Sunday, June 21, 2020

ELIYA WA BIBLIA SIO ILYAS BANDIA WA QURAN

ELIYA WA BIBLIA SIO ILYAS BANDIA WA QURAN

Tuanze kwa tafsir ya jina Elijah:

Kwa Kiebrania ni אליהו Hebrew: אֵלִיָּהוּ, Eliyahu, ina maana ya "My God is Yahweh. Mungu wangu ni Yehova.

Kwa Kiarabu ni إيليا 'iilia

Kwa Kiswahili ni Eliya.

Kama nilivyo anza kwa kuweka tafsiri ya jina la Nabii Eliya. Umeona kwa Kiarabu ni LILIA na sio Ilyas kama Waislam wanavyo dai. Swali la kujiuliza, kwanini Manabii wote wa Kiislam wana majina tofauti na tafsiri sahihi kwa Kiarabu?

Nabii Eliya ni mmojawapo wa watu wenye kuvutia na mtu maridadi zaidi katika Biblia, na Mungu akamtumia wakati wa kipindi muhimu katika historia ya Israeli kumpinga mfalme mwovu na kuleta ufufio katika nchi. Huduma ya Eliya ilisababisha mwanzo wa mwisho wa ibada kwa Baali katika Israeli. Maisha ya Eliya yalijawa na matatizo. Wakati mwingine alikuwa mwenye ujasiri na mwenye uwezo wa kufanya uamuzi, na wakati mwingine alikuwa mcha Mungu and msikifu. Kwa upande mwingine yeye ni dhihirisho la ushindi na uhodari, ikifuatiwa na kurudisha kilichopotea. Eliya alijua nguvu zote za Mungu na kina cha msononeko.

JE, KWENYE UISLAM NABII WAO BANDIA ILYAS ALIWEZA KUISHI NA KUFANYA MIUJIZA KAMA NABII ELIYA?

Suratul Ass Affat 123. Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume. 123

124. Alipo waambia watu wake: Hamwogopi? 124

125. Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji, 125

126. Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani? 126

127. Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa; 127

128. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. 128

129. Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye. 129

130. Iwe salama kwa Ilyas. 130

131. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. 131

132. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.

Na ametajwa tena kwenye (Al-An`am 6:85).

FIKICHA AKILI SASA:

Hapo juu ndio ujumbe kamili wa Nabii Ilyas wa Waislam na hakuna zaidi yake. Swali la kujiuliza, yupo wapi Elisha ambaye alichukua Joho lake wakati Eliya anapaa kwenda mbinguni?

Upo wapi mwisho wa Nabii Ilyas wa kwenye Quran na je unafanana na jinsi aliyo paa kwenda mbinguni?

Kwanini Ilyas wa Quran hakufanya miujiza kama Eliya wa kwenye Biblia?

SASA TUMSOME ELIYA WA KWENYE BIBLIA

Mara nyingine tunamwona Eliya akiwa mhusika mkuu ni katika makabiliano na manabii wa uongo wa Baali kwenye Mlima Karmeli (1 Wafalme 18: 17-40). Manabii wa Baali walimwita mungu wao mchana kutwa ili azushe moto kutoka mbinguni bila mafanikio. Kisha Eliya akajenga madhabahu ya mawe, akachimba shimo kando yake yote, akaweka dhabihu juu ya kuni na akaomba maji yamwagwe juu ya dhabihu yake mara tatu. Eliya akamwita Mungu, na Mungu akateremsha moto kutoka mbinguni, ukachoma ile dhabihu, kuni, na mawe na kuvyonza maji kwenye shimoni. Mungu alionyesha kuwa alikuwa na nguvu zaidi kuliko miungu ya uongo. Ilikuwa ni wakati huo Eliya na watu waliwaua manabii wote wa uongo wa Baali, wakifuata amri ya Mungu katika Kumbukumbu la Torati 13: 5.

Baada ya ushindi mku juu ya manabii wa uongo, mvua ikaanguka tena katika nchi (1 Wafalme 18: 41-46). Hata hivyo, licha ya ushindi huo, Eliya aliingia katika kipindi cha myumbisho wa imani na msononeko (1 Wafalme 19: 1-18). Ahabu alikuwa amekwishamwambia mkewe, Yezebeli, dhihirosho la nguvu za Mungu. Badala ya kumrudia Mungu, Yezebeli aliapa kumwua Eliya. Eliyo aliposikia jambo hili, alikimbilia jangwani, ambako aliomba Mungu ayachukue maisha yake. Na badala yake Mungu alimhuhisha Eliya kwa chakula, kunywaji, na usingizi. Kisha Eliya alishika safari ya siku arobaini kwenda Mlima Horebu. Huko mlimani Eliya akaficha ndani ya pango, huku akijihurumia mwenyewe na hata kukiri kuwa yeye pekee ndiye aliyekuwa amebaki kati ya manabii wa Mungu. Hapo ndipo Bwana alimwambia Eliya asimame juu ya mlima, Bwana anapopita. Kulikuwa na upepo mkubwa, tetemeko la ardhi, na kisha moto, lakini Mungu hakuwa katika yote hayo. Kisha kukaja sauti nyororo, ambayo Eliya alimsikia Mungu na kumwelewa. Mungu akampa Eliya maagizo ya chenye atafanya baadaye, ikiwa ni pamoja na kumtia mafuta Elisa ili achukue nafasi yake kama nabii na akamhakikishia Eliya kwamba bado kulikuwa na watu 7,000 huko Israeli ambao hawakuwa wamepiga goti lao kwa Baali. Eliya alitii amri za Mungu. Elisha akawa msaidizi wa Eliya kwa muda mfupi, na hao wawili wakaendelea kukabiliana na Ahabu na Yezebeli, pamoja na mwana wa Ahabu na mrithi wake, Ahazia. Badala ya kufa kifo cha asili, Eliya alichukuliwa mbinguni kwa upepo wa kisulisuli (2 Wafalme 2: 1-11).

Maswali:
Je, Eliya wa kwenye Biblia ndio yule Ilyas bandia kwa kwenye Quran?

Je, Eliya wa Biblia amabe jina lake maana ya Mungu wangu ni Yehova ni yule yule Ilyas wa Quran wa Allah?

Je, maana ya Eliya wa Biblia na Ilyas wa Waislam ni ilele yaani Mungu wangu ni Yehova?

Je, Allah ni Yehova?

HAKIKA ELIYA WA BIBLIA SIO ILYAS BANDIA WA KWENYE QURAN.

Shalom,

Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW