Saturday, November 16, 2013

NANI ANAPOTOSHA WATU ILI WAENDE JEHANNAM, ALLAH AU SHETANI?

Ndugu wasomaji. 

Kwa mara nyingine tena, tunaziona sifa za Shetani ndani ya Allah wa dini ya Kiislamu. Adhama ya kuwaongoza watu ili waende Jehannamu ni ya Shetani kama ilivyo semwa kwenye Biblia Takatifu. Lakini nilipo soma Koran kwa makini, nikagundua kuwa kumbe na Allah anayo hii adhama ya kupeleka watu Jehannam. 

Hebu tumsome Allah kwenye kitabu chake alicho kiteremsha kupitia Jibril kwa Wafuasi wake waitwao "WAISLAMU".

Kwanza: Tumsome Shetani anavyo jisifia kuwa yeye ndie anaye poteza watu. Soma:

Quran 4:119-120
119. Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Allah, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri. ***

Katika aya ya 119 hapo juu tumesoma kuwa Shetani amesema kiuwazi kabisa kuwa yeye ndie awapotezao watu ili wafuate njia iendayo Motoni.

120. Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shet'ani hawaahidi ila udanganyifu. ***

121. Hao makao yao ni Jahannamu, na wala hawapati makimbilio kutoka humo.

Shetani anaendelea kusema kuwa yeye ndie anaye tia watu tamaa mbaya na atawapeleka wote ambao watamfuata katika makao yake makuu ambayo ni Jehannam. Koran inasema kuwa Shetan ndie anaye wapoteza watu, au sio? Sasa tumsome Allah, anasema nini katika Koran hiyo hiyo?

Quran 16:93. Na Allah angeli taka, kwa yakini angeli kufanyeni umma mmoja. Lakini anamwachia kupotea anaye mtaka, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa kwa yale mliyo kuwa mkiyafanya. ***

Allah nayeye anasema yaleyale aliyosema Shetani. Allah anasema kuwa yeye anamwachia binadamu apotee kwa matakwa yake. Ikimaanisha kuwa Allah na yeye anapeleka watu Jehannam kama afanyavyo Shetani. Hii sifa ya kupeleka watu Jehannam ni ya Shetani, lakini sasa tunaiona hii sifa kwa Allah ambaye ni mungu wa Waislam.

Hebu tuendelee kusoma Allah kwa ushaidi zaidi.

Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.

Allah katika aya hapo juu ameamua kuwa muwazi zaidi kwa kusema kuwa, kumbe wale ambao ameamua kuwapeleka Jehannam ni Waislam ambao wanamuabudu na kujisifia kuwa wanafuata dini ya haki.

Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana katika dini na taifa la Kiislam. Allah kwa mara nyingine tena anasema kuwa Waislam wote wataingia Jehannam. Hayo ni matakwa ya Allah kutokana na Surah 16 aya 93.

Swali la kujiuliza ni hili: Ni Mungu gani huyu mwenye upendo awaingize watu wote wanao muabudu Jehannam? Je, Jehannamu ilitengenezwa kwa wanao mwabudu Mungu au wanao mwabudu Shetani? Je, kuna uwiano wowote ule kati ya mapenzi ya Allah na Shetani? Jibu umesha lipata kuwa Jehannam ilitengenezwa kwa ajili ya Shetani na Wafuasi wake, na si kwa wale wanao mfuata Mungu aliye hai, Mungu wa Biblia ajulikanaye kwa jina la Yehova. Allah kasema kuwa wale wote wanao mwambudu wataingia Jehannam. Je, Allah na Shetani ni yuleyule mmoja?

Ni mategemeo yangu kuwa, utachukua hatua na kuachana na Allah aliye sema kuwa ni matakwa yake kuwaingiza watu Jehannam.

Katika hudumua yake,

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW