Saturday, June 21, 2014

ALLAH ATEREMSHA UCHAWI NA KUMROGA MTUME MUHAMMAD

Nimenukuu quran aya ya 2:102 na maelezo/ufafanuzi wake hapo chini kutoka tafsiri mbili za quran (Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy na Tafsiri ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani). Aya hii na maelezo/ufafanuzi wake inaonesha mambo yafuatayo: (a) Uchawi umeteremshwa na malaika wa Allah (b) Kuna wachawi wa kiislam. (c) Uchawi ni amali ya ukafiri

Pia, kwa mujibu wa Sahih Bukhari juzuu ya 4, Kitabu cha 54, Hadithi namba 490 na Sahih Bukhari, juzuu ya 7, kitabu cha 71, hadithi namba 658; Muhammad alirogwa na akazurika na uchawi. Kisa cha mtume kurogwa na kuzurika na uchawi pia kinasimuliwa katika quran Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy ukurasa wa 977 na 978.

Swali (a) Ikiwa uchawi ni ukafiri, Kuna uhusiano gani kati ya Allah na ukafiri mpaka atelemshe uchawi?
(b)Mtume Muhammad alirogwa na wachawi wa kiislam au wachawi wengine?
(c) Mtume Muhammad alirogwa na uchawi ulioteremshwa na malaika wa Allah au uchawi mwingine?
(d) Mtume au nabii gani mwingine alirogwa na akaathirika na uchawi?

Quran 2:102 inasema:
Wa Attaba`ū Mā Tatlū Ash-Shayāţīnu `Alá Mulki Sulaymāna Wa Mā Kafara Sulaymānu Wa Lakinna Ash-Shayāţīna Kafarū Yu`allimūna An-Nāsa As-Siĥra Wa Mā 'Unzila `Alá Al-Malakayni Bibābila Hārūta Wa Mārūta Wa Mā Yu`allimāni Min 'Aĥadin Ĥattá Yaqūlā 'Innamā Naĥnu Fitnatun Falā Takfur Fayata`allamūna Minhumā Mā Yufarriqūna Bihi Bayna Al-Mar'i Wa Zawjihi Wa Mā Hum Biđārrīna Bihi Min 'Aĥadin 'Illā Bi'idhni Al-Lahi Wa Yata`allamūna Mā Yađurruhum Wa Lā Yanfa`uhum Wa Laqad `Alimū Lamani Ashtarāhu Mā Lahu Fī Al-'Ākhirati Min Khalāqin Wa Labi'sa Mā Sharaw Bihi 'Anfusahum Law Kānū Ya`lamūna

Quran 2: 102(Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy) inasema: Wakafuata yale waliofuata mashetani wakadai kuwa yalikuwa katika ufalme wa (Nabii) Suleiman; na Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi (waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani na uchawi) ulioteremshwa kwa malaika wawili, Harut na Marut, katika (mji wa) Babil. Wala Malaika hao hawakumfundisha yoyote mpaka wamwambie: “ Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru.” Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo). Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa mambo hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza ambayo yatawazuru wala hayatawafaa Na kwa yakini wanajua kwamba aliyehiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za Akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya hivi). (Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy ukurasa 25-26)


Nanukuu Maelezo/ Ufafanuzi wa quran 2: 102
Suleiman aliyetajwa hapa ni nabii, Mayahudi wanamwita Nabii Suleiman kuwa ni mfalme aliyepata ufalme kwa uchawi, si Mtume. Basi na hawa wachawi wa kiislam humnasibishia Nabii Suleiman hizo ilimu zao za uchawi. Basi Mwenyezi Mungu anamkanushia haya. Na aya hii yaonesha wazi kuwa (a) uchawi ni amali ya ukafiri na (b) kuwa mchawi hawezi kumdhuru mtu ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na (c) kuwa mchawi mwenyewe anadhurika kwa uchawi wake. Na anataja hapa Mwenyezi Mungu kuwa nyuma huko kabisa katika zama za mfalme

Qura 2:102.(Tafsiri ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani) Inasema:
Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW