Monday, December 28, 2015

TOFAUTI KUMI NA SABA (17) KATI YA YESU WA WAKRISTO NA ISA WA WAISLAM




Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” . 


Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”,

Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an.(Qur’an is a post Bible book).

Hoja yetu kwa Waislamu ni hii nani aliyebadilisha jina Yasu’a kuwa Isa?. Jina Yasu’a linashabihiana zaidi na Jina Yehoshua ambalo hilo ni katika lugha ya Kiebrania, na katika Kiyunani lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya anaitwa Iesous (tamka Yesu) tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mwokozi.

Tunasoma hayo katika Math 1:21-23 “ Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa Nabii akisema Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”

Hoja yetu Je Isa a.s naye ni Mwokozi na Imanueli kama alivyo Yesu Kristo?.

Jambo jingine tunalopaswa kulizingatia tunapoangalia tofauti zao ni kuhusu mama zao. Mama yake Yesu Kristo ni Mariam anayetoka katika ukoo wa Yuda. Tunasoma hayo katika kitabu cha Mwanzo 49:10 “ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii”.

Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo.Tunasoma hayo katika Waebrania 7:14 “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani”

Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”.

fafanuzi unaoifafanua aya hii ya 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi “ This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)”

Tafsiri “Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam”
Kwa mujibu wa Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma hayo katika kitabu cha Hesabu 26:59 “Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao”

Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao: ISSA KAUMBWA. Qur’an Suratul Imran, 3:59 “ Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa”

Lakini tusomapo kumhusu YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU.

Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”

Mika 5:2 “ Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”

Yoh: 8:58 “ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”.

Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe

Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”

Kol 1:16-17 “ Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana ; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake”


2) (A) ISSA A.S : BAADA YA KUONDOKA KWAKE, (KAMA WAISLAMU WANAVYOAMINI), HAJAWAHI KUTOKEA KWA NAMNA YOYOTE ILE.

Wednesday, December 16, 2015

UTAMU WA MAISHA YA NDOA

(Sehemu ya Kwanza)

NDOA NI NINI?Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao.
Kwa kuwa si kusudi letu kutafakari sheria za nchi zinasema nini kuhusu Ndoa, tungependa kujikita zaidi katika maana ya Ndoa kwa imani ya kikristo ambayo msingi wake unajengwa katika neno la Mungu. Hata hivyo tunapenda kuweka wazi kwamba Ndoa ni suala la kisheria, na ni muhimu sana kwa wanandoa kutambua kwamba zipo taratibu za kisheria zilizowekwa na serikali zinazosimamia masuala ya Ndoa. Kwa kuwa tumefanyika wana wa Mungu, mwenendo wetu na maisha yetu ya Ndoa yanaongozwa na imani yetu kwa Mungu na si sheria za kibinadamu.
Katika imani ya kikristo, Ndoa inaweza kutafsiriwa kama “AGANO KATI YA MWANAMKE NA MWANAMUME AMBAO WAMEKUSUDIA KWA HIARI KUAMBATANA NA KUISHI PAMOJA KAMA MKE NA MUME KWA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAO.” Jambo la msingi kulitambua hapa ni kwamba Ndoa ya kikristo ni AGANO. Kuna tofauti kubwa kati ya kile kinachoitwa “AGANO” na “MKATABA” kimsingi agano ni zaidi ya mkataba kwa namna nyingi.
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.
Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.
“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana naye”. Mwanzo 2:18.
Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.
Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.
i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe
ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana
iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.
TUWE MAKINI, NDOA SI JAMBO LA MCHEZOKatika maisha ya mwanadamu, kuna mambo mawili yaliyo muhimu zaidi. La kwanza ni uamuzi wa kumfuataYesu na la pili ni uamuzi wa kuoa. Tafakari, kuoa si sawa na kununua shati. Ukilichoka na shati unaweza kununua nyingine lakini, huwezi kumwacha mke wako hata kama ukimchoka. Neno la Mungu linatuonya hatari ya kuoa mwanamke asiye mchaji wa Mungu; Twasoma: “Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi” (Mithali. 21:19). “Kutonatona daima siku ya mvua nyingi, na mwanamke mgomvi ni sawasawa; 16atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo” (Mithali. 27:15-16). Zingatia: Pengine mtu atasema, “mchumba wangu ana imani tofauti, walakini tukioana nitamfundisha.”Lakini ikumbukwe mara nyingi, baada ya kufunga ndoa, watu hubadilika asitake kufundishwa tena.Tukumbuke mfalme Sulemani alikuwa na hekima kuliko wanadamu wote. Walakini, alipata hasara kubwa kwa sababu aliwapenda wanawake wageni wasio mcha Mungu na matokeo yake badala ya kuwafundisha imani yake, “yeye mwenyewe alinaswa na imani yao” (1Wafalme 11:1-4). Basi tujiulize, je sisi tunayo hekima kuliko Sulemani? Ni bora mtu amfundishe mchumba kabla hawajaoana na kuhakikisha kuwa ameamua kumfuata Bwana kwa moyo wake wote na si kwa sababu ya ndoa, ndipo atakapokuwa na amani na furaha katika ndoa yake. Tukumbuke faida moja wapo ya kuoa katika katisa ni kupata mke alifundishwa maadili na wanawake waliomtangulia; Twasoma: “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wautakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie – wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na uwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi,kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe, ili neno la Mungu lisitukanwe” (Tit. 2:3-5). Hivyo ni dhahiri kuna faida kwa mkristo kujipatia mke aliyefunzwa maadili ya ndani ya kanisa. Zingatia: Kuna baadhi ya watu wamevutwa sana na maumbile au mambo ya kimwili ya wachumba wao lakini Biblia inatukumbusha kuchunguza mioyo yao zaidi kuliko sura ya nje; Tasoma: “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa” (Mithali. 31:30). “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana” (Mithali 19:14). Je unazijua sifa za mke mwema? Mungu ameeleza peupe; Soma: (Mithali 31:10-31)
NDOA -TAASISI TAKATIFUNdoa yenye furaha na kuheshimika ni ile ambayo kila mmoja anafahamu na kutimiza wajibu wake katika ndoa kwa mujibu wa nafasi yake. Na hii ndio sharti la msingi kutupelekea kwenye ndoa yenye mafanikio.
i) Kumheshimu mwenzi wako kutokana na hadhi aliyonayo kama MUNGU alivyoagiza.
ii) Heshima inasaidia kutuepusha na ubinafsi na kuongozwa na hisia.
iii) Heshima katika ndoa inachochea mapenzi.
HATARI YA KUOANA NA ASIYE MCHAJI WA MUNGUKama tulivyojifunza hako juu hatari moja wapo ya kuoana na wasio wachaji wa Mungu ni kuishia kuvutwa na upotofu na kuanguka kiimani; Twasoma:”Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi” (Kumbukumbu 7:4). Na hayo ndiyo yaliyomapata Suleima kama tulikwisha kuoona; Soma tena: (1 Wafalme 11:1-4) Tukumbuke ikiwa tutaanguka katika uovu, mwisho wake utakuwa ni kutupwa katika hukumu (adhabu ya milele); Twasoma: “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uachafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui,ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayo fanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” (Galatia 5:19-21) “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauwaji, na wazizi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili” (Ufunuo 21:8) “Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” (Ufunuo 20:14- 15) Zingatia: Ndoa ni kifungo hivyo tukumbuke tunapoana hatuna ruhusa ya kuacha hata kama wenzi wetu ni wabaya vipi; Twasoma: “Lakini wale waliokwisha kuoana nawagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.” (1 Wakorintho 7:10-11) “Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumwe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.” (1 Wakorintho 7:39)
Hivyo ni dhahiri tunaaswa kuwa makini tunapo wachagua wenzi wetu, tukikumbuka ya kuwa kifungo cha ndoa ni mpaka kifo.
NDOA NI KUTOA1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
Hapa tunajifunza
i) Ndoa ni fumbo la ajabu la kiroho linalowaunganisha watu wawili, mwanamume na mwanamke (mst.31)
ii) Ndoa ya kikristo inaliganishwa na uhusiano uliopo kati ya KRISTO na Kanisa (mst.32)
iii) Mpango wa MUNGU katika ndoa unahitaji upendo wa kujitoa sadaka kama KRISTO anavyofanya kwa Kanisa (mst.33)
2. Ndoa ya Kikristo ni kujitoa sio kupokea. Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake mwenyewe. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Hapa tunajifunza
i) Kutokuwa wabinafsi
ii) Unyenyekevu
iii) Roho ya kutoa na kujitoa.
Wewe mume/mke, mahusiano yako na mwenzi wako yakoje? Unampenda mwenzi wako kama KRISTO anavyolipenda Kanisa lake? Kama wewe ni mmojawapo wa wasiofuata kielelezo cha KRISTO katika ndoa usijisikie vibaya kwani hakuna aliye mkamilifu. Hata hivyo wajibu huu haukwepeki kwani ni agizo la MUNGU na lazima kutii maagizo yake, kumpenda MUNGU kwa moyo waklo wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Na kumpenda jirani yako kama nafsi yao. Marko 12:30-31. Hivyo, hii ni nafasi yako ya kumwonyesha mwenzi wako upendo ambao wa muda mrefu ameukosa, upendo ambao KRISTO ameuonyesa kwa kanisa lake.
Max Shimba Ministries

KWANINI HAKUNA NGUVU YA UPONYAJI KATIKA UISLAM? MBONA KATIKA UKRISTO WATU WANAPONA KWA JINA LA YESU?

1. KWANINI JINA LA ALLAH HALINA UWEZO WA KUPONYA MAGONJWA?
2. ALLAH ASHINDWA KUMPONYA MUHAMMAD
3. MAOMBI YA JIBRIL YAGONGA MWAMBA
4. LAKINI JINA LA YESU LINAPONYA MAGONJWA YOTE
5. JE, UMESHA WAI ONA KUNA MKUTANO WA UPONYAJI KATIKA USILAM?

Ndugu msomaji,

Uponyaji ni nini?
Ni tendo la kiimani la kupokea uzima katika roho au mwili kwa njia ya kuombewa,kuwekewa mikono au kulisikia neno sahihi la Kristo Yesu. Tendo hili la kiimani humletea mwamini uzima wa kiroho na afya ya kimwili pale ilipopunguka,kumbuka~wengi walipoponywa udhaifu wa miili yao,waliponywa pia na roho zao.

Hivyobasi, kwanini Allah alipo mtuma Jibril kwenda kumuombea uponyaji Mtume wake Muhammad kwa ugonjwa uliosababishwa na kula sumu, maombi yao hayakufanya kazi?

Hivyo basi, uponyaji haufanywi na mtu awaye yoyote yule isipokuwa Mungu. Hata madaktari bingwa wao hawaponyi bali hutoa tiba tu, mwenye kuponya ni Mungu. Watumishi wa Mungu pekee ndio hufanyika kama daraja au chombo cha kuleta uponyaji ulioachiliwa na Bwana kwa muhusika mwenye kuhitaji.

HEBU SASA TUMSOME ALLAH NA JIBRIL KATIKA JARIBIO LAO LA KUMPONYA MUHAMMAD:
Ibn Sa'd Ukurasa wa 265
Aisha, Mke wa Mtume Muhammad alikuwa akisema, "Wakati Nabii wa Allah alipo kuwa anaumwa, Jibril alikuwa anamwombea Muhammad kwa Allah kwa kusema haya "Katika Jina la Allah ambalo litakuponya kutoka kila magonjwa na maumivu na kutoka kila wenye ubaya nawe na kila wanakuombea ubaya, utapona..

Je, jina la Allah liliweza kumponya Muhammad? Hebu tusome Sahih hadith kama ilivyo letwa na Al Bukhari:


MAJIBU YA MUHAMMAD BAADA YA KUOMBEWA UPONYAJI NA ALLAH/JIBRIL:
Bukhari's Hadith 5.713:
Imesemwa na 'Aisha:
Mtume Muhammad wakati alipo kuwa anaumwa na kuchukuliwa na kifo alikuwa akisema, O Aisha, bado nasikia maumivu makali sana kutokana na chakula nilicho kula kilicho kuwa na Sumu kule Khaibar, na wakati huu nasikia kama nyongo yangu inakatwa kutokana na ile Sumu niliyo kula.

Hivi Mungu anaweza kuomba na ashindwe? Mbona Allah na Jibril maombi yao ya uponyaji kwa Muhammad hayakufanya kazi?


SASA TUMSOME YESU WA KWENYE BIBLIA, JE ALIWEZA KUPONYA WATU?
“ Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia.” Mathayo 8:14-15

Biblia haituambii kwamba Bwana Yesu alimwombea huyu mama,bali tunachoweza kuona ni kwamba Bwana Yesu alimgusa mkono,homa ikamwacha. Mguso tu wa mtu wa Mungu ni dawa tosha,hata kama hakuomba sababu upako ungalimo ndani yake. Maana hata wakina Petro waliweza kuponya wagonjwa kwa kivuli chake tu,sababu ya upako. (Matendo 5:15)


UMUHIMU WA KUWEKA IMANI YAKO KATIKA JINA LA YESU KRISTO
“Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali , saa tisa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao. Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda …” (Matendo ya Mitume 3:1 – 8)

Ukifuatilia historia ya kilema huyu aliyeponywa utaona ya kuwa alikuwa hivyo tangu kuzaliwa, na alipopona alikuwa na umri uliopita miaka arobaini (Matendo ya Mitume 4:22).

Siri ya muujiza huu ilikuwa ni nini? Je! kilema huyu alipona kwa uweza wa Petro na Yohana au kwa uweza wa jina la Yesu Kristo?
Nauliza maswali haya kwa kuwa watu wengi wakimwona mtu anatumiwa na Mungu katika uponyaji wanaweka imani katika mtu huyo badala ya kuweka imani katika jina la Yesu Kristo.

Na ndivyo ilivyokuwa wakati kilema huyu alipopona, watu waliokuwa hekaluni waliwashangaa wakina Petro na Yohana kama vile kilema huyo alipona kwa uwezo wao. Petro alipoona hali hiyo, aliamua kuwaeleza watu hao ukweli ulivyo; alisema hivi;

“Basi (Yule aliyekuwa kilema) alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana. Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kama kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi au kwa utauwa (utakatifu) wetu sisi?” (Matendo ya Mitume 3:11 – 12).

Petro alikuwa anafanya jambo muhimu hapa kwa kusaidia kubadilisha mawazo ya watu ya kufikiria kuwa uwezo uliomponya kilema ulikuwa ni wa Petro na Yohana ambayo haikuwa si kweli. Kama uwezo huu haukuwa wao, muujiza huu siri yake ni nini? Petro aliendelea kusema hivi;

“Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu ….. Na kwa IMANI KATIKA JINA LAKE, JINA LAKE LIMEMTIA NGUVU mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele zenu ninyi nyote” (Matendo ya Mitume 3:13 – 16).

Hebu tafakari maneno haya ya Petro; “Na kwa IMANI KATIKA JINA LAKE JINA LAKE LIMEMTIA NGUVU MTU HUYU….” Wakina Petro na Yohana waliweka imani yao katika jina la Yesu Kristo. Walikuwa na uhakika mioyoni mwao kuwa siri ya miujiza imo katika jina la Yesu Kristo – ndiyo maana walipomkuta huyo kilema walimwamuru asimame kwa jina hilo!

Weka imani yako katika jina la Yesu Kristo ukitaka kuona ishara na miujiza ya Yesu Kristo maishani mwako na kwa wale unaowahudumia pia. Wakijua hili wanafunzi wa kwanza wa Yesu Kristo walipokatazwa “wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu” na Anasi kuhani mkuu, waliomba wakasema; “…Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ISHARA NA MAAJABU vifanyike kwa JINA LA MTUMISHI WAKO MTAKATIFU YESU” (Matendo ya Mitume 4:18,29 – 31)

Ni muhimu kuwaeleza na kuwakumbusha watu umuhimu wa kuweka imani zao katika jina la Yesu Kristo wakitaka kuona mkono wa Bwana ukiponya, ukifanya ishara na miujiza.

Ndugu msomaji, kwanini upoteze muda wako kwa waganga wa kienyeji au wapiga ndumba? Hebu liite Jina la Yesu aliye hai, maana anataka kukuponya magonjwa yako yote.

Kama unasumbuliwa na ugonjwa wowote ule, tafadhali wasiliana nasi kwa kupitia maxshimbaminsitries@gmail.com au tupigie simu (347) 770-4886. Haijalishi ni ugonjwa gani, wewe wasiliana nasi, na hakika Jina la Yesu litakuponya.

Max Shimba Ministries 2015

Monday, December 14, 2015

JINSI YA KUTOA PEPO WABAYA/CHAFU

Maana ya neno pepo linamaanisha, pepo mbaya, shetani, mwovu, mharibifu na mwangamizi. Hao ni malaika waliomuasi Mungu wakatupwa duniani. “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka (Shetani), Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, Yule wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufu 12:7-9.
1. Ili kutoa pepo, kuna mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa:
Ni lazima uwe na nguvu za Roho Mtakatifu.Tunaweza kujifunza kwa Yesu alivyoweza kutoa pepo kwa uwezo na nguvu za Roho. Imeandikwa, “…..awaaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36.
2. Kutoa pepo kwa jina la Yesu. Aliye na amri na mamlaka ya kutoa pepo ni mkristo ambaye amemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo……” Math 16:17. Wale ambao bado hawajamwamini Yesu na kuokoka, Si vyema kujaribu kutoa Pepo kwa sababu hatatoka, vile vile wanaweza kushambuliwa na hao walio na Pepo, kama wale wana wa Skewa, Kuhani Mkuu.
“.....wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nakuapisha kwa Yesu, Yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, Kuhani Mkuu, walifanya hivyo..... na yule mtu aliye pagawa na pepo wachafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.” Mdo 19:13-16.
3. Kufanya maombi kila siku na wakati mwingine kufunga. Bila kufanya hivyo haiwezekani kwa neno lolote, ndio maana Yesu alisema “Lakini kwa namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.” Mat 17:21.
4. Kutoa pepo kwa imani. Unaweza kujifunza kwa wale wanafunzi wa Yesu waliposhindwa kumtoa pepo Yule kijana. Walishindwa kwa sababu ya upungufu wa imani. Wangekuwa na imani wangeweza kumtoa Yule pepo. “Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakisema, mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia kwa sababu ya upungufu wa imani yenu…..” Mat 17:19-20.
5. Kutoa pepo kwa amri na mamlaka. Unaamuru kwa jina la Yesu atoke naye hutoka. Tunaweza kujifunza kwa Mtume Paulo alivyomtoa pepo Yule kijakazi, akaamuru kwa kumwambia Yule pepo, “..…nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu, Akamtoka saa ile ile.” Mdo 16:18.
6. Makosa yanayofanyika kwa wale ambao wanakemea pepo, kwa kuwaambia ninakuangamiza kwa damu ya Yesu, ninakuteketeza kwa moto, au ninakufunga. Kufanya hivyo ni kinyume na mamlaka ya Mungu aliyowapa watoto wake. Kwa sababu hiyo, Mungu hajatupa mamlaka ya kuwaangamiza, Kuwateketeza, wala kuwafunga. Bado pepo watakuwepo katika dunia hii kwa sababu wakati wao wakuhukumiwa na kuteswa haujafika. Ndio maana pepo walipomuona Yesu, “…..wakasema,Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” Mat 8:23.
7.Wakati wa kumhudumia mwenye pepo si sahihi kuongea na mapepo na kuwaliza maswali wametoka wapi, nani akawatuma, ni kwa nini wanamtesa huyo mtu. Hatupaswi kumsikiliza shetani na mapepo yake kwa sababu wao ni waovu na waongo siku zote. “....Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewwe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo” Yn 8:44. Yesu Krsto hakufanya hivyo ambaye ndiye kielelezo chetu katika utumishi, ijapokuwa alimwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na kuteseka siku nyingi alimuuliza swali akitaka kujua jina lake, si jina la pepo.Badala yake pepo waliokuwa wamemtawala yule mtu walijibu wao ni jeshi. “Yesu akamwuliza jina lako nani? Akasema jina langu ni jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia”. LK 8:30.
Pepo atolewapo hutaka kurudi.
Pepo anapotolewa ndani ya mtu aliyempagawa huondoka na baadae hurudi na kuangalia kama anaweza kuingia tena.Ikiwa mtu huyo anaishi maisha ya dhambi huona nyumba ni chafu na kuingia."Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, aspate. Halafu husema, nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda akachukua pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya". Mt12:43-45.

ZIJUE AHADI ZA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO

Mungu hutimiza ahadi zake. Imeandikwa katika 2Wakorintho 1:19-20 "Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yaani mimi na Silwano na Timotheo hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa sisi."
Mungu hazirudishi ahadi zake au kuzibadilisha. Imeandikwa katika Zaburi 89:34 "Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno lililotoka mdomoni mwangu."
Hakuna mojawapo ya ahadi za Mungu ambazo hazijatimika. Imeandikwa katika Yoshua 23:14 "Angalieni mimi nimekwenda njia ile waendayo watu wote wa ulimwengu...... Mungu wenu katika habari zenu yote yametimia kwenu hapana neno lo lote mlilopungukiwa."
Tumeahidiwa uzima wa milele. Imeandikwa katika 1 Yohana 2:25 "Nahii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani uzima wa milele."
Mungu aweza kufanya mambo yasiyowekana. Imeandikwa katika Luka 18:27 "Akasema yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa mungu." Tume ahidiwa moyo mpya na maisha mapya Imeandikwa Ezekieli 36:26 "Mimi nitawapa moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama." Ametuahidi kutusamehe dhambi zetu. Imeandikwa katika 1Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."
Ametuahidi tunda la roho. Imeandikwa katika Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la roho ni upendo, furaha amani, uvumilivu, utu wema fadhili uaminifu, upole, kiasi juu ya mambo kama hayo hakuna sheria."
Ametuahi kututoa katika hofu. Imeandikwa katika Zaburi 34:4 "Nilimtafuta Bwana akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote."
Ameahidi wokovu. Imeandikwa katika Isaya 49:25, "... Kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu."
Ameahidi Roho mtakatifu Imeandikwa Luka 11:13 "Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho mtakatifu hao wamwombao?."
Atatutimizia mahitaji yetu. Imeandikwa katika Wafilipi 4:19, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu."
Hatatunyima lililo jema. Imeandikwa katika Zaburi 84:11 "Kwa kuwa BWANA, Mungu ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu."
Ametuahidi hekima. Imeandikwa katika Yakobo 1:5 "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa."
Mungu ametuahidi amani. Imeandikwa katika Isaya 26:3 "Utamlida yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini."
Mungu ametuahidi kutuepusha na majaribu. Imeandikwa katika 1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya binadamu; ila Mungu ni mwaminifu; hatawacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wakutokea ili muweze kustahimili."
Tumeahidiwa afya njema na tiba. Imo katika Biblia, Yeremia 30:17 "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA..."

YESU NI MUNGU AMBAYE ANAPONYA MAGONJWA YOTE

Yesu alisema kwamba ishara moja itakayofuatana na waaminio ni kwamba wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapona (ona Marko 16:18).
[Yesu] Akawaambia, Enendeni ulimwengu mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya (Marko 16:15-18).
Mtumishi afanyaye watu kuwa wanafunzi, akiwa anaiga huduma kamilifu ya Kristo, hakika atatumia vipawa vyake kuendeleza huduma ya uponyaji wa Mungu katika eneo lake la ushawishi. Anajua kwamba uponyaji wa Mungu hukuza ufalme wa Mungu kwa njia mbili. Kwanza – miujiza ya uponyaji ni matangazo mazuri sana kwa Injili, kama mtoto yeyote anayesoma Injili au kitabu cha Matendo atakavyoelewa (ingawa watumishi wengi wenye madigirii makubwa wanaonekana hawaelewi). Pili – wanafunzi wenye afya njema hawazuiwi kufanya huduma kwa magonjwa binafsi.
Pia, mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi anahitaji kuwa makini kwa wale katika mwili wa Kristo wanaohitaji uponyaji, ila wana shida ya kupokea. Mara nyingi wanahitaji mafundisho ya taratibu na kutiwa moyo kwa upole, hasa kama wamefikia mahali pa kupingana na ujumbe wowote wa uponyaji. Mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi anakabiliwa na uchaguzi: anaweza kuepuka kufundisha kuhusu uponyaji wa Mungu moja kwa moja. Akifanya hivyo, hakuna atakayekwazika wala hakuna atakayeponywa. Au, anaweza, kwa upendo sana, kufundisha somo hilo na kudiriki kuwakwaza wengine huku akiwsaidia wengine kupokea uponyaji. Mimi binafsi nimeamua kufanya la pili, nikiamini kwamba ni kufuata mfano wa Yesu.
Uponyaji Pale Msalabani
Mahali pazuri pa kuanza kujifunza kuhusu uponyaji wa Mungu ni katika sura ya hamsini na tatu ya kitabu cha Isaya, ambayo huhesabika kuwa unabii kuhusu Masiya. Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Isaya anaeleza vizuri sana juu ya kifo cha Yesu cha kujitoa dhabihu na kazi ambayo angetimiza msalabani.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu. Lakini tuimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, na BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi sote (Isaya 53:4-6).
Kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu, Isaya alitangaza kwamba Yesu alibeba huzuni na masikitiko yetu. Tafsiri nzuri ya lugha ya asili ya Kiebrania inaonyesha kwamba Yesu alichukua magonjwa na maumivu yetu.
Neno la Kiebrania huzuni katika Isaya 53:4 ni neno choli, ambalo pia linapatikana katika Kumbu. 7:15; 28:61; 1Wafalme 17:17; 2Wafalme 1:2; 8:8; na 2Nyakati 16:12; 21:15. Katika maandiko haya yote linatafsiriwa kama magonjwa au maradhi.
Neno masikitiko katika Kiebrania ni makob, ambalo pia linapatikana katika Ayubu 14:22 na 33:19. Pote hapo linatafsiriwa maumivu.

YESU NI MUNGU NA ANATAKA KUKUOKOA

Watu wengi wanaelewa kuwa Yesu alikuwa mtu ambaye aliishi Israeli miaka 2000 iliyopita. Takribani kila dhehebu ulimwenguni lamchukulia Yesu kama mwalimu mwema/nabii. Huku hayo mambo yakiwa kweli kuhusu Yesu, hayaangazii kabisa Yesu kwa ni nani, ama kuelezea jinzi au kwa nini Yesu aokoa. Yesu ni Mungu katika mwili wa binadamu (Yohana 1:1,14). Yesu ni Mungu, alikuja ulimwenguni kama mwanadamu wa kweli (1Yohana 4:2). Mungu alikuja akawa mwanadamu katika Yesu ili atuokoe. Hiyo yaleta swali lifuatalo: Ni kwa nini tunaitaji kuokolewa?
Yesu anawaokoa wale wote wanaopokea tuzo lake la wokovu. Yesu anawaokoa wale wote wanaomwamini katika dhabihu yake pekee kama fidia ya dhambi (Yohana 3:16; Matendo 16:31). Huku Yesu kama dhabihu ilikuwa kamilifu na yatosha kulipia dhambi zote za binadamu, Yesu pekee ndiye aweza kuokoa wale pekee wanaoipokea zawadi yake (Yohana 1:12)
Kama sasa unaelewa yamaanisha nini Yesu aokoa, na unataka kuweka imani kwake kama mwokozi wa maisha yako, akikisha kwamba unaelewa na kuamini yafuatayo, na kama hatua ya imani, nena maneno yafuatayo,
SALA YA TOBA
Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako. Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.
Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa wewe kuokoka. Lakini napenda kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma Wakolosai 1:13,14 na Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na Yohana 3:7. Ni vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.
Kwa hiyo kama unataka kuokoka - tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa sauti sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu.
Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Baada ya kuokoka
Unapoanza maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:
1.Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3.Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4.Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5.Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
Ukipenda unaweza kuniandikia kwa anwani hii hapa chini juu ya uamuzi uliofikia leo wa kuokoka, ili tumshukuru Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia, tukutumie maandiko mengine ya kukusaidia: maxshimbaministries@gmail.com
Max Shimba Ministries

UTHIBITISHO 12 KUWA ALLAH SIO MUNGU

Leo nitawapa Sababu 12 kwanini allah sio mungu.
1. ALLAH NI MUNGU ASIYE NA JINA KAMILI
Qr. 17 au surat Bani Israil 110 (Wana wa Israil)
Sema; muombeni (Mwenyenzi Mungu) kwa (jina la) Allah au muombeni (kwa jina la) Rahman. Kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa). Kwani ana majina mazuri mazuri………
2. ALLAH NI MUNGU MWENYE MAADUI AMBAO NI WAKRISTO NA WAYAHUDI
mungu wao ana maadui wake ambao ni wakristo na wayahudi
Qr. 4:51 na 57 (surat Al Maida)
Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika hao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
3. ALLAH NA WAISLAM WOTE KUINGIA JEHANNAM
Wafuasi wote wa Allah wanangojea moto wa jehanam kisha waokolewe waislam baadaye kutoka motoni
Qr. 19:70-72
Tena hakika sisi tunawajuwa vyema Zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia.
Hiyo ni hukumu ya Mola wako mlezi ambayo lazima itimizwe. Kisha tutawaokoa wale waliomcha Mungu; na tutawaacha madhalimu humo hali wamepiga magoti motoni.
4. ALLAH ANAINGIA JEHANNAM WAKATI MUNGU WA BIBLIA HATA INGIA JEHANNAM
Allah wao ataionja jehanamu pia
Qr. 50 au Surat Qaf 30 (kuapa)
Siku tutakayoiambia Jahanamu, ‘Je! Umejaa?’ Nayo itasema ‘Je kuna ziada (zaidi? Naije tu!
Imesimuliwa na Anas kuwa: Mtume alisema watu watatupwa jahanamu, Naye Allah ataiuliza jahanamu akisema je umejaa nayo jahanamu itasema kwani kuna nyingine zaidi na ije tu? Mpaka Allah atakapo ingiza mguu wake nayo jahanamu itasema inatosha! Inatosha
5. ALLAH HANA UWEZO WA KUPONYA MAGONJWA WAKATI MUNGU WA BIBLIA ANAPONYA WAGONJWA!!
Kwanini Allah alipo mtuma Jibril kwenda kumuombea Muhammad ugonjwa uliosababishwa kula sumu, maombi yao hayakufanya kazi?
Ibn Sa'd Ukurasa wa 265
Aisha, Mke wa Mtume Muhammad alikuwa akisema, "Wakati Nabii wa Allah alipo kuwa anaumwa, Gibril alikuwa anamwombea kwa Allah kwa kusema haya "Katika Jina la Allah ambalo litakuponya kutoka kila magonjwa na maumivu na kutoka kila wenye ubaya nawe na kila wanakuombea ubaya, utapona..
Cha kushangaza, Allah na Jibril pamoja walishindwa kumponya Muhammad, huu sasa ni Ushahid tosha kuwa Allah hana uwezo wa kuponya bali ndie anaye tupia watu Magonjwa.
6. ALLAH NDIE HUWAPA WATU MAGONJWA

USIKUBALI KUWA MPUMBAVU KWA KUKATAA KUWA HAKUNA MUNGU NA KUWA YESU NI MUNGU

Kuna imani nyingi sana hapa duniani, zingine zinadai kuwa "Hakuna Mungu" eti, kwasababu wameshindwa kuongea nae na au kumwona; Imani zingine zinadai kuwa "Hakuna Mungu" eti kwasababu Sayansi inashindwa kuhakikisha uwepo wake scientifically; Imani zingine zinadai kuwa, kivipi Yesu awe Mungu na biandamu kwa wakati mmoja, zinadai eti, Mungu halali, wala hali chakula, lakini wakati huo huo wanakiri kuwa Mungu anaweza kufanya jambo lolote lile atakalo; Haya yote ni madai ambayo hawawezi kuyathibitisha.
Hebu tusome Biblia:
2 Samweli 2:31-34 na Zaburi 14:1 ‘Mpumbavu amesema moyoni, mwake hakuna Mungu…..’ Mpenzi msomaji naamini unaendelea vema kwa ujumla kimwili na kiroho. Katika mwezi huu nataka niseme nawe juu ya kifo cha kipumbavu.
Mpumbavu ni nani? Kibiblia ni mtu yoyote aliyekataa kuwa na ufahamu au elimu ya Mungu ndani yake. Mtu aliyekataa uwepo wa Mungu au kuwa na Mungu maishani mwake.
Hivyo basi mpumbavu ni mtu ambaye moyoni mwake amesema hakuna Mungu. Mauti inayomkuta mtu ambaye amekana elimu au ufahamu au uwepo wa Mungu katika maisha yake ni mbaya sana, maana mwisho wake ni Jehannam. Mauti inayommkuta mtu kabla hajakubali uwepo wa Mugu katika maisha yake. Kifo kinachomkuta mtu ambaye hajampa Mungu nafasi ya utawala moyoni mwake mwisho wake ni ziwa la moto. Je wewe unataka kuishi milele yote kwenye ziwa la moto?
YESU ANAKIRI KUWA YEYE NI MUNGU KATIKA KITABU CHA UFUNUO:
Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.
Ukikataa kuwa Yesu sio Mungu, basi wewe ni mmoja wa lile kundi la Wapumbavu. Katika Zaburi, tumeambiwa kuwa Mpumbavu kasema kuwa Hakuna Mungu.
Tujifunze kwa Abneri. 2 Samweli 2:22-39 ukisoma vema hapa utaona habari za shujaa mmoja aliyeitwa Abneri. Kwa kifupi Abneri alikuwa;
Kiongozi wa majeshi ya Sauli, mpinzani mkubwa wa Daudi, baadaye alipelekea Daudi kuitawala Israeli yote, Alimwua Asaheli shujaa wa Daudi ndugu yake Yoabu, kiongozi wa majeshi wa Daudi. Na mwishowe Yoabu ndiye aliyemwua Abneri ili kulipiza kisasi cha kifo cha nduguye.
Sasa baada ya kifo cha Abneri, ndipo Daudi akamlilia Abneri akasema, ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu?, mikono yako haikufungwa wala miguu yako haikutiwa pingu; aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.
Ukiendelea kusoma habari hii utaona kwamba siku ile Daudi alikataa kula akimliilia Abneri, akisema hamjui ya kuwa mkuu mmoja, naye ni mtu mkubwa ameanguka leo katika Israeli?
Je kwa mazingira ya leo, mtu anawezaje kufa kifo cha kipumbavu?Unaposhindwa kutumia fursa zilizopo kuiponya nafsi yako matokeo yake ni kifo cha kipumbavu. Abneri hakufungwa mikono wala miguu lakini aliuawa. Daudi alikuwa akimuuliza Abneri kwa nini usitumie mikono na miguu yako kuiponya roho yako? .
Katika Zaburi 14;1 TUMEONA MPUMBAVU NI MTU YULE AMBAYE MOYONI MWAKE AMESEMA HAKUNA MUNGU, kwa lugha nyepesi amekataa kuwa na Mungu moyoni mwake na kwa sababu hiyo amekataa uongozi wa Mugu katika maisha yake.

UTHIBITISHO 10 KUWA YESU NI MUNGU

“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!
Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.” Kwa madai haya hata kwenye Qurana hawawezi thibitisha kuwa Allah Allah ni mungu, zaidi ya hapo, hata Utume wa Muhammad unakuwa kwenye njia panda, maana hakuna aya kwenye Quran Muhammad anasema mimi Muhammad ni mtume wa Mungu.
Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).
Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.

1. YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUZALIWA
Ufuatao ni ushahidi wa kibiblia kwamba YESU KRISTO ni Mungu.
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.
NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).
Mwanadamu yuko kwa sababu Mungu alisababisha awepo. Gari liko kwa sababu injinia au mbunifu alisababisha liwepo. Nyumba ipo kwa sababu fundi alisababisha iwepo. Lakini Mungu YEYE YUKO TU!! Hayupo kwa kusababishwa na yeyote! Ndiyo maana akasema MIMI NIKO AMBAYE NIKO! Yesu ni NIKO. Kwa hiyo, Yeye ni Mungu.
2. YESU NA BABA NI WAMOJA
Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
Waislamu wana msemo wao kwamba eti, Yesu na Mungu ni wamoja katika malengo, si katika asili yao. Basi huwa nawauliza swali kuhusu aya ifuatayo ya Isaya, nao wanazimika na kukosa jibu:
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu MTOTO amezaliwa, Tumepewa MTOTO MWANAMUME; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, Mfalme wa amani.
Aya hii iko wazi kabisa. anayetajwa ni Yesu kwamba Yeye ni Mungu mwenye nguvu.
Yohana 14:9
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Maneno haya Yesu aliyasema baada ya kuulizwa swali lililo wazi kabisa, ambalo lilikuwa na lengo la kumjua MUNGU BABA! Imeandikwa: Filipo akamwambia, Bwana, UTUONYESHE BABA, yatutosha. Ndipo Yesu akajibu waziwazi: ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA. Maana yake ni kuwa, “Mimi ndio Baba mwenyewe.”
3. YESU NI MWANZO NA MWISHO
Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.
4. YESU NI NENO
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.
Andiko hili Waislamu hawalipendi kabisa. ni kwa sababu liko wazi mno. Yesu ni Neno; na Neno ni Mungu; hivyo, Yesu ni Mungu!
5. THOMASO AKIRI KUWA YESU NI MUNGU, NA YESU HAKUKATAA KUITWA MUNGU
Yohana 20:28
Tomaso akajibu, akamwambia, BWANA WANGU NA MUNGU WANGU!
Tomaso aliposema hivi, Bwana Yesu hakukanusha na kusema, “Mimi sio Mungu.” Badala yake: Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. (Yoh 20:29).
Kama Thomaso alikuwa muongo, kwanini Yesu hakukataa kuitwa Mungu. Imani zote zinakiri kuwa Yesu hakufanya dhambi na hakuwa na dhambi.
6. DAMU YA YESU INAMAMLAKA
Matendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.
Ni Mungu gani mwenye damu huyu? Jibu liko wazi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ndiye aliyetoa uhai wake na kumwaga damu yake msalabani; na hapo ndipo alipoanzisha Kanisa.
7. KATIKA YESU, KILA KITU KILIUMBWA
Wakolosai 1:16
Kwa kuwa KATIKA YEYE VITU VYOTE VILIUMBWA, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Katika Yeye Yesu vitu vyote viliumbwa. Ina maana kuwa vitu vyote vilitokana na Yesu; maana Yesu ni Neno la Mungu. Na tunajua kuwa Muumba wa vitu vyote ni Mungu; hivyo, Yesu ni Muumba – Yeye ni Mungu!!
8. KATIKA YESU, UNAKAA UTIMILIFU WA MUNGU
Wakolosai 2:9
Maana KATIKA YEYE UNAKAA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.
Sisi sote ni watu wasio wakamilifu. Tunaanguka tena na tena kwenye dhambi. Kwa hiyo, hakuna mwanadamu wa kawaida ambaye anaweza kujigamba kwamba yeye ametimia kama alivyo Mungu. Lakini katika Yesu “utimilifu WOTE wa Mungu unakaa.” Kwa nini? Kwa sababu Yeye ndiye Mungu huyohuyo.
9. YESU NI MUNGU PAMOJA NASI "EMMANUEL"
1Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Ni Mungu gani aliyedhihirishwa katika mwili? Jibu liko wazi. Ni Yesu Kristo peke yake.
10. YESU NI MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Tito 2:13
….tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Yesu Kristo ni Mungu Mkuu!!
Shida KUU ya Waislamu ni hii: Wanampima Mungu kwa vigezo vya kibinadamu. Mungu anasema: Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? (Yer 32:27)
Jibu liko wazo. HAKUNA!
Lakini utakuta Waislamu wanauliza maswali ya ajabu sana. Eti, kama Yesu ni Mungu, wakati amekufa, nani alikuwa anaangalia dunia?
Hili ni swali linalofaa kuulizwa juu ya kiumbe. Kama tungesema kuwa mwanadamu fulani alikuwa amekufa, ndipo kuna mantiki kuuliza kwamba, wakati amekufa nani alikuwa anatunza familia yake? Maana hili ni swali linalohusu tabia za kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuwa mahali kuwili au zaidi kwa pamoja. MUNGU SI MWANADAMU! ANAWEZA YOTE – NA HASA MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO!
YESU NI MUNGU MILELE NA MILELE!!
HALELUYA!!
Tafakari
Hoji mambo
Chukua hatua!

UPONYAJI KATIKA JINA LA YESU

Leo ninaweka aya kadhaa zinazo tupa mamlaka ya kuombea wagonjwa.
Mungu akubari mpendwa na pokea uponyaji wako leo katika Jina la Yesu aliye hai.
Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote. - [Zaburi 34:19]
Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. - [Yakobo 5:14-16]
Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. - [Zaburi 107:20]
Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana. - [2 Wafalme 20:5b]
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. - [Yeremia 30:17a]
Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. - [Isaya 40:29]
Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, - [Zaburi 103:3]
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. - [Isaya 53:5]
akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye. - [Kutoka 15:26]
Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika. - [Luka 17:14b]
Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. - [Mathayo 10:1]
Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini. - [Malaki 4:2a]
Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka. - [Matendo ya Mitume 9:34]
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. - [Marko 16:17-18]
mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe. - [Waebrania 12:13]
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. - [2 Wakorintho 12:7-9]
Baada ya kusoa hizo aya, sasa pokea uponyaji wako katika Jina la Yesu alie hai.
Max Shimba Ministries 2015

MAOMBI YA USHINDI KWA MAISHA YAKO

Baba katika Jina la Yesu.
Laana zote nilizo tupiwa na wabaya wangu zimeshindwa kwa jina la Yesu na nazivunja na kuzisambaratisha kwa Damu ya Yesu. Mshindwe wote mnao tuma laana kwangu katika Jina la La Yesu.
Nawavunja na kuwaharibu na kuwakatakata Wachawi wote kwa damu ya Yesu.
Nasambaratisha kila neno la uovu lililosemwa juu yangu na familayangu katika jina la Yesu.
Naharibu na kuisambaratisha madhabahu yenu mliyo fanyia kafara kwa damu ya Yesu.
Navunjavunja na kubomoa kila uovu na uchawi mnaonifanyia katika jina la Yesu.
Nairudisha misukule yote na majini yote yawarudie nyie na kuwalipa dhambi zote mnazo fanya katika jina la Yesu.
Naharibu kila uchawi, kila urogi, kila ndumba kila aina ya uovu ambao mnaufanya ili uniumize mimi na familia yangu katika jina la Yesu.
Nawateketeza kupitia damu ya Yesu Wachawi wote walio tumiwa kunitumia uchawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwaharibu majini yote yaliyo tumwa kuja kufanya kazi hiyo waliyo tumwa na Wachawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwauwa Makuhani wote ambao walienda kunishitaki kwa Wachawi ili waniharibie maisha, nawateketeza kupitia damu ya Yesu. Nawachoma kwa Moto wa Roho Mtakatifu katika Jina la Yesu.
Nateketeza aina zote za vyombo vya kichawi vilivyo tumiwa kuja kunichunguza katika jina la Yesu.
Naharibu fikra zao zote ambazo wanazitumia kufanya kazi zao za kichawi katika jina la Yesu.
Nafuta kumbukumbu zoote zangu ambazo wamewapa Mashetani, Majini, Roho chafu, nafuta hizo kumbukumbu kwa kutumia damu ya Yesu, katika jina la Yesu aliye hai.
Nawateketeza waweka kumbukumbu wa kimashetani kupitia damu ya Yesu aliye hai. Naharaibu na kuchoma kupitia moto wa Roho Mtakatifu makabrasha yote yenye kumbukumbu zangu katika jina la Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuharibu maisha yangu na ubomoa kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuniua nauvunja na kuuteketeza kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili kuja kuiba mali zangu, nauvunja na kuubomoa na kuuharibu kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanya kuja kuniharibia familia yangu, nausambaratisha na kuuvunja na kuubomoa katika jina la Yesu.
Kila neno la kichawi lililo tumwa ili kuja kuniharibia, kunidhihaki, kunitendea mabaya nalirudisha kwa aliye lituma katika jina la Yesu.
Kila uovu, uchawi, wanga, ndumba, ramli, yaliyo tumwa kuja kwangu navunja yote hayo kupitia damu ya Yesu na katika Jina la Yesu.
Nyota yangu ambayo wanaita nairudisha kupitia damu ya Yesu. Nyota yangu ya baraka nailinda na kuzungushia na kuizingira na damu ya Mwana Kondoo katika jina la Yesu.
Namteketeza yule mtu aliye kuja kuiba nyota yangu katika jina la Yesu.
Nateketeza mbinu zote wanazo tumia ili kuja kuiba nyota yangu katika jina la Yesu.
Nateketeza wivu wao, chuki yao, laana zao, maovu yao na kila aina ya uchafu ambao wanao kwa ajili yangu katika jina la Yesu.
Naizungushia na kuizingira nyumba yangu na damu ya Yesu.
Naishungushia na kuizingira familia yangu na damu ya Yesu.
Nashungushia na kuzingira maisha yangu yote na damu ya Yesu.
Navunja laana zote zilizo semwa na mabau zangu katika jina la Yesu.
Navunja laana zato ambazo zilisemwa bila ya mimi kufahamu, nazivunja na kuziharibu kupitia damu ya Yesu na katika jina la Yesu.
Narudisha kila mali walizo ziiba kutoka kwangu katika jina la Yesu.
Narudisha kila baraka walizo ziiba kwangu katika jina la Yesu.
Narudisha amani na upendo katika familia yangu.
Damu ya Yesu ipo juu ya Maisha yangu na inasafisha kila uovu, kila uchawi unaaribiwa na damu ya Yesu katika jina la Yesu.
Leo hii mtaiona Nguvu iliyopo katika damu ya Yesu.
Katika Jina la Yesu aliye hai ninaomba.
Amen
Max Shimba Ministries Org

MAOMBI YA KUFUNGA MWAKA NA KUANZA MWAKA MPYA 2016 KWA BARAKA TELE KUTOKA KWA MUNGU MKUU, YESU KRISTO ALIYE HAI

Ndugu msomaji na mpendwa katika Bwana. Bwana Yesu apewe sifa.
Mpendwa, yawezekana umekuwa ukiishi bila kutambua uwezo wa jina la Yesu katika kukuonyesha mwelekeo wa maisha yako.Je, unahitaji mwelekeo mpya katika maisha yako? Je, unahitaji kujua njia ya kutoka katika hali uliyonayo?
KAMA UMECHOKA NA MAISHA YA TABU, KAMA UMECHOKA KUISHI NA MAGONJWA, KAMA UMECHOKA KUWA MASKINI, KAMA UNAHITAJI KAZI, BIASHARA YAKO IFANIKIWE N.K. BASI HUU UJUMBE NI WAKO.
Napenda kukufahamisha kuwa, tupo katika Maombi kila siku mpaka tutakapo maliza mwaka huu wa 2015. Nafahamu wengi mmepata baraka tele katika Mwaka wa 2015 na labda wengi mmlikuwa katika mashindano na vita kubwa na nguvu za giza. Kumbuka USHINDI ni wetu katika Jina la Yesu.
Mpendwa , pengine hali ya maisha uliyonayo imekufanya ukate tamaa na kujiona kwamba hakuna njia ya kukufanya utimize furaha ya ndoto zako. Je, unahitaji njia ya kuishi kwa amani na furaha; njia ya kuwa na mahusiano mazuri katika ndoa yako; njia ya kuwa na mahusiano mazuri na ndugu zako, kazini kwako, kwenye biashara yako; unahitaji njia ya kuacha ulevi wa pombe na madawa ya kulevya, njia ya kuacha kuabudu sanamu, njia ya kuacha uongo, njia ya kuacha uzinzi, njia ya kuacha uchawi, njia ya kuacha tamaa ya mali zisizo halali; njia ya kuponywa maradhi, njia ya kupata utajiri, njia ya kupata kazi, njia ya kupata mtaji , njia ya kutoka kwenye madeni, njia ya kupandishwa cheo, njia ya kutimiza ndoto zako? Yesu ni njia ya kila mahitaji yetu hapa duniani, pia yeye ni njia ya kutufanya tujue kweli ya neno lake na tuweze kuurithi uzima wa milele.
Kama unahitaji lolote lile ambalo unataka upokee jibu kutoka kwa Mungu Mkuu, Yesu aliye hai, basi nakusihi ututumie hilo hitaji lako haraka ili tuwe pamoja katika maombi katika muda huu wa kumaliza mwaka wa 2015. Tuma ombi lako kupitia barua pepe maxshimbaministries@gmail.com
Matayo 7:7-11Neno: Biblia Takatifu (SNT):
7 “Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. 8 Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.
9 “Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?
Yesu katika Matayo hapo juu anakwambia "OMBENI NANYI MTAPEWA' Sasa Mpendwa unasubiri nini kumwomba Mungu Mkuu? Au unapenda kuwa katika matatizo na shida? Shetani teyari alisha wekwa chini ya miguu yetu.

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW