Saturday, November 16, 2013

NI NANI MWANZILISHI WA MABAYA NA MAZURI?

Koran inakujibu kuwa Allah ndie mwanzilishi wa dhambi!!!!

Somo letu la leo ni kujifunza asili ya Ubaya(dhambi) na Mambo Mema kutoka na imani ya Kiislamu. Koran inakiri kwamba Mambo yote Mabaya na Mema asili yake na au mwanzilishi wake ni Allah. 

Hebu tusome Koran iliyo jaa shaka. Quran 16:93. Na Allah angeli taka, kwa yakini angeli kufanyeni umma mmoja. Lakini anamwachia kupotea anaye mtaka, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa kwa yale mliyo kuwa mkiyafanya.

Kitendo cha Allah kuwaongoza watu ili wafanye dhamb, hapo ni kutuonyesha kuwa kumbe mwanzilishi wa dhamb ni Allah wa Islam. Aya inatuambia kuwa ni Allah anaye waongoza watu katika dhamb.

Endelea kusoma Koran

Quran 15:39. Shetani akasema: Oooh Allah! Ilivyo kuwa umenifanya niwe mtenda dhambi, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,

Shetani analalamika kwa Allah. Shetani anasema kuwa ni Allah aliye mfanya awe mtenda dhamb. Kumbe Allah wa Uislam ndie mwanzilishi wa dhambi.

Endelea kusoma Koran

Quran 67:2. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.

Allah anaendelea kukiri kuwa yeye ndie mwanzilishi wa MAUTI, wakati katika Biblia tunafundishwa kuwa Mauti ilikuja kwasababu ya dhambi. Soma neno la Mungu katika Biblia Takatifu.

Warumi 6: 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Biblia inatuambia kuwa, mshahara wa dhambi ni Mauti, na wakati huohuo Allah anasema kuwa yeye ndie anatoa Mauti!! Kumbe Allah ndie dhambi. Kumbe kumfuata Allah kunazalisha mauti. Sasa kwanini tumfuate Allah ambaye ndie mwanzilishi wa mauti? Kumbuka Mshahara wa dhambi ni Mauti.

Lakini Mungu wa Biblia anasema kuwa yeye ndie Mtoa uzima wa Milele, rejea katika Warumi 6:23 Nukuu “bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Ndugu wasomaji. Mpokeeni Yesu aliye hai ili upate karama ya Mungu ambayo ni Uzima wa Milele katika Kristo Yesu.

Biblia inaendelea kusema kuwa Yesu ndie Njia kweli na Uzima. Mtu haendi kwa Baba bila kupitia kwa Yesu.

Ni mategemeo yangu kuwa, utachukua hatua na kuachana na Allah aliye sema kuwa yeye ndie mwenye MAUTI. Mpokee Yesu aliye hai.

Katika hudumua yake,

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW