Monday, May 12, 2014
USHAIDI WA BIBLIA NA KURUAN (SEHEMU YA PILI)
Ndugu wasomaji: Leo ningependa tujifunze sifa za Mungu kupitia Biblia na Kuruani kama ushaidi zaidi wa Umungu wa Yesu.
Hapa chini nitaziweka sifa na au adhama za Mungu na tutaziangalia kama hizo zote zipo kwa Yesu Kristo.
1 Mungu ni wa milele
2 Mungu ndiye muumbaji,
3 Mungu yupo mahali popote,
4 Mungu ndiye anaye samehe dhambi za watu,
5 Mungu anajuwa na kufahamu yote hata yaliyomo mioyoni mwetu,
6 Mungu ni Nuru ya Mbinguni na Duniani
7 Mungu ndiye anaye watuma Mitume na Manabibii!
8 Mungu anauwezo wa kujidhihilisha (kuonekana) na tena mngu ni wa sili (kuto onekana)
JE, YESU WA KWENYE BIBLIA ANAZO HIZO SIFA?
1 MUNGU NI WA MILELE
Quran 2:255, Sifa ya milele ni ya Mungu pekee Je Yesu hiyo sifa unayo?
Waebrania 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule jana na leo na hata milele,
Sifa ya Umilele teyari Yesu amesha inyakuwa.
2 MUNGU NDIE MUUMBAJI
Je, hii sifa ya Uumbaji Yesu wa Biblia anayo?
Quran 5: 110. Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!
Zaburi 33: kwaneno la Bwana Mbingu zilifanyika na jesh lake lote kwa pumzi ya kinnywa chake,
Wakolosai 1:16 -17 kwakuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbingun na vilivyo juu ya nchi, vinavyo onekana na visivyo onekana.......
Waebrania 1:1-2 mungu ambaye alisema zaman na baba zetu katika manabii kwa sehem nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika mwana, aliye muweka kuwa mrith wa yote tena kwa yeye aliufanya ulimwengu,
3 MUNGU YUPO MAHALI POPOTE
Je, Yesu anayo hii sifa ya kuwa kila mahali?
Mungu yupo kila mahali wakusanyikapo watu wawili au watatu, MATHAYO 18:20 (Yesu) Kwakuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina Langu, nami nipo papo hapo katikati yao, soma Mathayo 28:20 na Yohana 1:47-49.
4. MUNGU NDIE ANAYE SAMEHE WATU DHAMBI
Je, Yesu anayo hii sifa ya kusamehe watu dhambi?
Yesu ndiyo Mungu anaye samehe dhambi, Marko 2:1-11 Mathayo 1: 21
Zaburi 68:20,
5. MUNGU ANAJUWA NA KUFAHAMU YOTE HATA YALIYOMO MIOYONI MWETU
Je, Yesu anayo hii sifa ya kufahamu yalio kwenye mioyo yetu?
Quran 17:25 Mungu anayajuwa yote hata yaliyo katika mioyo yetu,
lakin Yesu hakujiaminisha kwao, kwakuwa yeye aliwajuwa wote na kwa sababu hakuwa na haja ya mutu kushuhudia habari za mwanadamu kwa maana yeye mwenyewe aliyajuwa yaliyomo ndani ya mwanadam,
Marko 2:8 Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikili hivyo nafisini mwao.....
Quran 58:7, na Yeremia 23:23-24
6 MUNGU NI NURU YA MBINGUNI NA DUNIANI
Je, Yesu anayo hii sifa ya Nuru?
Quran 24: 35 Mungu ni nuru ya mbingu na aridhi,
Yesu ndiye Nuru yangu, Soma Yohana 8:12 Matendo 9:3-5,,
7 MUNGU NDIE ANAYE WATUMA MITUMIE NA MANABII
Je, Yesu alituma Mitume na Manabii?
QUR AN 22 75 Mungu ndiye anaye watuma mitume na manabii,
Yesu ndiye aliye watuma manabii. soma Mathayo 23 34
Yesu ndiye aliye wachaguwa mitume kisha akawatuma, soma Mathayo 10 :1-2.
Yesu ndiye aliye watuma Malaika, Soma Ufunuo 22:16,
8 MUNGU ANA UWEZO WA KUJIDHIHIRISHA (KUONEKANA) NA TENA MUNGU NI NI WA ASILI (KUTO ONEKANA)
Je, Yesu anazo hizi sifa za asili na kujidhihirisha?
(1) Ufunuo 1:17-18 Yesu niye wakwanza na wamwisho,
(2) Tmotheo 2, 3:16 Yesu ndiye Mungu aliye jidhihilisha katika mwili,
(3) Timotheo 1, 6:14-16, Yesu ndiye Mungu ambaye sasa yupo katika siri haonekan,
NABII MIKA ALITABILI, BWANA MUNGU ATASHUKA, Mika 1:2-3, Bwana aliyeshuka na kukanyaga Dunia ni Yesu. Ushaidi zaidi soma Yohana 6:51,,
NA BII ISAYA ALITABILI KUWA MUNGU ATAKAPO KUJA YATAFANYIKA HAYA, Isaya 35:3-6 itieni nguvu mikononi iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyo legea, waambieni walio na moyo wa hofu jipeni moyo misiogope: tazama mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi, ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa, ndipo mutu alie kilema ata ruka ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba...... BILA SHAKA HAYO YOTE YALIFANYWA NA BWANA YESU ALIPO KUJA, HILO HALINA UBISHI, soma kuhusu kipofu Mathayo 9:27 -30, kiziwi Marko 7:32-35, kupooza soma Yohana 5:9. Matendo 3:1-5.
QUR AN 39:29 ALLAH aliwaagiza watu washugulike na Bwana Mmoja tu naye alisema hivi...Mwenyezi Mungu anakupigieni mfano wa mtu mwenye mabwana washilika wanao gombana na mutu mwingine, aliyehusika na bwana mmoja tu, J! wako sawa katika hali zao? alhamd lilahi, lakin wengi wao hawajui basi shugulika na bwana wako mmoja tu mwenyez mungu. Yesu ndiye Mungu aliye wapigia watu mfano, soma Mathayo 13:13-15, 18, 36 -43,
YESU NNDIYE BWANA MMOJA YAANI MUNGU, Wafilipi 1:10-11.
YESU ANAFUNDISHA YEYE NI MWALIMU NA BWANA, soma Yohana 13:13
Yeremia 10:10.
YESU MWNYEWE ALIJIDHILISHA KUWA NI MUNGU, soma yohana 14: 7-9 na 10 30,
MITUME WA YESU WALIMTAMBUWA YESU KUWA NI MUNGU, soma Yohana 20:26-29.
Warumi 9:5 ambao mababu ni wao na katika hao alitoka krsto kwa jinsi ya mwili, ndiye aliye juu ya mambo yote mungu mwenye kuhimidiwa milele AMINA.
WAKOROSAI 2:2 Wapate kujwa kabisa siri ya mungu YAANI KIRSTO,
TITO 213 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa kiristo yesu, MUNGU MUKUU NA MWOKOZI WETU,
Wakorintho 2, 4:4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Krsto aliye sura ya mungu,
MAANDIKO HAYA MACHACHE YAPO NA MENGINE MENGI YANAYO ELEZEA KUWA YESU NI MUNGU KWA %100, KWAHYO SISI WAKRISTO HATUNA MASHAKA JUU YA HILO, Usipo sadiki kuwa yesu ni mungu utapata madhara gani? soma yohana 8:24.
ALLAH ANAMALIZA KWA KUSEMA KATIKA UMMAH YAKE KUWA:
QUR-AN SURATUL YUNUS 10:94 INASEMA HIVII Kama unamashaka juu ya hayo tuliyo kuteremshia, waulize wale wasomao vitabu kabla yako nao ni MAYAHUDI NA WAKRSTO.
Allah anawaambrisha Waislam kuwa, WAJIFUNZEkuhusu Mungu kupitia Wakristu na Wayahudi na sio KUPITIA Muhammad na Kuruan yake.
Leo tumejifunza kuwa hata kwenye Kuruani, Yesu ni Mungu na atabakia kuwa Mungu milele na miele.
Mungu awabariki sana na endelea kujifunza neno kila siku.
Katika Huduma yake
Max Shimba Ministries Org.
1633 Broadway, 30th Floor, New Yor, NY 10019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Muhammad’s Fear Of Judgment Day
Muslims beware! The next eclipse could be the Day of Judgment . This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment