Wednesday, September 23, 2020

Asili ya Uislamu

 


IJUE DINI YA UISLAMU NA ASILI YAKE

Na Mwalimu Eleutary H. Kobelo.

Utangulizi

Kwa miaka mingi waislamu duniani, wanatuhimiza sana sisi Wakristo tuache imani na dini yetu, ili tuingie katika dini yao ya uislamu. Waislamu wanasema dini yao ndio ya haki, mbele ya Mwenyezi Mungu, na tena wasema manabii wote walikuwa waislamu, wanaendelea kusema kuwa hata Bwana Yesu naye alikuwa mwislamu, waislamu wanaendelea kusema kwamba dini ya Islamu haikuchukua au kurithi hata chembe (kidogo) ya tabia ya mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahili (yaani ujinga), kwani wanasema Uislamu ni dini safi kuliko zote. Swali la muhimu ni hili. Je, ni kweli kwamba dini ya uislamu haikuchua tabia na mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahilia? Ili kujua yote hayo fuatilia kwa makini somo hili lililoandikwa na Mwalimu wangu Mwinjilisti Kobelo na kupitiwa upya nami Mwalimu Chaka.


Sehemu kuu tano za somo

  1. Je, manabii wote walikuwa waislamu?
  2. Maana ya neno Islam.
  3. Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?
  4. Je, dini ya kiislamu imechua ibada za waarabu za zama ujahilia (yaani ujinga)?
  5. Wajibu wa mkristo baada ya kujua Uislamu.

1. Je, Manabii wote walikuwa waislamu?

Hoja kubwa ya waislamu ni kule kutuhimiza wakristo tukubali kuwa waislamu kwa kusema kwamba manabii wote wa Mungu walikuwa waislamu, hivyo wanataka tuache imani yetu tuwe waislamu. Lakini inafaa kwanza kuvichunguza vitabu vya kiislamu kuhusu ujio wa Qurani inafundisha nini? Na je, ni nani aliyeleta dini hiyo? Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia hivi;

Qurani 6:14 Suratul An-Am (Wanyama)

Sema: hakika nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu.

Katika aya hii tunaona Muhammad ndiye mtu wa kwanza kuamrishwa asilimu.

Imesimuliwa pia ya kwamba Muhammad S.A.W. alisema, “Sisi waislamu ndiyo wa mwisho kuja” hayo tunayasoma katika Sahih Al-Bukhari vol. ix Hadithi na 587.


Muhammad vilevile aliwaambia wafuasi wake wafuate njia ya waliowatangulia. “nchi kwa nchi, hatua kwa hatua hata kama ikiwa waliingia katika shimoni mwa mjusi” masahaba zake wakauliza “Layahud waal Na-swara? Yaani wayahudi na wakristo? Akawajibu Farman? Yaani nani zaidi? Hayo tunayaona katika Sahih Muslim vol. iv katika Al-lim, hadithi na 6448. Kutokana na jibu hili la Muhammad (S.A.W.) ni dhihiri kuwa dini ya Uislamu ilitanguliwa na dini yetu Wakristo na hata ile dini ya Kiyaudi.

  1. Manabii wa Mungu Yehova walifuata dini (njia) hii.

Tunaposoma maandiko matakatifu ya Biblia yanatufundisha kuwa manabii waliongozwa na huyu.

1 Petro1:10-11

katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakati upi na wakati wa namna gani ulioonywa na roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao.

1 wakorintho 10:1-4

kwa maana ndugu zangu,sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu. Wote wakapita kati ya bahari,wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingi na katika bahari; wote wakala chakula kilekile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata na mwamba ule ulikuwa ni kristo.

Katika aya hizi tunaona wazi wazi kuwa manabii wote waliongozwa na roho wa Kristo Yesu ambaye alikuwa ndani yao. Musa pamoja na watu wake pia walifuatwa na kristo naye aliwalisha na kuwanywesha. Wote waliongozwa na Bwana Yesu yeye mwenyewe aliwaita “watu wa Kristo” Soma Marko 9:38-41 hii ni kwasababu Bwana Yesu ndiye kiongozi wetu. Tazama Mathayo 23:9, tena Bwana Yesu ndiye njia (dini) ya kweli na uzima Yohana 14:6 hivyo manabii wote walikuwa ni watu wa Kristo kwasababu roho yake Yesu ulikuwa ndani yao ikiwaongoza.

  1. Maana ya neno Islam

Neno islam ni la lugha ya Kiarabu. Maana yake ni “Utii” au “Amani” katika Qurani neno Islam limetajwa mara 38. ijapokuwa neno Islam limetajwa mara nyingi lakini neno hilo ni tofauti na dini ya uislamu hii ni kwasababu dini a Uislamu maana yake ni kujisalimisha chini ya amri za Allah au amani chini ya sheria za Allah. Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia kumhusu Muhammad (s.a.w.) hivi.

Qurani 6:163 Suratul Al-An-Am (Wanyama)

Na haya ndiyo nilivyoamrishwa na mimi ni wa kwanza wa wanaojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu).

Qurani 39:12 Suratul Az-zumar (Makundi/Vikosi)

“Na pia nimearishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu.”

  1. Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?

Tunaposoma katika ufafanuzi wa aya ya 19-20 kati ka suratul Yusuf ulio ndani ya Qurani juzuu ya 12 chapa ya tatu ya kiswahili ukurasa wa 311 kuna maneno ambayo yanaelezea mtu aliyekuja na dini ya kiislamu hapa duniani na maneno yenyewe ni haya…

Unaona kwanza kulikuwako zaidi ya miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo Nabii Muhammad khalafu wakausingizia Uislamu kuwa ndio ulikuja na kuuza watu.

Kadiri ya ufafanuzi huu uliomo ndani ya qurani, na ushahidi wa vitabu maarufu vya hadithi za muhammad katika sahih Al-Bukhari na sahih muslim. Na vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na masheikh wa dini ya kiislamu, inathihirika waziwazi kuwa dini ya uislamu imeletwa na kuanzishwa na Muhammad (s.a.w.) mfano mzuri wa mwanzo wa dini ya uislamu tunauona katika kitabu kiitwacho maisha ya nabii muhammad (s.a.w.) kilichotungwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa zanzibar na baadaye nchi ya kenya marehemu sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy. Katika ukursa wa 18 kuna maneno yanayo husu mke wa muhammad aliyeitwa khadija binti khuweylid nayo yanatuhadithia hivi…

Akarejea kwa mkewe bibi khadija, akamsimulia habari hii. Palepale bibi huyu akamwamini, akawa ndiye mtu wa awali kabisa kushehedusha shahada ya uislamu. Basi mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke.

Katika kitabu hicho hicho cha maisha ya nabii muhammad ukurasa wa 18 kifungu c. wametajwa waislamu wa awali kabisa nao ni hawa…

(i) Mwislamu wa kwanza

Bibi Khadija bint Khuweylid

Mtume aliamrishwa kufundisha dini siku ya jumatatu na bibi huyu alisilimu siku hiyo hiyo akafanya ibada na mtume usiku ule ule kabla ya mtu yeyote ulimwenguni huyu ndiye aliyefuzu kwelikweli.

(ii) Mwislamu wa pili

Sayyidina Ali bin Abi Talib bin Abdul Muttalib

Alipomwana mtume na bibi Khadija usiku ule wanafanya mpya aliwauliza, “hii ni ibada gani?” mtume alimfahamisha na akamtaka awe pamoja nao lakini yeye alikataa kwanza akasema mpaka niende nikamshauri baba yangu”. Mtume akamkataza kuitoa siri ile nje. Mara asubuhi ya usiku ule ule, kijana huyu akaja kwa mtume akampa habari kuwa yeye yu pamoja nao. Akawa ndiye islamu wa pili duniani. Aliposilimu alikuwa kijana wa miaka 10 hivi.

(iii) Mwislamu wa tatu na wa nne.

Zayd bin Haritha Al Ka’bi na Bibi Aymana.

Huru wa mtume na mwanawe wa kupanga alikuwa akikaa pamoja na mtume na akasilimu kama sayyidina Ali mchana wa jumane. Alisilimu yeye na mkewe, bibi ummu Aymana yaya wa mtume.

Hawa wote ndio waislamu wa awali kabisa ambao walisilimu mara baada ya muhammad s.a.w. kuleta dini ya uislamu ambayo alianzisha rasmi hapa duniani jumatatu ya siku ya 17 ya mwezi wa ramadhani sawa sawa na 27th december ya mwaka wa 610 baada ya kristo. Kabla ya muhammad dini ya kiislamu haikuwepo kabisa duniani.

  1. Je, dini ya uislamu imechukua ibada za waarabu wa zama za ujahilia (yaani ujinga)?

Wakati wa ujahilia (ujinga) kabla ya dini ya uislamu makureshi ambalo ni kabila la muhammad s.a.w. na waarabu wenzao, walikuwa wakiabudu miungu mingi yapata 360 hivi. Kawaida hiyo ya kuabudu kwao miungu mingi kumesimuliwa waziwazi katika quarani na vitabu mbalimbali vya kiislamu. Vitabu hivyo vimeandikwa na masheikh na wanachuoni wengi, nitawataja baadhi yao nazo ni hawa…

(i) Maulamaa sayyid Abul A’la Maududi

Katika kitabu chake kiitwocho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 42-44 kuna maneno haya…”Bara Arabu mwina wa kiza wafanya biashara waarabu walijikokota masafa marefu ilikuwa vigumu kwao kupata hata chembe ya elimu wachache waliojua kusoma na kuandika walikuwa wakiabudu mawe, miti, masanamu, nyota na pepo, kwa ufupi kila kilichowapitia akilini mwao, hawakujua hata kidogo mafunzo ya mitume waliowatangulia. Walikua na dhana kuwa ibrahimu na ismail walikuwa babu zao, lakini walikuwa hawajui kitu kuhusu mafunzo yao ya dini na Mungu waliyemwabudu.

(ii) Sheik Abdullah saleh Al-Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu zanzibar na baadaye nchini Kenya

Katika kitabu chake kiitwacho maisha ya nabii muhammad s.a.w. ukurasa wa 6 kuna maneno haya… “Hata ilipokuwa karibu atadhihiri mtume mapadiri wa kinasara na makuhani wa kiyahudi waliokuwa wakikaa bara arabu walikuwa wakiwataharisha majirani zao wa kiarabu waliokuwa wakiabudu masanamu;

Qurani imetaja miungu mbalimbali iliyoabudiwa na makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia

(i) Waliabudu maandazi.

Qurani 25:43-44 Suratul Al;- furqan (Qurani)

Je umemuona yule aliyefanya matamanio yake (kile alichokipenda). Kuwa mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi) na haya, na hali ya kuwa hataki?) au je, unafikiri ya kwamba wengi katika wao wanasikia au wanafahamu? Hawa kuwa hao ila ni kama wanyama bali wao wanapotea zaidi njia.

Ufafanuzi wa aya ya 43 ulio katika qurani juzuu ya 19 ni huu, “waarabu kwa ujinga wao wa kuabudu chungu ya miungu walikuwa baadhi yao wakiona chochote kile kikawapwndeza hukiabudu hata andazi lililokaa kwa sura nzuri.

Hapa tunaona kuwa qurani inasimulia wazi wazi kwamba waarabu waliabudu hata andazi na tena ni wajinga “yaani majahalia”

(ii) kuabuduwa kwa miungu ya sanamu.

Qurani 71 22-23 Suratul Nuh (Nuhu)

Na walifanya hila kubwa kubwa za (kubatilisha dini). Na waliwaambia (wafuasi wao): “Msiache miungu yenu wala msiwaache waddi wala suwa’a wala yaghuta wala ya’uqa wala Nasra”. (Majina ya waungu wao wa kisamu).

Hii ni miungu ya uongo ya sanamu ambayo iliabudiwa na waarabu mungu waddi alikuwa na umbo la mwanamke yaghuta umbo la simba, ya’uga umbo la farasi hayo yanapatikana katika kitabu kiitwacho “history of Islam kilichoandikwa na Pro. Masudul Hassan ukurasa wa 43

(iii) kuabudiwa kwa miungu iitwayo lata, uzza na manata

Qurani 53:18-20,23 suratul An-najm

kwa yakini aliona nabii muhammad mambo makubwa kabisa katika alama (Qudra) za mola wake.je mume waona lata na uzza? Na manata mungu wenu mwingine wa tatu, kuwa ndio waungu hao badala ya mwenyezi mungu? Hayakuwa hayo majina ya lata mungu mwanamke, na uzza mungu mwanamke mwenye enzi na manata, mungu mwanamke anaye neemesha ila ni majina tu mliwapa nyinyi na baba zenu…

(iv) kuabudiwa kwa Allah (s.w.) na majahilia (wajinga)

makureshi pamoja na waarabu wenzao ambao walikuwa wakabudu miungu mingi kama tulivyoona huko juu. Vilevile miongoni mwa hiyo miungu walimuabudu Allah (S.W.) ambaye ndiye aliyekuwa mungu mkubwa, na miungu ya hata na uzza na manata wakawaitakadi kuwa mi waungu wanawake ama wake zake Allah au watoto wake. Hayo tunayaona katika ufafanuzi wa aya ya 180 katika Qurani suratul Al- A’raf na pia katika kitabu kiitwacho history of isalmu kilichoandikwa na pro masudul hasan ukurasa 43. ushahidi wa wazi zaidi wa kuonyesha kuwa waarabu majahilia walimuabudu Allah tunaupata katika vitabu vifuatavyo…

(i) kuzaliwa kwa Muhammad S.A.W. mtume wa waislamu

maombi na dua ya abdul mutalib kwa Allah.

Tunaposoma kitabu cha maisha ya Muhammad S.A.W. kilitangwa na sheikh Farsy ukurasa wa 5 kuna maneno hayo…


Pale pale alfajiri alipokwisha kuzaliwa mtume alikwenda kuitwa babu yake kuja kumwona mjukuu wake. Babu huyu alifurahi sama na akamfunika manguo mjukuu wake, na akamfunika manguo mjukuu wake, akajikongoja naye mpaka kwenye Al-ka’ba akafungua mlango akaingia ndani, akasimama, akamwombea dua kwa mashairi mazuri ya kiarabu aliyoyatunga mwenyewe wakati ule ule, kisha akarejea naye na jua bado halikuchomoza.

Ushahidi wa wazi unaothibitisha kuwa baba yake Muhammad Abdul muttalib aliomba dua kwa Allah tunaupata tunaposoma utangulizi wa suratul al-fyl ulio katika juzuu ya ukurada wa 946 Qurani iliyotafsiriwa kwa kiswahili chapa ya nane tunasoma maneno hayo. “chifu mkuu wa makka zama hizo alikuwa Abdul muttalib, alikwenda al ka’ba pamoja na baadhi ya machifu wa kikuraish na akilishika komeo la chuma la mlango wa al-ka’ba, akamwambia Allah (S.W.0 kuilinda nyumba yake pamoja na wahudumu wake. Zama hizo kulikuwa na masanamu 360 ndani na kando ya Al- ka’ba.”

(v) imani ya Abdul muttalib ilikuwa hii.

Katika kitabu kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu wa kiislamu aitwae ale muhsin barwani ukurasa wa 153 tunasoma maneno haya; “hapakutokea mwarabu ambaye alipewa jina hilo na babu yake tangu kuzaliwa kwake, na huyo babu hakuwa mkristo bali alikuwa akifuata mila za kishirikina.” Na wala hakujua taurati wala injili.

(vi) himizo la Muhammad (S.A.W.) kwa makureshi wenzie kuhusu mungu aitwae Allah.

Katika kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu kilichotungwa na sheikh said moosa muhamed al kindy juzuu ya mwanzo na pili chapa ya kumi ukurasa wa 130 tunadoma maneno haya: “katika wakati wa ujaahiliya kabla mtume (S.A.W.) kupata utume alikuwa akiwaambia waru “enyi watu semeni laa ilaha illah laah mtafuzu” yaani hana mola ila Allah mtafuzu.

Huu ni ushahidi wa wazi kabisa ya kwamba Allah aliabudiwa na makureshi ma waarabu wenzao hao watu walikuwa washikina , wapagni na majahilia (wajinga). Kumbuka Muhammad alikuwa ni mkureshi naye aliposema “hapana mola ila Allh” alikuwa yupo za ujahilia na hakuwa anajua kitabu wala imani tazama Qurani 42:52 Suratul shuraa.

(vii) je, mungu anayeabudiwa ba waislamu jina lake ni nani?

Qurani 17:110 suratul ban israil wana wa Israel

sema: “mwombeni mwenyezi mungu kwa jina la Allah au muombeni kwa jina la rahman kwa jina lolote mtakalo mwita katika hayo itaifaa: kwani ana majina mazuri mazuri,” wala usiiseme sala yako kwa sauti kubwa wala usiseme kwa sauti ndogo, bali shika njia baina ya hizo katikati si kwa kelele wala kimya.

Katika aya hii tunaona jina la mungu anayeabudiwa ba waislamu anaitwa Allah. Katika qurani jina hilo limetjwa mara 2,866 kumbuka kuwa makureshi na waarabu wenzao waliokuwa washirikina wapagani na majahilia wajinga kabla ya uislamu walimuabudu mungu huyo aitwae allah swali muhimu je, waislamu hawakutithi mungu wa makureshi? Tafakari kwa makini.

(viii) mji mkuu wa makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia ambako walikuwa wanaenda kuhiji ni huu

Tunaposoma utangulizi wa suratul Quraysh katika juzuu ya 30 ukurasa wa 950-951 chapa ya nane ya Qurani ya kiswahili kuna maneno haya…kabila la kureshi lilikuwa limetawanyika kote hijaz hadi zama za Qusayy bin kilaab mmoja wa mababu wa mababu wa mtume (S.A.W.). kwanza kabisa Qusayy aliwakusanya makureshi pamoja huko makka, na hivyo kabila hili likawa wadhamini wa Al-ka’ba kwa msingi huo, Qusayy alikuwa akiitwa mujammi mkusanyaji wa wartu wa habila lake. Mtu huyu kwa busara yake aliweza kuasisi serikali katika mji wa makka, na akaweka mipango mizuri kwa ajili ya mahujaji wajao toka kote arabuni, na matokea yake ni kuwa makureshi walipata umaarufu mkubwa miongoni mwa makabila ya kiarabu.

Hapa tunaona kuwa zama za ujahilia na upagani kabla ya dini ya uislamu waarabu wote walienda kuhiji katika mji wa makka kwenye nyumba ya Al-ka’ba inayoitwa “Bait-ullah” yaani nyumba ya allah. Kumbuka nyumba hiyo hiyo wapagani wa kiarabu zama za ujahilia (ujinga) waliabudu miungu 360 na Allah ndiye mungu wao mkuu.

Mji mkuu wa hija kwa waislamu ni huu.

Qurani 3:96 suratul Al-aal-imran (watu wa imran)

kwayakini nyumba ya kwanza iliyewekwa kwa ajili ya watu kufanya ibada ni iloe iliyoko makka, na yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote.

Qurani 22:27-29 suratul Al-Hajj. (Hijja)

Na (tukamwambia “utangaze kwa watu habari ya Hijja, watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyekonda kwa machofu ya njiani wakija kutoka katika kila njia ua mbali; ili washuhudee manufaa yao na ili wakushirishe kulitaja jina la mwenyezi mungu katika diku zinazojulikana fadhila zake na juu ya yale aliyowaruzuku, nao mi wanyana wenye miguu mine. Na kuleni katika wanyama hao na mlisheni mwenye shida na fakiri. Kasha wajisafishe toka zao, na watimize hadhiri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe Al-ka’ba.)

Tunaposoma ufafanuzi wa aya ya 29 ulio ndani ya Qurani katika juzuu ya 17 kuna maneno haya; “kabla ya uislamu waarabu walikuwa wakiitukuza Al-ka’ba. Na kwa ilivyokuwa ni jingo la zamani sana waliita Al-Baytul’Atiq yaani nyumba ya kale.”

Kama vile waarabu wapagani, makafiri na majahilia mji mkuu wa Hijja ni makka kule Saudi Arabia ndivyo ilivyo kwa waislamu nao mji wao mkuu ambao wanaenda kuhiji ni makka. Isitoshe Qurani inasimulia kuwa makka ni mama wa miji soma hayo katika Qurani 6:92 suratul Al- An-Am (wanyama) waislamu popote walipo duniani wanaambiwa wanaposali waelekeze nyuso zao mahali maalumu,

Qurani inasimulia hivi

Qurani 7:29Suratul Al- Araf

Sema: mola wangu ameamrisha uadilifu, na ameniambia nikuambieni elekezeni nyuso zenu kwake wakati wa kila sala…

Je mola huyo ambaye anasema kuwaambia wenye kufuata Qurani waelekeze nyuso alipo huko ni wapi?

Qurani 27:91 suratul An-Naml

Bila shaka nimeamrishwa nimwabudu mola wa nji huu wa makka ambaye akadiri ya aya hizi tunaona kuwa qurani inasimulia kuwa mola huyo ni wa mji wa makka ambaye…

Katika ibada zao waislamu huelekeza nyuso zao kibla nako ni katika msikiti wa Al' ka’ba iliyoko makka Qurani 2:144-150 mola wa mji wa makka ndiye Allah ambaye aliabudiwa na waarabu washirikina zama za ujahilia, na ndiye huyo huyo anoyeabudiwqa na waislamu.

(ix) kuzunguka Al- ka’ba wakiwa uchi wakati wa ibada.

Kabla ya dini ya uislamu makureshi na waarabu wenzao walikuwa wakiizunguka Al-ka’ba “bait ullah’ yaani nyumba ya Allah wakiwa uchi wake kwa waume walikuwa wakiitikadi nguo ni kitu kinachopata uchafu kwa hivyo hakistahiki kuvaliwa wakati wa ibada hayo tunayaona katika kitabu cha maisha ya Muhammad ukura wa 4 kilichotungwa na shikh Abdullah saleh Al Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu wa Zanzibar baadaye nchini Kenya. Siyo Farsy peke yake ambaye aliyeandika hayo bali na mwanachuoni maarufu aitwae Abul A’la maududi katika kitabu chake kiitwacho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 43 aliwaelezea waarabu hivi: maisha yao yalikuwa ya kishenzi. Mambo yao yalikuwa ya kishenzi na wakati wote walisherekea uzinzi kamari na ulevi. Kuteka nyara na kunyang’anya ulilokuwa useni wao, kuu na kutwaa wanawake kwa nguvu ndizo zilikuwa tabia zao halisi. Wakiweza kukao tupu uchi mbele za wenzao pasina haya wala hata kuona wamefanya jambo lolote la fedheha. Hata wake zao walikuwa wakiizunguka al-ka’ba uchi. Kwa ajili ya fikira za ujinga mtupu ati wa kuchunga heshima zao, waliwaua mabinti zao ili asije mtu akawa mkwa wao. Walikuwa wakiwaoa mama zao wa kambo baada ya kufa baba zao. Walikuwa wajinga hata wa mambo madogo ya kula, kuvaa na kunawa. Ama katika imani zao za kidini, walikuwa na ugonjwa ule ule uliotokana na uovu uliokuwa ukipoteza ulimwengu mzima.

Kumbuka Allah ndiye mungu waliomuabudu waarabu hao na nyumba yao ya ibada ni Al-ka’ba jambo la kushangaza maulamaa Abul A’la maududi ana sema kuwa waarabu hao walikuwa na uovu ulioupoteza ulimwengu mzima. Swalli je, kuzunguka Al-ka’ba na kumwabudu Allah ndio kuupoteza ulimwengu?

Je, waislamu wanapoenda Hijja wanaizunguka Al-ka’ba?

Kabla ya kujua mambo wanayoyafanya waislamu kule Al-ka’ba inafaa tujue jinsi Al- ka'ba ilivyo. Neno ka'aba ni la kiarabu lina maanisha kitu cha mirabo sita iliya sawa, ka’ba ni la kiarabu linamaanisha kitu cha miraba sita iliya sawa. Ka’aba ni jingo lenye ureru wa meta 12 upana meta 10 na urefu kwenda juu meta 15 jengo hilo lipo makka kule daudi Arabia. Jingo hilo limefunikwa na na mapazia meusi yaliyotariziwa aya za Qurani kwa herufi za kiarabu kwa kutumia uzi wa dhahabu halisi. Katika pembe ya mashariki ya ka’aba kuna jiwe jeusi katika kiarabu jiwe hili linaitwa “hajarul Aswad”.

Qurani inawaagiza waislamu wafanye ibada zao za Hija hivi…

(i) kuzunguka Al-ka’aba

qurani 22:29 suratul al-Hajj

Na kasha wajisafishe taka zao na watimize nadhitri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe ya Al-ka’ba)

kadiri ya aya hii tunaona kuwa Allah anawaagiza waislamu waizunguke Al- ka’ba huko nyumba tuliona kuwa waarabu wapagani waliizunguka Al-ka’ba wakiwa uchi bila nguo je waislamu wao wanaizunguka Al-ka’ba wakiwa vipi?

Tunaposoma kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikwa na mwanachuoni wa kiislamu aitwae A. sulemani ukurasa wa 16 kuna maneno hayo: “ni haramu kuvaa nguo zilizoshonwa kwa mwanamume muhrim anayekwenda kuhiji makka kwenye Al-ka’ba (msikiti). Kushona hapa ina maana kushona kwa ajili ya kuvaliwa siyo kama kiraka, vazi linalozunguka mwili kama shati, suruali na kadhalika anaruhusiwa kufunga kwa pini au mkanda nguo za hiramu ili zisivuke yaani nguo mbili kama mgolole.

Kadiri ya maneno haya waislamu katika hija yao kule ka’ba wazunguka ka’ba wakiwa wanavaa nguo sisizo shonwa zinaitwa “ihram” yaani mashuka mawili meupe.

(x) ibada ya kuomba kubusu na kuliheshimu jiwa jeusi “hajarul Aswad” katika Al-ka,aba msikiti wa makka.

Makureshi pamoja na waarabu wenzao kabla ya uislamu walikuwa wakiheshimu sana nyumba ya allah al-ka’ba pamoja na jiwe jeusi liitwalo kwa kiarabu “hajaral Aswad” wakati huo wakiendeleza ibada zao za kishiriki kipagani na zilizojaa ukafiri. Jambo linalotuthibitia kuwa makureshi waliheshimu al kaba na jiwa jeusi tulipata katika kitabu cha maisha ya Muhammad (s.a.w) kilitungwa na sheikh Abdullah saleh Al-Farsy ukurasa wa 15-16 kuna maneno haya: “kujengwa kwa Al- ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-kaba ilifanya nyufa kubwa, na ikakaribia kuvunjika, makureshi wakafanya shauri ya kuivunja na kujenga yote upya, Al-ka’ba ilikuwa haina sakafu…lakini Hajarul Aswad lilipokuwa likitaka kuwekwa mahali pake baina ya ukuta wa kusini na mashariki. Hapo ndipo walipogombana kilaukoo ukitaka mkubwa wao aliweke. Ugomvi ukashika nguvu. Kazi ikazuilika kwa muda wa siku tano, panangojewa vita tu, tumbo litakalo shinda ndilo liweke jiwe la Hajarul Aswad…mara kwa bahati nzuri aliingia mtume, alikuwa hakupata utume bado. Na hapo wote wakasema kwa umoja wao: “Hadhal Amin huyu yule mwaminifu na sote tumekubali” mtume akalichukua lile jiwe akalitia katila shali yake, akamwita kila mkubwa na ukoo; kisha akawaamrisha walichukue kiti mpaka mahjali pake. Hapo mtume akapokea akaliweka yeye kwa mikono wake na kwa radhi yao wote.

Huu ni ushahidi kuwa makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja walikuwa wanaihwshimu sana Al-ka’aba na jiwe jeusi lililokuwa ndabi ya msikiti huoj wa la’aba. Ambamo ndiyo sehemu waliokuwe wakizunguka wakiwa uchi wake kea waume, na hata Muhammad tunaoma alishiriki katika Al-ka’ba hiyo kwani na yeye aliweka hilo jiwe keusi na makureshi wote walikubali afanye hivyo. Swali la muhimu la kujuuliza je waislamu hawakurithi ibads hizo za ujahilia? Endelea…

Je, waislamu wanafanya ibada ya kuomba, kugusa, kubusu na kuliheshimu jiwe jeusi “Hajarul aswad”

Tunaposoma vitabu mbalimbali vya kiislamu tunaona namna ambavyo waislamu wanavyo fanya ibada ya kuliheshimu jiwe jeusi lililo katika msikiti mkuu wa makka uitwao Al-ka’ba unaofahamikakuwa ni “bait ullah” yaani nyumba ya Allah. Baadhi ya vitabu hivyo ni hivi…

  1. kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu mtungaji sheikh said moosa muhamed al-kindy ya 3-4 chapa ya 14 ukurasa wa 75 kuna maneno haya; kasema mtume (S.a.W.) ya mwenyezi mungu katika Ardhi. Basi atakaye ligusa basi kafungamana na wenyezi.
  2. katika kitabu cha hadithi za Muhammad cha sahih al-bukhari vol. Ii ukurasa wa 397 hadithi na 682. kastika hadithi hii tunaambiwa kwamba “kila wakati mtume saw alikuja kwenye jiwe jeusi akalielekezea kikdolw na kusema Takbirt maana yake Allah ni mkuu.
  3. swahaba kwa mtume aliyeitwa umar bin khattab alilibusu jiwe jeusi al Al-ka’ba kasha akadema: “bila shaka nafahamu wewe ujiwe lisiloweza kumfaidia wala kumdhuru mtu yeyote. Kama nisingalikuwa nimemwons mtume )S>A.W.) akibusu mimi nisingalikubusuu” kiarabu chepesi cha maneno hayojni hivi; inna alamu annakha hajarul atadhura wala tanalwau. Walaula annahu tahiyyatu rasul Allah (S.A.W.) yakabalka makabul atukha.”
  4. kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikdwa na A-sulelman ukurasa wa 29-30 kuna maneno haya: Hajar-al Aswad (jiwe jeusi) “kabla ya kuanza kuzu\nguka Al-ka’ba ni uzuri kwanza kuliendea hajar-Al Aswad lililoko Al-ka’aba hapo husogea karibi ikiea inayumkinika kikaribia bila ya kuumiza watu unalikabili Hajar-Al Aswad una lieekea mkona na bila ya kusema unalikabili Hajar-Al Aswad unaliweka mkono na bila ya kusema unalibusu mara tatu na kuligusisha kipaji chako cha uso mara tatu kwa wawake kufanya hivi ni suna ikiwa hapana zogo la dwaru, ikiwa hulifikiri liashire kea mkono. Tena mtu hurudi kwenye Hajar-al Aswad na kuligusa, kulibusu mara tatu na kugusisha kipaji cha uso mara tatu kama vile mwanzo tena utasema Allahu Akbaaar mara tatu (huku ukilashiria hajar kea mikono yote miwili ikisha utaongeza “Alla humma iimana bika wartaddika bikitabika wafaa biahdika wattibaa lisunnat nabiyyika salla ila hu Alayhi wassalim.” Kiwsaili. “ewe mola kwa imani yengu juu yako na kuthibitisha kitabu chako na kutekeliza ahadi yako uya kufuata mwendo wa mtume. Tena hapo utapita kulipita Hajar-Al Aswad ukilielikea huku ukiendelea kuzunguka Al-ka’aba yote nzima.
  5. kumbuka tendo la kuzunguka Al-ka’aba lilifanya washirikina na dwapagani wa kiarabu zama za ujahilia kabla ya dini ya uislamu kuanza. Na waislamu noo huizunguka Al-ka’aba swali je, waislamu hawakurithi eneo la ibada za ujahilia tafakari.

Mungu wetu yehova anavyotufundisha kuhusu ibada ya jiwe.

Mambo ya walawi 26:1

Msifanye sanamu yeyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jifee lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kilisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana mungu wenu.

Kadiri ya mafundisho ya mungu wet yehova ambaye wakristo tumuabudu ni kakosa makubwa kuchukua jiwe na kulisujudu. Tafakari kuhusu waislamu na matendo yao katika jiwe la jeusi “Hajarul Aswad.”

(xi) ibada ya kuzunguka majabali (vilimo) vya safaa na marwa huko makka kabla ya uislamu.

Qurani 2:158 suratul Al-Baaraqh (Ng’ombe jike) hakika safaa na marwa (majabali mawili yana yofanyiwa ibada ya kusai huko makka) ni katika alma za kuadhimisha dini ya mwenyezi mungu basi anayehiji kwenyu nyumba hiyo ar kufanya umra. Si kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili na anayefanya wema (atalipwa) kwani mwenyezi mungu ni mwenye shukrani na mjuzi wa kila jambo.

Ufafanuzi wa aya hiii ya 158 ulio katika qurani ni huu katika ibada ambazo hazisihi kufanywa ila makka ni hizi (a) Hijja na (b) umra. Na takriba zote mbili hizi ni sawa sawa ila zinakhitalifiana. Kidogo to. Moja katika hitilafu zao ni kuwa Hijja haifanyi ila miezi makhususi: na mwisho wa miezi ya Hijja ni kumi la mwanzo la mfungo tatu…ama mengine bi sawa. Nayo ni: (1) kuzunguka Al-ka’aba mara 7 (2) kwenda matiti mara 7 baina ya majabali hayo mawili ambalo moja linaitwa safaa na moja linaitwa marwa (3) kunyoa nywele au kuzikata. Majabali hayo kabla ya uislamu yalikuweka yamewekwa juu yake madanamu na makafiri wakiyaabudu. Basi ulipokuja uislamu. Waislamu wengine waliona labda si vizuri kufanya ibada haopo penye majabali hayo. Basi wakaambiwa kuwa si vibaya.

Maelezo ya aya hii yanafanana na yle yaiyo katika saqhih Al-Bukhari volii ukurasa wa 415-416 hadith no. 710 pale Asim alipomuuliza Anas bin maliki (A.S.) hivi: je, ulikuwa ukichukia kufanya tawaf (yaani kuzunguka) kati ya safaa na marwa? Akasema ndiyo kwaqsababu ni matendo ya kwaida (sherehe) iliyofanyofanyika wakati wa ujinga kutajua kabla ya uislamu kuja. Imesimuliwa pia kuwa Muhammad alifanjya tawwaf ya ka’aba na sa’I ya safa na marwa ili kuonyesha nguvu zake kwa safa na marwa. Hayo yamesimuliwa katika sahih Al Bukhari vol ii hadithi no.711. jambo linaloshangaza ni kuwa ibada hiyo ilifanywa na makafiri zama za ujahilia (ujinga) na waislamu nao wazunguka vilima hivyo isitoshe insshangaza kuona Allah mungu anayeabudiwa ba wislamu anayaita majabali hayo minshahilillah yaani alama za mungu au kwa kiingereza “symbols of Allah” hii ni ajabu kuona vilima vinaitwa hivyo.

Bwana yesu anatufundisha nini kuhusu ibada ya milima? Yohana 4:19-22

Yule mwanamke akamwambia bwana naona ya kuwa unabii, baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko yerusalemu ni mahali patupa sapo kuabudjiwa. Yesu akamwambia mama, unisadiki saa ubajyha ambayi gamtamwabudu baba katika mlima huu, wala kule yersalemu, ninyi mnaabudu msichokijua sisu tunaabudu tukijuacho kwa kuwa wokovu watoka kwa wayahudi.

Katika aya hizi Bwana Yesu anatuambia kuwa wale wanaofanya ibada katika mlima hawajui wachokiabudu. Ndugu tafakqari ibada ya waislamu katika vilima je, wanajua wanachokiabudu?

(xii) mwezi wa ramadhani.

Tunaposoma katika kitabu cha maisha ya muhammaf ukurasa wa 32 kilichotungwa na sheikh Farsy tunaona kuwa miezi iliyotumiwa na waarabu kabla yo dini ya uislamu ndiyo inayotumiwa ba waislamu. Kitabu hicho kinasomeka hivi…”Makka tangu kabla ya uislamu, ilikuwa ni mahali patakatifu kwa waarabu wote. Kila mwaka walikuwa wakija kuhiji miezi hii hii wanayoitumia sasa waislamu katika kuhiju kwao.

Waarabu walikuwa washirikina na wapagani majahilia. Walikuwa na mwezi wa ramadhan nalo ndio mwezi ambao dwaislamu wana amini kuwa Muhammad alipata utume. Tazama kitabu cha maisha ya Muhammad ukurasa 16-17.

Ibada ya kufunga katika mwezi wa Ramadhan kwa waislamu

Qurani 2:183 suratul Al-Baarah (Ng’ombe jike)

Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyoiazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu.

Imeelezwa katika sahih Bukhari volii Hadith 662 vol. Iii Hadith no. 219 na 220 pia vol vi Hadith no.31 ya kuwa Muhammad aliamuru waislamu wafunge siku ya Ashura siku ya 10 ya mwezi kwanza katika mwaka wa kiislamu yaani mweziuitwalo muharram) kufunga huko kaqbla ya uislamu ilikuwa ni desturi katika dini ya Hums na uislamu ukaichukua.

(xiii) kumpiga mawe shetani katika bonde la wadah muhassir.

Miongoni mwa tendo moja kubwa linalofanya na waislamu wanapofika hija huko makka ni kumpinga mawe shetani. Kitabu kiitwacho vipi uhiji ukurasa wa54,55,61 kuna maneno haya…”Mahujaji wanapofika bonde liitwalo wadi ah muhasisi karibu na mina ni suna kunyapuka hao huelikea jamrat al a quba (shetani mkubwa) na hupiga yale mawe saba waliyoyaokota muzdelifa baada ya kupiga mawe jamarati Al-Aqaba hufuatiwa na kuchinja.

Kwa sisi wakristo tunajua shetani ni roho ya uasi waefeso 2:1-5 na ni roho ya udanganyifu 1 Timotheo 4:1-2. Hivyo huwezi kumshinda shetani kwa kumpiga kwa mawe maana ni roho tu. Roho ni upepo au pumzi. Biblia inatufundisha kuwa tunamshinda shetani kwa njia ya imani sahihi ya mungu, kushika neon la mungu, dala, na maombi, hivyo tutamshinda shetani soma waefeso 6:11-18.

  1. Wajibu wa Mkristo baada ya kuujua uislamu.

Ninaamini kuwa imejifunza mengi kuhusu dini ya uislamu, na umeona mambo mengi yuanayotendeka na waislamu kule makka wakati wa hija. Mambo hayo yalifanywa na makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja, na tena umeona kuwa mungu tunayemwabudu wakristo hataki ibada zinazoshirikisha mawe na milima. Basi wajibu wako mkristo kuwafikishia injili waislamu na watu wa dini nyingine zisizomuamini Bwana Yesu, ili wamdwamini na wapate kuokolewa. Kumbuka injili ndio uweza wa mungu uletao wokovu Warumi 1:16. na tena injili ndilo neon la kweli Wakolosai 1:5. bwana akubariki sana ni mimi katika utumishi wa Bwana Yesu Mwalimu;

Eleutary H. Kobelo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW