Je! kiini cha sheria ni nini? Imeandikwa, Warumi 13:10 "Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria."
Sheria za Mungu ni upendo. Imeandikwa, Mathayo 22:37-40 "Akamwambia mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote hii ndiyo amri iliyo kuu tena ni ya kwanza na yapili yafanana nayo, nayo ni hii mpende jirani yako kama nafsi yako katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii."
Kupitia kwa Yesu amri za Mungu zime dhibitishwa. Imeandikwa, Mathayo 5:17-18 "Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua torati au manabii, la, sikuja kutangua bali kutimiliza kwa maana amin nawaambia mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie."
Sheria yaonyesha mwelekeo wala haziondoi dhambi. Imeandikwa, Wagalatia 2:15-16 "Sisi tulio Wayahudi kwa asili wal si wakosaji wa mataifa hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa imani ya Kristo Yesu sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo wal asi kwa matendo ya sheria maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki."
Ni wajibu wetu kutii sheria za Mungu. Imeandikwa, Mhubiri 12:13 "Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; mche Mungu nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo ipasayo mtu."
Je! Kuna uhusiano gani kati ya sheria na dhambi?. Imeandikwa. 1Yohana 3:4 "Kila atendaye dhambi ni uasi."
Je! Ni muhimu kushika sheria zote?. Imeandikwa, Yakobo 2:10-11 "Maana mtu ye yote atakaye ishika sheria yote ila akajikwa katika neno moja amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, usizini, alisema usiue, pasi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria."
Je! Twaweza kumjua Mungu bila kutii sheria?. Imeandikwa, 1Yohana 2:4-6 "Yeye asemaye nimemjua wala hazishiki amri zake ni mwongo wal kweli haimo ndani yake. Lakini yeye aliyeshika neno lake katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli katika hiyo twajua tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake imempasa kunenda mwenyeewe vile vile kama yeye alivyoenenda."
Umuhimu wa sheria ni upi? Imeandikwa, Warumi 3:20 "Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maan akutambua dhambi huja kwa njia ya sheria."
Je! Twaokolewa kwa kutii sheria?. Imeandikwa, Warumi 3:27-31 "Ku wapi basi kujisifu? kumefungwa nje. kwa sheria ya namna gani? kwa shgeria ya matendo? la bali kwa sheri aya imani basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? siye Mungu wa mataifa pia; kama kwa kweli Mungu ni mmoja; atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. Basi Je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? hasha! kinyume cha hayo twaidhibitisha sheria."
Kwa Idhini
Max Shimba
Kwa Idhini
Max Shimba
No comments:
Post a Comment