Tuesday, June 3, 2014

JE MUNGU WA WAISLAMU (ALLAH S.W) NA MUNGU WA WAKRISTO (YEHOVA) NI MMOJA?



UTANGULIZI.
Imekuwa ni kawaida sasa kwa miaka zaidi ya ishirini hivi, kusikia katika mihadhara inayoendeshwa na wahadhiri wa dini ya Uislamu, ambayo imeenea sehemu mbalimbali Duniani na haswa katika nchi za Africa Mashariki na Kati,(East and Central Africa). Wahadhiri hao hufundisha jamii kupitia Qurani na Biblia kwa kusema kuwa Mungu ni Mmoja tu. Wasema Mungu kwa Kiebrania anaitwa Yehova , kwa Kiarabu Allah, kwa Kiingereza God na kwa Kiswahili ni Mungu. Kwa hivyo wasema Mungu Allah kama Qurani inavyofundisha, ndiye Yehova kama Biblia inavyofundisha. Mihadhara hiyo inayoendeshwa na Waislamu imeenea sana, mfano Nchini Tanzania kuna vikundi vingi na kimoja wapo kinaitwa Al-Marid International Propagation Center. Hawa wameandika katika bango lao kwa kunukuu katika Biblia maneno aliyoandika Mtume Paulo katika Waefeso 4:4-6. Maneno waliyoyanukuu yanasema hivi “Bwana mmoja , Imani moja ….., Mungu mmoja , naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote. Nilipotembelea mkoa wa Morogoro pale mjini, eneo la kiwanja cha ndege nikaona Msikiti mmoja umeandikwa maneno haya ya Waefeso 4:4-6. Na nilipotembelea mji wa Nairobi Nchini Kenya pia nikaona kuna vikundi vingi vinavyoendesha mihadhara na kikundi kimoja wapo kinaitwa Kibera Islamic Propagation Centre. Hawa nao katika bango lao wameandika ujumbe unaosema hivi “Acha Biblia Ijisemee na kunukuu injili aya hii” Yohana 8:32 Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Kwa hivyo utaona kuwa wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia na kusema Allah Sub-Hana Wataala ndiye YEHOVA. Fundisho hili wanalieneza kwa kupitia Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingawa hawajabadili dini wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila mkristo, je, ni kweli Mungu Allah kama inavyotuhadithia Qurani ndiye Yehova kama Biblia inavyotufundisha? Nakusihi fuatilia somo hili kwa makini ili kujua Ukweli……

SEHEMU KUU ZA SOMO HILI NI HIZI……

1. Hoja za waislamu kusema Allah ndiye Yehova.

2. Je, jina la Mungu kadiri ya Qurani na Biblia ni moja?

3. Je, Malaika mkuu wa Allah ndiye wa Yehova?

4. Je, ni nani muumba,Allah au Yehova?

5. Mji aliochagua Allah je, ni sawa na wa Yehova?

6. Allah anavyofundisha kuhusu kujitakasa nafsi je, ni sawa na Yehova?

7. Je, mbingu ya Yehova ni sawa na ya Allah?

8. Mwisho wa wanaomwabudu Allah ni wapi?



1. Hoja za waislamu kusema Allah ndiye Yehova

Wahadhiri wa Dini ya Uislamu wanasema Mungu Allah ndiye Yehova kwa sababu Manabii wa Mungu kadiri ya Biblia na Qurani walifundisha kwa kusema Mungu ni mmoja tu. Na wanasoma aya hizi…


Nabii Musa alivyosema

Kumbukumbu la Torati 6:4

Sikiza ee Israeli; BWANA Mungu wetu BWANA ndiye mmoja.

Nabii Isaya alisema hivi

Isaya 45:18,21

Maana BWANA , aliyeumba mbingu, asema hivi, yeye ni Mungu ,ndiye aliyeumba Dunia na kuifanya ….. si mimi BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi. Mungu mwenye haki , mwokozi hapana mwingine zaidi ya mimi.

Nabii Daudi Alisema

Zaburi 86:10

Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, wewe ndiwe mfanya miujiza , ndiwe Mungu peke yako.



Yesu alisema hivi

Yohana 17:3

na uzima wa milele ndio huu wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliye mtuma

Paulo naye Alisema hivi

1 Wakorintho 8:4

Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na yakuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.

Hapa wahadhiri wa Dini ya Uislamu wanasema Manabii wote kadiri ya Biblia wanafundisha kuwa Mungu ni mmoja tu. Je, Muhammad (s.a.w.) alifundisha nini kuhusu Mungu? Wanasoma aya hizi za Qurani……..

Qurani 41:6 Suratul Haa Mym Sajdah (Kusujudu)

Sema; bila shaka mimi ni mtu kama nyinyi. Nimeletewa Wahyi (inafunuliwa kwangu)ya kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja tu……

Hapa wahadhiri wanasema kama vile manabii wote walifundisha Mungu mmoja ndivyo ilivyo fundisha Muhammad.

Qurani 29:46-47 Suratul Al- Ankabuut (Buibui).

Wala mshibishane na watu waliopewa kitabu (kabla yenu) ila kwa yale (majadiliano) yaliyo mazuri, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni :tunaamini yaliyoteremshwa kwetu, na yaliyoteremshwa kwenu. Na mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja : nasi ni wenye kunyenyekea kwake. Na namna hivi tumekuteremshia kitabu (hiki cha Qurani) basi wale tuliowapa kitabu (kabla ya hiki kama taurati na injili) wanakiamini (hiki kitabu ulichoteremshiwa kwani hakipingani na hivyo walivyoteremshiwa). Na miongoni mwa hawa (Waarabu wasiokuwa na Kitabu chochote)wako wanaokiamini. Na hawazikatai aya zetu isipokuwa wale wanaotaka kuficha haki.



Hapa wahadhiri wa kiislamu wakisha soma aya hizi husema vitabu vya Torati na Injili havipingani na Qurani, na vitabu hivyo walipewa Wayahudi na Manasara(yaani Wakristo) na Mungu wa Waislamu na Wakristo ni mmoja tu.

Je, hoja hii ni kweli? Nitaijibu huko mbele.



Majibu kuhusu Mungu mmoja

Ukitazama kwa haraka haraka namna wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu wanavyolinganisha aya za Qurani na Biblia unaweza ukashawishika kuamini hicho wanachokifundisha, lakini ni vyema tukajifundisha kwa undani kadiri ya Qurani na Biblia na kisha tuone kama kuna ukweli juu ya hayo mafundisho yao, ya kusema Allah Sub-hana Wataala ndiye Yehova.tukumbuke kuwa Mungu tunayeabudu alitutahadhalisha sana Wakristo kwa kusema hivi…

Kutoka 20:1-3

Mungu akanena maneno haya yote akasema Mimi ni BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa usiwe na Miungu mingine ila mimi.

Tahadhari hii Ya Mungu wetu ya kusema usiwe na Miungu inamaanisha kuwa Miungu mingine yenye kuabundiwa na watu ipo. Kwa sababu katika Biblia neno Mungu Kiebrania“Elohim” Kiyunani "Theos" limetanjwa mara 3979 lakini pia miungu ya uongo imetanjwa mara 271. baadhi ya miungu hiyo ya uongo ni hii


mungu Dargoni Waamuzi16:23

mungu Baal Wafalme 18:21

mungu mke wa Waefeso aitwae Artemi Matendo 19:24-28.


Aidha tusomapo Qurani pia imetaja miungu mbalimbali iliyokuwa inaabundiwa kule Makka nayo ni hii;

Qurani 53:19-20,23 Suratul An- Najm (Nyota).

19. Je, mumewaona Lata na Uzza? 20. Na Manata (mungu wenu) mwingine wa tatu (kuwa ndio waungu hao badala ya mwenyenzi mungu)? 23. hayakuwa haya (majina ya Lata mungu mwanamke na Uzza mungu mwanamke mwenye enzi. Na Manata mungu mwanamke anayeneemesha ila ni majina tu mliowapa nyinyi na baba zenu…..

Hivyo basi tunaona kuwa miungu yenyewe kuabudiwa ni mingi na kila mwenye kuabudu humtegemea huyo mungu wake na kusema ni mmoja. Mfano waliyemuabudu Dagoni walisema ni mungu mmoja, waliyemwabudu Baali walisema ni mungu mmoja , waliyemwabudu Artemi walisema Artemi ndiye mungu mkuu. Kadharika Manabii.

walimtumikia Mungu mmoja aitwaye Yehova, naye Muhammad alimwabudu mungu mmoja aitwaye Allah. Ninachotaka kukifundisha kwa jamii ijue je, huyo Allah ndiye Yehova?,

2: Je, jina la Mungu kadiri ya Qurani na Biblia ni moja?

Jambo moja la msingi linalo tambulisha kitu au mtu, mnyama au chochote kile ni jina , hivyo ili tuweze kujua kama Mungu anayeabudiwa na Waislamu ndiye tunayemuabudu Wakristo, ni lazima tuangalie jina. Je, ni moja?

Qurani 17: 110 Suratul Bani Israil (Wana wa Israil)

Sema; muombeni (Mwenyenzi Mungu) kwa (jina la )Allah au muombeni (kwa jina la ) Rahman. Kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa). Kwani ana majina mazuri mazuri………

Hapa tunaona Allah anafundisha kwa Waislamu kuwa wamuombe kwa jina la Allah au Rahman. Ukisoma Qurani utaona jina Allah limetajwa mara 2,866, kumbuka Qurani ina Juzu 30 Sura 114. hivyo Mungu anaye abudiwa na Waislamu kadiri ya Qurani jina lake anaitwa Allah.

Jina la Mungu anayeabudiwa na Wakristo ni hili;

Kutoka 6:2-3

Kisha Mungu akasema na Musa akamwambiaaa “Mimi ni YEHOVA Nami nalimtokea Ibrahimu, na Isaka na Yakobo, kama Mungu mwenyenzi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.

Hapa tunaona Mungu tunayemuabudu Wakristo analitambulisha jina lake kwamba ni Yehova katika Biblia limetumika neno au jina BWANA, kwa Kiingereza wanasema LORD, likimaanisha jina lililo Takatifu sana la Mungu katika Biblia jina hili limetanjwa mara 6751. kumbuka Biblia ina jumla ya vitabu 66 Sura 1189 Aya 31,102.

3: Je, Malaika mkuu wa Allah ndiye wa Yehova?

Ikiwa Allah ndiye Yehova, basi ni wazi kuwa malaika mkuu atakuwa mmoja pia. Ikiwa si mmoja hata malaika mkuu watakuwa tofauti. Tuanze kuangalia Allah anavyosimulia katika Qurani naye anasema hivi

Qurani 81:19-21 Suratul At-Takwyr( Kukunja/jua litakapokunjwa)

Kwa hakika hii (Qurani ) ni kauli (aliyokuja nayo) mjumbe mtukufu (Jibrili) Mwenye nguvu,mwenye cheo cha hishima kwa mwenyenzi Mungu. Anayetiiwa huko (mbinguni na malaika wenziwe) kisha muaminifu.

Ufafanuzi wa aya hizi.

ulio ndani ya Qurani unaelezea aya hizi 19-21, unafundisha hivi…….

Mjumbe mtukufu na mwenye kutiiwa huko mbinguni ni Jibrili, ambaye ndiye mkubwa wa malaika wote


Malaika mkuu wa Mungu Yehova ni huyu;

Yuda 1:9

Lakini Mikaeli Malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthumbutu kumshitaki kwa kumlaumu bali alisema Bwana na akukemee

hapa tunaona aya zinatufundisha waziwazi kuwa malaika mkubwa wa Mungu aitwae Allah anaitwa Jibril na Malaika mkuu wa Mungu wetu Yehova anaitwa Mikaeli. Swali; Kwa kuwaMalaika hao ni tofauti, je, Allah ndiye Yehova? Kwa kujua zaidi tofauti ya malaika, jipatie nakala ya somo la: Malaika Jibrili na Gabrieli, je ni Malaika mmoja. Somo hilo tunalo, jipatie.

4: Je, ni nani muumbaji, ni Allah au Yehova?

Kila mtu mwenye kufuata Dini huamini kuwa Mungu ndiye muumbaji ambaye ameumba wanandamu, wanyama na vyote tunavyoviona na vile tusivyoviona. Hivi yafaa tuangalie kile kinachosemwa na Yehova kuhusu uumbaji na vile Allah anavyosema. Je, kauli zao zinapatana au zinatofautiana?

Je, mtu ameumbwa kwa mfano wa nani?

Allah anasema hivi;-

Qurani112:1-4 Suratul Al-Ikhlas (utakaso)

Sema: Yeye ni Mwenyenzi Mungu mmoja (tu) Mwenyenzi Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea) Hakuzaa wala hakuzaliwa Wala hana anayefanana naye hata mmoja.

Kadiri ya aya hii Allah asema kuwa mungu hakuzaa wala hakuzaliwa wala hana mfano wa mtu au watu Yehova anasema hivi kuhusu mtu au watu……


Mwanzo1:26-27

Mungu akasema “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na wanyama , na nchi yote, pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Hapa tunaona Mungu wetu Yehova ameumba mtu kwa mfano wake, lakini Allah anasema hana anayefanana naye hata mmoja……Swali kwako mfuatiliaji: Je, Allah ndiye Yehova? Tafadhali usome aya hizi ili kujua zaidi (Mwanzo 5:1-2, 9:6, 1Korintho 11:7, Kolosai 1:15, 3:10, Matendo 17:28-29, Yakobo 3:9). Pengine waweza kusema Je, Mungu amefanana na mimi kivipi?Jua kwamba Mungu ni Roho (Yohana 4:24) Naye alitupa pumzi(yaani roho ya uhai (Mwanzo 2:7))isitoshe Mungu ndiye Baba wa roho zetu (Waebrania 12:9) Mungu anasema Roho zetu ni mali yake(Ezekieli 18:4,Hesabu 16:22)

Kuapa kwa Mungu kuhusu viumbe

Qurani 91:1-7 Suratul Ash-Shams (Jua)

Naapa kwa jua na kwa mwangaza wake. Na kwa mwezi unapoliandama. Na kwa mchana unapolidhihirisha. Na kwa usiku unapolifunika.Na kwa mbingu na kwa Aliyezijenga. Na kwa ardhi na Aliyeitandaza. Na kwa nafsi (roho) na Aliyeitengeneza.

Qurani 92:1-3 Suratul Al-Layl (Usiku)

Naapa kwa usiku ufunikapo (kila kitu). Na kwa mchana uangazapo. Na kwa aliyeumba kiume na kike.

Hapa tunaona Allah Mungu anayeabudiwa na Waislamu anaapa kwa mbingu na kwa aliyezinjenga, kwa ardhi na aliyeitandaza. Je, huyo mtandazi wa ardhi na mjengaji wa mbingu ni nani? Qurani inaendelea kuhadithia hivi……..

Qurani 45:22 Suratur AL- Jathiyah (kiyama/ kupiga magoti)

Na mwenyenzi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki…

Qurani 44:7-8 Suratul Ad-Dukhan (moshi)

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake,ikiwa mnayo yakini (basi yakinisheni haya) Hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye anahuisha na kufisha. Mola wetu na ni mola wa wazee wenu (wote) wa mwanzo (na mola wa kila kitu)

Hapa tunaona kuwa Allah kupitia Qurani anasema kuwa mwenyenzi Mungu ameziumba mbingu na ardhi na tena anasema hakuna aabudiwaye ila yeye. mjengaji wa mbingu na mtandazaji wa ardhi anajieleza hivi ……


Isaya 44:24

BWANA,mkombozi wako yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi, “Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote, nizitandaye mbingu peke yangu, niienezaye nchi. Ni nani aliye pamoja nami?”

Mungu wetu Yehova anasema mimi ninafanya vitu vyote.

(Soma Isaya 45:6-7, 11-12, Yeremia 27:5) Bila shaka Yehova ndiye muumbaji wa vitu vyote

JE Mungu Yehova aliapia vitu alivyoviumba kama Allah?

Isaya 45:22-23

Niangalieni mimi mkaokolewe, Enyi ncha zote za dunia. Maana mimi ni Mungu hapana mwingine. Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba, mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.

Waebrania 6:13-16

Kwa maana Mungu alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake. akisema “Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza, Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo kwa kuyathibitisha.

Hapa tunaona Mungu wetu Yehova haapi kwa mtu wala vitu alivyoviumba kama Allah anavyoapa, bali Yehova anasema “Naapa kwa nafsi yangu”.Waweza pia kusoma jinsi Yehova alivyoapa kwa nafsi yake katika aya hizi;-(Isaya 14:24 na Mwanzo 22:16)

5: Je, mji aliouchagua Allah ni sawa na wa Yehova?

Mji wa Allah:

Qurani 27:91 An-Naml (sisimizi/mchwa/wadudu chungu)

Bila shaka nimeamrishwa nimuabudu mola wa mji huu (wa Makka) ambaye ameutukuza na ni vyake tu (Mwenyezi Mungu) vitu vyote…

Qurani 3:96 Suratul Aal-Imran (watu wa Imram)

Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyo Makka yenye baraka na uwongozi kwa ajili ya walimwengu wote.

Qurani 106:3-4 Suratul Quraysh (Makureshi-kabila)

Basi nawamuabudu Bwana wa nyumba hii (Al-ka'ba) Ambaye anawalisha (wakati Waarabu wenzi

wao wamo) katika njaa na anawapa amani wakati wenzi wao wamo katika khofu.

Hivyo tunaona kuwa Allah ndiye bwana wa Al-ka'ba kadiri ya aya hii na Al-ka'ba iko katika Makka. Kupitia aya hizi tunaona Allah mungu anayeabudiwa na Waislamu amechagua mji wa Makka kuwa ndio mji wake mtakatifu na tena Muhammad (s.a.w) aliamrishwa amuabudu mola wa mji huo wa Makka ambaye ndiye Allah.

Je, Mungu wetu aitwae Yehova alichagua mji gani? Endelea ……..

Mji aliouchagua Mungu wetu Yehova ni huu…

2 Nyakati 6:4-6

Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza kwa mikono yake, akasema, Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wowote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu yeyote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo, na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli.
Maandiko hayaelezi mji mwingine wowote aliouchagua Mungu wetu hapa duniani bali ni mji wa Yerusalemu tu. (tazama 2 Nyakati 12:13,Ezra 6:12; 7:15,27; Zaburi 26:8; Zakaria 2:12)

Kupitia aya hizi tunaona Mungu wetu Yehova, mji wake aliouchagua niYerusalemu. Neno Yerusalemu ni la lugha ya Kiebrania na maana yake ni "chimbuko la amani". Hata Waisraeli walipokuwa mbali na mji wa Yerusalemu bado walipiga magoti na kuelekeza nyuso zao Yerusalemu. (Tazama Danieli 6:10). Mji aliouchagua Yehova ni Yerusalemu, na mji aliouchagua Allah ni Makka. Na hii ndio tofauti ya mji wa Allah na Yehova.

6: Allah anavyofundisha kujitakasa nafsi, je ni sawa na Yehova?

Allah anafundisha hivi….
Qurani 53:32 Suratul Al-Najm (nyota)

Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipokuwa makosa hafifu (hakuma aliyesalimika nayo) bila shaka, mola wako ndiye mwenye maghufira mengi yeye ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. basi msizitakase nafsi zenu….

Qurani 12:53 Suratul Yusuf

Nami sijitakasi nafsi yangu, kwa hakika (kila) nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo mola wangu ameirehemu. Hakika mola wangu ni mwingi wa kusamehe (na) mwingi wa kurehemu.

Kadiri ya Qurani Allah anayo nafsi pia Tazama Qurani 5:116. Kwa hivyo hapa tunaonaAllah ana agiza watu wasizitakase nafsi zao na tena anasema sijitakasi nafsi yangu. Hii ni ajabu sana!

Mungu wetu Yehova anavyosema kuhusu kujitakasa nafsi, yaani utakatifu:

Isaya 43:3

Maana mimi ni BWANA Mungu wako, mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako. Nimekutoa Misri kwa ukombozi wako, nimetoa Kushi na Sheba kwa ajili yako.

Hapa tunaona Mungu anasema ‘Mimi ni mtakatifu’, hili pia ni jina la sifa la Mungu wetu Yehova kwa lugha ya Kiebrania husema ‘kadosh’. Nabii Isaya ameandika kuwa Mungu ni Mtakatifu mara 32 kwa ufupi tu soma Isaya 40:25, 48:17 na 57:15. Isitoshe kwa kuwa Mungu wetu Yehova ni mtakatifu pia aliagiza kwetu hivi.

Walawi 11:44

Kwa kuwa mimi ni BWANA Mungu wenu takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu, wala msitie uchafu nafsi zenu…

Mtume Petro anatuagiza hivi;

1 Petro 1:15-16

Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.Kwa maana imeandikwa, mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

Mtume Paulo pia ameagiza kujitakasa nafsi na kuwa watakatifu(2 Wakorintho 7:1) waweza pia kusoma agizo hilo la kuwa watakatifu katika Walawi 19:2, 20:26.

Kwa hivyo tunaona Yehova anaagiza tujitakase nafsi zetu ili tuwe watakatifu, lakini Allah anaagiza kwa Waislamu kuwa wasizitakase nafsi zao.

Swali kwako mfuatiliaji, Je, Allah ndiye Yehova?


7: Je, mbingu ya Yehova ni sawa na pepo (mbingu) ya Allah?

Mbingu ya Yehova:

Luka 20:34-36

Yesu akawaambia wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa, lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule. Na kule kufufuka katika wafu hawaoi wala hawaolewi. wala hawawezi kufa tena. Kwa sababu huwa sawa sawa na malaika, nao ni wana wa Mungu kwa vile walivyo wana wa ufufuo.

Maandiko haya yanatuthimbitishia Wakristo kuwa tutakapofufuliwa na kuingia mbinguni, hakuna mambo ya kuolewa wala kuoa, maana tutakuwa na miili ya kiroho (1 Korintho 15:43-54) Aidha maandiko yanatufundisha kuwa ufalme wa Mungu siyo kula wala kunywa bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Tazama Warumi 14:17). Mungu wetu anafundisha wazi wazi kuwa kule mbinguni katika ufalme hakuna njaa, wala kiu wala jua kutupiga (Ufunuo 7:16-17.)

Pepo au Mbingu ya Allah itakuwa hivi:

i). Maghorofa

Qurani 39:20 Suratul Zumar (makundi/vikosi)

Lakini waliomcha mola wao watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa chini (mbele) yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyenzi Mungu, Mwenyenzi Mungu havunji ahadi yake.

ii) mito ya maji, maziwa, ulevi, asali na matunda

Qurani 47:15 Suratul Muhammad

Mfano wa pepo waliyoahidiwa watawa (wacha Mungu itakuwa hivi). Imo mito ya maji yasiyovunda, na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao na mito ya asali iliyosafishwa. Tena humo watapata matunda ya kila namna, na samahani kutoka kwa mola wao. Basi hao watakuwa sawa na wale wataokaa motoni na kunyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao?.

Je Matunda hayo ni sawa na ya wapi?

Qurani 2:25 Suratul Al- Baqarah (ngombe jike)

Na wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake. Kila mara watakapopewa matunda humo kuwa ni chakula watasema “haya ndiyo yale tuliyopewa zamani (ulimwenguni) kwani wataletewa (matunda hayo) hali yatakuwa yamefanana (na yale waliyokuwa wakiyajuwa ulimwenguni wataletewa kwa sura hiyo lakini


utamu mwingine kabisa) na humo watapata wake waliotakasika (na kila mabaya na machafu) na watakaa milele humo.

iii). Watapata wanawake aina hizi na nyama za ndege

Qurani 56:15-23 Suratul Al Waaqiah (Tukio) nanukuu aya ya 21-23 tu

Na nyama za ndege kama watakavyotamani (wenyewe). Na wanawake wenye macho mazuri na makubwa (ya vikombe). (wanapendeza na safi) kana kwamba ni lulu zilizofichwa (katika machaza yake, ndio kwanza zinapasuliwa)

Qurani 37:48-49 Suratul As-Saaffat (Wapangao mistari)

Na pamoja nao watakuwa wanawake wenye macho mazuri makubwa. (Safi) wanawake hao kama mayai (ya mbuni) yaliyohifadhiwa.

Qurani 37:44-46 Suratul As-Saaffat (Wapangao mistari)

Wako juu ya vitanda (viti vya enzi vya fahari), wamekabiliana (wanazungumza). Wanazungushiwa gilasi zenye (vinywaji) safi.Vyeupe yenye ladha kwa hao wavinywao.

Kupitia aya hizi tumeona kuwa Allah Sub-haana Wataala Mungu anayeabudiwa na Waislamu ametoa ahadi ya kuwaingiza Waislamu peponi (mbingu) na kuwa watapata mito ya maji, mito ya maziwa na ulevi na pia mito ya asali vilevile watapata matunda,nyama ya ndege na pia wataozeshwa na Allah mungu wao wanawake wenye macho makubwa kama mayai ya mbuni. na wengine makubwa kama vikombe.

Jambo la kushangaza zaidi ni pale tunaposoma kitabu cha Hadithi, maana imani ya Dini ya Uislamu imejengwa pia katika vitabu vya hadithi. Soma

Qurani 42:10 Suratul Ash-Shuura (mashauriano)

Mkihitalifiana katika jambo lolote (rejeeni kitabu cha Mwenyenzi Mungu na Hadithi za mtume kwani)…

Tunaposoma kitabu cha Hadithi ya mtume kiitwacho Sunnan Ibn-1- Majah vol 5 ukurasa wa 546 Hadithi No: 4337 kuna maelezo haya

Imesimuliwa na Abu' Umama ya kuwa mjumbe wa Allah (baraka na amani ya Allah iwe juu yake) alisema Allah hatamruhusu yeyote kuingia peponi ila kwa idhini ya Allah, Mwenye nguvu na utukufu naye atamwozesha mwanamume wake sabini na mbili. Wawili watakuwa mabikira (mahurul-ain) yaani wanawake wa peponi wenye macho makubwa, na sabini watakao warithi ambao watu (mabwana zao) wametupwa katika moto wa jahanamu kila mmoja wao (hao wanawake) wana uke wa kupendeza. Na mwanamume, Nguvu ya uume wake katika kujamiana hautapinda (kusinyaa) bali utadumu sana

Kwa kiingereza Hadithi hii inasomeka hivi:-

Abu-Umama (Allah be pleased with him) reported that Allah's messenger (peace and blessings of Allah be upon him)said Allah will not admit anyone in the paradise but Allah the mighty and Glorous, will marry him with seventy two wives two will from virgins (haurine) with big eyes and seventy will be his inheritance from the people of the Hell- Fire (1).Everyone of them will have apleasant vagina and he (the man) have sexual organ that does not bend down (during sexual intercouse)

Hivi ndivyo Allah Mungu wa Waislamu alivyoahidi. Hili ni jambo ambalo kwa Mkristo linamshangaza sana kwani jambo hili linalofundishwa na Allah halipo kabisa kwa Mungu wetu Yehova hapa ulimwenguni ndiko kwenye ulevi,matunda,nyama za ndege, kuoana, maghorofa, magari, mito, bahari na vinginevyo.

Tafakari, je huyo Allah ni nani?

8: Mwisho wa wanaomwabudu Allah ni wapi?

Tunajua kuwa Wakristo tutaishi na Mungu wetu Yehova milele (tazama 1Thesalonike 4:13-17 na Ufunuo 21:3-7) Hivyo Mungu wetu hana mwisho ni wa milele. Lakini tunaposoma Qurani na Hadithi za Muhammad, mtume wa Waislamu tunaona mafundisho haya…

Qurani 51:56 Suratul-Adh-Dhaariyat (upepo)

Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu

Qurani 6:128 Suratul Al An-Am (Wanyama)

Na (wakumbushe) siku atakapowakusanya wote (awaambie) "Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu" na marafiki wao katika wanadamu (watawagombania) waseme "mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao, na tumefikia muda wetu uliotuwekea" Basi (Mungu) atasema:"moto ndio makazi yenu, mtakaa humo milele…..

Katika aya hizi tunaona kuwa majini pamoja na watu wote watatupwa motoni. Je Allah naye ni vipi? tunaposoma kitabu cha hadith za mtume (s.a.w) cha Sahih al-Bukhari Vol: VI Hadithi No: 371.ukurasa wa 353 Kuna maneno haya:

Qurani 50:30 Suratul Qaf (kuapa)

Siku tutakayoiambia Jahanamu, ‘Je! Umejaa?’ Nayo itasema ‘Je kuna ziada (zaidi?Naije tu!

)

Imesimuliwa na Anas kuwa: mtume alisema watu watatupwa jahanamu, Naye Allah ataiuliza jahanamu akisema je umejaa nayo jahanamu itasema kwani kuna nyingine zaidi na ije tu? Mpaka Allah atakapo ingiza mguu wake nayo jahanamu itasema inatosha! Inatosha

Kwa kiingereza Hadithi hii inasomeka hizi:-

Allah's statement:It (Hell) will say Are there any more (to come)? (50:30).

Narrated Anas: The prophet said the people will be thrown into the (Hell) Fire and it will say Are there any more (to come)?' (50:30) till Allah puts His Foot over it and it will say Qai! Qat!(Enough! Enough!)

Katika aya hii tunaona Allah mungu wa Waislamu anaiuliza Jehanamu kama imejaa, nayo Jehanamu itamuuliza Allah je, kuna zaidi. Yaani swali hili linaonyesha kuwa Jahanamu ilikuwa bado haijajaa,.

Maelezo ya Hadithi hii inadhibitisha kuwa Allah ataingiza mguu katika Jahanamu na ndipo Jahanamu itakaposema kuwa inatosha! Inatosha!, yaani imejaa kwa tendo la Allah kuingiza mguu wake humo. Jambo hili ni tofauti kabisa na ilivyo kwa Mungu wetu Yehova., Mungu wetu ameiweka jahanamu maalum kwa ajili ya watu wabaya, na ibilisi, pamoja na malaika zake. Tafadhali soma aya hizi; Mathayo 25:41,46, Ufunuo 20:10, 21:8.

Aya hizi zote zinaonyesha kuwa mwisho wa wabaya, Ibilisi na malaika zake ni katika ziwa la moto. Swali kwako Ndugu mpendwa, Je, Allah ni nani?

Ni matumaini yangu kuwa umeweza kujua kwa undani kupitia Qurani na Biblia na vitabu vya Hadith za mtume wa Waislamu aitwae Muhammad kuwa Allah Sub-Haana Wataala Mungu anayeabudiwa na Waislamu. Siyo Yehova Mungu tunaye muabudu Wakristo.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW