Thursday, November 7, 2013

MUHAMMAD ANADAI KUWA ALIMUONA ALLAH: AISHA ANASEMA YEYOTE YULE ASEMAYE MUHAMMAD ALIMUONA ALLAH NI MUONGO

Kama kawaida, naendelea kufunua uongo na vituko vilivyo jaa kwenye Koran na Hadith. Katika somo letu la leo, tutajifunza uongo ulio semwa na Muhammad, eti, alimuoana Allah. Soma aya ifuatayo kutoka Koran iliyo shushwa na Jibril.

Quran 81:15. Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, ***16. Zinazo kwenda, kisha zikajificha, ***17. Na kwa usiku unapo pungua, ***18. Na kwa asubuhi inapo pambazuka, ***19. Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, ***20. Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, ***21. Anaye t'iiwa, tena muaminifu. *** 22. Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. ***23. Na hakika yeye alimwona Mwenyezi Mungu kwenye upeo wa macho ulio safi. ***24. Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. ***25. Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. ***26. Basi mnakwenda wapi? ***27. Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. ***28. Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. ***29. Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.  *** 

Katika aya ya 23, Koran inatuambia kuwa Muhammad alimwona Bwana wake/Allah kwenye upeo wa macho ulio safi. Lakini Maswahiba wa Allah walipo Muuliza mke wake Aisha kama ni kweli Muhammad alimuona Allah, Aisha alikana na kusema asemaye kuwa Muhammad alimwona Allah ni MUONGO. Pata ushaidi hapa chini:

(Sahih al-Bukhari, Volume 9, Book 93, Number 477)
Amehadithia Masruq:
Mimi nilimuuliza 'Aisha, "O Mama! Je Mtume Muhammad aliwai kumuona Bwana wake?" Aisha akasema, "Kile umesema hufanya nywele yangu kusimama juu ya mwisho kujua kwamba kama mtu atakwambia moja ya mambo matatu yafuataho, HUYO NI MUONGO!. Yeyote atakayekwambia kwamba Muhammad alimwona Bwana wake, NI MWONGO"

Ndugu zanguni, leo tumejifunza kuwa, kumbe Muhammad alikuwa MUONGO, pale alipo dai kuwa eti, alimwona Bwana wake. Aisha amesema kuwa YEYOTE YULE ATAKAYE SEMA KUWA MUHAMMAD ALIMWONA BWANA WAKE NI MUONGO.

Je, Maneno ya Aisha yanaukweli, Hebu tuangalie Biblia inasema nini. Katika Injili ya Yohana Biblia inasema kuwa, HAKUNA ALIYE MUONA MUNGU, ISIPOKUWA MWANA(YESU).

Yohana 1: 18Hakuna mtu ye yote aliyemwona Mungu wakati wo wote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye memdhihirisha.

Biblia ipo wazi kuwa, Mwenye uwezo wa kumwona Baba ni Mungu Mwana. Leo tumejifunza kuwa Yesu ni Mungu Mwana. Mtu wa kawaida hawezi kumuona Mungu na akaishi. Zaidi ya Hapo leo tumejifunza kuwa Mtume wa Allah ni MUONGO.

Nakukaribisha kwa Mungu Mwana ambaye yeye yupo Upande wa Kulia wa Baba. Mwamini Yesu hii leo ili upate uzima wa milele.

Katika huduma yake.

Max Shimba

For Max Shimba Ministries


Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW