Friday, June 19, 2015

UTATA NA SHAKA KUBWA KATIKA QURAN KUHUSU MUSA KUMSHUTUMU HARUN NA MSAMARIA KWA KUTENGENEZA NDAMA WA DHAHABU

Ndugu Msomaji,

Hebu rejea katika Surat Taha iliyo teremka Maka katika aya ya 92 mpaka 95.
92. (Musa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilicho kuzuia, ulipo waona wamepotea, ***
93. Hata usinifuate? Je, umeasi amri yangu? ***
94. Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu. ***
95. (Musa) akasema: Ewe Msamaria! Unataka nini ? ***

Aya hapo juu zinasema kuwa Musa alimkaripia Harun na “Msamaria Mwema” kwa kutengeneza Ndama wa Dhahabu kwa wana wa Israeli wakati Musa alipo kuwa katika Mlima wa Sinai. Je, haya madai ni kweli?

HEBU TUANGALIE USHAHID WA KIHISTORIA
Wa Assyria waliwashinda Wayahudi wa Ufalme wa Kaskazini katika mwaka 722 BC (Kabla ya kuzaliwa Kristo),  na kuhamia uhamishioni na kuleta watu wengine walio tekwa kutoka falme mbali mbali, ambao baadae waliona na Wayahudi wa kabila la chini ambao waliruhusiwa kukaaa hapo na wa Assyria.

Sasa basi, watoto wao ndio waliitwa “Wasamaria” kwasababu walikaa katika ardhi ya Samaria ambayo iliitwa kutoka mwenye ardhi hiyo aliye julikana kwa jina la “Shermer” (Soma 1 Wafalme 16:24) .
1 Wafalme 16: 24 Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbilia za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
Wayahudi waliwadharau Wasamaria kwa sababu mbili, moja kwa  mchanganyiko wao damu “mixed race” na kwa ajili ya kuanzisha mahekalu yao wenyewe kushindana dhidi hekalu la Yerusalemu.

MASHAKA NA UTATA UNAANZIA HAPA:
Tukio la Ndama wa Dhahabu lililo tokea karibu na Mlima Sinai kama lilivyo tajwa kwenye Quran Sura 20: 92-95 hapo juu lilitokea miaka 1446 BC (Kabla ya Kristo), ambayo ilikuwa ni miaka 725 kabla ya Msamaria wa kwanza kuzaliwa mwaka wa 721 BC.

Ndugu zanguni,

Leo kwa mara nyingine tena, tunaoana jinsi Quran ilivyo jaa shaka na utata kila sehemu.
Katika aya za Quran hapo juu na ukilinganisha na ushahid wa historia ya tukio la Wasamaria, unaona tofauti kubwa sana tokea Wasamaria walipo anza kuzalia na tukio halisi la Ndama wa Dhahabu. Tukio la Ndama wa dhahabu lilitokea miaka 1446 KK ambayo ni miaka 725 kabla ya Msamaria wa kwanza kuzalia, lakini Allah yeye anasema eti, kulikuwa na Wasamaria wakati wa tukio hilo.  Hivi, kwanini Allah anashindwa kuweka takwimu zake vyema?
MASWALI:
1. Kwanini Allah ameshindwa kusema ukweli wa tukio la Ndama wa dhahabu na kulazimisha kuwa lilitokea wakati wa uzao wa Wasamaria?
2. Je, inawezekana kuwa labda kuto kuwa na elimu kwa Muhammad kulisababisha Muhammad kushindwa elewa nini Jibril alikuwa anasema?
3. Je, inawezekama kuwa labda Jibril alipo pewa ujumbe na Allah nayeye Jibril alishindwa kumweleze Muhammad kwa usahih?
4. Je, tunaweza iamini Quran inayo shindwa kuweka takwimu zake kwa usahihi kuwa ni kitabu kisicho kuwa na shaka ndani yake?

Histori ya Ndama wa dhahabu ipo sio tu katika vitabu vya dini bali hata vitabu vya historia. Lakini katika Quram hii habari imesemwa kwa uongo mkubwa sana.

Kama kweli Allah ndie aliye iteremsha Taurat kwa Musa, kwanini alishindwa kusema ukweli?
Kama kweli Allah ndie aliye iteremsha Taurat kwa Musa, je, Waislam na Allah, mnaweza tuonyesha ipo wapi hiyo Taurat iliyo teremshwa kabla ya Quran?

Ndugu wasomaji, Quran haikuteremshwa na Allah bali iliandikwa na watu hapa duniani, kama Waislam wanabisha, basi watueleze kwanini Allah anashindwa kusema ukweli na kujaza shaka kwenye Quran?

Hakika Msingi wa Dini ya Uislam ni Allah ambaye amesha pokea sifa ya kuwa ni Baba wa Uongo. Hebu rejea na soma hii aya kutoka Biblia kitabu cha Mungu:

Yohana 8: 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.

Biblia imesha kujibu kuwa baba wa Uongo ni Ibilisi na husema yaliyo yake mwenyewe. Kumbe basi, ndio maana Allah wa Waislam nayeye anasema yaliyo yake.

Nakukaribisha kwa Mungu Mkuu ambaye yeye sio Baba wa Uongo bali ndie Muumba wa kila kitu na alikufa kwa ajili ya dhambi zako.

Mpokee Yesu leo na upate Uzima wa Milele.

Mungu awabariki sana.

Max Shimba Ministries Org.

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED


Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW