Tuesday, May 26, 2015

Kwa nini imani ya Kikristo ni bora zaidi ya Kiislamu?

1. Utangulizi


Kuamini juu ya Mungu Mmoja, ni imani katika Uwepo wa Utendaji wa Mungu mmoja [1]. Dini za Kiyahudi, Kikristo na Kiislamu hutofautiana na dini zingine kwani wao wanaamini katika nafsi ya Mungu [2]. 

Dini zinazoamini juu ya Mungu mmoja ni dini zilizo bora zaidi ya dini zingine kwa sababu wao wanaufunua Umoja wa Mungu pasipo ubaguzi wowote. Dini ya Kiyahudi imefungamana na Utaifa, wakati dini ya Kiislamu inahusiana na elimu dunia. Imani ya Kikristo haihusiani na Utaifa kama ilivyo imani ya Kiyahudi tena iko huru mbali na elimu dunia iliyoko kwenye uislamu. Hivyo basi Imani ya Kikristo ndio imani iliyo safi zaidi ya imani zote zingine zinazoamini katika Mungu mmoja [3]. 

Kwa sababu Uislamiu ni dini yenye kutumia tafakari ya kiakili, yenye kujitoa, yenye falsafa ya kupendwa, na ni dini ya kihujuma.
Imani ya Kikristo haswa imejengwa katika kuthamini uadilifu kwa kiwango cha juu sana, zaidi ya Uislamu kama ilivyo kwenye Mathayo 5. Katika imani ya Ukristo kila kitu kinachofanyika huwa ni kwa kusudi la kuuleta Ufalme wa Mbinguni mahali hapo.


2. Kweli
Agano la wana wa Israel lilishindwa, hivyo dini ya Uyahudi ambayo ni ya kwanza miongoni mwa dini zenye Imani ya uwepo wa Mungu mmoja, iliitwa ili kuleta suluhisho. Suluhisho lilikuwa ni kuongeza maboresho ili kuweza kushinda ugumu uliokuwamo ndani ya agano, au kulifanya agano hilo liweze kubebeka. Uislamu wenyewe uliongeza fikra za kimantiki, na kuingiza uwezo wa kibinadamu. Imani ya Kikristo iliongeza upendo wa Mungu kama nguvu ya uvuvio kwao. Hakuna sehemu yoyote nyingine ambapo nguvu hii ya upendo imekuwa ikionekana wazi kama ilivyo kwenye Ukristo [4]. Imani hizi zote yaani Uislamu na Ukristo huendelea kutenda kazi katika mambo ya kawaida, na katika hayo zimejikita kipekee. Hivyo basi maamuzi yoyote katika imani huweza kufanywa kwa njia ya ufunuo tu [5]. Swali hasa linalokuja hapa ni kwamba, je katika historia yote, ufunuo wa Mungu ni upi hasa? Swali hili haliwezi kujibiwa kwa njia ya mashindano ya kihoja, kwa sababu njia za hoja za kifikra pamoja na kweli za kibinadamu ni vigezo tofauti. 

Hata hivyo watu wameyaunganisha mambo hayo mawili ndani ya dini. Na kila dini ina njia zake za kuonyesha sababu zake zenye mantiki. Mashindano na mabishano ni namna tu ya kuwashawishi waumini wa dini hiyo. Katika imani ya Kikristo, wazo la kuutafuta ukweli kwa njia za kibinadamu imeachwa, kwa sababu Roho Mtakatifu ndiye anayeweza kuifunua kweli. Ni Mungu tu anayeweza kujitambulisha mwenyewe kwetu. Ukweli kuhusiana na Imani ya Kikristo kamwe haiwezi kuelezewa kwa kutumia njia za kibinadamu, bali hujifunua yenyewe kwa msikiaji kupitia matangazo pamoja na kuufunua muktadha wa imani, kwa sababu yeye ndiye ajuaye kuwa hii ndio kweli ya Mungu [6]. 



3. Wokovu
Ufunuo kuhusu kweli ya Mungu, ni Wokovu wa kweli wa Mungu. Maelezo haya hufunua kweli iliyofunuliwa inayohusisha mambo muhimu matatu:

A: Dhambi: Imani ya Kikristo inakubaliana na wazo la dhambi. Kwamba kila mwanadamu katika uhalisia wake ana mapungufu. Kutokana na hayo basi, ndipo mateso, maumivu pamoja na kifo viliingia katika maisha ya mwanadamu.
B: Mwokozi wa wanadamu: Yesu Kristo Mwokozi wa wanadamu: Watu wanahitaji kuwa huru mbali na mateso yao yote, maumivu na hata mauti. Kwa hivyo basi, mwanadamu anatakiwa kuwa huru mbali na dhambi.
C: Msamaha wa dhambi: Mwokozi wa wanadamu wote, Yesu Kristo hutoa msamaha wa dhambi, na mwamini atavikwa na Uweza wa Roho Mtakatifu kama muhuri wa Imani. Muamini anatakiwa kujua kwamba hii ndiyo kweli ya Mungu.


4.Hitimisho
Kwa nini kila mtu anapaswa kuamini Ukristo kuliko Uislamu?. Ni kwa sababu ya ufunuo wa Mungu juu ya uhalisi wa kweli. Ahadi za ujio wa Mwokozi wa wanadamu, zinakamilika ndani ya imani ya Kikristo. Muswada mkubwa wa udhihirisho sahihi wa macho na Injili. Kwa hiyo basi tunaweza kuamini juu ya kile kilichoandikwa katika Injili. Ni katika imani ya Ukristo tu ndiko Mwokozi wa wanadamu alikotokea, aliyejaribiwa kama wanadamu wengine, na kushinda majaribu yote ya kiuadilifu. Kwa hiyo basi, ni Yesu pekee aliye na haki ya kusema : “Mimi ndimi Njia na Kweli na Uzima” (Yohana 14:6).


Rejea:
1. Hans Dieter Betz (ed.), Religion, Past & Present, Volume VIII, Brill, Leiden, 2010, 527.
2. Albert Hourani, Islam in European Thought, Cambridge University Press, Cambridge, 1992, 24
3. Friedrich D. E. Schleiermacher, The Christian Faith (translated by H. R. Machintosh and J. S. Steward), Edinburgh: T. & T. Clark, 1928, 38.
4. Hendrikus Berkhof, Sierd Woudstra, Christian Faith: An Introduction to the Study of the Faith, Wm. B. Eerdmans Publishing, Grand Rapids, 2002, 23.
5. Friedrich D. E. Schleiermacher, The Christian Faith (translated by H. R. Machintosh and J. S. Steward), Edinburgh: T. & T. Clark, 37.
6. Hendrikus Berkhof, Sierd Woudstra, Christian Faith: An Introduction to the Study of the Faith, Wm. B. Eerdmans Publishing, Grand Rapids, 2002, 23.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW