Wednesday, July 1, 2015

Uislam na Fani ya Tiba

Uislam na Fani ya Tiba
Mchango katika Historia
 

Toleo la Juni 2006
Kwa kiasi kikubwa, fani ya tiba ya kisasa imetokana na fani ya tiba ya kimagharibi (Ulaya), ambayo ina asili ya fani ya tiba ya Ugiriki na Urumi kale. Ingawa jambo hili ni sahihi, limerahisishwa kupita kiasi; watu wengi zaidi, Waislam kwa wasio Waislam, hawafahamu kuwa fani ya tiba ya kimagharibi isingekuwa hapa ilipo sasa bila ya mchango mkubwa na muhimu sana wa fani ya tiba ya Kiislam. Yafuatayo ni maelezo kwa muhtasari ya baadhi ya michango, yakifuatiwa na mafundisho ya Koran na Hadithi kuhusu fani ya tiba.
Mwanzo wa Fani ya Tiba katika Uislam
Ingawa Waarabu kabla ya Muhammad walikuwa na ufahamu wa fani ya tiba ya kale, Wamisri, Wabizanti (Byzantines) na Waajemi walikuwa wameendelea sana. Walifanya upasuaji, walikuwa na dawa nyingi zilizotokana na mitishamba na mimea mingine, waliunganisha mifupa, walifahamu kuondoa maji machafu na takataka, na waliwatenga wenye ukoma. Hata hivyo, palikuwa na ushirikina mwingi na dawa mbaya za tiba pia.
 
Waislam wanakubaliana kwa ujumla kuwa Waabbasidi (Abbasids) hawakuwa waangalifu sana katika imani yao kama Waislam (mtawala mmoja alizama kwenye dimbwi la mvinyo), lakini kupitia kwao kuvumiliana, sayansi na fani ya tiba vilishamiri.
 
Madaktari wa kwanza kwenye ulimwengu wa Kiislam kwa kiasi kikubwa walikuwa ni Wakristo wa Kinestoria kama hawa wafuatao. Jurji bin Bakhtishu’ kutoka Iran ya magharibi (aliyekufa mwaka 830 B.K., 215 A.H.) na wanawe walikuwa madaktari chini ya khalifa al Mansur. Yuhanna ibn Masawayh (aliyekufa mwaka 243, 857) Mnestori Hunayn ibn Ishaq (miaka kama 800- 873 B.K. (260 A.H.)) aliteuliwa na al Ma’mun kuwa kiongozi wa Dar al Hikmah (Nyumba ya Hekima), na ndiye aliyetafsiri kazi nyingi za tiba ya fani na za sayansi kuwa Kiarabu. (Tazama http://www.masnet.org/history.asp?id=1033) na http://www.nlm.nih.gov/hmd/arabic/bioI.html
Kwa habari zaidi).

Hata hivyo, kufikia mwaka 931 B.K., madaktari 869 walikuwa katika mtihani wa hati ya Khalifa al Muqtadir mwaka 931 B.K.

Waganga na Wafamasia Muhimu Zaidi wa Kiislam

‘Ali bin Radha al- Tabari (='Abdullah ibn Sahl Rabban) karibu mwaka 855 B.K.Kimsingi alianzisha fani ya tiba katika uislam kwa kuandika ensaiklopidia iitwayo Paradiso ya Hekima
Rhazes (Al-Razi) Karibu mwaka 850- 925Mwanafunzi wa al-Tabari, pamoja na Avicenna walikuwa ni madaktari wawili muhimu zaidi kati ya karne za 5 na 18. Mkemia wa kale (alkemia) Muajemi aliyetengeneza plasta ya jasi (Plaster of Paris-POP) alisomea ‘antimony’
Albucasis (al-Zahrawi) (aliyefariki mwaka 1013 B.K.)Kutoka Kordoba, mpasuaji mkubwa zaidi wa Kiislam. Aliandika kitabu bora zaidi cha upasuaji, michoro 200.
Al-Buruni (aliyefariki mwaka 1051 B.K)Aliandika kitabu kilicho kamilika zaidi cha taaluma ya utayarishaji na utoaji madawa (famasia)
Avicenna (Ibn-Sina) Mwaka 979/980-1037 B.K.Pia mwanasayansi, mwanafalsafa, na mtaalamu wa mantiki aliyeandika vitabu karibu 200. Albert Magnus wa Uingereza alijifunza mambo mengi kutoka kwake.
Averroes (Abu al-Walid Mohammed … ibn Roshd) mwaka 1126-1198 B.K.Mtoa maoni wa Aristotle. Alisema kuwa umaskini na mateso mengi hutokana na jinsi Waislam wanavyowatendea wanawake
Madawa na Ufamasia
Ja'far al Sadiq (aliyefariki mwaka 140/757) alijifunza fani ya madawa ya Kigiriki toka kwa Muislam Khalid, aliyejifunza toka kwa mtawa mwanaume wa Kibinzati Marianos. Jabir ibn Hayyan, al Kindi, na al Razi wote walichangia ufahamu wetu wa madawa. Al-Biruni (aliyefariki mwaka 1051 B.K.), aliandika kitabu kilicho kamilika zaidi cha madawa. Kabla ya hapo, Sabur ibn Sahl (aliyefariki mwaka 255/868).
 
Ni kweli hatutaki kufuata kila kitu kuhusu fani ya tiba ya mashariki ya kati. Waajemi walisifia bangi, pia kuimeza kama kidonge au kuila pamoja na sukari kama pipi, kwa mujibu wa Drugs uk.59. Ni vema ikafahamika kuwa jambo hili halisimuliwi na Hadithi, kwa sababu kitu chochote kinachokuwa na ulevi kimezuiliwa, ama kwa kiasi kidogo au kikubwa. Ibn-i-Majah juzuu ya 4 na.3386-3391 uk.496-498; juzuu ya 4 na.3393-3398 uk.498-499. Vinywaji vyote vyenye kulevya vimezuiliwa (Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 4 sura ya 75 na.243 uk.153).
 
‘Ali ibn ‘Abd al-‘Azim al-Ansari (aliyeshamiri miaka ya 1268-1270 B.K.) aliandika vitabu viwili vinavyohusu viuasumu. Aliitaja "theriac", kiuasumu kinachopooza nguvu za sumu za aina mbalimbali.
Hospitali za Kiarabu
Khalifa Umawi Walid ibn ‘Abdul Malik alijenga hospitali ya kwanza mwaka 706 B.K. Baadaye Waarabu walikuwa na hospitali za aina mbalimbali: magonjwa ya akili, magonjwa ya kuambukiza, na magonjwa ya mwili yasiyo ambukiza. Waislam pia waligundua ‘hospitali inayotembea.’ Hospitali inayobebwa juu ya ngamia kwenye msafara, chakula, maji, madawa, vyumba vya upasuaji na vyumba vilivyotengwa na vingine, na kundi la madaktari, wauguzi, wahudumu, maafisa, na watumishi. Hospitali hii yenye kutembea ilisafiri toka mji mmoja hadi mwingine au kijiji kimoja hadi kingine, kushughulikia milipuko ya magomjwa na majeruhi wa maafa ya kiasili. Hospitali za Kiislam pia zilikuwa na vifaa vya burudani na wanamuziki kadhaa walioajiriwa.
  
Ahmad ibn Tulun
 alijenga moja ya hospitali maarufu sana huko Kairo Misri mwaka 872 B.K.
  
Qalawun
 alijenga hospitali ya Dar al Shifa', huko Kairo mwaka 1284 B.K., hospitali ambayo ilitumika hadi wakati wa uvamizi wa Napoleon huko Misri mwaka 1798 B.K.
  
Al Muqtadir
 alijenga hospitali maarufu sana huko Baghdad mwaka 915 B.K..
Avicenna
(Avicenna) Ibn Sina (mwaka 979/980-1037 B.K.) alikuwa mmoja wa madaktari wawili wa mashariki ya kati wakubwa zaidi kwenye historia; Wazungu walimwita "mfalme wa waganga." Aliandika kitabu maarufu zaidi cha fani ya tiba: Kanuni za Tiba. Hiki kilikuwa ni kitabu muhimu zaidi cha kazi ya tiba Ulaya kwa zaidi ya miaka 600 mpaka karne ya 19. Avicenna aligundua ugonjwa wa uti wa mgongo na dawa nyingi. Aliona kuwa dawa na chakula vinahusiana katika tiba. Alifahamu kuwa baadhi ya vidonda vya tumbo vinasababishwa na vyanzo vya kimwili, na vingine na hofu katika mawazo na majonzi. Avicenna aliwasihi wapasuaji kuondoa kansa na alitumia muziki kutibu wagonjwa wake. Alilazimika kukimbia toka sehemu aliyokuwa anafanya kazi na kuifanya falsafa yake iangamizwe kwa sababu haikuwa ya kweli.
 
Madawa ya Kiarabu hayakuwa mimea tu iliyosaidia magonjwa kwa kubahatisha bali pia yalitengenezwa kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, , Drugs uk.22-23 kinatoa mfano wa tiba ya Kiarabu ya tumbo ambayo ilikuwa ni mchanganyiko wa manemane, airisi, pilipili nyeupe na anise iliyovundikwa kwa siku tatu kwenye jagi la mvinyo. Mvinyo ilichujwa na dawa ilinywewa baada ya mazoezi. Kwa bahati mbaya Avicenna aliagiza mpako wa shaba na dhahabu kwenye baadhi ya vidonge vyake. Kwa upande mwingine, Abu Dawud juzuu ya 2 sura ya 1469 na.3861,3865 uk.1086,1087 inasema kuwa kitu kisichoruhusiwa (kama mvinyo) hakiwezi kutumika kwenye dawa.
Urithi Usio na Bahati wa Avicenna: Kuchoma kwa Moto Ili Kuondoa Vijidudu
Avicenna alikuwa ameendelea sana kuliko wenzake wa wakati ule hata madaktari hawakuhoji ufahamu wake kwa karne nyingi. Jambo hili ni baya kwa kiasi Fulani kwa sababu kwenye Kanuni za Avicenna alifikiri kuwa wapasuaji wasitumie visu bali wachome wagonjwa kwa chuma chenye moto. Ingawa Albucasis alipendekeza njia hii karne ya 11, ushawishi mkubwa wa Avicenna kwenye karne ya 14 uliieneza imani hii. The Physician uk.33 inasema kwamba Kanisa Katoliki lichukua hekima ya Avicenna na chuma cha moto kikawa ndio tiba kuu. Madaktari wa Kiajemi pia walitibu ukoma na magonjwa mengine kwa kutumia moto. Hata hivyo daktari wa Kifaransa Ambrose Pare, mwaka 1536, alikuwa anatibu watu waliokuwa na majeraha wakati mafuta ya kuchomea kwa moto yalipokuwa yameisha. Badala ya kutokufanya kitu chochote, alifunga majeraha kwa kutumia terafini na mafuta ya waridi. Siku iliyofuata, kwa mshangao mkubwa, alikuta kuwa askari hao walikuwa na hali nzuri zaidi ya wale waliochomwa na vyuma vya moto.
 
Avicenna hakuwa Muislam wa kweli kabisa, alitumia mvinyo na kushika mafundisho yasiyokuwa ya kweli. Lakini kama angezingatia Hadithi ingeweza kumsaidia hapa. Ingawa Hadithi zilisema kwa makosa kuwa kuchoma na chuma cha moto kunasaidia, Muhammad alizuia jambo hilo kwa wafuasi wake.
  
Kuchoma kwa chuma cha moto [kuziba jeraha kwa kutumia moto] kunasaidia, lakini Waislam hawapaswi kufanya hivyo. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3489 uk.32. Kwenye Abu Dawud juzuu ya 3 sura ya 1465 na.3857 uk.1085 Muhammad alimchoma kwa chuma cha moto Sa
d bin Muadh (ambaye baadaye alikufa), lakini jambo hili lilikuwa mwanzoni mwa utume wa Muhammad. 
 
"Uponyaji upo kwenye vitu vitatu: kubwia asali, mwumiko au kuchoma na chuma cha moto.Lakini nawazuia wafuasi wangu kutumia kuchoma kwa chuma cha moto." Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 3 na.584 uk.396. Sahih Muslimjuzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5467, 5468 uk.1199, 1200 hufundisha kitu hicho hicho.
Rhazes na Tabibu Wengine
(Rhazes, au Ibn Riza) Abu Bakr Muhammad al-Razi (mwaka 855 – karibu 925/932 B.K.) alikuwa mganga mwingine kati ya wawili wakubwa zaidi miongoni mwa waganga wa Kiislam. Alikuwa mpuliza filimbi kabla ya kwenda kujifunza falsafa chini ya Abu Zayd al Balkhi, na baadaye kugeukia uganga kwenye hospitali ya Baghdad. Mwaka 902 B.K. kwa ombi la gavana wa Rayy, aliondoka Baghdad na kurudi mji wa nyumbani kwake, Rayy, kuongoza hospitali. Aliandika vitabu vingi zaidi kikiwemo kimoja kinachohusu magonjwa ya akili, na kingine usafi wa hospitali. Alitumia pombe kama kemikali inayozuia kukua kwa bakteria na zebaki kama haluli. Al-Razi aliwafanya wanafunzi wake wachukue elimu ya kujiendeleza. Kitabu chake bora zaidi, ensaiklopidia ya tiba iliyoitwa Al Hawi fi al Tibb, (kilifahamika kama Continens Ulaya) kilikuwa ni kitabu cha kwanza cha tiba kuchapishwa Ulaya mwaka 1486 B.K. na kilitumika hadi karne ya 18. Rhazes alitumia muziki kutiba wagonjwa wake, na alitofautisha ndui na surua.
 
Khalifa wa Kimisri Fatimid al-Hakim (mwaka 855-karibu 925 B.K.) alikuwa mtu wa ajabu sana, alichoma makanisa, na kuwazuia wanawake kuvaa viatu, lakini alihakikisha kuwa Kairo ina hospitali nzuri nyingi. Madaktari mashuhuri walikuja toka kila sehemu, ikiwa ni pamoja na Ibn Butlan aliyeandika Kalenda ya Afya, na Ibn Nafis, aliyegundua mzunguko wa damu wa kwenye mapafu karne kadhaa kabla ya Michael Servetus.
 
(Albucasis) Khalaf ibn 'Abbas al Zahrawi (aliyekufa mwaka 1013 B.K.), huenda ndie mpasuaji mkubwa zaidi wa Kiislam, kutoka Cordoba. Alipewa jina la al-Zahrawi kwa sababu alikwenda al Zahra’, mji mpya uliojengwa na Umayyad mtawala wa Al Nasir Hispania. Aliandika kitabu cha upasuaji kilichofahamika kama Concessio huko Ulaya. Kitabu hiki kilikuwa na michoro zaidi ya 200. Wapasuaji wa Ulaya walimnukuu mara nyingi sana mwishoni mwa karne ya 16.
 
(Averroes) Abul Warid Muhammad Ibn Rushd (aliyefariki mwaka 1198 B.K.) alizaliwa Cordoba. Alikuwa daktari, mwanafalsafa, na pia jaji. Alikuwa ni mtu wa kwanza kuona umuhimu wa mazoezi ya mwili kwenye afya.
 
Katikati ya karne ya 12, Myahudi Maimonides alimfanyia upasuaji Saladin.
 
Huko Uhispania, familia ya Ibn Zuhr ilikuwa na madaktari wengi na wazuri. Abu Marwan 'Abd al-Malik aliyekuwa tabibu mashuhuri wa Magharibi. Wanafalsafa maarufu, Ibn Tufayl na Ibn Rushd, pia walikuwa tabibu maarufu sana.
 
Baada ya Wamongoli kuivamia Mashariki ya kati, Waislam walizigeukia dawa na sindano vya Kichina.
Mapigo
Kama ilivyokuwa Ulaya, ulimwengu wa Mashariki ya Kati ulikumbwa na mapigo makubwa. Haya ni baadhi yake:
Baadhi ya Mapigo ya Mashariki ya Kati
627-628 B.K. Pigo la Ctesiphon
638-640 B.K. Pigo la ‘Amwas na Syria
668-689 B.K. Pigo la Basra
706 B.K. Pigo la Maidens
716-717 B.K. Pigo la Notables
1403-04 B.K. Tauni, iliua watu 620,000
Baadhi ya Mapigo ya Ulaya
664-683 B.K. Tauni Uingereza
740-744 B.K. Tauni Uturuki na Ugiriki 200,000
1345-47 B.K. Tauni Urusi
1347-51 B.K. Tauni Ulaya Magh. 25-75,000,000
1485-1550 B.K. Jasho Uingereza, vifo 3,000,000
1493 B.K. Pigo Genoa (80% walikufa)
1660-79 B.K. Tauni Ulaya, vifo 14,400,000
 
Ingawa kila mtu alipatwa na mapigo, Waturuki walipata suluhu. Waligundua kuwa ikiwa mtu mwenye afya nzuri atawekewa kiasi kidogo cha usaha toka kwenye lengelenge, mtu huyu atapata ndui lakini atashinda 99% ya mara zote. Hii ilikuwa ni njia bora ya kupata ndui kuliko ile ya kawaida.
Tafadhali naomba unisamehe endapo sehemu hii iliyotangulia imekuchosha, lakini urefu wake unaonyesha michango ya watu wa Mashariki ya Kati katika fani ya tiba ambayo wanaweza kujivunia kuwa wameitoa duniani. Mafanikio haya ni makubwa sana, kwa mujibu wa mafundusho ya Hadithi za Kisuni na Koran.
Lini Muhammad Alishauri Kuchovya Nzi Kwenye Kinywaji Chako?
"Kama nzi ataangukia kwenye kinywaji cha yoyote kati yenu, itafaa kumchovya (kwenye kinywaji), kwani moja ya mbawa zake ina ugonjwa na linguine lina tiba (kiuasumu cha ugonjwa) (1). Maelezo chini ya ukurasa (1) yanasema "Tazama Hadithi na.673 juzuu ya 7 (kwa maelezo)" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 15 na.531 kabla ya uk. 335.
 
"Abu Huraira alisimulia: Nabii alisema, ‘Kama nzi wa nyumbani ataangukia kwenye kinywaji cha mmoja wenu, na amchovye nzi huyo (kwenye kinywaji), kwani moja ya mbawa zake ina ugonjwa na nyingine ina tiba ya ugonjwa huo." Bukharijuzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 16 na.537 uk.338.
 
Kwa taarifa, nzi aliyeshiba vizuri huenda haja kubwa kila baada ya dakika tano kwa mujibu wa http://www.thebestcontrol.com/bugstop/control_flies.htm.
  
Abu Hureira ana kumbukumbu halisi
: "Abu Huraira alisimulia: Nilimwambia Mtume wa Allah ‘Nimesikia simulizi (Hadithi) nyingi kutoka kwako lakini nimezisahau.’ Mtume wa Allah alisema, ‘Tandaza Rida (vazi) lako’ nilifanya kama alivyosema na kisha akaitembeza mikono yake kana kwamba anaijaza na kitu fulani (na kisha akaikunjua kwenye Rida langu) na kusema, ‘Chukua na jifunike shuka hili mwilini mwako.’ Nilifanya hivyo na baada ya hapo sijawahi kusahau kitu chochote." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 3 sura ya 43 na.119 uk.89. Pia Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 27 na.841 uk.538; Bukhari juzuu ya 9 sura ya 23 na.452 uk.332.
 
"Abu Huraira anasimulia: Mtume wa Allah alisema, ‘Ikiwa nzi ataangukia kwenye chombo cha yoyote kati yenu, mtu huyo na amchovye (kwenye hicho chombo) na kumtupa mbali, kwani kwenye bawa lake moja kuna ugonjwa na kwenye bawa linguine kuna uponyaji (1) (kiuasumu chake) yaani, tiba ya huo ugonjwa." Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 uk.58 na.673 uk.452-453.
 
Maelezo chini ya ukurasa (1) yanasema, "Kwa mujibu wa fani ya tiba sasa inafahamika sana kuwa nzi hubeba vijidudu vyenye kusababisha magonjwa (pathogens) kwenye baadhi ya sehemu zake kama ilivyosemwa na Nabii (karibu miaka 400 kabla wakati ambapo wanadamu walikuwa na ufahamu mdogo sana wa tiba ya kisasa). Kwa namna hiyo hiyo, Mungu aliumba viumbe na njia nyingine ambavyo vinaviua vijidudu hivi vinavyosababisha magonjwa k.m. kuvu la penisilini huua vijidudu kama Staphalococci na vinginevyo. Hivi karibuni majaribio yaliyofanywa chini ya usimamizi yameonyesha kuwa nzi hubeba vijidudu vyenye kusababisha magonjwa (pathogens) pamoja na viuasumu vya hivyo vijidudu. Kwa kawaida nzi anapogusa kimiminika kinachotumika kama chakula huathiri kimiminika kwa vijidudu vyake vinavyosababisha magonjwa, kwa hiyo ni lazima kumchovya ili kutoa pia kiuasumu cha vijidudu vyenye kusababisha magonjwa ili vipambane na vijidudu hivyo. Kuhusiana na somo hili, nilimwandikia pia rafiki yangu Dr. Muhammad M. El-SAMAHY mkuu wa Idara ya Hadithi ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar Kairo (Misri) ambaye aliandika makala ya Hadithi hii na kuhusiana na fani ya tiba amesema kuwa wataalamu wa viumbe vidogo (mikrobiolojia) wamethibitisha kwamba kuna chembe chembe za chachu za longitudino zinazoishi kama vimelea ndani ya tumbo la nzi na chembe chembe hizi za chachu, ili kurudia mzunguko wao wa maisha huchomoza kupitia kwenye neli za kupumulia za nzi na endapo nzi atatumbukizwa tena kwenye kimiminika, chembe hizi hupasuka kwenye kimiminika na vitu vilivyomo ndani yake ni kiuasumu cha vijidudu vyenye kusababisha magonjwa ambavyo nzi huvibeba."
 
Kama angalizo, maelezo ya chini ya ukurasa yanamnukuu Daktari huyu kutoka kwenye idara ya Hadithi; hawakupata nukuu toka kwenye idara ya tiba au afya.
 
Bawa moja la nzi lina ugonjwa na bawa linguine lina tiba. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3835 uk.1080. 
 
Kama nzi ameangukia kwenye kinywaji, chovya bawa lake lingine kwenye kinywaji. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3504-3505 uk.38-39.
Muhammad na Maji Safi
Udhibiti wa afya kwa kuondoa maji machafu na takataka (Sanitation): Watu walipomuliza kuhusu kunywa maji ya kwenye kisima chenye nguo za hedhi, mbwa waliokufa, na vitu vyenye kunuka, Muhammad alisema kuwa maji ni safi kabisa na huwa hayachafuliwi na kitu chochote. Abu Dawud juzuu ya 1 sura ya 35 na.66-67 uk.16-17.
Kutumia Mkojo wa Ngamia kama Tiba
Kwa mujibu wa Muhammad, watu waliteswa kwenye makaburi yao kwa sababu ya kujichafua na mkojo [wao wenyewe]. Bukhari juzuu ya1 kitabu cha 4 sura ya57 na.215 uk.141; Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 4 sura ya 57 na.217 uk.142.
 
Hata hivyo Muhammad aliwaamuru baadhi ya watu kumfuata mchungaji wake na kunywa maziwa na mikojo ya ngamia. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 6 na.589, 590 uk.398, 399 na juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 29 na.623 uk.418.
 
Muhammad pia alisema kuwa mkojo wa ngamia ni dawa nzuri. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3503 uk.38. 

Baadhi ya Waislam waliambiwa kunywa mkojo wa ngamia, waliishia kuwa waasi na kumuua mchungaji. Muhammad aliamuru wakatwe miguu na mikono yao na macho yao yachomwe. Sunan Nasa’i juzuu ya 1 na.308-309 uk.255-256. Tazama pia Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 152 na.261 uk.162.
Tongoo za Kidini Kama Tiba ya Kuumwa na Nge
Muhammad aliwafanyia tongoo watu wa Ansar kwa ajili ya kuondoa sumu iliyotokana na kuumwa na nge. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5442-5444, 5448 uk.1192, 1196.
Muhammad na Tiba Nyingine
Hakuna magonjwa yasiyokuwa na tiba kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 3 uk.1199, 1200.
 
Allah ametengeneza dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa uzee. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3846 uk.1083. 


Kitabu chote cha 31 kwenye Ibn-i-Majah (juzuu ya 5) kinahusu tiba. Kinasema kuwa kila ugonjwa isipokuwa uzee una tiba yake. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3436 uk.1.
 
Muhammad aliwaambia watu waliokuwa na maumivu kwenye miguu yao kujipaka hina. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3849 uk.1084.
 
Collyrium (dawa ya kuoshea macho) hufanya macho yawe maangazu zaidi na kuzifanya nywele zikue. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3497 uk.35. Hata hivyo, collyrium inapaswa kutumiwa kwa kiasi cha namba witiri. Ibn-i-Majahjuzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3498 uk.35-36; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.35 uk.8.
 
Kiuasumu cha sumu: "Mtu anayekula tende ‘Ajwa saba kila asubuhi, hatadhurika na simu au uchawi siku atakapoila." Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 65 sura ya 44 na.356 uk.260 na Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 72 sura ya 56 uk.451; Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5080 uk.1129; juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5081 pia inaongeza uchawi. 
"Aisha alinisimulia kuwa alimsikia Nabii akisema, ‘Kumini (cumin) nyeusi huponya magonjwa yote isipokuwa As-Sam.’ ‘Aisha alisema, ‘As-Sam ni nini?’ Nabii alimwambia, ‘Kifo.’" Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 7 na.591 uk.400. Pia juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 7 na.592 uk.400 na Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 10 na.596 uk.402. 

Nigella Sativa huponya kila kitu isipokuwa kifo. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 24 na.5489-5490; Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3447 uk.8; juzuu ya 5 na.3449 uk.9.
 
Tiba ya mshipa wa nyonga ni matako ya kondoo. Ibn-i-Majah juzuu 5 na.3463 uk.18-19. 
 
Tiba ya uvimbe wa kwenye mapafu ni [mtishamba uitwao] ‘vita’ (wars), mshubiri wa India na mafuta ya mzeituni. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3467 uk.21. 
 
Tazama www.MuslimHope.com/IslamAndScience.htm jinsi Muhammad alivyosema ni tiba ya kutupiwa kijicho.
Ushauri wa Muhammad Kuhusu Kuumika
Kuumika ni njia ya tiba ya kale inayohusisha kuweka kikombe chenye moto kwenye ngozi ya mgonjwa. Wakati kikombe na hewa ndani yake vinapoa, vinasababisha uwazi unaovuta damu nje.
 
Muhammad alisema kuwa njia ya kuumika ilikuwa ni tiba nzuri. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5467 uk.1199; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2740, 2741 uk.594; Ibn-i-Majah juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3476 uk.24; juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3478 uk.25. 
 
Kuumika ni tiba nzuri zaidi. Abu Dawud
 juzuu ya 3 na.3848, 2850, 2851 uk.1084.
  
Muhammad alisema pia kuwa ikiwa watu watajiumika tarehe ya 17, 19 au 21 ya mwezi itakuwa ni tiba kwa kila ugonjwa. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3852 uk.1084.
 
Abu Hind alimuumika Muhammad kwa mujibu wa Abu Dawud juzuu ya 2 na.2097 uk.562. Pia tazama Abu Dawud juzuu ya 3 sura ya 1464 na.3855 uk.1085; Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2162-2163 uk.302-303; Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 29 sura ya 11 na.361, 362 uk.38-39; Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 12-15 na.598-602 uk.403-405. Huu ulikuwa ni wakati alipokuwa anafunga. Ibn-i-Majah juzuu ya 4 na.3081 uk.330; Tirmidhi’s Shamaa-il sura ya 49 na.1, 2, 3, 4, 5, 6.
 
Hata malaika waliimwambia Muhammad aumikwe. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3477 uk.25 juzuu ya 5 na.3480-3481 uk.26.
Tofauti na Biblia
Kila mtu anafahamu kuwa tiba za kale zilikuwa na imani nyingi zenye dosari, lakini je unafahamu kuwa mwandishi wa Injili ya Luka aliyewahi kuandamana na Mtume Paulo, alikuwa daktari? Hata hivyo tunaona kuwa hakuna hekima au mashauri ya kidaktari ya Luka (hata kama yalikuwa sahihi) yaliyoingia kwenye Injili ya Luka au Kitabu cha Matendo ya Mitume. Luka alikuwa mwanahistoria mwangalifu na mwenye usahihi, na kama angeongeza mambo ambayo Mungu hakupenda afanye hivyo, ni dhahiri angeongeza mashauri ya fani ya tiba ambayo aliyaona kuwa mazuri.
 
Kwa hiyo, ingawa Hadithi zina mashauri kuhusu kuumika, namna ya kuepuka kupigwa kijicho, n.k., Agano Jipya halina mashauri yasiyokuwa sahihi ya kidaktari. Ushauri pekee wa tiba ni ule ambao Paulo alimwambia Timotheo kutumia mvinyo kidogo wakati wa kula kwa ajili ya maumivu yake ya mara kwa mara ya tumbo. Kwenye Agano la Kale mashauri ya moja kwa moja ya tiba hayakutolewa kwa kawaida (isipokuwa kutumia mkuyu wa moto kutibu jipu la tumboni mwa Hezekia), lakini sheria za vitu visafi na vitu najisi zinaonyesha kuwa za kiafya hasa.
 
Ukweli ni kwamba, usafi na afya vya mwili vina umuhimu mdogo kuliko usafi na afya ya roho. Jambo hili linatakiwa kufanywa, lakini linaweza kufanywa na mtu mmoja tu tunayemwita "Mganga Mkuu" – Yesu Kristo. Mwombe akusafishe na kukufungua macho ili uweze kuifahamu kweli.
Vitabu vya Rejea na Kujifunza Zaidi
Al-Bukhari Sahih Al-Bukhari. (kimetafsiriwa na Muhammad Muhsin Khan na kimechapishwa na al Maktabat Al Salafiat Al Madinato Al Monawart. (mwaka haufahamiki) (juzuu 9) (Mkusanyiko mzuri zaidi wa Hadithi za Wasuni).
 
Arbury, A.J. The Koran Interpreted. Macmillan Publishing Co., Inc., 1955. (Tasfiri ya Yusuf Ali inaonyesha kuwa sahihi zaidi kuliko hii).
 
Campbell, William. The Qur’an and the Bible in the Light of History and Science. Arab World Ministries. 1986, 2002. Dr. Campbell ni daktari anayeongea kiarabu na amefanya kazi Afrika Kaskazini.
  
Encyclopaedia Britannica
. Encyclopaedia Britannica, Inc. 1958 juzuu ya 13 uk.7-8.
  
English Translation of the Meaning of AL-QUR'AN : The Guidance for Mankind
. Iliyotafsiriwa na Mohammad Faroog-i-Azam Malik. The Institute of Islamic knowledge 1997.
  
Holy QUR-AN, The
. (Kiarabu na Kiingereza). Ilifanyiwa masahihisho na kuhaririwa na Rais wa Islamic Researches, IFTA, Call and Guidance. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (Tafsiri ya Kiingereza ilifanywa na Abdullah Yusuf Ali) 1410 A.H.
 
Lee, Russel V. and Sarel Eimerl. The Physician. Time-Life Books 1967.
 
Modell, Walter and Alfred Lansing. Drugs. Time-Life Books. 1967.
 
Muslim, Imam. (ilitafsiriwa kwa kiingereza na 'Abdul Hamid Siddiqi) Sahih Muslim. International Islamic Publishing House. (mwaka haufahamiki) (juzuu 4).
 
Nasa’i, Imam Abu ‘Abd-ur-Rahman Ahmad. Sunan Nasa’i imetafsiriwa na Muhammad Iqbal Siddiqi. Kazi Publications. 1994.
  
Sunan Abu Dawud
. Imetafsiriwa na Ahmad Hasan. Sh. Muhammad Ashraf Publishers.1984-1996.
  
Sunan Ibn-i-Majah
. Imetafsiriwa na Muhammad Tufail Ansari. Kazi Publications. 121-Zulqarnain Chambers (Pakistan) 1994.
  
World Book Encyclopedia
. World Book, Inc. 1990.
 
Yahya Bin Sharaf An-Nawawi, Imam Abu Zakariya (mkusanyaji taarifa), S.M. Madni Abbasi (mtafsiri) Riyadh-Us-Saleheen. International Islamic Publishing House. (mwaka haufahamiki) (juzuu 2).
Tazama
http://www.nlm.nih.gov/hmd/arabic kujua historia ya fani ya tiba kwenye ulimwengu wa Kiarabu/Ajemi. 

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW