku omba rakah mara nyingi isivyo kawaida. Sunan Nasa’i juzuu ya 2 na.1295 uk.392; juzuu ya 2 na.1711-1712 uk.398 juzuu ya 2 na.1714-1718 uk.399-400; juzuu ya 2 na.1724 uk.403-404; juzuu ya 2 na.1725-1730 uk.404-405; juzuu ya 2 na.1759 uk.415.
 
Jitakase pua yako mara nyingi isivyo kawaida. Ibn-i-Majah juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.406 uk.228.
 
Mwislamu anahitaji kuomba maombi mara nyingi isivyo kawaida. Ibn-i-Majah juzuu ya 2 na.1169-1170 uk.194-195.
Imani Zingine za Kishirikina
"Mtu ataliyekula tende zilizo katikati ya ukanda wa lava hizi mbili asubuhi, hakuna sumu itakayomdhuru hadi itakapokuwa jioni." Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5080 uk.1129. juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5081 pia yaongezea mambo yakimazingara.
 
Baadhi ya mazingara ni sawa, kwa sababu Sa’id bin Jubair alitumia hirizi alipoumwa na inge. Alijifunza kwa Muhammad. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.625 uk.141.
 
Muhammad aliwapa Waansar mazingaombwe [kama vile albadiri] kwa ajili ya kuondoa sumu ya inge. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5442-5444, 5448 uk.1192, 1196.
 
Dumba hufanya kazi, lakini si kwa matumizi ya Waislamu. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3530 uk.51-52.
Nyoka husababisha kutoka mimba kabla ya kukomaa. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3534-3535 uk.54-55.
 
Vaa ndala ya kulia kwanza, na kisha vua ndala ya kushoto kwanza. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3616 uk.95-96.
 
Mtu anayesema mambo fulani hatasumbuka kutokana na dhiki ya ghafla siku au usiku huo. Abu Dawud juzuu ya 3 na.5069 uk.1411.
 
Gabriel alimponya Muhammad kutokana na kila ndumba na jicho ovu dhidi yake kwa kutumia ndumba. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3533 uk.47.
Kumfuata Nabii Aliyewahi Kurogwa???
Muhammad kuna wakati alirogwa: "Ilielezwa na ‘Aisha: nguvu za kimazingaombwe zilifanywa dhidi ya Nabii kwa hiyo akaanza kufikiri kwamba alikuwa akifanya kitu ambacho kwa hakika hakuwa akikifanya. Siku moja alimwomba akimsihi (Allah) kwa kipindi kirefu na kisha akasema, ‘Najihisi kuwa Allah amenivuvia jinsi ya kujitibu mwenyewe.’…" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sehemu ya 10 na.490 uk.317. Pia soma juzuu ya 4 sehemu 34 na.400 uk.267, juzuu ya 8 sehemu ya 56 na.89 uk.56-57, juzuu ya 8 sehemu ya 59 na.400 uk.266-267. juzuu ya 7 sehemu ya 47-49; na.658-660 uk. 441-443.
 
Kuna habari zaidi katika maelezo haya. Ilielezwa na ‘Aisha: Nabii aliendelea kwa kipindi hiki na kile alidhani kuwa alikuwa ameshajamiiana na mkewe, lakini kwa hakika alikuwa hajafanya hivyo. Siku moja aliniambia, "O ‘Aisha! Allah amenielekeza kuhusu jambo hili nililomwuuliza. Ndipo waliponijia wanaume wawili, mmoja wao alikaa karibu na miguu yangu, aliyekuwa kichwani pangu akauliza (huku akinisonda kwa kidole) ‘Kuna tatizo gani na mtu huyu?’ Yule mwingine alijibu, ‘Lubaid bi A’sam." Wa kwanza akauliza, ‘Ni malighafi gani ilitumika.’ Mwingine akajibu, ‘ngozi ya sehemu ya kiume ya mti wa tende na suke lake pamoja na nywele zilizoshikamanishwa pale, na Kutunzwa chini ya jiwe katika kisima cha Dharwan.’" Kisha Nabii alikwenda kwenye kisima na akasema, "Hiki ni kisima sawa na kile nilichooneshwa kwenye ndoto. Vilele vya tende za mtende ule zilionekana kama vichwa vya mashetani, na maji yake yalionekana kama mvuke wa Henna."…’Aisha aliongeza, "(Mwanamazingaombwe) Lubaid bin A’sam alikuwa mtu kutoka Bani Zuraiq, na mshirika wa Wayahudi." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sehemu ya 56 na.89 uk.57 Pia soma Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sehemu ya 59 na.400 uk.266.
 
Labid bin el-Asam Myahudi alimweka Muhammad chini ya kupiga ramli. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3435 uk.60-61.
Muhammad alirogwa Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5428-5429 uk.1192-1193; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 4 na.1888 uk.411.
 
Pia ikiwa mtu alisema uongo kwa kukusudia kwa Muhammad, hatima ya watu hao ilikuwa Jehanam (akhera). Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3754 uk.161-162, pia Abu Dawud juzuu ya 3 sehemu ya1372 na.3643 uk.1036. Kwa hiyo, kwa kuzingatia hili, Muislam anapaswa kuwa mwangalifu ikiwa atasema kitu anapaswa kuamini na kufuata yote ya BukhariSahih MuslimIbn-i-Majah, ambayo hujenga mengi yaliyo msingi wa Sharia ya Muislam.
Imani katika Mungu ina maana ni Kuachana na Imani zote za Kishirikiana
Vitabu vya Rejea

Al-Bukhari Sahih Al-Bukhari. kilichotafsiriwa na Muhammad Muhsin Khan na kuchapishwa na al Maktabat Al Salafiat Al Madinato Al Monawart. (tarehe haijaonyeshwa) (juzuu 9) (Na mkusanyiko wa hadithi zenye mamlaka zaidi za Sunni [Sunni Hadiths]).
 
Arbury, A.J. The Koran Interpreted. Macmillan Publishing Co., Inc., 1955. (tafsiri ya Yusuf Ali kwa kawaida ndiyo iliyo sahihi zaidi kuliko hii.)
 
Campbell, William. The Qur’an and the Bible in the light of history and science. Arab World Ministries. 1986, 2002. Dk. Campbell ni dakitari wa afya anayeongea Kiarabu na amefanya kazi Afrika Kaskazini.
  
Encyclopaedia Britannica
. Encyclopaedia Britannica, Inc. 1958 juzuu ya 13 uk.7-8.
  
English Translation of the Meaning of AL-QUR'AN : The Guidance for Mankind
. By Mohammad Faroog-I-Azam Malik. The Institute of Islamic knowledge 1997.
 
Geisler, Norman L. Baker Encyclopedia of Christian Apologetics. Baker Books 1999.
  
Holy, QUR-AN, The
. (Kiarabu na Kiingereza) Nakala iliyorudiwa na kuhaririwa na Presidency of Islamic Researches, IFTA, Call and Guidance. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (Tafsiri ya Kiingereza ya Abdullah Yusuf Ali) 1410 BH.
Muslim, Imam. (iliyotolewa katika Kiingereza na 'Abdul Hamid Siddiqi) Sahih Muslim. International Islamic publishing House. (tarehe haijaonyeshwa) (juzuu 4).
 
Nasa’i, Imam Abu ‘Abd-ur-Rahman Ahmad. Sunan Nasa’i imetafsiriwa na Muhammad Iqbal Siddiqi. Kazi Publications, 1994.
 
Sagan, Carl, Jonathan Norton Leonard. Planets. Time-Life Books, 1969.
  
Sunan Abu Dawud
. Kimetafsiriwa na Ahmad Hasan. Sh. Muhammad Ashraf Publishers,1984-1996.
  
Sunan Ibn-i-Majah
. Kimetafsiriwa na Muhammad Tufail Ansari. Kazi Publications. 121-Zulqarnain Chambers (Pakistan), 1994.
  
Van Nostrand’s Scientific Encyclopedia
, 4th edition. D. Van Nostrand Company, Inc. 1968.
  
World Book Encyclopedia
. World Book, Inc. 1990
 
Yahya Bin Sharaf An-Nawawi, Imam Abu Zakariya (mkusanyaji), S.M. Madni Abbasi (mfasiri) Riyadh-Us-Saleheen. International Islamic Publishing House, (tarehe haijaonyeshwa) (juzuu 2).
 
http://www.nlm.nih.gov/hmd/arabic kwa historia ya dawa katika ulimwengu wa Kiislam na Kiajemi.
http://www.masnet.org/history.asp?id=1033

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW