Sunday, November 24, 2013

UTATA KATIKA UUMBAJI, ALLAH KAUMBA KILA KITU KATIKA JOZI (PAIR):

Allah wa dini ya Kiislamu amekuwa na tabia ya kuchanganya mambo, jambo ambalo linafanya wataalam wa mambo ya dini kujiuliza maswali ambayo yanakosa majibu kutoka kwa Allah.

Katika somo letu la leo, Allah anasema kuwa, aliumba kila kitu katika “JOZI” (Pair). 

Quran 51:49. Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. 

Allah anadai kuwa kila kitu amekiumba kwa jinsia mbili, jinsia ya kiume na jinsia ya kike kama alivyo sema kwenye aya hapo juu.

Hebu tumwangalie binadamu, je, kuna jinsia mbili za kiini cha damu yako (blood cell). Kufuatana na madai ya aya hapo juu, Allah anasema kuwa hata kiini cha damu yako kipo kwa jinsia mbili. Hivi, kweli Allah aliumba? Mbona anaonyesha upungufu wa hekima na uelewo wa sayansi? Unaweza kusema kuwa, labda Max Shimba anamsingizia Allah au labda Max Shimba ameshindwa kuielewa hiyo aya, kwasababu ya kushindwa kuisoma katika lugha yake ya asili, nikimaanisha Kiarabu. Endelea kusoma Koran na tuone kama kweli ni makosa ya kusoma na kuelewa au ni Allah mwenye kukosa ufahamu katika uumbaji.

Allah kaumba Matunda Dume na Matunda Jike:
Quran 13: 3. Na ndiye aliye itandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya dume na jike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.

Allah anasema kuwa Nukuu “Na katika kila matunda akafanya dume na jike”. Ameumba Matunda Dume na Jike!!! Haya kweli ni maajabu ya uumbaji wa Allah. Labda ndugu msomaji wewe umesha wai ona Ndizi Dume na Ndizi Jike? Labda umesha wai kubahatika kula Embe Jike na Embe Dume, lakini katika dunia tunayo ishi hii leo, hayo madai ya Allah yanashindwa kujitekeleza na kukosa ushaidi wa aina yeyote ile. Huu ni Msiba katika dini ya Allah.

Hebu tuangalie baadhi ya viumbe ambavyo haviitaji jinsia mbili ili vizaliane.

Bakteria, Kuna kundi zima la fungi (Deuteromycete / Fungi Imperfecti ) ambao hawana mizunguko ya ngono. Kuna kundi zima la viumbe wich ambalo haliitaji ngono ili kuzaliana. Mimea yote ni ya jinsia moja.
Basi, kuna minyoo ambayo huzaliana kwa kujamiiana lakini wote ni wa jinsia na au aina moja, wanaitwa “huntha". Konokono karibia wote ni wa aina ya huntha (hermaphrodite).

Kufuatana na ukweli niliouweka hapo juu, basi lazima tujiulize maswali yafuatayo:

1. Je, inawezekana kuwa labda Allah alikosea kuteremsha aya hizi za Koran?
2. Au inaweza kuwa kwamba mtu ambaye alikuwa anamakosa hakuwa Allah bali ni Jibril aliye shusha hizi aya kimakosa?
3. Labda ukosaji wa Elimu wa Muhammad ulisababisha makosa haya ya kisayansi?

Ndugu wasomaji:

Mungu huwa hafanyi makosa wala hatendi dhambi. Hiyo ni sifa na adhama pekee ya MUNGU. Lakini, Allah ameonyesha MAKOSA NA UTATA MWINGI SANA katika Koran.

Je, Allah aliumba? Hebu soma hii aya:
QURAN 92 1-3
1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..

Katika aya hapo juu, ALLAH ANAAPA KWA ALIYE UMBA KIUME NA KIKE

Je Nani kaumba Kiume na Kike?

Ni mategemeo yangu kuwa, kijarida hiki kitakusaidia kuelewa kuwa. Mungu muumbaji ni Jehova wa Biblia na Allah wa Koran anaapa kwake.

Mungu awabairiki sana

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW