Thursday, July 30, 2015

NANI KAMPA UTUME NA UNABII MTUME MUHAMMAD?


           


Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu.

Twazidi pia kukushukuru kwa ajili yakuyafuata mafundisho haya ya Biblia Takatifu.

Twaamini mada ile ile lakini ya tatu kuhusu imani ya kiislamu itakusaidia ukiwa mkristo wa kweli kutoishiriki mihadhara ya ubishi kati ya waislamu na wakristo.
Sababu ya pili, ni kwako ndugu na dada ambaye ungali bado katika upotevu wauislamu bila yako kujuwa ukweli kwa wazi.

Katika zile sababu zaidi ya 25 zinazotudhihirishia uongo na upotevu wa dini ya uislamu tumetamani kuchimbua «Utume na unabii wa nabii Muhammad s.a.w» 

Tunazo sababu zaidi ya mia (100) kuwauliza waislamu na kitabu chao qura'n swali tulilolitaja hapo juu na maswali mengine kuhusu UISLAMU na Qura'n! na moja ya hayo maswali ni sababu kitabu chao yaani Qur’ani kinatutaka sisi wakristo kusilimu, lakini kabla tusilimu nakuingia dini ya uislamu ni sherti tumjuwe vyema vilivyo huyu nabii sababu Yesu Kristo anatuonya kwamba manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi yamkini hata wachaguliwa wa Mungu. Mathayo 7 :15-20. Kwa hivi ni sherti Muhammad atumbukizwe ndani ya Biblia iliyokitangulia kitabu alichopewa ijapokuwa baadaye tutajuwa alikipewa na nani ? na akizama ndani ya Biblia hatuna budi kumfwata na kumtumikia Allah subhanahu wa tahalah! Lakini ikimtema kando huyo si nabii na mtume wa Yehova Mungu.

Kama mimi mwenyewe Fred Nguli MWAMBA niliyewahi kunaswa nakujikuta katika wavu wa hiyo imani nilizidi kujiswali maswali mengi huku nikifanya uchumguzi kwakulinganisha maandiko ya kiislamu na yale ya kikristo lakini nisiupate ukweli huko na neema yake Kristo Yesu ikanirudisha kwa mara ingine katika imani ya kweli katika yeye Kristo Yesu na ukristo wake.

Ukweli ambao hatuwezi kuupinga ni kwamba Biblia Takatifu ambayo waislamu pia huitumia kwakuichezea-chezea na isitoshe pia kwakuitumia kuwapiga wakristo waliopofushwa wakidhani kwamba waislamu wanaiamini, hiyo Biblia imekuwapo duniani zaidi ya miaka 2000 kabla ya Qur’ani tukufu kuwepo.
Biblia Takatifu inasema hivi:
Kutoaka 20:1-3
«Mungu akanena maneno haya yote akasema,  Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi
Hapa Mungu alitutahazarisha mapema kumpitia mtumishi wake nabii Musa ya kwamba tuepuke kuwa na miungu mingine ila yeye pekee ambaye jina lake ni Yehova!
Haya maneno sawa na Mathayo 7:15-20 Mungu aliyasema kabla ya Muhammad kuwepo, kabla ya Qur’ani kuwepo na kabla kuwepo kwa wanaume 4 walioiandika Qur’ani tukufu ambao ni:Seidinah Umar, Osman, Abubakar na Ali.

Inamaanisha nini?
Ni kwamba kama Mungu mwenyezi anavyokuwa na watumishi kama vile mitume na manabii, vilevile miungu nayo yaweza kuwa namitume na manabii wake.
Kwa mujibu wa Mathayo 7:15-20, Yesu Kristo anatupatia alama yakuwatambuwa manabii wa uongo akisema katika mstari wa 16 hivi « Mtawatambua kwa matunda yao » 
Basi natujaribu kuliangalia andiko lingine jinsi gani twaweza kuwatambua,
1Yohana 4:1-3, 15
«Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 
Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. 
Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.»

15 «Kila akiriye ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu
Hiki ni kipimo tunachokitumia kuwapima mitume na manabii! 
Mathayo 7:15-20
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazurina mti mwovu huzaa matunda mabaya.
Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.»

Hebu niseme hivi kulingana na tahazari ambayo Mungu ametupatia katika maandiko hayo mawili hapo juu:

‘Muhammad namlinganisha na mti, sasa matunda yake yakiwa mazuri sina ubishi nitamfuata, lakini yakiwa ni matunda kinyume na hayo nitamhesabu kama nabi iwa uongo’.

Je, katika Qurani Allah wa waislamu na Muhammad anasemaje?

Qr. 112 au surat Al-Ikhlas’
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.
Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.
Hakuzaa wala hakuzaliwa.
Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.

Qr. 19 au surat Maryam 35
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanau, Yeye ametakasika! Anapolihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
Huyu ni mungu tofauti na Mungu wa mbinguni ambaye jina lake ni Yehova! na tukilinganisha na yale maandiko ya Mathayo na waraka wa kwanza wa Yohana ukweli uko wazi kama huyu hatokani na Mungu na kwamba huyu ni Anti-Kristo! Kwani Biblia inasemaje ?
1Yohane 2:22-26,
Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.
Na hii ndiyo ahadi aliyoyuahidia, yaani, uzima wa milele.
Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.
Wakolosai 1:13-15,
Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
Yohane 3:16-17,
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Kwa maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

Kwahivi sisi wakristo tunazo sababu zaidi ya 100 kwanini hatumtambui mtume Muhammad, dini yake na mungu wake ambazo Mungu akituwezesha tutaziweka wazi moja kwa moja.

Ila hatuwezi kutosema hii moja ambayo ni hii:

Katika kitabu cha Qura’n tukufu kuanza na surat Al-Faatihah hadi surat Al-Nasmaandishi yake yanampinga Yehova Mungu wa israel.

CHIMBUKO NA UKOO WA UTUME NA UNABII WA MUHAMMAD

Kwanza kabisa, sote twajuwa kama kila mtoto huenda na kabila, lugha na mil aya babaake ila si ya mamaake. Hilo halina shaka hata kidogo!
Ibrahimu babaake Isaka na Ismail kabla aitwe na Mungu alikuwa ni mwarabu wa ki kurdi na baadaye Mungu aliyeviumba vyote akambadilisha na uzao wake wote baadaye ukawa ni waebrania.

Mwanzo 12:1-3
«Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa

Lakini Muhammad, Qur’ani na wafuasi wake huzidi kuhakikisha kuwa Muhammad ni wa ukoo wa Ibrahimu wakati Ibrahimu si mwarabu tena!

Katika kitabu cha «maisha ya mtume Muhammad sw», twahakikishiwa kwamba Muhammad ni mwarabu wa kabila la Makureshi. 

                   KUPEWA UTUME
Nilipokuwa nikichunguza kitabu cha historia ya Muhammad, kwa umri wake wa miaka 12 alikwenda na Abu Talib baba yake mdogo  huko Shamu (Syria) kwa safari ya biashara, njiani wakakutana na mwanamume nabii wa kikristo ambaye jina lake alikuwa ni Bahirah naye akatowa unabii kuhusu Muhammad kwa maneno haya:
« Ewe Abu Talib;
Mtunze vema mtoto huyu kwa maana naona alama za umaarufu kwa mtoto huyu katika siku zake za usoni naye atapata kazi ya kumtumikia Mungu
Ni katika kitabu cha Maisha ya mtume Muhammad, ukurasa namba 4. Swali ni hili, lini nabii wa kikristo akatabiri uislam? Jibu ni hapana sababu neno la unabii kutoka kwa Mungu haliwezi kamwe kutabiri imani kinyume na Mungu na Kristo mwana wake wa pekee!

Mithali 8:7-9
«Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi. Yote humwelea Yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa

2Petro 1:20-21
« Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu

Tito 1:2
« katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu»

Kumbe ni wazi kwamba nabii huyu alikuwa na ujumbe muhimu kwamba siku moja Muhammad angalimtumikia Kristo Yesu na Ukristo lakini kwa bahati mbaya shetani akaubadilisha mwelekeo wa huyu maskini baadaye kama tutakavyoona katika wito wake.

Pangoni la Jabal Hira kaskazini mwa Mekka ndiko Muhammad alikuwa akienda kuabudu siku zote lakini alikuwa akimwabudu nani? Nakuomba tusome huu wito wake wa utume hapo chini.




































Huu ni uhakikisho kwamba Muhammad hakupewa utume na Mungu wa israeli, sababu ukisoma pia kitabu chawakeze wakubwa na wanaweukurasa wa 12 kuna maneno yanayorudilia haya ambayo tumeyasoma hapo juu yakisema hivi:
Nanukuu, 
Basi mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe, akamwadithia na palepale homa kubwa kabisa ikampanda, akataka afunikwe na maguo mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema: «Najihofia nafsi yangu kuchezewa na mashetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga!» 
Hapo katika pango la Jabal Hira ndipo waislamu na qura’n hudai kwamba ndipo alipopokea Wahyi wa qura’n, utume na unabii.
Lakini twaona na kusikia maneno ya mtume mwenyewe yanashuhudia alichokutana nacho pangoni ambacho ni shetani sababu hata Biblia Takatifu hushuhudia hivi:      

1Yohana 1:3
Hilo tuliloliona nakulisikia, twalihubiri na nyinyi: ili na nyi pia  mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo

Ukweli ni kwamba huyu shetani aliyekutana na maskini Muhammad pangoni hakumpa hata utume wala unabii isipokuwa mkewe Hadidja na Bwana Waraqa bin Naufal ndio waliomshauri Muhammad kujibashiria kuwa yeye ni mtume wa uma kama tulivyo soma katika kurasa ambazo tumekuwekea picha zake hapo juu.
Ikumbukwe vizuri kwamba haya yalitokea wakati ambao uislamu na qura’n havikuwepo kwanza na historia ya maisha ya mtume kinamtambuwa Waraqa bin Naufal kama mtu ambaye hakuwa naabudu sanamu za waarabu wenzake! Lakini yeye ni nani kutowa ruhusa kwa mtu kama Muhammad ili ajibashirie utume? Hapo kuna mashaka mengi.

Vipi kwa Hadidja?
Mjane aliyefiwa na waume wake 2 kisha akajichukulia Muhammad kama mume wake wa tatu, Huyu ndiye aliyeingia wa kwanza katika imani potofu ya uislamu. Lakini natujiulize hili swali: « je, inakuwaje mtu ambaye bado ni mkafiri kutowa utume kwa mwingine kabla yeye hajajuwa ujumbe wa mtume huyo nakuuamini?»  Bila shaka jibu laweza kuwa ni upumbavu wakupindukia.
Hebu tuone qura’n inavyosema kuhusu kupewa utume, kupewa wahyi au ujumbe,

Qr.7:144 au surat Al-A’raaf 144
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteuwa wende kwa watu na ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukuwa niliyikupa na uwe katika wale wanaoshukuru.
Kwanini Allah Subhanau Watahallah hakufanya hivihivi kwa Muhammad s.a.w katika pango la Jabal Hira?
Swala la Muhammad kuwa ni mtume katika maandishi ya qura’n na hadithi zote siyo hoja lakini hoja yetu ni «Kapewa na nani huo utume?» 
Tuchunguze na kuchimbua tena hili andiko la Qura’n,
Qr. 13:43 au surat Ar-raa’d 43
Na waliokufuru wanasema kuwa wewe si mtume, 
Sema, Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya kitabu.

Anayemwambia Muhammad kusema ni ALLAH wake na wa waislamu wote.
Anayedaiwa kuwa shahidi bain aya ALLAH na waislamu ni Mwenyezi Mungu.
Anayedaiwa kuwa ni mwenye ilimu ya kitabu ni Jibril.
Kwa wazi kabisa ni kwamba Allah wa awislamu ni tofauti na Mwenyezi Mungu sababu anamtowa kuwa shahidi kati yake na wafuasi wake yaani waislam. Je, Mwenyezi Mungu anasemaje kuhusu miungu mingine?
Isaya 42:8
«Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu
Isaya 48:11
«Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu
Kumbukumbu 18:18
« Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. 
Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa
Uislamu na qura’n wanadai aliyetabiriwa na nabii Musa kwamba ni Muhammad s.a.w lakini kama tulivyochunguza katika yale matoleo ya kwanza ni kwamba sio Muhammad bali alikuwa Yesu ambaye angekuwa masihi na Kristo wa dunia yote! Kwa sababu hizi chache tu:

      ALLAH S.W NA MUHAMMAD S.A.W
       YEHOVA MUNGU NA YESU KRISTO
     mungu asye na  jina kamili
Qr. 17 au surat Bani Israil 110 (Wana wa Israil)
Sema; muombeni (Mwenyenzi Mungu) kwa (jina la) Allah au muombeni (kwa jina la) Rahman. Kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa). Kwani ana majina mazuri mazuri………
        Mungu anayejulikana
 Kutoka 6:2-3,
Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, mimi ni YEHOVA;
Nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
  mungu wao ana maadui wake ambao ni wakristo na wayahudi
Qr. 4:51 na 57 (surat Al Maida)
Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika hao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

