Tuesday, February 24, 2015

Uislamu ulianza lini?


YAMEKUWEPO madai kwamba Uislam ulianza tangu kuumbwa kwa dunia. Na wapo watu wanaotuaminisha hayo. Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK. Yesu mwenyewe hakuanzisha Ukristo. Alisali katika Mahekalu ya Wayahudi. Masinagogi.

Maelezo haya yana msingi wa kihistoria na sio propaganda za kidini. Ndio ni propaganda kwa sababu dini zote zimekuwa na tabia ya kuonyesha kwamba zenyewe ndizo za kweli kuliko dini nyinginezo hata ikibidi kwa kuichezea historia.

Na ni bahati mbaya kwamba Dini zimekuwa na tabia ya kufanana ya kuzima uwezo wa waumini wake kuhoji lolote kwa kuwajengea hofu ya kujitafutia laana.

Qur’an inatupa maelezo yanayopinzana kuhusu lini hasa Uislamu ulianza. Baadhi ya mistari katika kitabu hicho zinadai kwamba ‘nabii’ Muhammad ndiye aliyekuwa Mwislamu wa kwanza. Kwa mfano, ukisoma Sura. 6: 163 anasema yeye ndiye wa kwanza kwa Waislamu hii ikiwa na maana kwamba yeye ndiye mwanzilishi wa Uislamu na kwamba Uislamu haukuwapo kabla yake.


Lakini katika maeneo mengine, Qur’an inadai kuwa Musa ndiye Mwislamu wa kwanza. Soma Sura 7:143. Sasa Mussa inajulikana kabisa ndiye mhusika mkuu wa dini ya Uyuda.

Kwa mshangao mkubwa zaidi, mahali pengine inadaiwa kwamba Adam, Abraham na Yesu wote walikuwa waislamu!

Hili, kwa hakika ni jambo la ajabu sana. Unapodai Yesu alikuwa Mwislamu, wakati mafundisho yake yanapingana pakubwa na Uislamu, huo ni ushahidi wa mkanganyiko ambao kwa hakika yeyote anapaswa kuuona bayana.

Kwa maoni yangu, dini hii yaweza kudai kuanza tangu kuumbwa kwa Ulimwengu ili tu kuonyesha kwamba yenyewe ndiyo ya kweli kuliko nyinginezo.

Ukweli uko wazi kwenye Qur’an yenyewe (hata kama inajichanganya) kwamba Muhammad ndiye alikuwa mwanzo wa Uislamu ndio maana anaitwa 'mtume' yaani mleta Uislam.

Sasa sisemi Uislam ni Dini potofu. Hiyo sio kazi yangu. Lakini sikubaliani na wanaodai kwamba Uislamu ulianza tangu enzi za Adam. Ndivyo ilivyo pia kwa Ukristo, dini nyingine yenye asili yake kule kule Mashariki ya kati.
Mambo mengine ni muhimu kuyaelewa hata kama yanaonekana kuwa kinyume na ‘ukweli’ wa kidini. Ikiwa unadhani kwa kujadili haya maana yake ni chuki kwa Uislamu, basi unahitaji kujielewa sasa hivi. Maana ni wazi umejitia kifungo cha hiari.

HUU NI MSIBA NDUGU ZANGU WAISLAM
Itaendelea...

Bb Sheik Mstaaf Eden Hazard kwa Max Shimba Ministries

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW