Monday, March 18, 2019

Israel yapeleka kitabu cha Biblia mwezini


BIBLIA NDIO KITABU PEKEE NA CHA KWANZA KUFIKA MWEZINI
ISRAEL imetuma chombo cha anga za mbali ambacho kimeanza safari yake ya miezi miwili kabla ya kutua mwezini kikiwa na Biblia na vitu vingine mbalimbali ambayo vitaachwa huko.
Gharama za kuisafirisha Biblia ni jumla ya Dola Milioni mia moja za Kimarekani.
Chombo hicho kilichorushwa majira ya saa 8:45 usiku wa Alhamisi kutokea Cape Canaveral, Florida, Marekani, kikiwa kinasafirishwa na roketi ya Falcon 9 kutoka kampuni binafsi ya SpaceX inayomilikiwa na bilionea Elon Musk, kina uzito wa kilo 585 na kimepewa jina la Beresheet linalomaanisha “Mwanzo” kwa lugha ya Kihebrania.
Beresheet imeweka rekodi ya kuwa chombo cha kwanza kilichopelekwa mwezini kwa ufadhili binafsi na chombo cha kwanza kwa taifa la Israel na endapo kitafanikiwa kutua mwezini, Israel itajiunga na Marekani, Urusi na China kama nchi pekee zilizowahi kufanikiwa kutua vyombo kwenye uso wa mwezi.
Chombo cha ”Mwanzo” kikifanikiwa kuingia kwenye mzunguko wa dunia na kuzunguka kwa muda wa wiki tatu, kitakutana na nguvu ya mvuto wa mwezi na kinatarajiwa kutua mwezini Aprili 11, 2019, ambapo kitapiga picha na kuzituma duniani kwa siku mbili kabla ya kujizima.
“Mwanzo” kimebeba vitu mbalimbali vya kuvipeleka mwezini vikiwemo kumbukumbu za Myahudi aliyepona katika Mauaji ya Hitler, Biblia ya dijitali, bendera na wimbo wa taifa la Israel na michoro mbalimbali ya watoto.
Inasemekana gharama ya chombo hicho hadi kupaishwa kwake, ni ndogo zaidi ya gharama za vyombo vingine viliyvowahi kufanya safari kama hiyo.
Shalom

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW