Saturday, November 2, 2013

Yesu ni Mungu Kutokana na Koran (Sehemu ya Kwanza)

Waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidini kupitia wahadhiri wao wa Dini wamekuwa wakipinga kuwa Yesu Kristo si Mungu kwa madai kuwa, Mungu hawezi kuzaliwa.

Ndugu msomaji, nakusihi ufuatilie somo hili kwa makini ili ujue ukweli kuhusu Umungu wa Yesu Kristo katika Koran:

Je Yesu anazo sifa za kipekee za Mungu kutokana na Quran? Hebu tuanze utafiti wetu kwa kusoma Quran na tujionee wenyewe kama kweli Yesu ni Mungu au la.

Adhama ya Kwanza kutokana na Quran: Mungu ni Mfalme:

Koran inasema kuwa, sifa Moja ya Mungu ni “Mfalme”. Je, Yesu anayo hii sifa ya “Mfalme”? Haya tusome Quran kwanza.

Quran 59: 23
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Sasa tuangalie kama kweli Yesu anayo hii sifa ya Mfalme ambayo ni adhama ya Mungu pekee kutokana na Koran.

Biblia takatifi inasema yafuatayo kuhusu Yesu Kristo:
Ufunuo 17:14
Hawa watafanya vita na Mwana Kondoo na Mwana Kondoo atawashinda, kwamaana yeye ni Bwana wa Bwana na Mfalme wa Wafalme.

Katika aya hii tunasoma kuwa Yesu anaitwa “Mfalme wa Wafalme” ambayo ni adhama ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo shaidiwa na Koran Surah ya 59 na aya 23. Hivyo basi , Allah na Koran wamekiri kuwa Yesu ni Mungu kwasababu Biblia imetuthibitishia kuwa Yesu ni Mfalme wa Wafalme katika Ufunuo 17 na aya 14.

Tuendelee na ushaidi mwingine kutoka Koran ambao unatuhakikishia kuwa Yesu ni Mungu.

Adhama ya Pili kutokana na Quran: Mungu ni Mtakatifu:

Je, Yesu anayo hii sifa ya “Mtakatifu”? Tusome Quran kwanza:

Quran 59: 23 Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Katika Quran tumesoma kuwa, moja ya sifa za Mungu ni “Mtakatifu”, Je sifa hii ya utakatifu Yesu anayo?

Nenda kwenye hihiyo Kuran 19:19 Malaika akasema hakika mimi ni mjumbe ili nikupe Mwana Mtakatifu -Isa Bin Maryam.

Koran hiyo hiyo inatuhakikishia na kutujibu kuwa Yesu ambaye anajulikana kwa jina la Isa Bin Maryam katika Quran ni Mwana Mtakatifu. Hivyobasi, hii adhama ya Utakatifu ambayo ni ya Mungu pekee, tunasoma katika Quran iliyoteremshwa an Allah kuwa Yesu ameinyakua. Yesu anaitwa Mwana Mtakatifu.

Adhama ya Tatu kutokana na Quran: Bwana ni Mwenyezi Mungu

Hebu tufungue Quran na tusome kuhusu Bwana:

Quran 3:39 Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni Bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema naye ni Nabii Isa. 

Quran 39: 29
Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanao gombana, na wa mtu mwengine aliye khusika na Bwana Mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao? Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui. 

Quran 39:29 inasema kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana na hiyo ni sifa njema kwa Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hapo, Koran hiyo hiyo (Quran 3:39) inasema kuwa Isa Bin Maryam ni Neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu na ni Bwana. Koran imejibu kuwa, sifa ya Bwana ambayo ni ya Mungu pekee ni ya Yesu. Sasa tusome na Biblia kwa ushaidi zaidi kuhusu Yesu ni Bwana.  

Ufunuo 17:14
Hawa watafanya vita na Mwana Kondoo na Mwana Kondoo atawashinda, kwamaana yeye ni Bwana wa MaBwana na Mfalme wa Wafalme.

Katika Ufunuo tunasoma kuwa Mwana Kondoo ambaye ni Yesu Kristo anaitwa Bwana wa Mabwana. Hivyobasi, hii adhama ya “Bwana” ambayo ni ya Mungu pekee tunasoma katika Quran iliyoteremshwa an Allah kuwa Yesu ni Bwana na ameinyakua, vilevile, katika Biblia Takatifu tumesoma kuwa Yesu anaitwa Bwana, ambayo ni Sifa ya Mungu Pekee kutokana na Quran.

Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni Mungu kwa kuwa Yesu anazo adhama zote na/au sifa zote za Mungu.

Katika huduma yake,

Max Shimba


Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW