Friday, August 3, 2012

Damu Ya Yesu Kristo


picture of jesus blood
Mara nyingi imesemwa katika Agano Jipya ya kwamba kuhesabiwa kwetu haki na kupata wokovu ni kwa damu ya Yesu (K.m 1Yoh 1:7; Ufu 6:9; 12:11; Rum 5:9). Kufahamu maana ya damu ya Kristo, yatupasa tuelewe ya kuwa ni neno la awali la Biblia kwamba "uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake" (Law 17:14). Pasipo damu mwili hauwezi kuishi; kwa hiyo ni mfano wa uhai. Hii yaeleza uzuri wa maneno ya Kristo, "Msipo ula mwili wake mwana wa Adamu, na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu". (Yoh 6:53).

Dhambi huleta mauti (Rum 6:23), yaani, kumwaga damu ambayo hushika uhai uzima. Kwa sababu hii wana wa Israel walitazamiwa kumwaga damu kila wakati walipotenda dhambi, ili kuwakumbusha kuwa dhambi inaleta mauti. Na katika torati (ya Musa) karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo (la dhambi Ebra 9:22). Kwa sababu hii, Adamu na Hawa walipojifunika wenyewe na majani ya mtini hayakukubalika; badala yake, Mungu alimchinja mwanakondoo na kuwagawia ngozi za kujifunika dhambi zao (Mwanzo 3:7,21). Vivyo hivyo, dhabihu za wanyama wa Abeli ilikubalika zaidi kuliko matoleo ya mboga ya Kaini, kwa kuwa alielewa jambo hili ya kwamba pasipo kumwaga damu ingekuwa vigumu kusamehewa na kukubalika kumkaribia Mungu (Mwanzo 4:3-5)


Matukio haya yanalenga mbele kwenye umuhimu mkubwa wa damu ya Kristo. Hasa haya kivuli chake ni kwenye Pasaka, ambako watu wa Mungu iliwabidi kupaka damu ya mwana kondoo juu ya miimo ya nyumba yao ili kuokolewa kutokana na mauti. Hii damu ilikuwa inaonyesha mbele kwa ile ya Yesu, ambayo yatupasa sisi tufunikwe. Kabla ya wakati wa Kristo wayahudi iliwabidi kutoa dhabihu za wanyama kwa ajili ya dhambi zao, kufuata sheria ya Mungu kwa mkono wa Musa. Walakini, huku kumwaga damu ya mnyama ilikuwa kwa madhumuni ya kufundisha. Dhambi inaadhibiwa kwa mauti(Rum 6:23); haiwezekani kwamba wanadamu waweze kuua mnyama kuwa badala ya mauti yake yeye mwenyewe. Mnyama aliyekuwa anamtoa hakufahamu jema na baya; hakuwa mwakilishi wake kabisa: "Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi". (Ebr. 10:4)

Basi swali linajitokeza, ni kwa sababu gani Wayahudi inawabidi kutoa sadaka za wanyama walipotenda dhambi? Paulo anajumlisha majibu mbali mbali kwa swali hili katika Gal. 3:24; "Torati ilikuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo". Wanyama walio waua kuwa matoleo ya dhambi ilibidi wawe hawana doa - bila waa (Kut 12:5; Law 1:3, 10 n.k). Hizi zililenga mbele kwa Kristo, "Mwana kondoo asie na ila" (1Petr. 1:19). Damu za hao wanyama zilikuwa zipo badala ya ile ya Kristo. Zilikubaliwa kama dhabihu kwa ajili ya dhambi kwa kuwa zililenga mbele kwenye sadaka kamili ya Kristo, ambayo Mungu alijua ataifanya. Kwa sababu hii Mungu aliweza kusamehe dhambi za watu wake walioishi kabla ya kuja Kristo. Mauti ya Kristo "ilifanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya Agano la kwanza" (Ebr 9:15) , Yaani, Torati ya Musa (Ebr 8:5-9). Dhabihu zote zilizotolewa chini ya Musa zililenga mbele kwa Kristo sadaka kamili kwa ajili ya dhambi, yeye, "azitangue dhambi kwa dhabibu ya nafsi yake" (Ebr 9:26; 13:11’12; Rum 8:3; 2Kor 5:21).

Tulielezwa katika sehemu ya 7.3 jinsi gani Agano la kale lote, hasa Torati ya Musa, ilionyesha mbele kwenye ujio wa Kristo. Chini ya Torati njia ya kumkaribia Mungu ilkuwa kwa kuwakilishwa na Kuhani Mkuu alikuwa mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu chini ya Agano la Kale kama ilivyo chini ya Agano jipya (Ebra 9:15). "Torati yawaweka wanadamu walio wanyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo nenola kiapo….. limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele" (Ebr 7:28). Kwa kuwa wao wenyewe walikuwa wakosaji, watu hawa hawakuwa katika nafasi ya kuwapatia watu msamaha wa kweli. Wanyama waliowatoa kwa ajili ya dhambi kwa kweli hawakuwa wawakilishi wa kweli wa wakosaji. Sadaka iliyotakiwa ni mwanadamu mkamilifu, ambaye kwa vyovyote ni mwakilishi wa mwanadamu mkosaji, ambaye anatoa dhabihu inayokubaliwa kwa ajili ya dhambi ambayo watu wanaweza kufaidika kutokana na kujiunga na dhabihu hiyo wao wenyewe. Kwa namna hii, Kuhani mkuu mkamilifu alitakiwa ambaye aweza kuwasaidia wenye dhambi ambao huwafanyia suluhu, na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa (Ebra 2:14-18).

Yesu kwa matakwa haya kwa ukamilifu anafaa. "Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu", asiye na uovu, asiyekuwa na waa lolote" (Ebra 7:26). Haina haja daima ya kutoa daima dhabihu ya dhambi zake mwenyewe wala kustahili kifo tena (Ebra 7:23,27). Kwa mwangaza huu maandiko yanatoa ufafanuzi juu ya Kristo kuwa ni kuhani wetu mkuu;" Naye kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa kupitia kwake; maana yu hai siku zote ili awaombee" (7:25). Kwa sababu alikuwa na asili ya mwanadamu, Kristo, akiwa ni kuhani wetu mkuu asiye na kombo lolote, "aweza kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea; kwa kuwa yeye mwenyewe yu (alikuwa) katika hali ya udhaifu" (Ebra 5:2). Kulingana na Kristo taarifa hii inarudia ya kwamba, "yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo" alitwaa mwili wetu (Ebra. 2:14).

Ikiwa kuhani mkuu wa kiyahudi alifanya upatanisho kwa watu wa Mungu pekee. Israel, basi Kristo ni kuhani pekee wa Israel wa roho, waliobatizwa katika Kristo, wakiisha ifahamu Injili ya kweli. Yeye ni kuhani "mkuu wa Nyumba ya Mungu" (Ebra 10;21), ambayo ina wale waliozaliwa tena kwa kubatizwa (1Petro 2:2-5), wakiwa na tumaini la kweli la Injili (Ebra 3:6). Tukifahamu faida za ajabu za ukuhani wa Kristo basi zaweza kututia moyo tubabatizwe katika jina lake; bila hizi hawezi kutuombea.

Tukiisha batizwa katika Kristo, kwa bidii tutautumia vya kutosha ukuhani wa Kristo, kweli, tuna wajibu halisi kulingana na unavyotupasa kuutendea kazi. "Basi , "Kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima (Ebra 13:15). Mpango wa Mungu kutupatia Kristo kuwa kuhani wetu ilikuwa kwamba tumtukuze; kwa hiyo tutumie siku zote njia yetu kuelekea kwake Mungu katika Kristo ili tumtukuze. Ebra 10:21-25 inaorodhesha idadi ya majukumu ambayo tunayo kwa sababu ya Kristo kuwa kuhani wetu: "Akiwa ni kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu.
  1. Na tumkaribie (Mungu) wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya; tumeoshwa miili kwa maji safi". Kuuelewa ukuhani wa Kristo maana yake ni kwamba tubatizwe kwa yeye ("miili yetu ioshwe"), kamwe tusiendeleze dhamiri mbaya mioyoni mwetu. Kama tukiamini upatanisho wa Kristo, tunakuwa kwenye umoja na Mungu (KUWA- PAMOJA-NA MUNGU) kwa dhabihu yake Kristo.
  2. "Na tushike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke". Tusiende upande toka kwenye mafundisho ya kweli yaliotufanya tuulewe ukuhani wa Kristo.
  3. " Tuangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja". Kwa upendo tujifunge pamoja na wengine wanaoelewa na kufaidika kutokana na ukuhani wa Kristo; tendo hili hasa ni kwa kukusanyika pamoja katika ibada ya ushirika, kwa hiyo tunakumbuka dhabihu ya Kristo (tazama sehemu ya 11.3.5)
Kufahamu mambo haya yatatujaza ujasiri wa unyenyekevu ambao kwa kweli yatatufikisha kwenye wokovu, kama tukibatizwa na kudumu ndani ya Kristo. "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri; ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" (Ebra. 4:16).

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW