UTATA KATIKA KUUMBA DUNIA
Je, Allah aliumba Dunia kwa siku 6 au 8?
Katika somo letu la leo, tutajifunza kuhusu
uumbaji wa Dunia. Allah wa Uislam, anasema kuwa yeye ni Mungu na aliumba Dunia
na vitu vyote vilivyo ndani yake. Hebu tuanze somo letu kwa kusoma aya za
Quran.
Allah anasema katika Sura 7:54, 10:3, 11:7,
na 25:59 kuwa, aliumba dunia kwa siku 6.
Soma aya hizi hapa chini kwa ushaidi zaidi.
Quran 7:54. Hakika Mola Mlezi wenu ni
Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala
juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua,
na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni
zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Surah 10: 3. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba
mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha
mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi
Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?
Lakini Ndugu zanguni, nilipo endelea
kuchunguza Quran nikagundua kuwa, kumbe Allah alidanganya pale alipo sema kuwa
aliumba Dunia kwa siku sita. Sasa ungana nami katika uchunguzi wa uumbaji wa
dunia kama ulivyo wekwa kiuwazi zaidi kupitia Quran iliyo shushwa na Jibril.
Sasa tutasoma Surah ya 41: 9-12. Katika hizi
aya tutakazo zisoma, utangudua kuwa Allah hakuumba Dunia kwa Siku 6 kama alivyo
dai hapo mwanzoni.
HII AYA INASEMA ALLAH KAUMBA KWA SIKU MBILI
(2)
Quran 41:9. Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba
ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa
walimwengu wote.
+
HAPA ALLAH ANAUNGANISHA
MAWINGU NA ARDHI KWA SIKU NNE(4)
Quran
41:10. Na akaweka humo
milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika
siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza 11. Kisha akazielekea
mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa
nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu.
+
HAPA ALLAH ANAZITENGENEZA
MBINGU KWA SIKU MBILI (2)
Quran
41:12. Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na
akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na
kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua.
HIZI ZOTE KWA PAMOJA NI SIKU NANE (8)
Siku mbili kwa ajili ya viumbe wa dunia, basi
siku nne kujaza ardhi na milima baraka, na chakula kwa ajili ya wakazi wake
wote, na mwisho kwa siku mbili zaidi ili kujenga mbingu saba na kujenga nyota
yao. Hii inaongeza hadi 2 + 4 + 2 = siku 8 kinyume na siku 6 zilizotajwa katika
aya nyingine.
NGOJA NIWEKE KWA UFUPI
Muundo ni wazi sana: Haya ni Matabaka Matatu ambayo
ni umbaji chini hadi juu:
Quran 41:9*** Mbingu
[angani, "dari" juu ya dunia] katika siku 2
----------
Quran 41:10*** BARAKA [kujaza dunia na kila kitu zinahitajika kwa
ajili ya maisha] katika siku 4
---------
Quran 41:12***EARTH [msingi] kukamilika katika siku 2
Ndugu
zanguni, hivi Allah alishindwa mahesabu au ndio kutuhakikishia kuwa yeye hakuwa
Muumbaji? Kwanini Allah afanye makosa makumbwa namna hii? Leo Allah kwa mara
nyingine tena ametuhakikishia kuwa yeye si Muumbaji. Uchaguzi ni wako, kufuata
Allah asiye fahamu aliumba Dunia kwa Siku Ngapi au Jehova ambaye alisema
aliumba Dunia kwa siku 6.
Katika huduma yake.
Max Shimba
For Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment