ALFA NA OMEGA.
“Alfa” ni herufi ya kwanza katika alfabeti za lugha ya kiyunani kama ilivyo “A” katika alfabeti za Kiswahili na Vivyo hivyo “Omega” ni herufi ya mwisho katika alfabeti za kiyunani kama ilivyo “Z” katika alfabeti za Kiswahili. Yesu Kristo anaposema hivyo anamaanisha kwa undani sana kwamba hata herufi zote za Alfabeti zinamzungumza yeye katika lugha yoyote duniani na siyo kiyunani pekee Yesu ni Mwanzo na mwisho wa alfabeti zote zote humtaja yeye na kumtukuza hii pia humaanisha ya kuwa yeye ni yote katika yote.
YESU NI A.
Yesu kristo anaitwa A yaani ni Afya yetu Zaburi 42;5.11, 43;5 Yeye ni Afya yetu na Mungu wetu tunapokuwa na upungufu wowote katika Afya zetu yeye3 alikuja ili sisis tuwe na uzima tena tuwe nao tele Yohana 10;10 Yeye pia ni Ahadi ya uzima 2Timotheo 1;1 mganga yeyote akikuhaidi uzima ahadi hiyo inaweza isiwe na uhakika lakini ahadi za Yesu ni ndiyo yaani ni hakika 2Wakoritho 1;19-20 Hesabu 23;19. Anaitwa pia Aliye juu Zaburi 46;4 wengine wako chini Yeye yu juu ya yote Yeye pia ni Aliyeko,Aliyekuwako na Atakayekuja Ufunuo 1;8,Yeye pia ni Amani ya Bwana. Zaburi 129;8 Yeye ni Amina Ufunuo 3;14. Anaitwa Arabuni ya roho zetu Efeso 1;14 yaani ni muhuri au uhakika.
YESU NI B.
Yesu huitwa Bwana wa mabwana Ufunuo 19;16 na pia huitwa Bwana mkubwa Luka 8;24 Huitwa pia Baraka ya Bwana Kumbukumbu 33;23 ni Bwana wa vita Yoshua 10;14 kutoka 15;3 ni Bwana harusi wa kanisa Mathayo 9;15
YESU NI C.
Ni chakula cha uzima Yohana 6;35 vyakula vingine hutupa uzima wa muda tu chakula hiki hutupa uzima wa milele yeye ni Chanda cha Mungu Kutoka 8;19 huitwa chapa ya nafsi ya Mungu Waebrania 1;13 na ni chemichemi ya maji ya uzima Yeremia 2;13 pia huitwa Chipukizi la haki Zekaria 6;12
YESU NI D.
Yesu Kristo ni dhabihu yetu Waefeso 5;2 alitolewa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu na kwa kupigwa kwake sisi tunmepona Isaya 53;5 hatuna haja tena ya kutoa kafara nyingine kama mbuzi kuku, na kuwapelekea waganga wa kienyeji
YESU NI E.
Yesu pia huitwa Elimu ya utukufu wa Mungu angalia katika 2Koritho 4;6 hakuna aliye na Elimu yenye utukufu kama Kristo wanadamu wenye madigrii kibao wana sehemu ndogo sana ya maarifa ukilinganisha na Kristo mwenye maarifa yote, ikumbukwe kuwa maarifa yote yanatoka kwake.
YESU NI F.
Yesu anapotajwa kama F katika Maandiko yeye ni Fadhili za Mungu Zaburi 57;3 tukikosa fadhili kwa wanadamu tumwendee Yesu yeye ni mfadhili wa ajabu atatupa mahitaji yetu yote Bure bila ya masharti.Huitwa pia Fahari ya Yakobo Zaburi 47;4 Yeye ni fahari yetu hatupaswi kumuonea aibu yeye pia ni Faraja Yetu au faraja ya Israel Luka 2;25,Ni fimbo ya Mungu Kutoka 4;20 na ni furaha ya bwana Nehemia 8;10
YESU NI G.
Yesu Kristo huitwa Gumegume Isaya 50;7 Gumegume ni aina Fulani ya jiwe ambalo ni gumu sana kwa kiingereza huitwa Flint mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika na yeyote ambaye litamwangukia jiwe hili litamsagasaga tikitiki Mathayo 21;44 Chochote kilichokigumu magonjwa mikosi balaa tuvilete kwa Yesu vitapondwapondwa kabisa
YESU NI H.
Yesu Kristo anatajwa pia kuwa ni Haki ya Mungu 2Koritho 5;21 hakuna mtu yeyote atakayehesabiwa haki mbele za Mungu isipokuwa katika Yesu Kristo aliye haki ya Mungu Warumi 3;26,5;1 Yeye pia ni Hakimu Zaburi 50;6 ndiye atakaye uhukumu ulimwengu Kristo pia ni Hekima yetu kwani huitwa Hekima ya Mungu 1Koritho 1;30iwapo tunalo hitaji la Hekima leo
YESU NI I.
Yesu huitwa pia Immanuel Mathayo 1;23 yaani ni Mungu pamoja nasi anatajwa pia kuwa ni Ishara Yesu ni udhihirisho wa uwezo wa Mungu mahali alipo kuna ishara Isaya 11;10
YESU NI J.
Jina la Yesu ni Jina lipitalo majina yote Wafilipi 2;9 si hilo tu Yesu ni Jiwe kuu la pembeni Matendo 4;11 Jiwe lililo hai 1Petro 2;24. Uimara wetu unatokana na jiwe kuu la msingi la pembeni na lililo hai yaani Yesu Kristo bila yeye hakuna uimara wowote
YESU NI K.
Yesu anaitwza kichwa cha kanisa Waefeso 5;23 yaani ndiye kiongozi mkuu wa kanisa lote,huitwa pia kiongozi mkuu wa wokovu wetu Waebrania2;10. Katika Waebrania 7;17;10;21 Ni Kuhani mkuu maana yake ndiye mpatanishi wetu mkuu 1Timotheo 2;5 yeye pia huitwa kweli Yohana 14;6 pia ni Kimbilio letu
YESU NI L.
Yesu Kristo ni Lulu moja ya thamani kubwa Mathayo 13;46 tukimpata katika maisha yetu tumepata lulu moja ya thamani kubwa yeye ndiye wa kumshika na sio dini Ufunuo 3;11 Dini au dhehebu Fulani sio lulu moja ya thamani
YESU NI M.
Ni Mfalme wa Wafalme Ufunuo 19;16 yapasa tumuogope na kumtii na kumuheshimu Ni Mfinyanzi wetu Isaya 64;8,Yeremia 18;1-6. Huitwa Mchungaji mkuu wa kondoo Waebrania 13;20 ni Mchungaji mwema Yohana 10;14. Ni Mlango wa kondoo Yohana 10;7 ni Moto ulao Waebrania 12;29, ni Mungu mkuu Tito 2;13 ni Mwana wa Mungu Yohana 9;35-37 ni Mwana wa Adamu Mathayo 26;64 Ni Mwokozi Tito 1;4,Mwalimu Yohana 3;2,na Muhukumu wetu siku ya mwisho Yohana 5;22
YESU NI N.
Yeye ndiye Nabii yule Yohana 6;14 huitwa pia Njia pekee ya kuingia mbinguni Yohana 14;6 ndiye Nyota ya kung’aa asubuhi Ufunuo 22;16 au Nuru ya ulimwengu Yohana 8;14 akiwa ndani yetu hatuta kwenda gizani kamwe yeye ni Neno Yohana 1;1
YESO NI O.
Yeye hutajwa kama Ondoleo la dhambi zetu Matendo 10;43 tukimuamini hutupa ondoleo la dhambi
YESU NI P.
Pendo la Mungu Warumi 5;5 ni chimbuko la upendo la kweli
YESU NI R.
Ni Rafiki Luka 12;4.pia ni mwalimu mkuu sana anayeheshimika Rabi au Rabon Yohana 20;16
YESU NI S.
Yeshu huitwa Shahidi aliye mwaminifu Ufunuo 1;5 ni Simba wa kabila la Yuda Ufunuo 5;5
YESU NI T.
Tabibu mkuu Mathayo 9;11-12,Yeye ni Tumaini letu kuu Zaburi 71;5 ni Taraja letu Zaburi 71;5 ni Tegemeo letu Yeremia 17;5-8.
YESU NI U.
Yesu Kristo ni uzima wa milele Yohana 14;6 na ukombozi wetu 1Timotheo 2;6 na ndiye upanga wa utukufu Kumbukumbu 33;29 upanga huu unaweza kushughulikia na yeyote anaye kutesa
YESU NI V.
Yesu ni Vazi jipya Luka 5;36 Torati ni vazi kuu kuu lakini Kristo ni vazi jipya
YESU NI W.
Ni Wokovu wetu Zaburi 27;1 tukiwa na Yesu hatupaswi kumuogopa mtu awaye yote Hesabu 23;23 hata wachawi hatupaswi kuwaogopa kwani Yesu ni wokovu wetu
YESU NI Y.
Huitwa Yesu Mathayo 1;21 yeye ndiye aokoanye watu wake na dhambi zao bila Yesu hakuna wokovu.Yeye ni Yeye yule jana leo na hata milele,ni Yeye ajaye wala hatakawia Ebrania 10;37.
YESU NI Z.
Yesu ndiye Zeri ya Gileadi Yeremia 46;11 nyakati za Biblia kulikuwa na dawa iliyoitwa zeri ambayo ilikuwa ikipatikana huko Gileadi dawa zote zikishindwa ndipo ilibidi itumike zeri ya Gileadi ilikuwa ni dawa isiyoshindwa ni zaidi ya muarobaini Zeri ni Yesu Kristo dawa isiyoshindwa kila kitu kinaposhindikana ndipo tumuitie Yesu yeye hashindwi kitu.
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekim
No comments:
Post a Comment