USHAIDI WA KIBIBLIA
NA KORAN
Waumini wa dini ya
Kiislam wamekuwa na tabia ya kuseka kuwa, eti, Yesu alikuwa ni Muislam. Madai
haya ya Waislam yamekuwa yakisemwa katika mihadhara yao ya kidini bila ya kuwa
na ushaidi yakinifu kusaidia madai yao.
Leo nitajibu madai
haya kwa kutumia Biblia na Koran kama ifuatavyo:
YESU
HAKUWAI SEMA SHAHADA
Kufuatana
na sharia za Kiislam, ili mtu awe Muislam lazima aseme na au afanya shahada.
Yesu hakusema SHAHADA (La ilaha illallah) na hakuna ushaidi
wa Kibiblia au Koran unao sema kuwa Yesu alisema SHAHADA. Hivyo basi, Yesu
hakuwa Muislam.
YESU
HAKUWAI KUMWABUDU ALLAH
Yesu hakuwai kuomba
na au kumwabudu “Allah”, lakini kutokana na Biblia, Yesu aliomba kwa Baba yake,
Yohana 17:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho
yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao,
ili Mwana wako naye akutukuze wewe. Koran na Uislam unakiri kuwa Allah si Baba
na hakuna hata aya moja inayo mwita Allah Baba. Yesu hakuwa Muislam.
YESU
HAKUWAI KUOMBA HUKU AKIANGALIA MAKKAH
Yesu hakuwai kusujudu huku akiangalia
Makkah, jambo ambalo ni moja ya masharti katika kumwomba na au abudu “ALLAH”. Quran
2:149. Na popote wendako elekeza uso
wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi.
Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. 150. Na popote wendako elekeza uso wako
kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili
watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Basi
msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na
ili mpate kuongoka.
Sasa tumsome Yesu katika Biblia, wapi
aliangalia wakati akiomba.
Yesu aliomba huku akiangalia Mbinguni
soma: Marko 6: 41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama
mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie;
na wale samaki wawili akawagawia wote.
Katika aya tuliyo isoma hapo juu, imetupa
ushaidi kuwa Yesu aliangalia Juu Mbinguni ambapo Baba yake alipo na si Makkah.
YESU
HAKUFUNDISHA KUHUSU KAABA
Yesu
hakuwai sema na au fundisha wanafunzi wake kuhusu “KAABA”. Jambo ambalo tunaona
linafanywa na Waislam na lilifundishwa na Muhammad mtume wa Allah.
YESU
HAKUFUNGA SWAUMU KILA MWAKA
Yesu
hakuwa anafunga Ramadhani/Saumu kila mwaka, jambo ambalo ni sehemu ya Uislam
kufunga ramadhani kila Mwaka. Quran 2:183, Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu,
kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.
Hakuna hata sehemu moja katika Biblia ambayo tunasoma kuwa Yesu alitoa
amri kwa wafuasi wake kuwa ni lazima wafunge swaumu kila mwaka, lakini tunasoma
kuwa Mathayo 6:16-18: Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana;
maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin,
nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. 17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe
uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
YESU
HAKUFANYA JIHAD
Yesu
hakufanya Jihad kama ilivyo amri ya kila Muislam kufanya Jihad. Quran 2:216. Mmeandikiwa
kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni
kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu
anajua na nyinyi hamjui. Lakini Yesu alisema yafuatayo kuhusu kupigana: Yohana
18: 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu.
Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania,
nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.
Katika aya hapo juu, Yesu anatufundisha kuwa Ufalme wake si
wa hapa Duniani bali Mbinguni, hivyo basi hawezi kufanya Jihad kama Allah
alivyo waamrisha Waislam. Yesu hakuwa Muislam na hakufanya Jihad.
YESU ALISEMA PENDENI ADUI ZENU, WAKATI ALLAH ANASEMA
WACHUKIENI WAKRISTO NA WAYAHUDI
Yesu hakuwachukia watu ambao walikuwa wanampinga, lakini
aliwapenda na kuwaombea, kinyume na maamrisho ya Allah kwa Waislam wote. Soma
Mathayo 5:44. lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu,
waombeeni wanaowaudhi.
Sasa Msome Allah anavyo panda chuki kwa
wafuasi wake. Quran 5:51. Enyi mlio amini! Msiwafanye
Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni
mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi
Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
YESU HAKUFUNDISHA KUPIGA WAZINZI
MAWE
Yesu hakupiga watu Mawe na wala hakufundisha kuwa Wazinzi wapigwe Mawe
kama ambayo inafundishwa kwenye dini ya Uislam. Msome Yesu hapa: Yohana 8: 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate
sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na
dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Lakini katika Uislam tunamsoma Muhammad
akitoa amri ya kupigwa mawe mdhinifu: Volume 2, Kitabu 23, Namba 413:
Alisimulia 'Abdullah bin' Umar:
Myahudi kuleta kwa Mtume Muhammad watu wawili Mwanaume na
mwanamke ambao walikamatwa wakifanya uzinzi kinyume cha sheria za ngono. Mtume
Muhammad aliamrisha wote wawili wapigwe mawe mpaka kifo, karibu na mahali pa
sadaka ya sala ya mazishi iliyopo kando ya msikiti.
Hivyo basi Yesu hakuwa Muislam na hakupiga wazinzi mawe
lakini tunamsoma Muhammad akipiga watu mawe na akifundisha kupigwa mawe kwa
Wazinzi katika Uislam.
YESU HAKUFUNDISHA WATU WATAWADHE KABLA YA KUOMBA
Yesu hakufanya na au fuata sharia za kuosha na au kutawadha kama
ambavyo Waislam wanafanya kila siku. Msome Yesu katika Mathayo 15:2-11. Lakini Allah
anafanya mila za kuosha na au kutawadha mwili kabla ya kumwabudu. Quran 5:6.
Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na
mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka
vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au
mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi
tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi
Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza
neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.
Yesu hakuwa anatawadha kabla ya
kumwomba Baba yake kama ilivyo katika Uislam. Yesu hakuwa Muislam.
YESU HAKUWAI TUMIA MANENO “SAW”
AU “PBUH”
Yesu hakuwai waambia watu waandike vifupisho “SAW” na “PBUH” baada ya
kutaja majina yao, kinyume chake Allah na Mtume wake wanafundisha kusema hivyo
katika Uislam baada ya kutaja majina ya Mitume na Manabii.
Ndugu wasomaji, leo tumemsoma Yesu na
tumesoma tabia yake na mafundisho yake
machahe ambayo yote yanapinga sheria na mila za kiislam.
Ni mategemeo yangu kuwa, kijarida hiki kitakusaidia kuelewa
kuwa Yesu hakufuata mila za Kiislam na wala hakumwabudu Allah.
Mungu awabairiki sana
Katika Huduma Yake
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment