Pamoja na mengine yote Yesu aliyoyasema juu yake mwenyewe, wanafunzi wake waliamini u mungu wake pia. Waliamini kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi jambo ambalo Mungu pekee ndiye mwenye uwezo nalo kwa kuwa ni Mungu anayechukizwa na dhambi (Matendo 5:31; Wakolosai 3:13; na kuendelea. Zaburi 130:4; Yeremia 31:34). Pamoja na haya Yesu ndiye atakayekuja, “kuhukumu wafu na walio hai” (Timotheo wa pili 4:1). Tomaso akamlilia Yesu Akisema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” (Yohana 20:28). Paulo anamwita Yesu, “ Mungu Mkuu na Mwokozi” (Tito 2:13), na anaelezea ya kuwa Yesu, “alikuwa katika hali ya Mungu” (Wafilipi 2:5-8). Mwandishi wa kitabu cha waebrania asema juu ya Yesu kuwa, “ Kiti chako cha enzi wewe Mungu, kitadumu milele na milele” (Waebrania 1:8). Yohana aeleza kuwa, “Hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwako kwa Mungu, naye neno (Yesu) alikuwa Mungu” (Yohana 1:1). Mifano ya aya zinazofundisha juu ya u Mungu wa Yesu ni mingi (pia Ufunuo wa Yohana 1:17; 2:8; 22:13; Wakorintho wa kwanza 10:4; Petro wa kwanza 2:6-8; Zaburi 18:2; 95:1; Petro wa kwanza 5:4; Waebrania 13:20), kila mojawapo ya aya hizi inatosha kukujulisha ya kwamba wanafunzi wa Yesu walimwamini kuwa Yesu alikuwa Mungu.
Yesu pia apatiwa adhama ambazo zina Yahweh pekee (Jina maalum la Mungu) katika agano la kale. Adhama ya “Mkombozi” (Zaburi 130:7; Hosea 13:14) inatumika juu ya Yesu katika agano jipya. (Tito 2:13; Ufunuo wa Yohana 5:9). Yesu anaitwa Immanueli (“Mungu pamoja nasi” katika mathayo 1). Katika Zakaria 12:10, ni Yahweh anayesema, “watanitazama mimi waliyenipasua.” Lakini agano jipya haya yanatumika kwa kusulibiwa kwake Yesu (Yohana 19:37; ufunuo wa Yohana 1:7). Kama ni Yahweh mwenye kupasuliwa na mwenye kutazamwa, na Yesu ndiye aliyepasuliwa na kutazamwa basi Yahweh ni Yesu. Paulo anatafsiri Isaya 45:22-23 kama yale ya Yesu katika wafilipi 2:10-11. Pia Jina la Yesu linatumika pamoja na la Yahweh katika sala, “Neema na amani kutoka kwa Mungu baba na Bwana wetu Yesu kristo iwe kwenu” (Wagalatia 1:3; Waefeso 1:2). Hili lingekuwa kufuru kama Yesu hangekuwa Mungu. Jina la Yesu linapatikana tena na la Yahweh katika amrisho la ubatizo Yesu aliposema, “kwa Jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19; pia tazama wakorintho wa pili 13:14.
Matendo ambayo yanaweza kufanywa na Mungu Pekee yanaonyeshwa yakifanywa na Yesu. Licha ya kuwa alifufua wafu (Yohana 5:21; 11:38-44), na kusamehe dhambi (Matendo 5:31; 13 38), aliumba ulimwengu (Yohana 1:2; Wakolosai 1: 16-17)! Jambo hili linatia msisitizo wakati tunapochukulia ya kwamba Yahweh aliumba akiwa peke yake. (Isaya 44:24). Hata hivyo, Yesu ana sifa sawa na Mungu, kama Umilele (Yohana 8:58), kuwa kila mahali (Mathayo 18:20, 28:20), kufahamu yote (Mathayo 16:21), muweza yote (Yohana 11:38-44).
Yesu alithibitishi wengi kuwa yeye ni Mungu kwa ishara na miujiza mingi aliyoifanya na hata akafufuka kutoka kwa wafu. Baadhi ya miujiza hiyo ni kubadilisha maji kuwa Divai (Yohana 2:7), kutembea juu ya Maji (Mathayo 14:25), kubariki vitu vya kidunia kuwa vingi (Yohana 6:11), kuponya vipofu (Yohana 9:7 ), Vilema (Marko 2:3 ),na wagonjwa (Mathayo 9:35; Marko 1:40-42), na kufufua wafu (Yohana 11:43-44; Luka 7:11 -15; Marko 5:35). Kristo mwenyewe alifufuka kutoka kwa wafu. Hakuna dini nyingine yenye miungu yenye uwezo wa ufufuo. Kulengana na maoni ya Daktari Gary Habermas, kuna vitendo zaidi ya kumi na viwili vya kihistoria ambavyo wanavyuoni wasiokuwa wakristo huvikubali:
1. Yesu alikufa kwa kusulibiwa.
2. Alizikwa.
3. Kifo chake kilisababisha kuvunjika mioyo kwa wanafunzi wake na kukosa tumaini.
4. Kaburi la Yesu liligunduliwa kuwa tupu siku chache baadaye.
5. Wanafunzi waliamini kutokewa mara kwa mara na Yesu aliyefufuka.
6. Baada ya haya wakabadilishwa kutoka wenye shaka mpaka watu wenye imani kubwa na ujasiri.
7. Ujumbe huu ulikuwa msingi wa mahubiri ya kanisa la kwanza.
8. Ujumbe huu ulihubiriwa Yerusalemu.
9. Hatimaye kanisa likazaliwa na kukua kwasababu ya mahubiri haya.
10. Siku ya kufufuka, Jumapili, ikachukua nafasi ya sabato (Jumamosi) kama siku ya ibada.
11. Yakobo, asiyeamini, akabadilishwa baada ya kumuona Yesu aliyefufuka.
12. Paulo, adui wa ukristo, alibadilishwa na mambo aliyoyaeleza kuwa ni kutokewa na Yesu kristo aliyefufuka.
Hata kama mtu angekataa baadhi ya matukio haya, machache ya haya yanatosha kumfanya akubali kufufuka kwa Yesu na kuthibitisha Injili: Kufa kwa Yesu, kuzikwa, kufufuka, na kuonekana kwake baada ya kufufuka (Wakorintho wa kwanza 15:1-5). Ufufuo unajibu mambo yote. Ingekuwa uongo watu hawangeokolewa na kumgeukia Yesu kama walivyofanya. Wanafunzi hawangekubali kufa vifo vya mateso kama walivyovikubali kwa ajili ya imani yao. Hakuna anayekubali kufa kwa ajili ya jambo analolitambua kuwa la uongo.
Kwa kumalizia, Yesu alisema yeye ni Yahweh, na alikuwa Mungu (Mwenyezi Mungu), Wafuasi wake (wayahudi waliokataa miungu mingine nje ya Mungu wa mbinguni) wakamwamini na wakamwita hivyo. Yesu kristo akathibitisha kuwa yeye kweli ni Mungu kwa kufanya miujiza pamoja na kufufuka. Hakuna jambo lengine linaweza kuyaeleza kwa nini haya yaliwezekana kufanywa na Yesu isipokuwa Yesu alikuwa Mungu.
No comments:
Post a Comment