Adui wa Jibril au Roho Takatifu?
Somo letu la leo tutazungumzia utata ulio jaa ndani ya Koran. Leo hii tutajinfunza kuhusu nani alikuwa wa kwanza kuteremsha Koran kwa Mtume wa Allah.
Katika Qura 2:97 tunasoma kuwa, Jibril ndie aliye kuwa wa kwanza kushusha aya za Quran kwa Mtume wa Allah. Soma kifungu hiki hapa:
Quran 2:97. Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.
Hiyo aya hapo juu ipo wazi kabisa kuwa, aliye kuwa adui wa Jibril ndie aliye kuwa mshushaji wa Quran kwa Mtume wa Allah ajulikanaye kwa jina la Muham'mad. Hebu tuendelee kusoma Quran hiyo hiyo na tuone kama ni kweli adui wa Jibril alikuwa wa kwanza kufanya hiyo kazi au kulikuwa na mtu mwingine aliye kuwa anafanya kazi hiyo hiyo ya kushusha Quran kwa Mtume wa Allah.
Rejea hapa:
Quran 16:102. Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu.
103. Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu mbayana.
Katika aya tulizo zisoma hapo juu, tunagundua kuwa Allah alimtumia Roho Takatifu kushusha Aya kwa Mtume wake na si Jibril kama wanavyo dai Waislam na tulivyo soma kwenye Surah 2 aya 97 ni Adui wa Jibril ndie aliye shusha Quran.
Katika Surah 2:97 tunasoma kuwa Mteremshaji wa Quran ni adui wa Jibril.
Katika Surah 16:102-103 tunasoma kuwa Roho Takatifi ndie anateremsha Quran.
Ndugu zanguni. Hivi kwanini Koran inamakosa namna hii? Nani alikuwa mteremshaji wa Koran? Ni Adui wa Jibril au Roho Takatifu?
Nimategemeo yangu kuwa, hili soma litawafungua macho na kufahamu ukweli kuhusu Quran. Kama kweli Allah ni Mungu na yeye ndie aliye kuwa anaishusha Quran kupita Jibril, basi asinge fanya kosa la kumsingizia Roho Takatifu kuwa na yeye alikuwa anashusha Quran au Adui wa Jibril.
Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini afanye makosa makubwa namna hii?
Je, Roho Takatifu ni adui wa Jibril?
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Max Shimba
For Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Muhammad’s Fear Of Judgment Day
Muslims beware! The next eclipse could be the Day of Judgment . This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment