Kalenda ya Kiyahudi (pia: Kalenda yaKiebrania) ni kalenda inayotumiwa katika dini ya Uyahudi na pia nchini Israel. Inatumiwa kupanga tarehe za sikukuu za Kiyahudi na utaratibu wa kusoma Torati kwa kila wiki.
Kanuni za msingi
Kalenda ya Kiebrania ni kalenda jua-mwezi.
- Miezi ya kalenda hiyo hufuata mwonekano halisi wa Mwezi angani, sawa na kalenda ya Kiislamu. Mwezi mpya unaanza wakati wa kuonekana kwa hilali.
- Wakati huo huo, Pasaka ya Kiyahudiinapaswa kutokea kwenye majira ya machipuo. Kanuni hii inasababisha kwamba makadirio ya mwaka unafuata mwaka wa jua.
- Hii inasababisha ulazima wa kupatanisha tofauti kati ya muda wa mwaka wa Jua (siku 365) na muda wa mwaka wa Mwezi (takriban siku 354).
- Hapo kalenda ya Kiebrania inaongeza mwezi wa nyongeza mara saba katika kila kipindi cha miaka 19. Kwa hiyo kuna miaka ya kawaida yenye siku 354 na miezi 12. Lakini kila mwaka wa pili au tatu ni mwaka mrefu wenye miezi 13 na siku 384.
Juma
Nje ya kalenda hiyo kuna utaratibu wa wiki yasiku saba zinazoendelea mfululizo, sawa na kalenda ya kimataifa. Hutumiwa kubaini siku ya Shabbat, ambayo ni siku ya kupumzika. Wiki haitegemei mwaka wa jua wala wa mwezi. Badala yake, inategemea hesabu ya siku saba ambazo zinaaminika kurudi nyakati za zamani za Babeli na kutajwa katika masimulizi ya kuumbwa kwa Dunia katika Biblia.
Siku za juma la Kiyahudi
Siku ya juma (Kiebrania) | Tafsiri | Siku inaanza kutoka kuzama kwa Jua | Siku inaendelea mpaka kuzama kwa jua |
---|---|---|---|
יום ראשון yom rishon | siku ya kwanza | Jumamosi | Jumapili |
יום שני yom sheni | siku ya pili | Jumapili | Jumatatu |
יום שלישי yom shelishi | siku ya tatu | Jumatatu | Jumanne |
יום רביעי yom revi'i | siku ya nne | Jumanne | Jumatano |
יום חמישי yom hamishi | siku ya tano | Jumatano | Alhamisi |
יום ששי yom shishi | siku ya sita | Alhamisi | Ijumaa |
שבת shabbat | Shabbat (Sabato) | Ijumaa | Jumamosi |
Miezi
Mwezi namba katika Biblia | Jina la mwezi | Jina la mwezi kwa Kiebrania | Idadi ya siku | Wakati wa mwaka | Maelezo |
---|---|---|---|---|---|
1 | Nisan | נִיסָן | 30 | Machi - Aprili | Mwezi wa Pasaka |
2 | Iyar | אִייָר | 29 | Aprili- Mei | |
3 | Sivan | סִיוָן | 30 | Mei- Juni | Mwezi wa Shavuot |
4 | Tammuz | תַּמּוּז | 29 | Juni- Julai | |
5 | Av | אָב | 30 | Julai- Agosti | Mwezi wa Tisha B'Av |
6 | Elul | אֱלוּל | 29 | Agosti- Septemba | |
7 | Tishrei | תִּשְׁרֵי | 30 | Septemba- Oktoba | Mwezi wa Rosh Hashanah, Yom Kippur na Sukkot |
8 | Heshvan (au Marheshvan) | (מַרְ)חֶשְׁוָן | 29 au 30 [1] | Oktoba - Novemba | |
9 | Kislev | כִּסְלֵו | 30 au 29 | Novemba - Desemba | Mwezi wa Hanukkah |
10 | Tevet | כִּסְלֵו | 29 | Desemba- Januari | |
11 | Shevat | שְׁבָט | 30 | Januari- Februari | |
12 | Adar | אֲדָר | 29 | Februari-Machi | Katika mwaka mrefu, mwezi wa 13 unaongezwa unaoitwa pia Adar, lakini inapewa namba; kwa hiyo katika mwaka mrefu kuna Adar I na Adar II |
Siku na wiki
Katika kalenda ya Kiyahudi, siku inafafanuliwa kufuatana na Biblia ya Kiebrania: [2] "Na ilikuwa jioni, na ilikuwa asubuhi, siku moja". Kwa sababu "jioni" inakuja kabla ya "asubuhi", siku katika kalenda ya Kiyahudi huanza jioni baada ya machweo . Ni muhimu kuhakikisha kuwa siku iliyopita imekwisha kabisa, hivyo siku mpya huanza wakati wa usiku umeanza. [3]
Katika kalenda zinazochapishwa, tofauti hii haionekani maana hapa tarehe za kalenda ya Kiyahudi na tarehe za Kalenda ya Gregorizinazoanza usiku wa manane huonyeshwa kandokando. Ineleweka kuwa watu wanaotumia kalenda hizi wanajua utaratibu wa kuanza siku baada ya machweo. Wakati wowote sikukuu, siku ya kuzaliwa au ya kumbukumbu ikionekana kwenye kalenda iliyochapishwa, kwa kweli huanza jioni iliyotangulia, baada ya machweo.
Molad
Hesabu ya kalenda ya Kiebrania mwaka na mwezi huanza na molad inayomaanisha hilali. Molad ni neno la Kiebrania linalomaanisha "kuzaliwa". Neno hilo linamaanisha "kuzaliwa" kwa mwezi mpya kila mwezi. Kalenda ya kisasa ya Kiebrania hutumia molad iliyohesabiwa: urefu wa wastani wa muda kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya. Urefu wa Molad ni siku 29, masaa 12, dakika 44, sekunde 3 na nusu. [4]
Tanbihi
- ↑ Idadi inaweza kubadilika katika miaka kadhaa
- ↑ Genesis 1:5
- ↑ The Jewish Day. Chabad.org. Iliwekwa mnamo 11 May 2016.
- ↑ Bromberg. Moon and the Molad of the Hebrew Calendar. Iliwekwa mnamo 19 May 2016.
Marejeo
- Msimbo wa Maimonides (Mishneh Torah), Kitabu cha Tatu, Tolea Nane: Utakaso wa Mwezi Mpya . Ilitafsiriwa na Solomon Gandz. Yale Judaica Series Vol XI, Press University University of Yale, New Haven, Conn., 1956.
- Bonnie Blackburn na Leofranc Holford-Strevens. Mpenzi wa Oxford kwa Mwaka: Uchunguzi wa Forodha ya Kalenda na Uhesabuji wa wakati . Vyombo vya Habari vya Chuo Kikuu cha Oxford; USA, 2000. pp 723-730.
No comments:
Post a Comment