Wednesday, November 6, 2013

KUTOKANA NA KORAN: YESU ANAUMBA, ANAPONYA, ANAFUFUA WATU, LAKINI MUHAMMAD HAKUWA NA UWEZO HUO

Koran leo imekiri kuwa Yesu ni zaidi ya Mtume. Ukisoma hii aya hapa chini utaona kuwa Yesu aliumba, hii sifa ya kuumba ni ya Mungu Pekee. Yesu alifufua watu, Yesu Aliponya watu. n.k. Lakini hatusomi kuwa Muhammad alifanya hayo.  Hebu soma Koran.

Quran 5: 110. Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!

Ndugu zanguni, leo tumejifunza kuwa Yesu hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa anafanya mambo ambayo ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya hao. Ushaidi huu umewekwa kwenye Koran. Madai ya kuwa Yesu alikuwa Mtume/Nabii kama wengine, yanashindwa nguvu, baada ya kusoma hii aya ambayo imetuonyesha adhama ya Mungu ndani ya Yesu. Je, kuna Nabii au Mtume yeyote Yule aliye wai kuumba?

Hebu tusome hadith ifuatayo kutoka kwa Al Bukhar.

Ibn 'Abbas akasema, "Hiyo ilionyesha kifo cha Mtume wa Allah ambacho Allah alimtaarifu." 'Umar alisema, "Sielewi haya isipokuwa kile wewe unakielewa." 'Aisha: Mtume katika maradhi yake ambayo yalimuua, Alikuwa akisema, "O' Aisha bado nahisi maumivu yanayosababishwa na chakula nilicho kula nilipo kuwa Khaibar, na kwa wakati huu, Najisikia kama aorta   yangu inakatwa kutoka sumu niliyo kula. "(Sahih al-Bukhari, Volume 5, Kitabu 59, Namba 713)

Kwenye Hadith tuliyo soma tunaona kuwa Mtume wa Allah alikuwa anasumbuliwa na Sumu aliyo lishwa kwa Mtego na Yule Mama wa Kiyahudi. Hadithi hii inatupa ushaidi kuwa Mtume wa Allah alikuwa akiomba uponyaji kutoka kwa Allah. Swali la kujiuliza, Je, Muhammad alipo baada ya maombi haya  kwa Allah?

Endelea kupata somo:

Kwenye hadith ifuatayo hapa chini, tunasoma kuwa Jibril nayeye amekuja kumuombea uzima Mtume wa Allah, lakini maombi hayo hayakumponya Mtume wa Allah.

Kutoka kwa Ibn Sad ukurasa 265
Mtume wa Mwenyezi Mungu aliugua na yeye yaani Gabriel, alimuombea juu yake, akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu mimi nakuombea uzima na nazuia kutoka kwenu kila kitu kibaya na madhara yeyote (kuizuia kwako wewe) dhidi ya hasidi kila na kutoka kila uovu na Allah atakuponya.

Je, Baada ya haya Maombi, Mtume wa Allah alipona? Kutokana na Hadith yetu ya kwanza, Mtume wa Allah hakupona licha ya kupata Maombi kutoka Malaika Jibri. Lakini katika Koran tunasoma kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kuponya watu, kufufua watu, kuumba, jambo ambalo Jibril na Mtume wa Allah, Muhammad hawakuwa nalo.

Ndugu zanguni,

Kwanini mfuate Mtume ambaye hakuwa na uwezo wa kuponya?

Kwanini mumsikilize, Malaika ambaye hakuwa na Nguvu za kuponya, licha ya kuwa alitumwa na Allah?

Kwanini Allah amtume Jibril kwenda kumwombea Mtume Muhammad, huku akifahamu fika kuwa Muhammad hato pona?

Hayo ni maswali machache tu ambayo unaweza jiuliza. Je, Allah ni Mungu? Kama ni Mungu, kwanini alishindwa kuponya Mtume wake Muhammad (Pbuh)?

Biblia inasema yafuato kupitia Injili kutokana na Marko.

Marko 16: 17“Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina Langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, 18watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu cho chote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,
nao watapona.”
Wakristo wamepewa uwezo wa kuombea wagonjwa katika Jina la Yesu, jamba ambalo halipo kwenye Uislam. Biblia inasema kwa Jina la Yesu, tutatoa Pepo Wachafu, n.k. Haya mamlaka tumepewa na Yesu. Yesu ametupa Jina lake ambalo lipo juu ya majina yote. Ndio jina pekee linaloweza kutoa pepo, kuponya, kufufua na kufanya mengi. Yesu hakuwa Nabii au Mtu wa Kawaida. Matendo yake yanajidhihiriza kila siku kupitia wafuasi wake.

Nawasihi mumpokee Yesu ambaye alikuwa na uwezo wa kufufua watu, kuponya watu na kuumba. Haya maneno yamesemwa na Allah kwenye Koran na Biblia inakiri hayo.


Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini alimtuma Jibril kumwombea Muhammad wakati akifahamu kuwa Muhammad atakufa?

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW