Monday, February 9, 2015

MUHAMMAD AKIRI KUWA ALLAH SIO MUNGU WA KWENYE INJIL NA TAURAT BALI NI MUNGU WA KIPAGANI


Je, Wakristo na Waislam, wanaabudu Mungu mmoja?
Je, Allah ni Mungu wa Kipagani?

Ndugu wasomaji, kwa mara nyingine tena, Nabii wa Allah amekiri kuwa Wakristo na Waislam hawaabudu Mungu mmoja na Allah ni mungu wa Kipagani.

Katika hiki kijarida tunaangalia ushahidi mbalimbali kuwa, Allah sio Mungu wa Adam, Musa na Mitume wote walio tajwa kwenye Biblia Takatifu.

Kutokana na Surat Al Kafirun iliyoteremka Makka, Nabii Muhammad anakiri kwa mdomo wake kuwa Wakristo na Wayahudi hawaabudu Mungu mbaye anaabudiwa na Waislamu.


Sura 109 1. Sema: Enyi makafiri!  2. Siabudu mnacho kiabudu; 
3. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.  4. Wala sitaabudu mnacho abudu. 5. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.  6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.  

Surah hii inamatatizo mengi sana ambayo ypo wazi kuwa, madai ya Wiaslam ya Mungu wa Wakrist na Mungu wao ni mmoja, ni batili na hayana ushahid.
TATIZO LA KWANZA: Hivi, hii Surah inamzungumzia nani?


(a)            Watu wa Kitabu (Wayahudi, Wakristo na labda Wasebia)?
(b)            Makafir wa Makkah?
Quran hapa imeshindwa kutueleza kuwa, Muhamamd alikuwa naongoa na ummah upi.

TATIZO LA PILI: Hata kama ni moja ya dai la (a) au (b) hapo juu, hii Surah ya 109 imejaa utata na kupinga aya mbaimbali za Quran ambazo zinadai kuwa Wakristo, Wayahudi na wengine wote wanaabudu Mungu mmoja ambaye anaabudiwa na Waislamu.

Surat Al Baqara 62. Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.

2: 139. Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu

Surah 3: 64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.

KWENYE Surat Al Ankabut 46. Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake. 


Kwenye hiyo aya hapo juu, Muhammad anadai kuwa Mungu wa Wakristo, Wayahudi na Waislam ni mmoja.

Hivyo basi, kwenye ushahidi tulio sona unaonyesha kuwa kikundi cha (b) nacho kinaabud Mungu wa Waislam ingawa vilevile kinaabudu miungu mingine na mbalimbali.


Surah 29: 61. Na ukiwauliza; Nani aliye umba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kuti'ii amri yake? Bila ya shaka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanako geuzwa? ***

62. Mwenyezi Mungu humkunjulia, na humdhikishia, riziki amtakaye katika waja wake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. ***

63. Na ukiwauliza: Ni nani anaye teremsha maji kutoka mbinguni, na akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake? Bila ya shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Bali wengi katika wao hawafahamu. ***

Surat An Nahl 35. Na washirikina wanasema: Mwenyezi Mungu angeli taka tusingeli abudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeli harimisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo walifanya walio kuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipo kuwa kubalighisha kwa uwazi? ***

Wapagani tulio wasoma hapo juu, walikuwa wanarudia na au sema maneno ambayo Allah aiyasema kwa Muhammad.


Surat Al Ana’am 107. Na lau Mwenyezi Mungu angeli penda, wasingeli shiriki. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao. ***

Mwisho basi:
Surat Azzumar 3. Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu. Na wale wanao wafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu - Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayo khitalifiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi aliye mwongo kafiri. ***

Katika aya hapo juu, tumejifunza kuwa mungu wa Wapagani ni Allah, na hao miungu wao wengine walikuwa ni wasaidizi katika kumwabudu Allah. Hivyo basi, Allah, ndie aliye kuwa MUNGU WA MKUU WA KIPAGANI.

Kuna aya moja katika Quran ambayo inawasema watu ambao wanamwamini Allah kama muumba wa vitu vyote:

Surah Luqman (31:25). Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Wewe sema: Alhamdulillahi! Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui kama hii aya inazungumzia kundi la A au B, au yote mawili, hii aya ipo wazi kuwa, Muhamamd alijua ni kuwa anamwamini Allah wa Magani wa Mekkah.
Ngoja niweke kwa kifupi hiyo aya:


1.    Wakristo na Wayahudi wanadaiwa kumwabudu Allah.
2.    Wapagani na waislam vilevile nao wanamwabudu Allah, ingawa walikuwa na miungu wengine.
Kama hii ndio dai letu, ni kivipi Surah 109 idai kuwa Makafiri hawamwabudu mungu wa Muhammad na hawaabudu anacho abudu Muhammad?


Kusema kuwa hii aya inahusu waabudu “idols” ni Wapagani peke yao, ni uongo kwasababu zifuatazo:
1.    Waislam wanafahamuje kuwa hii aya iliteremshwa kwa ajili ya Wapagani peke yao?
2.    Hata kama hii aya ilikuwa inawaongelea Wapagani peke yao, je, Quran si inasema kuwa Wapagani walijua kuwa wanamwabudu Allah, na hivyobasi walikuwa wanaabudu alicho kuwa anaabudu Muhammad.

Ni kweli kuwa Muhamamd hakuabudu miungu wao wote, lakini ukweli unabakia palepale kuwa wote Muhammad na Wapagani waliabudu mungu wa Kipagani aitwaye Allah kama ilivyo semwa kwenye sura 109:3.

Kwa mfano, Quran inadai kuwa Muhamamd aabudu ambacho Wapagani waliabudu isipokuwa Allah:

Surat Yunus (10: 104). Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mnayo shaka katika Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnao waabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namuabudu Mwenyezi Mungu anaye kufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.

Surat Ghafir (40:66). Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, zilipo nijia hoja zilizo dhaahiri kutokana na Mola wangu Mlezi. Na nimeamrishwa nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote.
Hizo aya hapo juu zinasema kuwa, Wapagani walikuwa wanamwabudu Allah, pamoja na miungu wengine wa kipagani.

Hivyo basi, leo tumejifunza kwa undani kabisha kuwa Muhammad alikuwa anamwabudu Allah ambaye ni mungu wa kipagani. Jina la Baba yake Muhamamd ni Abdallah, likimaanisha slave of allah. Inafahamika kuwa Muhammad ndie muislam wa kwanza, au sio. Kama hayo madai ni kweli, je, baba yake Muhammad alilipata wapi jina la Badallah kama si yule Allah mungu wa kipagani?

Hakika Allah aabudiwe na Wapagani ni yule yule ambaye aliabudiwa na Muhammad.
Katika Hudma yake

Max Shimba Ministries
@February 9, 2015

No comments:

WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"?

 WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"? Dr. Maxwell Shimba explains: The Word and the Divine Nature – A Comprehensive Exposit...

TRENDING NOW