Tuesday, May 13, 2014

UKANAJI MUNGU NI NINI?

“Ukanaji Mungu wazi,” pia waitwa “theolojia wazi” na uwazi wa Mungu,” ni jaribio la kuelezea ufahamu kuhusu Mungu kulingana chuguo huru la mwanadamu. Pingamizi la ukanaji Mungu wazi hasa ni huu: wanadamu wako huru kabisa; ikiwa Mungu alijua hatima, wanadamu hakika hawangekuwa huru. Kwa hivyo, Mungu kabisa hajui kila kitu kuhusu kesho. Ukanaji Mungu wazi washikilia kuwa kesho haijulikani. Kwa hivyo Mungu anajua kila kitu ambacho kinaweza julikana, lakini hajui kesho.


Ukanaji Mungu wazi waweka imani yao katika misingi ya kurasa za maandiko ambazo zaelezea Mungu “anabadilisha mawazo yake” au “kushangaa” au “kuonekana kupata hekima” (Mwanzo 6:6; 22:12; Kutoka 32:14; Yona 3:10). Kwa mwangaza wa maandiko mengine mengi ambayo yaelezea ufahamu wa Mungu wa kesho, maandiko haya lazima yaeleweke kama Mungu anajielezea kwa njia ambazo hatuwezi kuzielewa. Mungu anajua vile hatua zetu na maamuzi yatakuwa, lakini “Anabadilisha mawazo yake” kulingana na hatua yake ikitegemea hatua yetu. Chukizo la Mungu katika unyonge wa mwanadamu haimanishi kwamba hakujua kuwa hayo yatatokea.

Kwa hitalafiano na ukanaji wa Mungu wa wazi, Zaburi 139:4,16 yasema, “Maana hamna neno ulimini mwangu usilolijua kabisa, BWANA. Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.” Mungu angewezaje kutabiri mambo tatanishi katika Agano La Kale kuhusu Yesu Kristo kama hajui siku za usoni? Ni namna gani Mungu kwa njia yo yote ile anaweza kuruhusu wokovu wetu wa milele kama hajui chenye kesho imetubebea?

Mwisho, ukanaji Mungu wa wazi unaanguka kwa vile unajaribu kuelezea yenye hayawezi kuelezeka- uhusiano kati ya ufahamu wa Mungu na penzi huru la mwanadamu. Vile aina ya Kikalvinisti yakaenda kupita kiwango yalivyoanguka ya kuwa yakataa uwepo wa Mungu kila mahali na uwezo wake. Mungu lazima yaeleweke kupitia kwa imani, kwa maana “bila imani ni vigumu kumpendeza Mungu” (Waebrania 11:6a). ukanaji Mungu wa wazi kwa hivyo si wa kiroho. Ni njia nyingine ya mwanadamu aliye na hatima kujaribu kuelewa Mungu asiye na mwisho. Ukanaji Mungu wazi lazima ukataliwe na wafuasi wa Kristo. Huku ikiwa ukanaji wa Mungu wa wazi ni elezo la uhusiano kati ya ufahamu wa Mungu kabla ya uumbaji na penzi huru la mwanadamu, sio elezo la kibibilia.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW