Malaika
Watabiri Mwenendo wa Binadamu kabla ya kuumbwa. Allah atumia hila kuficha
udhaifu wake.
Katika
somo letu la leo, tutajifunza kuwa Malaika wa Allah wana Akili na ufahamu wa
mambo ya baadae kuliko Allah wa Islam.
Quran
Surah 2:
30.
Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi
Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na
kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu
wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua. ***
KATIKA
AYA YA 30. Tunasoma kuwa Malaika wanampa
darsah Allah, jinsi gani Mtu atakuwa kabla ya uumbaji wake. Malaika
wameonyesha upeo mkubwa kwa kufahamu maisha ya baada ya Adam/binadamu kabla ya
hata kuumbwa.
31.
Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na
akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. ***
Kwenye
aya 31 hapo juu, tunasoma kuwa Allah anamfundisha kwa siri Adam ili aweze
kuwazima mdomo Malaika. Kitendo cha Allah kumfudisha Adam ili kushindana na
Malaika haikuwa haki kwani Malaika walimpa changamoto Allah, Je, Allah ni
mwenye ufahamu wa yote?
32.
Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza
Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima. ***
Je, Allah
alipo tumia udanganyifu na uongo ili kujitetea mwenyewe dhidi ya mashtaka kwa
Adamu kama yalivyo letwa na Malaika (mashtaka ambayo aligeuka kuwa ni sahihi)
ni sahihi?
33.
Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema:
Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua
mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha? ***
34.
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis,
alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri. ***
35.
Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo
maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale
walio dhulumu. ***
36.
Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo, na
tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa
makaazi yenu na starehe kwa muda. ***
37.
Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia
toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. ***
38.
Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi
watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.
***
Katika
vifungu hapo juu, tumesoma kuwa Malaika wanaufahamu kama Mungu (Omniscient) na
ua wa Kimungu. Malaika waliweza kufahamu maisha ya Mwandamu kabla ya hata
kuumbwa. Jambo ambalo Allah wa Islam hakulifahamu na hakuwa na ufahamu huo.
Kwanza,
jinsi gani Malaika walijua hali ya mtu itakuwa kabla ya uumbaji wake? Malaika
walifahamuje kabla ya uumbaji kuwa, binadamu watakuwa na vurugu? Nani
aliwaambia? Nakala haisemi chochote juu ya Allah kuwapa kipande hiki cha
habari. Je, Malaika anayajua yote kama Mungu (Omniscient)?
Pili,
Mwenyezi Mungu kwa siri anafundisha Adam majina yasiyojulikana ili
kuwanyamazisha Malaika kwa kulalamika dhidi ya mtu. Je, hii ni haki? Kwa nini
Allah anatumia hila na hujmah, ili kuwafanya Malaika waonekane hawana ufahamu?
Je, Allah
alipo tumia udanganyifu na uongo ili kujitetea mwenyewe dhidi ya mashtaka kwa
Adamu kama yalivyo letwa na Malaika (mashtaka ambayo aligeuka kuwa ni sahihi)
ni sahihi?
Je,
si dhahiri kwamba Adamu angekuwa na ufahamu wakawaida kama Malaika kwasababu
Allah alikuwa bado hajawafundisha kuhusu uumbaji wake?
Kwanini
Allah wa Islam anatumia udanganyifu ili kuficha udhaifu wake katika uumbaji?
Ndugu
zanguni, leo tumejifunza kuwa Allah si msema ukweli na Allah hana ufahamu wa
mambo yote kama alivyo Yehova ambaye ni Mungu aliye semwa ndani ya Biblia.
Kama
unataka kufahamu kweli, basi nakusihi umpokee Yesu aliye hai, yeye ndie Njia,
Kweli na Uzima. Katika Yesu, hakuna udanganyifu wa Allah. Mpokee leo ili upate
uzima wa milele.
Katika
huduma yake.
Max
Shimba
For
Max Shimba Ministries
Copyright
© Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment