Somo
letu la leo ni la swali kwa Allah ambaye ameshindwa kujieleza, kuwa ni kipi
kinaingia Peponi kati ya Roho/Nafsi au Mwili?
Koran
inadai kuwa, baada ya ufufuo, ni mwili (baada ya kuungana na roho?) Ambayo
inaingia peponi. Haya madai yamewekewa mkazo katika Koran. Angalia mistari ifuatayo
13:05, 17:98-99, 20:55, 34:7, 75:3-4.
Hata
hivyo mistari ya 27-30 kwenye Sura 89 ipinga aya zilizo pita kwa kusema kuwa ni
nafsi (Nafs) tu ambayo inaingia Peponi!
Quran 17:99. Kwani
hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza
kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini
madhaalimu hawataki ila ukafiri.
Quran 75:3. Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya
mifupa yake? 4. Kwani! Sisi tunaweza
hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
Aya hizo
hapo juu, zinadai kuwa Nafsi na Mwili vitaungana na kuingia Peponi, hayo ni
maneno ya Allah kama alivyo yashusha kupitia Quran yake. Lakini Allah huyohuyo
anabadilika na kusema kuwa Nafsi ndio itaingia Peponi. Hebu soma aya zifuatazo.
Katika
aya hapo juu, Allah anaiamuru Nafsi irejee kwake. Sasa ni ipi kati ya Nafsi na
Mwili vitaingia Peponi? Utata huu ni Msiba Mkubwa kwa Allah ambaye hafamu nini
kati ya Nafsi na Mwili vitaingia Peponi.
Quran 31:28.
Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.
Allah anaendelea kusema kuwa ni Nafsi ndio itaingia
Peponi. Aya hizi zinapingana na maneno yake ya kwanza kuwa ni Nafsi pamoja na
Mwili vinaingia Peponi. Hivi Allah ni kweli aliumba Binadamu? Mbona hafahamu
nini kati ya Nafsi na Mwili itaingia Peponi?
Katika Uislamu, neema ya peponi haikamiliki bila
raha ya pamoja ya Mwili na akili, maana Allah katoa ahadi ya wake 72 kwa wale
wote watakao ingia Peponi. Vinginevyo, mtu atawezaje kunywa Zanzabil (76:17), na
kuifurahia hicho kinywaji (76:13), kufurahia wanawali (55:56) na kunywa asali
na maziwa (47:16-17) bila ya kuwa na Mwili?
Yousuf
Ali (Nakala 6128 kwa aya 89:27-30) pia anasema kwamba ni roho ambayo inaingia
mbinguni, na si mwili ambao utaharibika (Maoni yake ni kupingana na aya 75:3-4 zinavyo
sema!). Soma aya 31:28 pia. Inasema kuundwa kwa mtu au ufufuo ni katika nafsi.
Ndugu
wasomaji, Allah anaendelea kutoa utata katika uumbaji wake. Allah kwa mara
nyingine tena ameshindwa kuufahamisha umma wake kuwa, ni nini kati ya Nafsir na
Mwili vitaingia Peponi.
Koran si
kitabu cha Mungu bali ni maneno ya Muham-mad ambayo alindika ili kukuza maono
yake ya kisiasa. Kama Allah ni mungu, basi ifahamike leo kuwa Allah si Mungu
aliye umba Mbingu na Nchi. Si Mungu aliye muumba Adamu na Hawa, bali ni Mpinga
Mungu.
Katika
huduma Yake.
Max
Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment