Kuna utatanishi mwingi juu ya kumtambua Roho Mtakatifu. Wengine humchukulia kama nguvu Fulani zisizoonekana. Wengine huamini kwamba ni uwezo wa Mungu ambao Mungu huuachilia maishani mwa wale ambao ni waumini wa kristo. Je, biblia inasemaje juu ya Roho Mtakatifu? Kwa kifupi biblia inasema kwamba Roho mtakatifu ni Mungu. Pia biblia inasema kuwa Roho mtakatifu ni mtu, mwenye akili, hisia na mapenzi yake.
Swala la kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu limo ndani ya aya nyingi za biblia kama vile Matendo 5:3-4. Katika ayah ii petro anapambana na anania aliyemdanganya Roho Mtakatifu na nasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali Mungu.” Hili ni tangazo la wazi kwamba kumdanganya Roho Mtakatifu ni kumdanganya Mungu. Tunaweza pia kujua Roho Mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana tajwa na hali sawa na za Mungu. Roho Mtakatifu yuko kila mahali katika Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” tena katika wakorintho wa Kwanza 2:10 tunaona hali yakuwepo kila mahali kwa Roho Mtakatifu “Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake Mtakatifu. Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”
Tunaweza kujua kweli kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana akili, hisia na mapenzi yake. Roho Mtakatifu hufikiri na hujua (Wakorintho wa kwanza 2:10). Roho mtakatifu anaweza kuugua (Waefeso 4:30). Roho hutuombea (Warumi 8:26-27). Roho Mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11). Roho mtakatifu ni Mungu, sehemu ya tatu ya utatu wa Mungu. Kama Mungu, Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26).
No comments:
Post a Comment