Wafuasi wote wa Allah wanangojea moto wa jehanam kisha waokolewe waislam baadaye kutoka motoni
Qr. 19:70-72
Tena hakika sisi tunawajuwa vyema Zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo
Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako mlezi ambayo lazima itimizwe. Kisha tutawaokoa wale waliomcha Mungu; na tutawaacha madhalimu humo hali wamepiga magoti motoni.
Mungu wetu ni mwenye rehema na wafuasi wake hatuna adui
Mathayo 5:43-44
Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
                 Kwetu wakristo sivyo ilivyo!
Zaburi 9:17
Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
Luka 16:23
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
       Allah wao ataionja jehanamu pia
Qr. 50 au Surat Qaf 30 (kuapa)
Siku tutakayoiambia Jahanamu, ‘Je! Umejaa?’ Nayo itasema ‘Je kuna ziada (zaidi? Naije tu!
Imesimuliwa na Anas kuwa: mtume alisema watu watatupwa jahanamu, Naye Allah ataiuliza jahanamu akisema je umejaa nayo jahanamu itasema kwani kuna nyingine zaidi na ije tu? Mpaka Allah atakapo ingiza mguu wake nayo jahanamu itasema inatosha! Inatosha
  Dhawabu ya wakristo ni uzima wa milele
Yohana 14: 1-4
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia.

Hizi ni sababu ndogo kutoka katika zile sababu zaidi ya 100 ambazo ziko wazi kabisa kama Muhammad kapewa utume na yeye mwenyewe kwa shauri la mkewe Hadidja na Bwana Waraqa bin Naufal.
Twataka tukupe baadhi ya mashaka katika qura’n

# Katika Qura’n sur aya 3, aya yake ya 7 (surat Al I’mran) panasema kwamba kuna aya nyingi katika Qura’n ambayo   mwanadamu hana uwezo kuzisoma na kuzitafsiri isipokuwa Allah.

# Katika sura za 11:114, sur aya 17:78-79, sura ya 20:130, na sur aya 30:17-18 za qura’n Allah anasema kwamba kila mwislam analazimika kusali mara tatu kwa siku, lakini katika hadithi za mtume huyo huyo Allah anawalazimisha waislam kusali mara tano kwa siku. Je, Allah hana uamzi moja? Waislam kazi kwenu! 

# Katika sur aya 18:86 ya qura’n, Allah hukiri kwa Muhammad kwamba jua hutua katika dimbwi la maji machafu duniani.  Je, hiyo ni kweli? Kama Mwenyezi Mungu ni muumba jinsi gani anaweza kufanya makosa kama haya? Na je, Biblia inasemaje kuhusu uumbaji? Soma kitabu cha Mwanzo sura 1 na mbili.

# Katika sura 2:106 na sura 16:101 katika qura’n Allah anasema kama alirekebisha aya katika qura’n na kutangua au kubadilisha aya zingine ili kuweka zilizo bora zaidi. Je mungu ni mtu ili abadilishe neno lake? 

            Isaya 40:8, «Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele
Tunazo sababu zaidi tutakazoziweka hadharani katika sehemu zitakazofuata katika siku zinazokuja ili kukusaidia wewe muislam kuufikia wokovu kamili katika Kristo Yesu Bwana wetu na mwokozi wetu.
Twamalizia toleo hili tukikuomba katika upendo wa kristo kuikimbilia mbali sana ibada ya shetani katika dini ya uislamu na kukimbilia kwa Yesu Kristo ili upate uzima wa milele.

Matendo ya mitume 4:11,12
Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

                                MBARIKIWE NYOTE

                           Ndugu yako katika Kristo

11 comments:

Anonymous said...

Ndugu yangu ningekushauri usome kwa umakini Qur-an maana umesoma translation juu juu ukadhan umeelewa lakin soma vizur na mungu akipenda utaelewa.

Unknown said...

We mjinga acha kutusi dini,kama huna kaz BA's katafte wajinga wenzenu muvaliane nguo za kubana mukilana,na mupige mikelele kama mbwa,upo na shetani na utazikwa na shetani nyooooooooo

Unknown said...

Hebu tuonyesheni kusoma kwa makini kukoje?

Unknown said...

Hamna ajuae ukwel wa Dini mana wote tumezikuta ila kitakachokuponya n iman na matendo yako

Anonymous said...

Apana kumtusi kama mlivyo mtusi BWANA wa MABWANA yesu kristo atendaye haki anahaki mumwuwe radhi ye anasema ukweli.

Unknown said...

Hongera brother in Christ waambie waislamu na baadhi ya wakristo ambao hawajaokoka waokoke waache dhambi hasa waislam waachane na uongo wa Mohammed na Allah ambaye hana lingine isipokuwa jehanam (Qur'an 40:60)

Deus john said...

Be blessed broo

Deus john said...

Be blessed broo

Unknown said...

Msiba huu kwa Maislam wafuata Mkumbo

Anonymous said...

Waislam, badala ya kujibu hoja kwa aya na kuchambua, mnalalamika. Poleni kwa kuteseka

Anonymous said...

Ubarikiwe.... Anayesema soma quran vizuri unakuta yeye hajaisoma... Hlf pingeni kwa facts sio kutukana tuu...

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW