Monday, March 24, 2014

ASALIMISHA MANYANGA YA UCHAWI BAADA YA KUTEKWA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA

Ni maajabu makubwa ambayo Mungu anaendelea kufanya kupitia huduma ya Ufufuo na Uzima mkoani Arusha chini ya Mch. Frank Andrew; ambapo wiki hii kumetokea na jambo ambalo liliwaacha katika mshangao watu wengi walioudhuria ibada kanisani hapo.
Tukio hilo la aina yake lilimjumuisha dada aitwaye kwa jina la Lightness ambaye alisalimisha mambo yake ya uchawi ambayo kwa hayo alitesa maisha ya watu wengi. Mikoba hiyo ni pamoja na vyungu, ungo, shanga, pete, makombe na maji ya maiti.
Mapema wiki hii, mchawi mwingine alikamatwa usiku wa saa sita akiwa anawanga hali ya uchi wa mnyama; Mchawi huyo aliyefahamika kwa jina la Saidi alidai kukamatwa na nguvu za Mungu kutokana na watu waliokuwa mkesha usiku wa siku hiyo.
Pichani ni Lightness na manyanga yake baada ya kuchomwa moto yote. Mungu ni mkuu na njia za kutoka mautini zina yeye.
imeandaliwa na Information Ministry

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW