Saturday, December 13, 2014

Eti Biblia inataja mashehe, kwa hiyo inaunga mkono Uislamu!




Wahubiri wa ‘injili’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha quran kupitia Biblia. Nasema ‘kuhaha’ kwa sababu hakika kabisa wana juhudi kubwa mno lakini inasikitisha kwa sababu hakuna hata siku moja waliyowahi kusema jambo lenye ukweli kibiblia linalounga mkono quran kama wasemavyo wao – Mungu ni shahidi yangu. Mara waseme Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia; mara waseme Yesu aliposema kuwa ataletwa Msaidizi basi alimaanisha Muhammad, n.k. Ni kituko kimoja baada ya kingine. Na wanayemdanganya ni wao wenyewe pamoja na Wakristo wachache wasiojua Biblia.


Kwa msingi huohuo, wanasema eti Biblia imewataja mashehe; na kwa hiyo kwao huo ni ushahidi kuwa uislamu ulikuwapo tangu zamani.

Acha ninukuu hoja ya mmoja wao kama ilivyo, kuhusiana na suala hili, kisha kama kawaida, utaona jinsi hoja hiyo inavyosambaratika mbele za nuru ya Kristo, yaani neno lake.

Mtu huyu anasema:
Swali kwenu nyinyi ambao hamjabahatika kuwa waislam, yaani Wakristo. Kama uislam uliletwa na muhammad s.a.w, vipi masheikh watajwe ndani ya agano la kale?
Ndivyo walivyosimama mikutano miwili yao walioshukuru nyumbani mwa mungu, na mimi, na nusu ya mashehepamoja nami.” (Nehemia 12:40)
Mkristo jiulize mwenyewe hili swali; mashehe ni viongozi wa dini ipi? waislam...!? au wakristo?
Mwisho wa kunukuu.

Hapa huyu ndugu wa Kiislamu anaongea kwa ujasiri kabisa na kwa kituo. Na unaona kabisa kuwa moyoni mwake anawaza, “Hapa leo nimewapata Wakristo. Lazima waone kuwa Uislamu ndiyo dini ya kweli.”

Na hivi ndivyo ilivyo kwa hoja zao ZOTE kuhusiana na Ukristo. NI UONGO; NI UONGO; NI UONGO!! NI UPOTOVU MTUPU!!

Na mimi nilimpatia jibu fupi tu na rahisi. Kwanza nikamwambia acha nikupatie maana ya neno ‘shehe’ kutoka kwenye kamusi ya Kiswahili.



Kama inavyoonekana hapo juu, kuna maana mbili. Na ni wazi kabisa kuwa, kwa ufahamu wa kawaida kabisa, muktadha wa aya hii ya Nehemia haiongelei maana ya kwanza ya neno hili. Kwanza, wakati Nehemia anaandika, Uislamu haukuwapo. Uislamu ni wa juzijuzi tu; miaka 600 baada ya Yesu kuondoka duniani.

Kisha nikamwambia, soma pia aya hiyo kwa Kiingereza. Imeandikwa hivi: “So stood the two companies of them that gave thanks in the house of God, and I, and the half of THE RULERS with me”
Hilo neno ‘mashehe’ limeandikwa kama ‘rulers’ yaani viongozi. Na hii ndiyo maana inayoendana na ile ya pili kwenye kamusi, yaani wazee wenye busara.

Hitimisho
Usidanganywe na tafsiri za Biblia zinazotolewa na Waislamu (siongelei tafsiri za quran; hilo ni suala jingine). Tafsiri za Biblia zinazotolewa na Waislamu ni uongo na upotoshaji mtupu kwa asilimia 100. Kila wanachosema kuhusu Biblia ni kifungo kinachowapeleka watu kuzimu kama wakikiamini.

Ukiwaamini, utakuwa umetupa taji yako; na umeuza uzaliwa wako wa kwanza kwa ujira wa kunde kama Esau.

Bwana Yesu anasema:
“Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.” (Ufunuo 3:11)


Kaa chonjo; adui anahaha kila mahali kukuibia uzima wako wa milele.

Tafakari

Hoji mambo

Chukua hatua

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW