Monday, December 1, 2014

Jeneza la Kuhani Mkuu Aliyesimamia Hukumu ya Yesu Lagundulika

kayafa
Kayafa alikuwa ni kuhani mkuu wa Wayahudi kuanzia mwaka 27 hadi 36 baada ya Kristo.  Yeye alikuwa ni Sadukayo (Matendo 5:17). Alikuwa ni adui mkubwa wa Yesu Kristo.
Kayafa ndiye aliyetoa pendekezo kwa makuhani na wakuu wengine wa Kiyahudi walikokutana kujadiliana juu ya muujiza wa Bwana Yesu wa kumfufua Lazaro. Imeandikwa:
Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.
Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.
Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote;
wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. (Yohana 11:47-50).
Alikuwa ni Kayafa pia aliyemhoji Bwana Yesu baada ya kukamatwa. Imeandikwa katika Mathayo 26:57-66:
57 Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee.
58  Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.
59  Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;

60  wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa uongo wengi.
61  Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.
62  Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?
63  Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.
64  Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.
65  Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;
66  mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa.
Baada ya Bwana Yesu kufufuka kwa wafu na kupaa kwenda mbinguni, mitume wake ndio walioendeleza kazi yake ya kueneza Injili ya ufalme wa mbinguni. Kayafa aliendeleza chuki yake hata kwa mitume wa Yesu. Imeandikwa katika Matendo ya Mitume 4:1-6:
1  Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,
2  wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.
3  Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.
4  Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.
5  Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu,
6  na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.
Kuna watu wengi wanaotilia shaka Biblia na hata watu wa dini zingine wanasema kuwa Biblia imepotoshwa.
Mwaka 1990 mabuldoza yalikuwa yakisafisha eneo kwenye sehemu moja kusini mwa Yerusalemu ili kujenga kituo cha michezo ya watoto. Katika uchimbaji ule, jembe la buldoza lilitoboa mahali ambapo kulikuwa na sehemu ya kuzikia wafu ya zamani.
Kazi ilisimama na wataalamu wakaitwa. Wataalamu hao walikuta humo ndani majeneza yam awe (ossuaries). Haya ni majeneza ambayo yalitumika kuhifadhi mifupa ya wafu.
Wayahudi walikuwa na kawaida kwamba mtu akifa, mwili wake huweka kwenye mapango ya makaburi kwa mwaka mzima. Kisha baada ya kuoza na kubakia mifupa tu, mwaka mmoja baadaye wanakuja kufungua kaburi lile na kuweka mifupa yake kwenye hilo jeneza la jiwe. Na baadaye ndugu wengine wa familia wakifa, nao mifupa yao iliwekwa kwenye jeneza hilohilo. Linakuwa ni jeneza la familia.
Jeneza mojawapo katika kaburi hili lilikuwa limepambwa sana kwa michoro mizuri. Juu ya jeneza hilo kuliandikwa jina la Kayafa.
Caiaphas
Wasomi wa mambo ya kale waliochunguza mifupa iliyokuwamo humo wanakubaliana kwamba huyo alikuwa ni Kayafa kuhani.
Unaweza kusoma zaidi HAPA.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW