Tuesday, December 2, 2014

YESU KRISTO KWA MATAIFA YOTE

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake 

Hebu tusome Neno la Mungu katika Injili kama ilivyo letwa kwetu kupitia Matayo.

Matayo 28: 16 Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Yesu alikuwa amewaagiza. 17 Walipomwona, wakamwabudu, lakini baadhi yao wakaona shaka. 18 Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, 20 nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.’’ Amen.

NDUGU ZANGUNI:

Tumepewa kazi na Yesu Kristo ya kuihubiri Injili kwa Mataifa yote. Hii kazi ya kuhubiri Injil ni ya Wakristo wote, haijalishi wewe ni Meneja, Mwalimu, Mwanafunzi, Mchungaji, Polisi, Fundi, Dereva, na nk. Yesu amepewa Mamlaka yote Mbiguni na Duniani. Ushindi ni wetu katika jina lake lililo zaidi ya majina yote.

Mashetani yote yanatetemeka wanapo sikia Jina la Yesu.

Misukule yote inaachia na watu wanakuwa huru wanapo sikia Jina la Yesu.

Walio fungwa na Nguvu za Giza wanakuwa Huru katika Jina la Yesu.

Walio potea katika dhambi wanawekwa Huru kupitia Jina la Yesu.

Wagonjwa wanapona katika Jina la Yesu.

Jina la Yesu lina Mamlaka yote, duniani na Mbinguni.

Twendeni na tufanye kazi ya Bwana katika Mataifa yote.

Yesu ni yule yule, Jana, Leo na Hata Milele.

Mungu awabariki sana

Katika Huduma Yake.

Max Shimba

Max Shimba Ministries

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW