Sunday, January 19, 2014
KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA MAANDIKO.
Ningependa leo tujifunze na au tuangalie, ni wapi katika Biblia Yesu Kristo katajwa kuwa yeye ni Mungu. Karibu na Mungu akubariki sana.
Katika ( 1YOHANA. 5:20 ) “Nasi twajua kuwa Mwana wa Mungu amekwisha kuja,naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli.,yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye MUNGU WA KWELI NAUZIMA WA MILELE”.. Pia katika ( YOHANA 20:26-29 ) “basi,baada ya siku nane,wanafunzi wake walikuwamo ndani tena,na Tomaso pamoja nao.Akaja Yesu na milango ilikuwa imefungwa,akasimama katikati,akasema,Amani iwe kwenu.Kisha akamwambia Tomasolete hapa kidole chako;uitazame mikono yangu;ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu;wala usiwe asiyeamini;bali aaminiye.Tomaso akajibu akamwambia,BWANA WANGU NA MUNGU WANGU..Yesu akamwambia,wewe kwa kuwa umeniona umesadiki;wa heri wale wasioona wakasadiki”.
YESU KRISTO MUNGU MKUU, ( 1TITO 2:13 ) “Tukilitazamia tumaini lenye mafunuo ya KRISTO YESU MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU”.. YESU NI MUNGU aliyejifunua katika mwili ( WARUMI 9:5 ) “Na katika hao alitoka KRISTO KWA NJIA YA MWILI,NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE,MUNGU,MWENYE KUHIMIDIWA MILELE.AMINA..Mhalifu msalabani alimwita YESU Mungu na kumuomba YESU atakapokuwa katika ufalme wake amkumbuke mharifu huyo”. ( LUKA 23:39-43 ).Yesu hakukataa kuwa SI MUNGU bali alisema,Amini nakuambia leo hivi,utakuwa pamoja nami peponi.
YESU NI MUNGU ALIYEKUJA DUNIANI .( WAFILIPI 2:5-6 ) “Ambaye yeye mwanzo alikuwan yuna namna ya Mungu,naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho,bali alijifanya kuwa hana utukufu,akatwaa namna ya mtumwa,akawa ana mfano wa wanadamu”.YESU alijita-mbulisha kwao kuwa ni MUNGU lakini hawakuelewa ( YOHANA 10:30-33 ) “Yesu akawajibu,kazi njema nyingi niwewaonyesha zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu,kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe;bali kwa kukufuru,na kwasababu wewe uliye.mwanadamu wajifanya kuwa Mungu. Wayahudi walisema anakufuru kwa kusema kuwa yeye ni Mungu.Kimsingi Yesu ndiye Baba mwenyewe ndio maana anasema huwezi kumtenganisha na Baba; ukimwona yeye umemuona Baba. ( YOHANA 14:7-9 )
Katika mstari 8 na 9 Filipo akamwambia,Bwana,utuonyeshe Baba yatutosha. Yesu akamwambia,Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote,wewe usinijue,Filipo?
Ikiwa tu wanafunzi wa Yesu hatupaswi kubabaishwa na watu ambao hawana Roho wa Mungu.Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kusema Yesu ni Mungu..Kwasababu hiyo,wanatumia akili tu.Hawa ni watu wa tabia ya asili ambao hawawezi kuyaelewa mambo ya kiroho ( 1WAKORITHO 2:14 ) “Basi,mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kuyapokea mambo ya Roho wa Mungu;maana kwake ni upuuzi;wala hawezi kuyafahamu;kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni”
Yesu Ni Mungu
Max Shimba Ministries Org 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Muhammad’s Fear Of Judgment Day
Muslims beware! The next eclipse could be the Day of Judgment . This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment