Saturday, July 28, 2012

Biblia Inasema nini kuhusu uhusiano na Mapepo au Majini


Mungu ametuonya kutokuwa na uhusiano na pepo. Imeandikwa, Mambo ya Walawi 19:31 "Msiwaendee wenye pepo wala wachawi, msiwatafute ili kutiwa unajisi na wao mimi ndimi BWANA Mungu wenu."
Ilikuwa kawaida ya watu wa zamani enzi za Biblia kusali pepo. Mungu aliwaonya wana wa Israeli kuhusu uombaji wa pepo na uchawi. Imeandikwa katika Kumbukumbu la torati 18:9-12 "utakapokwisha ingia katika nchi akupayo BWANA Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto wala asionekane mtu atazamaye mbao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala msihiri wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo wala mtu apandishaye pepo wala mchawi wala mtu awaombaye wafu kwa maana mtu atandaye hayo ni chukizo kwa BWANA kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA Mungu wako anawafukuza mbele yako."
Biblia yatupa mwanga kuhusu hali ya pepo. Imeandikwa, katika Matendo ya mitume 16:16-18 "Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu wenye kuwahubiria njia ya wokovu akafanya hayo siku nyingi lakini Paulo akasikitika akageuka akamwambia yule pepo nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu akamtoka saa ili ile."

Pepo ni wale malaika waliomwasi Mungu kule mbinguni na kutupwa hapa duniani. Imeandikwa katika Ufunuo 12:7-9 "Kulikuwa na vita Mbinguni Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na Shetani adanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye."

Kwa sababu pepo za husiana na Shetani, mtu katika israeli angeonekana akifanya pepo ilibidi auawe. Imeandikwa, katika Mambo ya walawi 20:27 "Tena mtu mme au mke aliye na pepo au aliye mchawi hakika atauawa watawapiga kwa mawe damu ya itakuwa juu yao." Isaya 8:19 yasema "Na wakati watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndeye na kunong'ona je haiwabasi watu kutafuta habari kutoka kwa Mungu waoje! waende kwa watu walio kufa kwa ajili ya watu walio hai?."


Kwa Idhini


Max Shimba

No comments:

WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"?

 WHAT DOES IT MEAN "THE WORD OF GOD IS GOD"? Dr. Maxwell Shimba explains: The Word and the Divine Nature – A Comprehensive Exposit...

TRENDING NOW