Sunday, January 19, 2014

YESU MWALIMU WA MFANO

Yesu Kristo, Mwalimu wetu, katika mstari huu, anawauliza wanafunzi wake, “Wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwenda wapi?“. Siyo kwamba wanafunzi wake walikuwa hawajauliza kabisa swali hili. Petro aliuliza swali hili katika YOHANA 13:36, na Tomaso aliuliza swali lililokuwa na maana hiyo katika YOHANA 14:5. Hata hivyo, baada ya wanafunzi hawa kuuliza swali hili mara mbili, hawakumwuliza tena. 

Yesu alitaka wazidi kumwuliza, maana aliwaona bado hawajaelewa. Hapa, Yesu anatoa mfano kwa Walimu wote wa biblia. Furaha ya Mwalimu yeyote wa Biblia anayefuata mfano wa Yesu, ni kuona wanafunzi wake wanaelewa, na kuyatendea kazi yale wanayofundishwa. Mwalimu wa Biblia, hataridhika kuona anafundisha tu wakati wanafunzi wake hawamwelewi. Furaha yake itakuwa kuona wanafunzi wake wanauliza maswali tena na tena ili wapewe ufafanuzi kwa njia iliyo rahisi zaidi mapaka waelewe. 

Mwalimu wa Biblia anayefuata mfano wa Yesu, hatachoshwa na maswali au kuyachukia, ikiwa wanafunzi hao watakuwa wanauliza maswali hayo kwa lengo la kutafuta kuelewa. Sisi nasi kama wanafunzi wa Yesu, tunakumbushwa kuwa na bidii kuuliza maswali tena na tena, mpaka tuelewe, na kuishindania imani. Wanafunzi wengi wa yesu, huona aibu kuuliza maswali na kuogopa kuonekana kuwa hawajui. Kufanya hivyo kunatuweka katika hatari ya kuiacha imani kutokana na kutokuelewa, na kupata hasara ya milele. Petro alikuwa mwulizaji mkubwa wa maswali. Kutokana na maswali yake, tunapata mafundisho mengi ambayo tusingeyapata. Kwa mfano, Petro bila aibu, anamwuliza Yesu katika MATHAYO 18:21 “Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nimsamehe? Hata mara saba?“ Kutokana na swali hili, wote tunapata mafundisho kuhusu kusamehe.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW