Je, Allah na Shetani ni yule yule mmoja?
Katika ujumbe wa leo, nitaweka ushaidi wa Kibiblia na Koran ambao unatuambia kuwa, Allah ambaye ndie mungu wa dini ya Kiislamu ni muongo.
Biblia inasema kuwa MUONGO ni yeyote yule anaye sema Yesu si Kristo na anaye mkana Baba(Jehovah) na Mwana (Yesu).
Hebu tusome kwanza Biblia:
1 Yohana 2:22-26; Je, mwongo ni nani? Mwongo ni yule anayekana kwamba Yesu si Kristo. Mtu huyo ndiye mpinga-Kristo, anayemkana Baba na Mwana. 23 Mtu anayemkana Mwana hawezi kumjua Baba; mtu anayemkiri Mwana anamjua na Baba pia. 24 Hakikisheni kwamba ujumbe mliosikia tangu mwanzo unadumu mioyoni mwenu. Ujumbe huo ukikaa mioyoni mwenu, ninyi pia mtadumu ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Na yeye ametuahidi uzima wa milele. 26 Ninawaandikia mambo haya kuhusu wale wanaojaribu kuwapo tosha.
Biblia inatufundisha kuwa, mwongo ni mtu yeyote yule anaye pinga kuwa Yesu si Kristo, zaidi ya hapo, Biblia inaendelea kutufundisha kuwa mtu anaye mkana Yesu hawezi kumjua Baba yake. Kumbe ndio maana Waislam wanasema kuwa Mungu hawezi kuwa Baba na wala hana Mwana!
Allah wa Koran anamkata Yesu kama Mwana na anakana kuwa Jehovah si Baba wa Yesu. Soma Quran hapa chini.
Quran 19:35. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
Katika Surah Maryam hapo juu, Allah anasema kuwa Mwenyezi Mungu hana Mwana, jambo ambalo ni kinyume na aya tuliyo isoma kutoka Biblia kuwa, Muongo ni mtu na au kiumbe chechote kile kinacho pinga kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na anaye mkana Baba yake (1Yohana 2: 22-26). Allah amesha mkana Baba, hivyo basi Allah teyari amenyakuwa sifa ya uongo.
Je, Allah ni Mungo? Hebu tuendelee kusoma Koran. Quran 1539. Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenipotosha na kunitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
Katika aya hapo juu, Shetani anasema kuwa, Allah ndiye aliye mpotosha na kumfanya awe mbaya. Kumbe Allah ndie mwanzislishi wa upotoshaji/uongo? Ushaidi zaidi utaupata katia Surah na aya zifuatazo 3:54, 3:54, 7:123, 13:42, 14:46, 16:26, 16:45, 27:50, 40:45, 71:22 impf. act. 6:123, 6:123, 6:124, 8:30, 8:30, 8:30, 10:21, 12:102, 16:127, 27:70, 35:10 n.vb. 7:99, 7:99, 7:123, 10:21, 10:21, 12:31, 13:33, 13:42, 14:46, 14:46, 14:46, 27:50, 27:50, 27:51, 34:33, 35:10, 35:43, 35:43, 71:22 pcple. act. 3:54, 8:30
katika Surat-Nisai 171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu.
Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka.
Allah anasema kwamba watu wa Kitab ambao ni Wakristo wasisema mabaya kuhusu Allah ila, wakiri kuwa Yesu ni Mtume tu na wasiseme kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, wala wasiseme kuwa Kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Allah anaendelea kuonyesha tabia yake ya uongo katika aya hapo juu.
Sasa endelea kusoma Biblia na ufahamu sifa zaidi za muongo.
Yohana 8:44 Ninyi ni watoto wa baba yenu shetani; kwa hiyo mnapenda kufanya maovu kama yeye. Tangu mwanzo yeye alikuwa muuaji na hana uhusiano wo wote na mambo ya kweli; kwa maana hana asili ya kusema lililo kweli. Shetani anapodanga nya anadhihirisha asili yake kwa kuwa yeye ni mwongo na ni baba wa uongo.
Katika aya hapo juu tunafundishwa kuwa, watoto wa Shetani wanapenda kufanya maovu kama baba yao. Ndio maana tunasoma kwenye Koran kuwa, Allah ametoa amri kwa wafuasi wake kuuwa mtu yeyote yule anayekataa kuwa Muislam. Kuuwa ni kufanya maovu, lakini kwa Allah kuuwa ni kufanya jambo jema Quran 2:244, 3:151, 4:74, 4:89, 4:95, 4:104, 5:33, 8:12.
Allah akatika Surat An Nisaai anatimiza yale yote yaliyo semwa katika Yohana 8:44, ambayo ni adhama zote za Shetani:
Quran 4 Surat An Nisaai Allah anasema 74. Basi nawapigane katika Njia ya Allah wale ambao wanao uza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya Allah kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa.
Hii surah ambayo iliteremka Makkah inaonyesha dhahir tabia ya Allah ambayo haina tofauti na Shetani aliye semwa katika Biblia. Yesu anasema jinsi gani Shetani anafanya kazi, na nini hasa hufanya kwa binadamu. Soma Yohana 10:10 Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele.
Hiyo ndiyo kazi ya Shetani ambayo tunaiona katika Allah wa Koran. Shetani ni Baba wa Uongo, vivyo hivyo, Allah naye ni Baba wa Uongo katika Uislam. Shetani ni muuaji, vivyo hivyo, Allah nayeye anatoa amri ya kuuwa Makafir wote katika Koran 9:14, 9:20, 9:38-39. Suran 9:14. Piganeni nao, Allah awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.
Ndugu wasomaji, Allah ameonyesha adhama zote za Shetani kuwa ni zake. Mungu huwa hasemi uongo wala achonganishi watu ili wapigane kwa ajili yake. Allah si Mungu.
Nimategemeo yangu kuwa, utafanya utafiti zaidi ili uweze kuona tofauti zilizopo kati ya Mungu wa Biblia na Allah wa Koran.
Katika huduma yake
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment