Katika
hii mada ninawaletea ushaidi kuwa Uislam ni dini ya Waarabu peke yao.
Waislamu
bila kuchoka wamekuwa wakidai kuwa Uislamu utatawala dunia nzima. Katika
kufanya hivyo, wao watakuwa wamekwenda kinyume na maneno ya Allaha kama yarivyo
teremshwa kwenye Qur'an. Kwa hiyo, ni haki kwa kusema wao ni Makafiri.
Quran 10: 47. Na
kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu,
wala hawakudhulumiwa.
Angalia hii aya pia
Quran 14: 4. Na
hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah
humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye
nguvu na Mwenye hikima.
Kama
aya hizi ni kweli, basi Uislamu si kwa mashirika/mataifa/ummah yasiyo ya
Waarabu. Quran inasema kwamba kila watu wamepokea ujumbe wao kutoka kwa Mungu
katika lugha yao wenyewe ili waweze kuelewa na Qur'ani akaishuka kwa Waarabu ili Waarabu waweze kulewa nini
Allah anasema.
Dhana
hii ya Allah kushusha Kitabu kwa kila lugha ni muhimu sana kwasababu imejirudia
mara nyingi na ndio msingi wa hili somo.
Quran 16: 36. Na kwa hakika kwa kila
umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.
Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio
wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa
wanao kanusha.
Quran 5: 48. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi
kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi
hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio
yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake
na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma
mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya
kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale
mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Quran 36: 5. Uteremsho
wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 6. Ili
uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.
Hizi aya zimekamilka na kueleza kiuwazi kuhusu
kuja kwake kwa Waarabu pekee. Allah katika Koran anasema kwamba kila watu wamekuwa
na Mtume wao wenyewe ambao aliwaonya katika lugha zao wenyewe, na kwamba
amemtuma Muhammad kwa wale ambao bado hawajaanza mwongozo wowote, na ambao baba
zao hawakuonywa, yaani Waarabu. Kwa njia hii watakuwa hawana udhuru wowote na
hawezi kusema, lakini hatukuwai kupokea ujumbe wowote.
Endelea kusoma Koran hapa chini:
Quran 6: 156. Msije
mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi
tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma.
157. Au
mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko
wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na
rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara
za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu
adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
Quran
ni wazi ilitumwa kwa Waarabu. Wale ambao si Waarabu hawawezi kuielewa Koran,
hayo ni maneno ya Allah. Waislamu wanasisitiza kuwa hakuna tafsiri ya Qur'ani inaweza
kuwa sahihi. Hivyo, haiwezi kamwe kuwa wazi kwa mashirika yasiyo ya Waarabu na
haikutumwa kwa mashirika/ummah yasiyo ya Waarabu.
Uthibitisho
mwingine kuwa Qur'ani ilitumwa tu kwa ajili ya Waarabu ni katika mistari
ifuatayo hapo chini:
Quran 26:
198. Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, 199. Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
Kama ambavyo Waarabu wana
haki ya kuto amini kitabu chechote kile kilichotumwa kwa lugha ambayo si
yakwao, ikimaanisha Kiarabu, vivyo hivyo, mashirika yasiyo ya Waarabu nao wana
haki ya kuto iamini Koran, kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Ndio
kwasababu Koran inasema Allah atatuma mjumbe kwa kila lugha ili wao wenyewe kwa
wenyewe waweze kuelewa.
Kuhakikisha hakuta kuwa na kutokuelewana, Allah anashusha hii aya
05:19 Quran: Enyi Watu wa
Kitabu! Bila ya shaka amekujilieni Mtume wetu akikubainishieni katika wakati
usio kuwa na Mitume, msije mkasema: Hakufika kwetu mbashiri wala mwonyaji. Basi
amekujieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu anao uweza wa kila kitu.
Kwa mujibu wa Qur'an watu wote wamepokea ufunuo. Aya ya hapo juu inasema
Qur'ani ni kwa wale ambao kamwe hawakupokea ufunuo, iliwasije kusema, `kuwa sisi
hatuja wai kutumiwa mbashiri na hakuna mjuonyaji aliye tumwa kwetu'.
Jambo hili ni wazi, lakini Allah anataka liwe wazi hata na kwa asiye
na ufahamu wowote ule aelewe kuwa Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee kwa kuzitaja
sehemu halisi za kijiografia ambazo Muhammad alitumwa kama Mtume wa Allah.
Quran 6:92. Na hiki ni Kitabu
tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na
ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera
wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao.
Leo,
tumejifunza kuwa, Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee na si kwa Mataifa yote. Sasa,
nina uhakika baadhi ya Waislamu wanaweza kuleta aya nyingine zinazosema kwamba Uislamu
ni kwa wanadamu wote. Kama Waislam watafanya hivyo, basi waelekuwa kwa kufanya
hivyo ni kuthibitisha kwamba aya hapo juu ni za uongo.
Ama
Quran ni pakiti ya uongo na utata au ni tu kwa Waarabu wa Makkah na jirani yake
kama alivyo sema Allah ambaye ni mungu wa Waislamu.
Katika
huduma yake,
Max
Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment